JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NIGERIA: Mwanamuziki David Adeleke maarufu kama “Davido” amekanusha uvumi kwamba amekamatwa nchini Kenya alipokuwa katika ziara ya muziki Aprili 1, 2024 baada ya Dawa za Kulevya kupatikana kwenye ndege yake binafsi

Kufuata uvumi huo #Davido amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya aliyeanzisha uvumi huo bila kujali kuwa ulikuwa ni mzaha wa Siku ya Wajinga (April Fools)

Inadaiwa kuwa taarifa hiyo iliyochapishwa kwa mara ya kwanza na K24 TV ya Kenya (Siku ya Jumatatu) na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. K24 TV haijatoa kauli kuhusina na suala hilo

Soma https://jamii.app/DavidoKenya

#JamiiForums #JFEntertainment
1
MAREKANI: Google imekubali kufuta mabilioni ya kumbukumbu za Watumiaji wa Programu yake ya Faragha (Incognito) na kuridhia kuondoa uwezo wake wa kufuatilia taarifa za Watumiaji wa Programu hiyo

Sharti hili ni chini ya makubaliano ya kisheria yaliyopendekezwa ili kumaliza kesi iliyoishitaki kampuni hiyo kwa uvamizi wa Faragha za Watu kwa kukusanya kumbukumbu za taarifa za Watumiaji hata walipokuwa wakitumia mtandao huo kwa Faragha (Incognito mode)

Aidha, Google imetakiwa kulipa takriban Tsh. trilioni 12.9 (Dola Bilioni 5) kama fidia

Soma https://jamii.app/GoogleFaragha

#JamiiForums #DataPrivacy
👍91
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia Ujenzi wa Barabara ya Boko Bulumawe ili Mkandarasi awajibike na Barabara hiyo ikamilike kwa wakati

Soma zaidi https://jamii.app/BarabaraYaBulumawe

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Uwajibikaji
1👍1
Kuchagua jina la Biashara ni mchakato muhimu sana katika kuanzisha Biashara yoyote. Jina la Biashara lina uwezo wa kuwa nembo ya kuitambulisha Biashara yako kwa wateja na inaweza kuathiri jinsi wanavyoona #Biashara yako.

Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ambayo Mdau wa Biashara na Masoko ndani ya JamiiForums.com anashauri Watu wazingatie katika kuchagua Jina la Biashara

Soma kufahamu mengi zaidi https://jamii.app/KuchaguaJinaBiashara

#JamiiForums #Uchumi #Ujasiriamali
2👍1
#MICHEZO: Kocha wa #ManchesterUnited, Erik ten Hag, ambaye ameomba mabosi zake wasimfukuze kazi kwa alichodai kikosi kipo kwenye mchakato wa mabadiliko, amesema wanatarajia kufanya uchunguzi wa ndani kubaini sababu za Wachezaji wake kuumia mara kwa mara ikiwa ni siku chache baada ya #LisandroMartinez na #VictorLindelof kupata majeraha

Mpaka sasa United ina wachezaji nane majeruhi wa kikosi cha kwanza huku ikitarajiwa kucheza dhidi ya #Chelsea katika #PremierLeague, leo Aprilli 4, 2024

Soma https://jamii.app/ManUtdInjuries

#JFSports #JamiiForums
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema Serikali inatarajia kuongeza huduma ya matumizi ya Gesi Asilia kwa wakazi wa Dar es Salaam na tayari kuna mpango wa kuifikisha katika Nyumba 10,000 Jijini hapo

Ameongeza “Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imesambaza Miundombinu ya Gesi Asilia katika Nyumba 880 za Dar, imejenga Bomba la Gesi lenye urefu wa Kilometa 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach kupitia Barabara ya Bagamoyo na tayari Viwanda viwili na Hoteli sita vimeunganishwa na Bomba hilo.”

Soma https://jamii.app/BungeAprili4

#Governance #JFHuduma #JamiiForums
👍6
AFRIKA KUSINI: Beki wa kati wa Klabu ya Kaizer Chiefs, #LukeFleurs, amefariki Dunia ikidaiwa alitekwa na Watu ambao bado hawajafahamika kisha ya kuuawa kwa Risasi

Klabu ya #KaizerChiefs imesema tukio hilo lilitokea Jijini #Johannesburg na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi

Fleurs (24) alitua Klabuni hapo akitokea SuperSport United, Oktoba 2023

Soma https://jamii.app/LukeFleursDeath

#JFSports #JamiiForums
👍4
AFRIKA KUSINI: Spika wa #Bunge, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu Nafasi ya Spika pamoja na kiti cha Ubunge baada ya Mahakama kutupilia mbali ombi lake la kutaka kuzuia asikamatwe kwa tuhuma za #Ufisadi

#Nqakula anatuhumiwa kupokea hongo ya Dola 135,000 (Tsh. 347,625,000) kutoka kwa Mkandarasi wakati alipokuwa Waziri wa Ulinzi (2012 - 2021). Inadaiwa Fedha hizo alizipokea kati ya Desemba 2016 na Julai 2019 na kuna Fedha nyingine zaidi ya Dola 100,000 (Tsh. Milioni 258) ambazo hakuzipokea

Soma https://jamii.app/NgakulaResigns

#JamiiForums #Accountability #Governance #Democracy
👍4
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mwanamuziki Juma Nature, ameweka Video akizungumzia suala la Ulinzi Shirikishi maarufu kama Sungusungu au Makamanda na Usalama wa Mitaani

Nature amehoji kwanini bado vitendo vya Wizi wa Mitaani vinaendelea licha ya Wananchi kuchangishwa Fedha za Ulinzi?

Aidha, ametoa wito kwa Serikali kutoa Vitambulisho au Sare maalumu kwa vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuwatambulisha, akitoa mfano wapo Watu wanaojifanya kuwa Askari ambao hukaba na kuiba

Vipi Mdau, hali ya Ulinzi Shirikishi Mtaani kwako ipoje? Kuna usalama?

Soma https://jamii.app/UlinziShirikishi

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Uwajibikaji #Accountability #Governance
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS SAMIA: MAWAZIRI MKAJIBU HOJA ZA CAG

Siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Charles Kichere kuwasilisha Ripoti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 kwa Rais #SamiaSuluhuHassan, Mawaziri wametakiwa kujibu hoja za ripoti hiyo baada ya kufikishwa Bungeni na kujadiliwa ili hatua zichukuliwe

Maelekezo hayo yametolewa na Rais Samia wakati akiwaapisha Viongozi walioteuliwa hivi karibuni

Soma https://jamii.app/UapishoAprili4

#Governance #JamiiForums #Accountability
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan ameagiza Mabadiliko katika Mfumo wa ulipaji wa Huduma za Maji akielekeza mchakato ufanyike ili malipo yafanyike kadiri Mtu anavyotumia kama ilivyo kwenye ununuaji wa Umeme

Ameeleza kuwa Mfumo huo utasaidia Watu kujidhibiti katika matumizi yao ya Maji

Soma https://jamii.app/UapishoAprili4

#Governance #JamiiForums #Accountability
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan amesema Paul Makonda alikichemsha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokuwa akitumikia nafasi ya Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM – Taifa kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Amemtaka akafanye kazi katika majukumu yake mapya sababu ana Imani naye

Soma https://jamii.app/UapishoAprili4

#Governance #JamiiForums #Accountability
👍2🤔1
UPDATE: Aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula (67), amejisalimisha Polisi Siku moja baada ya kujiuzulu Nafasi ya Uspika pamoja na Kiti cha Ubunge kutokana na tuhuma za Ufisadi

Anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi huko Pretoria

#Nqakula anatuhumiwa kupokea hongo ya Dola 135,000 (Tsh. 347,625,000) kutoka kwa Mkandarasi wakati alipokuwa Waziri wa Ulinzi (2012 - 2021).

Soma https://jamii.app/NgakulaResigns

#JamiiForums #Accountability #Governance #Democracy
👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Mbunge Ester Bulaya amesema Serikali imechangia kupunguza nguvu ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwa chanzo cha kushindwa kuwalipa Wastaafu wanaowekeza katika Mifuko hiyo kutokana na kuchukua Fedha kisha kutozirejesha na kufanya Uwekezaji mbovu

Aidha, ameongeza kuwa kumlipa Mstaafu kiasi cha Tsh. Milioni 17 hakitoshi badala yake ameshauri walipwe zaidi ya Asilimia 50 ya kiwango walichochangia

Soma https://jamii.app/BungeAprili4

#JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums
👍3