JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, #NapeNnauye, amesema Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni chombo muhimu katika kuimarisha Misingi ya #Demokrasia, Utawala Bora na Utawala wa Sheria na hivyo kuzidi kuvutia Wawekezaji kutoka Nje

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan akizungumza katika uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam amesema baadhi ya taarifa zinaweza kutumika kuhujumu Jamii

Amesema β€œWakati mwingine taarifa ya Mtu inaweza kusababisha unyanyapaa, vurugu, vita na hata mauaji.”

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan ametoa maelekezo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kuhakikisha Taasisi zote za Umma na Binafsi zinasajiliwa na zinatekeleza Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kabla au ifikapo Desemba 2024

Amesema hayo wakati akizindua Tume hiyo, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #SamiaSuluhuHassan ameelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie na kuhakikisha Mifumo ya #TEHAMA Nchini inasomana, ametoa maelekezo hayo baada ya kuzindua Mfumo wa Kisera na Kisheria wa Kulinda Taarifa Binafsi

Soma https://jamii.app/UlinziTaarifaBinafsi

#UlinziWaTaarifa #Faragha #SheriaMpya #LindaTaarifaTZ #PDPCTZ #PersonalDataProtection #JamiiForums
πŸ‘1
NJOMBE: Mery James Numbi, ameshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa kinyume na Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (cap 329 Re 2022)

Mshtakiwa akiwa Mtendaji wa Kijiji cha Lupembe Wilayani #Njombe aliomba na kupokea #Rushwa ya Tsh. 200,000 kutoka kwa Irine Justine ili asimchukulie hatua za Kisheria kwa Mtoto wake kutopelekwa Shule

Mery alikana makosa yote na kupewa dhamana. Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena Aprili 17, 2024

Soma https://jamii.app/MtendajiNjombe

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #KemeaRushwa #TokomezaRushwa
πŸ‘4
MAREKANI: 'Rapa' #KanyeWest amefunguliwa mashtaka na aliyekuwa Mfanyakazi katika Shule yake ya 'Donda Academy' iliyopo Los Angeles, kwa tuhuma za Ubaguzi na #Unyanyasaji

#TrevorPhilips amedai Kanye alikuwa akiwabagua Wafanyakazi wenye ngozi nyeusi. Pia, anadai Kanye aliwaamuru Wanafunzi kunyoa upara na kutaka kujenga Vyumba vya Shule kama jela

Mwaka 2022 Kanye alishtakiwa kutokana na Mazingira mabovu ya Shule ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa Madirisha ya Vioo.

Soma: https://jamii.app/KanyeUnyanyasaji

#JamiiForums #HumanRights #Violence
πŸ‘7😁2
Mdau wa JamiiForums.com anasema Uhakiki wa madai ya zaidi ya Wastaafu 180 wa TAZARA wanaodai Stahiki zao ulishafanyika ambapo walionana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikathibitishwa kuwa wanapaswa kulipwa lakini hilo halijatekelezeka

Ameongeza suala hilo lilifika hadi Mahakamani na Wastaafu hao wakashinda shauri, baada ya hapo walionana na Waziri Mkuu kuwasilisha malalamiko yao, akawasikiliza na kuwakabidhi kwa Maafisa wake washughulikie lakini tangu wakati huo 'danadana' zimekuwa nyingi

Zaidi soma https://jamii.app/TAZARAWastaafu

#JamiiForums #Accountability #Governance #Uwajibikaji
πŸ‘7❀1
Kujitibu mwenyewe (#SelfTreatment) kunaweza kuwa na hatari nyingi. Mtu kujifanyia tathmini ya Kiafya (#SelfDiagnosis) bila mafunzo ya Kitaalamu inaweza kusababisha kutambua vibaya hali inayomsumbua

Hii inaweza kusababisha Matumizi mabaya ya Dawa au Tiba ambazo zinaweza kusababisha Usugu wa Dawa na kuzorotesha Afya

Mjadala zaidi https://jamii.app/KujitibuMwenyewe

#JamiiForums #PublicHealth #AfyaBora2024 #JFAfya
πŸ‘7❀3πŸ₯°1πŸ‘1
SIASA: Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemchagua Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo

Amechukua nafasi ya Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Soma https://jamii.app/UteuziAprili3

#JamiiForums #Governance #JFSiasa #Siasa
πŸ‘32❀7πŸ”₯4πŸ‘2😁2🀣1
ALLY HAPI ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi imemchagua Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania

Hapi ana chukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga

Aidha, Hapi amewahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Tabora, Mara na Iringa

Soma https://jamii.app/UteuziAprili3

#JamiiForums #Governance #JFSiasa #Siasa
πŸ‘8❀1
John Mongella amechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Mongella alitenguliwa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Machi 31, 2024, nafasi ambayo aliitumikia tangu Mei 19, 2021 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo

Mabadiliko hayo yamefanywa na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (#CCM) iliyokutana Jijini Dar es Salaam katika Kikao chake maalum chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 3, 2024

Soma https://jamii.app/UteuziAprili3

#JamiiForums #Governance #JFSiasa #Siasa
❀1πŸ‘1
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo Jokate Urban Mwegelo amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM

Jokate amechukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro

Kabla ya nafasi hiyo Jokate alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nafasi ambayo aliteuliwa Oktoba 1, 2023 ikiwa na maana amedumu kwa muda wa Miezi 6 katika nafasi hiyo

Soma https://jamii.app/UteuziAprili3

#Governance #JamiiForums #JFSiasa #Siasa
πŸ‘5❀1πŸ‘Ž1
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Eva Kiaki Nkya kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

Kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Soma https://jamii.app/UteuziMahakama

#JamiiForums #Governance
πŸ‘1πŸ‘Ž1
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Chiganga Mashauri Tengwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita

Soma https://jamii.app/UteuziMahakama

#JamiiForums #Governance
πŸ‘1πŸ‘Ž1
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sylvester Joseph Kainda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Kabla ya uteuzi huu Kainda alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani

Soma https://jamii.app/UteuziMahakama

#JamiiForums #Governance
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2024/25 Bungeni, leo Aprili 3, 2024, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema baada ya mafanikio ya Filamu ya Royal Tour, Serikali inatarajia kutoa Filamu ya #AmazingTanzania mnamo Mei 14, 2024 ikiwashirikisha Rais #SamiaSuluhuHassan na Rais wa #Zanzibar, #HusseinAliMwinyi pamoja na mwigizaji wa China, Jin Dong

Soma https://jamii.app/AmazingTanzania

#Governance #Dilomacy #JamiiForums
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema Seti ya kwanza ya treni ya kisasa ya Electric Multiple Unit (EMU), vichwa vitano vya umeme na mabehewa matatu ya Abiria vimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam

TRC imesema seti moja ina uwezo wa kubeba Abiria 589 na kutembea kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa na hadi sasa imepokea Mabehewa 65 ya Abiria, Vichwa 9 vya Umeme na Seti moja ya EMU huku seti nyingine zikiendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024

Taarifa imeeleza Maendeleo ya Mradi wa #SGR yamefikia 98.90% kwa Dar - Morogoro (KM 300), Morogoro – Makutupora (96.51%), Makutupora – Tabora (13.98%), Tabora – Isaka (5.44%) na Mwanza – Isaka (54.01%)

Soma https://jamii.app/TreniYaKisasa

#JFHuduma #ServiceDelivery #JamiiForums
πŸ‘5