JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Diwani wa Kata ya Olektore, Tarafa ya Ngorongoro, James Moringe amedai aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Richard Rwanyakaato Kiiza alitumia Tsh. Milioni 400 ndani ya Miezi mitatu ikiwa ni gharama ya Hoteli huku akikataa kuishi katika Nyumba aliyotengewa

Moringe amedai Kiiza ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na Rais #SamiaSuluhuHassan (Machi 15, 2024) alikuwa akilipa Tsh. Milioni 3.2 kama gharama ya Hoteli kwa Siku

Soma https://jamii.app/TuhumaNgorongoro

#JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums #Accountability
👍6👎41
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Diwani wa Kata ya Olektore, Tarafa ya Ngorongoro, James Moringe ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wafugaji amemtuhumu aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Richard Rwanyakaato Kiiza, kuhusika katika Ubadhirifu wa Fedha za Serikali

Ametoa mfano kuanzia Oktoba 1, 2023 hadi Februari 2, 2024 kiasi cha Tsh. Milioni 945 kilichotwa na Kiiza kwa kutumia baadhi ya Watu

Pia, amedai Fedha za Mradi wa Msomera (Kuhamia Tanga) zilizotumika bila kuzingatia taratibu za kifedha kwa kisingizio cha Kazi Maalum ni Tsh. Bilioni 1.6 kati ya Oktoba 2023 hadi Machi 2024, hivyo anaiomba Serikali kuchunguza tuhuma hizo

Ikumbukwe Machi 15, 2024, Rais #SamiaSululuHassan alitengua Uteuzi wa Kiiza katika nafasi ya Kamishna wa NCAA

Soma https://jamii.app/TuhumaNgorongoro

#JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums
👍6
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad amesema maelekezo aliyoyatoa ni kuwa wakamatwe Watu wanaovuta bangi na sio wanaokula mchana huku akisisitiza hakuna Sheria inayokataza kula mchana Visiwani #Zanzibar

Amesema “Nilipokea ‘clip’ ikionesha Vijana wanavuta bangi mchana, nikatoa maelekezo ifanyike oparesheni wakamatwe kwa kuwa ni kosa la jinai, shida iliyojitokeza wakakamatwa waliokuwepo na wasiokuwemo, wavuta bangi na wanaokula mchana”

Ameongeza “Nadhani ulimi uliteleza kwa aliyesema tunakamata Watu wanaokula mchana. Tunafahamu kuna oparesheni zinazofanywa na Mamlaka nyingine za Kiserikali za aina hiyo lakini wajibu wetu Jeshi la Polisi ni kusimamia ili zifanyike kwa Usalama na Amani”

Soma https://jamii.app/KulaMchana

#JFMatukio #CivilRights #HumanRights #Governance #JFUwajibikaji #JamiiForums
👍5🤣5
TABORA: Mdau wa JamiiForums.com anadai tabia ya baadhi ya Taasisi za Elimu kuwauzia au kuwapa ‘Mawakala’ Taarifa Binafsi za Watu wengine (Majina, Namba za Simu na Namba za Mitihani) bila ridhaa ya wahusika si sawa

Anadai amepokea ujumbe wa Simu (SMS) ukiwa na taarifa za Mtoto wake aliyehitimu Shule ya Sekondari ya Ndono (Tabora) kumshawishi kujiunga na Chuo, akidai hajawahi kutoa taarifa hizo kwa waliomtumia. Anasema kitendo hicho ni hatari kiusalama

Soma https://jamii.app/KeroTabora

#DataPrivacy #DigitalRights #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #Faragha #JamiiForums
👍10
Aprili 2 kila Mwaka ni maadhimisho Siku ya Uelewa wa Usonji, inayolenga kukuza Uelewa ili kuongeza ushirikishwaji wa Kijamii wa Watu wanaoishi na hali ya Usonji

Usonji ni changamoto ya Ukuaji ambayo hutokea pale ambapo Ubongo hufanya kazi kwa namna tofauti. Mtoto hupata changamoto hii anapokuwa Tumboni na dalili huonekana kuanzia Umri wa Miaka Mitatu na kuendelea

Watu wenye Usonji hupata changamoto hasa za Kuwasiliana. Kasi ya kukua kiakili kwa Watoto wenye #Usonji huwa ndogo ikilinganishwa na kasi ya kukua Kimwili

Soma https://jamii.app/AutismDay2024

#JamiiForums #Autism #WorldAutismDay2024 #PublicHealth
👍3
ZANZIBAR: Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi, CP Hamad Khamis amesema taarifa zinazosambazwa na Chama cha #ACTWazalendo katika Mitandao ya Kijamii kuhusu hali ya uhalifu kuongezeka Visiwani Zanzibar ni za upotoshaji na wanaofanya hivyo wana malengo Binafsi ya Kisiasa

Amesema “Taarifa hizo zina lengo la kusababisha hofu na taharuki, pia baadhi ya Viongozi wa ACT-Wazalendo hapa Visiwani wamekuwa wakishawishi Wananchi wasijiunge na Vikundi vya Ulinzi Sirikishi kwa madai hiyo ni Sera ya chama kilicho madarakani.”

Baada ya kutokea kifo cha Katibu wa ACT-Wazalendo (Jimbo la Chaani), Ali Bakari Ali (Machi 29, 2024), chama hicho kilidai Ali alitekwa, alishambuliwa na kutupwa na Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, pia kikadai kuna vikundi vya kihalifu vinavyojiimarisha kila siku bila Jeshi la Polisi kuonesha uwezo wa kuvidhibiti

Soma https://jamii.app/UhalifuZanzibar

#JFMatukio #CivilRights #Governance #JFUwajibikaji #JamiiForums
👍6
Baadhi ya mijadala inayoendelea ndani ya JamiiForums.com kupitia Jukwaa la JF Chit-Chats and Jokes

1. Wadau wamejadili kuhusu Afya na baadhi ya tabia za watu ikiwemo wenye hasira za karibu, harufu mbaya kinywani na kuongea wakati wa kula kuwa ni baadhi ya tabia zinazokera

Je, wewe unakerwa na vitu au tabia gani unapokuwa karibu na watu?

Shiriki mjadala https://jamii.app/MtuKaribuHupendi

2. Mdau anauliza kwa hali ya sasa ya Uchumi wako unaweza kununua kitu gani unachojisikia?

Soma zaidi https://jamii.app/UchumiKununua

3. Mdau anaeleza jinsi alivyoaminishwa akiwa mtoto kuwa akisoma kwa bidii na kufaulu vizuri atafanikiwa lakini jambo hilo halijatokea

Kitu gani uliwahi kuaminishwa utotoni?

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/EnziUtotoUongo
👍62🥰1
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za mafuta zilizoanza kutumika leo Aprili 3, 2024 ambapo kuna ongezeko la bei kwenye Petroli na Dizeli huku Mafuta ya Taa bei ikibaki kama ilivyokuwa Machi 2024

Upande wa Dar es Salaam bei ya Petroli ni Tsh 3,257 ikiwa ni ongezeko la Tsh 94, Dizeli ni Tsh. 3,210 kuna ongezeko la Tsh. 84, Mafuta ya Taa bei ni Tsh. 2,840 sawa na ilivyokuwa mwezi uliopita

Baadhi ya sababu zilizotajwa na #EWURA kuchangia mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa bei za Mafuta Yaliyosafishwa (FOB) katika Soko la Dunia kwa wastani wa 3.94% kwa Petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya Dizeli, kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia Fedha za Kigeni kwa 3.19% kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa

Soma https://jamii.app/BeiYaMafuta

#ServiceDelivery #Governance #JamiiForums #Economy #Uchumi
👍92👎2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan anatarajiwa kuzindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza Uchumi wa Kidigitali

Tume hii ina majukumu ya kusimamia Sheria na kushughulikia malalamiko ya Ukiukwaji wa Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍21
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza katika Uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Emmanuel Mkilia amesisitiza Watu Binafsi na Taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi kujisajili na kupata vibali vya kuendelea kufanya wanachokifanya

Aidha, amesema “Tume ilianzishwa rasmi Mei Mosi, 2023 na itatekeleza majukumu yake #TanzaniaBara na #Zanzibar kwenye masuala ya Muungano.”

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
👍21