JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema punguzo la asilimia 60 ya Ufadhili kwa Mwaka 2023 ndio kubwa zaidi katika Historia ya Miaka 60 ya Shirika hilo

WFP imesema imelazimika kupunguza mgao kwa karibu nusu katika Mataifa ya Afghanistan, Syria, Somalia na Haiti na kutahadharisha kuwa Watu milioni 24 huenda wakakumbwa na baa la njaa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/WFPPunguzoUfadhili

#JamiiForums #FoodCrisis #HumanRights
πŸ‘5
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuzungumza kuhusu Umuhimu wa Kulinda Uhuru wa Watu wakati wa Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo

#JamiiForums #JFDemokrasia #JFNukuu #SocialJustice #UhuruWaKujieleza #FreeSpeech
πŸ‘8
MWANZA: Kesi ya Uhujumu Uchumi inayowakabili Watumishi wa TANESCO, Abdukadri Lwassa (Fundi) na Respicius Rwegoshora (Afisa Bohari) inatarajiwa kutajwa tena leo Septemba 14, 2023 baada ya kushindwa kuendelea Sept. 13, 2023 kutokana na upelelezi kutokamilika

Watumishi hao wanakabiliwa na mashtaka 125 yakiwemo ya Kughushi Nyaraka, Ubadhirifu wa Mali ya Umma na Kutoa Nyaraka za Uongo ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Novemba 16, 2021 na Disemba 17, 2022 katika Ofisi za TANESCO, Nyakato

Soma https://jamii.app/MwanzaTANESCO

#JamiiForums #Governance #SerikaliBilaRushwa #JFUwajibikaji23 #JFHuduma
πŸ‘4πŸ‘1
LIBYA: Baada ya Mafuriko hayo yaliyoathiri zaidi Mji wa #Derna, Serikali imeeleza kuna miili ambayo imekuwa ikipatikana kandokando ya bahari

Wakati idadi ya Watu waliofariki inatajwa kuwa ni zaidi ya 6,000. Waokoaji wameendelea kufukua vifusi vya tope na majengo yaliyodondoka ambapo Watu zaidi ya 10,000 hawajulikani walipo huku wengine zaidi ya 30,000 wakiwa hawana makazi

Soma https://jamii.app/LibyaFloods

#ClimateChange #LibyaFloods #DernaFloods #JamiiForums
πŸ‘1πŸ€”1
Mdau wa JamiiForums.com anadai kwenye Barabara Kuu ya Tanga Mjini na Muheza michoro iliyopo kwenye Lami ikiwemo mstari wa katikati unaogawa Barabara inafutika na kupoteza ubora wa muonekano kwa haraka

Anasema kuwa inawezekana changamoto hiyo inatokana na Wajenzi kutumia Rangi zisizo na ubora unaofaa na kusababisha michoro kupotea ndani ya siku chache tangu ilipochorwa

Mdau anashauri TANROADS kuwajibika kukagua ubora wa vitendea kazi na vifaa vinavyotumika zikiwemo rangi ili kuhakikisha Barabara zinakuwa imara na zilingane na thamani ya Fedha kwa sababu hali hii inaweza kusababisha ajali za barabarani

Soma https://jamii.app/MdauTanga

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #JFUwajibikaji23
πŸ‘3
Asante kwa kushiriki Shindano la Uandishi wenye kuleta Tija. Oktoba 7, 2023 ndio siku ya kukabidhi zawadi kwa wale watakaoibuka kuwa Washindi

Wale wote wanaoelekea kuwa Washindi wanatafutwa kupitia Private Message (PM) katika akaunti zao ndani ya JamiiForums.com, hivyo kama ulishiriki tafadhali pitia jumbe zako mara kwa mara

#JamiiForums #SoC2023 #StoriesOfChange2023
❀4πŸ‘2
ZIMBABWE: Rais Emmerson Mnangagwa ameshutumiwa kuendesha Serikali kama Mali ya Familia, ikiwa ni siku chache tangu afanye uteuzi wa Baraza la Mawaziri akiwemo Mtoto wake wa Kiume atakayekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mpwa wake kuwa Naibu Waziri wa Utalii

Chama Kikuu cha Upinzani kilichoshika nafasi ya Pili katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2023 kimesema Rais ameingiza Marafiki, Familia, Wapambe wake na Watu wasio na sifa, kitu kinachofanya Baraza kuwa la ovyo tangu kupatikana kwa Uhuru mwaka 1980

Rais Mnangagwa amechaguliwa kuongoza Nchi hiyo kwa Muhula wa Pili wa Miaka 5 baada ya kutangazwa Mshindi katika Uchaguzi uliolalamikiwa kutokuwa Huru, Wazi na wa Haki.

Soma https://jamii.app/WateuleZMBW

#JamiiForums #Governance #Democracy #Accountability #AfricanPolitcs
😁4πŸ‘2
Mdau anadai Barabara ya Kahama (Shinyanga) hadi Kaliua Mjini (Tabora) kupita Ulyankulu, Mwamnange na Kashishi inatumiwa na watu wengi ikiwemo Wakulima na Wafanyabiashara, ina mashimo mengi, haina lami na wakati wa mvua hali inakuwa mbaya zaidi

Mdau anaomba Serikali iweke lami kwa kuwa mbali na magari kukwama pia kuna ajali ambazo zimetokana na ubovu wa Barabara hiyo

Soma https://jamii.app/KauliaKahama

#JFHuduma #Governance #JFUwajibikaji23 #JamiiForums
❀1
#ELIMU: Takriban Watahiniwa 49,948 kati ya 102,948 waliotarajiwa kufanya Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi Mkoani Kigoma, hawajafanya Mtihani huo unaotarajiwa kumalizika Nchini kote leo Septemba 14, 2023

Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa, Paulina Ndigeza ni kuwa Wanafunzi wengi hawakuweza kufanya Mtihani huo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoro na mwamko mdogo wa Wazazi katika kuwasimamia Watoto wao

Aidha, kwa mujibu wa #RipotiYaCAG ya Mwaka 2021/22, Shule za Msingi Nchini ziliripotiwa kuwa na upungufu wa Madawati 158,066, Vyoo vya Wanafunzi 56,530, Nyumba za Walimu 35,684, Viti na Meza 29,829, Madarasa, 27,316, Ofisi za Walimu 2,266 na Vyoo vya Walimu 622

Soma https://jamii.app/STD7KGM

#JamiiForums #Governance #JFHakiElimu #SocialJustice
❀2πŸ‘2πŸ€”1
RUVUMA: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (#MCT), Kajubi Mukajanga akiwa Songea amesema Vyombo vya Habari vinaendelea kupokea vitisho vya Kiutawala, changamoto za Kiuchumi, Kibiashara na nyinginezo, hivyo kukwamisha Utendaji wao

Pia, Wakili Fulgence Massawe akiwasilisha hoja kuhusu Sheria za kusimamia #UhuruWaKujieleza amesema matukio ya Watu kukamatwa, kukamata Mali, faini, kuharibiwa Vifaa, kuchunguzwa au kufuatiliwa Mawasiliano binafsi yanachangia kuminya #UhuruWaHabari

Mambo mengine ni kubambikiwa mashtaka, hofu ya kushtakiwa, kudhibitiwa kwa Maudhui katika Vyombo vya Habari au Mitandaoni

Soma https://jamii.app/UhuruWaHabari

#JamiiForums #PressFreedom #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘4πŸ€”3
Kupungua kwa ushindani kati ya Vyama vya Siasa na mgawanyiko wa Kisiasa ni jambo baya kwa Demokrasia

Bunge hupata urahisi katika kufanya Maamuzi ya pamoja ikiwa Mawazo ya Wanachama wote wa Kisisasa yataheshimiwa. Ikiwa Mawazo yanatofautiana, wanaweza bado kusimamia tofauti zao kwa kujadiliana, kufikia makubaliano na mara nyingine kwa kupiga kura

Soma https://jamii.app/DemocracyChallenges

#JamiiForums #Democracy #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘4
UGANDA: Jeshi la Polisi limepiga marufuku Mikutano ya Hadhara ya Chama Kikuu cha Upinzani, National Unity (NUP) kwa maelezo kuwa kilikiuka miongozo iliyokubaliwa na Kiongozi wake Robert Kyagulanyi (#BobiWine) ambaye amekuwa akizunguka katika Miji mbalimbali tangu Agosti 28, 2023

Taarifa ya Polisi imesema Mikutano hiyo imekuwa ikihamasisha Vurugu, Udini na kutoa uchochezi wa kuondolewa kwa Serikali iliyopo Madarakani pamoja na kashfa dhidi ya Rais #YoweriMuseveni

Hata hivyo Chama cha #NUP kimesema kitatoa ratiba mpya ya Awamu ya Pili ya Mikutano na Ziara zake na hawatositisha Mikutano kwasababu walijua mapema Serikali itachukua uamuzi huo.

Soma https://jamii.app/RalyUganda

#JamiiForums #Governance #Democracy #SocialJustice #PoliceBrutality #AfricanPolitics
πŸ‘7πŸ€”2πŸ₯°1
WASHINDI WA STORIES OF CHANGE KUTANGAZWA OKTOBA 7, 2023

Kamati imeanza kuwasiliana na Wanaoelekea kuwa Washindi kupitia Private Message (PM) katika akaunti zao ndani ya JamiiForums.com.

Kama ulishiriki shindano la #StoriesOfChange tafadhali hakikisha unasoma Jumbe zako mara kwa mara ili upate maelekezo

#JamiiForums #SoC2023 #StoriesOfChange2023
πŸ‘3
Jeshi la Polisi Mkoa wa #Iringa linamshikilia Aurelia Kalolo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 kwa tuhuma za kumpiga kichwani kwa kutumia rungu mumewe, Williad Ngamema ambaye ni Balozi wa Kitongoji cha Iwengi, Kijiji na Kata ya Ukumbi na kumsababishia kifo

Chanzo kimetajwa ni wawili hao kuwa na ugomvi wa mara kwa mara, ikielezwa kuwa siku ya tukio Aurelia alimshambulia mumewe wakati wakiwa katika majibizano

Soma https://jamii.app/TuhumaMauajiIringa

#MentalHealthAwareness #JFAfyaAkili #JFMatukio #JamiiForums
πŸ”₯3πŸ‘1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesisitiza kuwa Serikali imebaini baadhi ya Watumishi wa Umma wanatumia njia za udanganyifu na nyaraka za kughushi mtandaoni kufanikisha uhamisho wa Vituo vya Kazi

Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoani #Geita, amesema "Watu hao hutumia saini za Makatibu Wakuu Wawili, Katibu Mkuu Utumishi na Katibu Mkuu TAMISEMI lakini uhamisho huo ni feki, kinachokuja kusumbua ni pale wanapotaka kuhamisha mshahara"

Awali, Wadau wa JamiiForums.com walitoa wito kwa Serikali wa kuchukua hatua dhidi ya Watumishi wachache wa TAMISEMI wanaotengeneza mazingira ya rushwa ili kufanikisha Uhamisho wa Watumishi

Soma https://jamii.app/UhamishoUtumishi

#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #KemeaRushwa #JamiiForums
πŸ‘5
Utulivu wa Serikali nyingi umekuwa ukivurugika kutokana na Serikali hizo kushindwa kutoa Usalama wa Kiuchumi kwa Raia wao

Kutokana na Serikali nyingi kushindwa kutimiza mahitaji ya Raia wao, kutoaminika na kupuuzwa kwa thamani ya Demokrasia miongoni mwa Raia kumeongezeka. Kutoaminika huku kunajionesha katika kupungua kwa idadi ya Wapiga Kura, maoni ya Umma, Maandamano na hata Mapinduzi kwa baadhi ya Nchi

Soma https://jamii.app/DemocracyChallenges

#JamiiForums #Democracy #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘6❀1
SANCHO AZUIWA KUFANYA MAZOEZI NA KIKOSI CHA KWANZA CHA MAN. UNITED

Imebainika kuwa #JadonSancho amepewa zuio hilo hadi atakapomuomba radhi Kocha wake wa #ManchesterUnited, Erik ten Hag, hatua ambayo hajaitekeleza

Kinachoendelea ni kuwa Uongozi umemtaka Sancho afanye mazoezi na Wachezaji wa Kikosi cha Vijana cha timu hiyo kwenye Viwanja vyao vya Mazoezi vya #Carrington

Soma https://jamii.app/SanchoBan

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘5😁2❀1
JE, ULISHIRIKI SHINDANO LA STORIES OF CHANGE? PITIA β€˜PM’ YAKO

Tunaelekea Oktoba 7, 2023 ambayo ndio Siku ya kukabidhi zawadi kwa walioibuka kuwa Washindi wa Shindano la #StoriesOfChange

Kama ulishiriki Shindano hili usikae mbali na Private Message (PM) kwa kuwa wanaoelekea kuwa Washindi wanatafutwa kipitia PM

#JamiiForums #SOC2023
πŸ‘1
Siku ya Kimataifa ya Demokrasia huadhimishwa Septemba 15 kila mwaka kwa lengo la kuangazia hali ya Demokrasia duniani kote, Kuhimiza harakati za Kidemokrasia na Kukuza Uhuru, Amani na Haki za Binadamu

Siku hii ilianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2007 na kila mwaka tukio hili hujikita katika kuhamasisha masuala tofauti yanayogusa Demokrasia ikiwemo Uchaguzi wa Serikali zinazoongoza Nchi

Kwa misingi ya Demokrasia ya kweli, Wananchi wanakuwa na Haki na Wajibu mkubwa katika Serikali yao kwa Kuwachagua Viongozi wanaowataka na Kuwawajibisha

Soma https://jamii.app/IDD2023

#JamiiForums #JFDemocracyDay #JFDemokrasia #IDD2023 #DemocracyDay2023 #Governance
πŸ‘2
Mliosoma Somo la Uraia, mnakumbuka β€˜Definition’ ya Demokrasia?

Wakati Dunia ikiitambua Septemba 15, kuwa Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, ikiwa na lengo la kuangazia Hali ya Demokrasia Duniani, kuhimiza harakati za Kidemokrasia na Kukuza Uhuru, Amani na Haki za Binadamu, unakumbuka nini ulipokuwa unasoma kuhusu neno Demokrasia?

Soma https://jamii.app/DemokrasiaShule

#JamiiForums #JFDemocracyDay #JFDemokrasia #IDD2023 #DemocracyDay2023 #Governance
πŸ‘1🀯1