JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFDATA: Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Takwimu za Ajali za Barabarani kwa kipindi cha miaka 5 (2018-2022) zinaonesha kulikuwa na matukio 12,429 ya ajali ambapo kwa mwaka 2022 pekee ajali ziliua Watu 1,545

Wakati makosa ya Barabarani yakiongezeka kwa 46% mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021, ajali za barabarani zilipungua kwa 7% ikiwa ni idadi ndogo zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 2018

Aidha, katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo wa mwaka 2023 kumekuwa na ajali chache kwa 17%, Vifo 0.4% na Majeruhi 1% ikilinganishwa na miezi kama hiyo mwaka 2022

Soma https://jamii.app/AjaliStats

#JamiiForums #RoadSafety
🤔5👍3
Timu mbalimbali za Uokoaji zinaendelea kufanya kazi ya kuokoa na kutoa miili ya waathirika ambayo imesombwa na maji katika mafuriko hayo hasa katika Mji wa #Derna

Mabwawa mawili na madaraja manne yameporomoka na kuzamisha sehemu kubwa ya Mji baada ya eneo hilo kukumbwa na Dhoruba siku ya Jumapili

Soma https://jamii.app/LibyaFloods

#ClimateChange #LibyaFloods #DernaFloods #JamiiForums #StormDaniel
😢21👍1🤔1
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na idadi kubwa ya miili inayopatikana ambapo hadi sasa zaidi ya Watu 2,300 wamepoteza maisha na wengine 10,000 hawajulikani walipo

Mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa katika Mji wa #Derna ambao una Wakazi zaidi ya 89,000, ikielezwa kuwa 20% ya Mji imeharibiwa na mafuriko hayo

Soma https://jamii.app/LibyaFloods

#ClimateChange #LibyaFloods #DernaFloods #JamiiForums
😢6😱21👍1🤔1🤯1
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Mwisho ya Mkutano Maalum wa wa Siku 3 wa Vyama vya Siasa na Wadau ambapo wamejadili Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi, Hali ya Demokrasia na Siasa kwa ujumla Nchini

Katika Siku hii Wajumbe watajadili umuhimu wa Maridhiano, Ustahilimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya wa Taifa katika Shughuli za Kisiasa Nchini

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #JFDemocracy #Governance
👍1
Mdau wa JamiiForums.com anadai changamoto ya Watumishi kuomba kuhama kituo kimoja kwenda kingine ni kubwa, imekuwa ngumu kufanikiwa hata kama mhusika ana sababu za msingi za kufanya hivyo, hali ambayo inalazimika kutumia njia zisizo halali ili kufanikisha lengo

Anasema kuwa kuna Maafisa kadhaa wasiowaaminifu wa #TAMISEMI wanaotumia nafasi zao kuwashawishi wenye maombi ya kuhama kutoa ‘kitu kidogo’ ili maombi yao yashughulikiwe haraka

Anaomba Serikali iingilie kukomesha Watu wachache wanaharibu taswira ya Mamlaka

Soma https://jamii.app/TAMISEMIUhamisho

#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #KemeaRushwa #JamiiForums
👍51👏1
Mchakato wa kuwapata Washiriki waliofanya vizuri katika Shindano la #StoriesOfChange2023 unaelekea pazuri baada ya kukamilika kwa Uwasilishaji wa Makala za Washiriki

Washiriki wanashauriwa kukaa karibu na ‘Private Message’ (PM) kupitia akaunti zao za JamiiForums.com ili kutopitwa na ujumbe kutoka JamiiForums kwa wale wanaoelekea kuwa Washindi

#SoC2023 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #JamiiForums
👍62
Akizungumza katika Siku ya Mwisho ya Mkutano Maalum wa Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya #KikosiKazi, Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Deus Kibamba amesema "Napendekeza kuwa, hatua ya kwanza ni kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria wa Mabadiliko ya Katiba. Katika Muswada huo, yatakuwemo mambo mengi lakini mawili tu yasikosekane"

Akitaja mambo hayo amesema "La kwanza, ni Vifungu vinavyosema tukigombana kama Watanzania, kuanzia sasa mpaka tunakamilisha na kupata #KatibaMpya tutafanyaje. La pili, ni Hadidu za Rejea za Vyombo vyote vitakavyoundwa katika kukamilisha mchakato huu wa Katiba"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #JFDemocracy #DemocracyWeek2023 #WikiYaDemokrasia2023 #Democracy #Governance
👍21👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Sheikh Mussa Yusuph Kundecha wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania anasema Taifa kuwa na nyaraka bora haimaanishi matokeo yatakuwa bora pia

Amesema “Inawezekana utashi wa Kisiasa ukasababisha kikwazo katika kutafsiri nyaraka, kuna Profesa alisema Kenya ina nyaraka bora na za kusifiwa lakini tunaona kilichotokea baada ya Uchaguzi. Tujikumbushe pia dhambi ya Kisiasa ni mbaya kuliko kuiba pesa mfukoni mwa mtu.”

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍7
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mwenyekiti wa Chama cha #UDP, John Cheyo ameshauri Kamati ya Uongozi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya #KikosiKazi kuteua Kamati Ndogo ikamuone Rais Samia Suluhu ili kupunguza muda wa Miaka Mitatu ya Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Katiba

Amesema "Watanzania tusiwa-underrate; Watanzania wamefundishwa. Mzee Warioba ametembea nchi nzima. Amefundisha. Jaji Kisanga ametembea nchi nzima. Amefundisha. Kikosi Kazi na chenyewe kimetuita, tumeandika. Tunaelewa tunachozungumza. Bunge la Katiba limekaa karibu Miezi 6 live, tunaeleweshana. Tukubaliane, Kamati Ndogo iende ikazungumze na Rais tupunguze hiyo miaka mitatu ya kupata 'degree' ya Katiba, ili tuanze yale yanayowezekana yafanyike mara moja"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #DemocracyWeek2023 #Democracy #WikiYaDemokrasia2023 #Governance
👍8😁1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baruani Mshale wa Taasisi ya #Twaweza anasema “Ustahimilivu ni muhimu kwa muktadha uliopo na huko tunakoelekea, kuna Mapinduzi katika Nchi kadhaa hivi karibuni na Wananchi wanashangilia, inaonesha hawana imani na kinachoitwa #Demokrasia.”

Ameongeza “Mabadiliko hayo yanatufanya tuzingatie ustahimilivu, kuna mabadiliko ya kijamii, uchumi, mazingira n.k. Siasa ina jukumu muhimu la kutengeneza mustakakabari wa baadaye, lakini je siasa zetu zinazingatia ustahimilivu."

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍7
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baruani Mshale wa Taasisi ya #Twaweza anasema “Ni muhimu kujiuliza umuhimu wa mageuzi ni kwa maslahi ya nani? Lazima tuangalie raia wa kawaida anataka nini na yanagusa maisha yetu ya kila siku?”

Anaongeza “Mwananchi akisikia Wanasiasa wanazungumzia mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi anaona wanajitengenezea fursa za kuingia madarakani na kubaki kuwa na uhalali bila kujali maisha ya Mwananchi wa kawaida.”

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman amesema Rais Samia Suluhu Hassan amezielekeza Taasisi za Serikali zilizotajwa katika mapendekezo ya Kikosi Kazi kufanya mazingatio ya utekelezaji wa maoni yaliyopendekezwa

Amesema “Kupitia maoni hayo ya Kikosi Kazi hatua zimechukuliwa, Mikutano ya Hadhara na ya ndani imeendelea kufanyika. Serikali inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo yote, yale yanayohusiana na utekelezaji wa masuala ya Sheria tunaendelea kuyafanyia mazingatio ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa ufanisi zaidi"

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Pili wa Rais wa #Zanzibar, Hemed Suleiman amewasihi Wanasiasa kutumia nafasi zao kuendeleza Amani iliyopo Nchini kwa kufuata Kanuni na Taratibu za Nchi hasa wakati wa kuendesha Mikutano ya Hadhara

Amesema “Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa na baadhi yetu sio nzuri na zinaweza kusababisha mpasuko wa umoja katika Taifa letu. Tusipokuwa makini jambo hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa Amani.”

Soma https://jamii.app/MkutanoSikuYa3

#JamiiForums #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023 #Democracy #Governance
👍21
SARATANI ZINAZOWASHAMBULIA WATOTO

1. Saratani ya Damu (#Leukemia): Mtoto huishiwa Damu mara kwa mara au inawezekana akawa akitokwa na Damu ovyo kupitia sehemu za wazi za Mwili

2. Saratani ya Macho (#Retinoblastoma): Ni Saratani inayoathiri takriban Watoto 8000 Duniani kila Mwaka. Jicho la Mtoto hupatwa na Uvimbe mdogo, kuwasha na Uvimbe huongezeka mpaka Mtoto kushindwa kuona vizuri

3. Saratani ya Ubongo: Ni saratani ya pili inayosumbua Watoto baada ya Leukemia. Mtoto hupata Uvimbe kwenye Ubongo ambao huathiri mwenendo wake wa Ukuaji

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
WAKILI MKUU WA SERIKALI: UVUNJAJI HOLELA WA MIKATABA CHANZO CHA MIGOGORO YA MADAI

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende ametaja changamoto za ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuwa ni kutofuatwa kwa Sheria za Mikataba hadi hufikia hatua ya kuisababishia Serikali hasara kwa kutozwa fidia

Amesema baadhi ya Taasisi za Umma zimekuwa zikivunja Mikataba au Kuingia Makubaliano na Kampuni Binafsi bila kuihusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, zimesababisha Migogoro ya Kibiashara

Ikumbukwe, baadhi ya Migogoro imewahi kuigharimu Serikali na pia kuna kusababisha kukamatwa kwa Ndege za ATCL na Mashauri mengine ambayo Serikali ilitakiwa kulipa Fidia kutokana na Uvunjaji Holela wa Mikataba

Soma https://jamii.app/Migogoro

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji23
👍2