JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mwembe huo ulipandwa kwa pamoja na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume na ukapewa jina la "Mwembe wa Muungano"

Udongo uliochanganywa pamoja na vifaa vilivyotumika wakati wa tukio la Muungano ulihifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa. Udongo kutoka Zanzibar ulitolewa Kizimbani, Unguja huku ule wa Tanganyika ukitolewa Jijini Dar es Salaam

Hadi sasa, Mwembe huo bado upo katika Viwanja vya Ikulu.​

Fahamu zaidi https://jamii.app/MwembeIkulu

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFKumbukizi
MWANZA: Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mkazi wa Kitongoji cha Nyaruhama, Kijiji cha Nyangomango, Kata ya Usagara Wilayani Misungwi anadai kuna changamoto ya uharibifu wa mazingira eneo hilo unaochangiwa na utaratibu mbovu wa uchimbaji moramu

Anadai mashimo hayo wakati wa mvua yanajaa maji, pia kuna utamaduni wa kulipua mawe kwa baruti maeneo haya bila kufuata utaratibu hali ambayo ni hatari pia kwa Wananchi

Anatoa wito kwa Mamlaka za ngazi za juu kufuatilia changamoto hiyo ambayo anadai inaendana na mazingira ya uwepo wa Rushwa

Soma https://jamii.app/UsagaraArdhi

#JamiiForums #ClimateChange #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
πŸ‘1
Mtanzania Juma Ally Maganga (45) aliyeshikiliwa Nchini Sudan Kusini akituhumiwa kugonga mtu na kusababisha kifo chake Februari 2025 amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani ambacho pia kinaweza kuongezeka kama hataweza kulipa faini ndani ya siku 14 tokea siku ilipotolewa hukumu ambayo ni Aprili 23, 2025

Awali, mke wa Maganga, Rehema Mongi (38) alisema aliyegongwa alikuwa akiendesha Pikipiki, alifariki papo hapo na kwamba Familia ya marehemu ilihitaji ilipwe faini ya Tsh. Milioni 72 ili ikubali mtuhumiwa aachiwe

Februari 2025, JamiiForums iliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ilisema inafuatilia kuhusu Mtanzania huyo kupitia Idara ya Afrika kwa karibu na Ubalozi uliopo Kampala kwa kuwa hakuna uwakilishi upande wa Sudani Kusini

Soma https://jamii.app/AllyMgangaUpdates

#JamiiForums
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai ni zaidi ya miezi sita tangu ujenzi huo uanze lakini hawaoni jitihada za kuharakisha kipande hicho kukamilika ili kuwezesha shughuli nyingine kuendelea

Anatoa wito kwa mamlaka kufuatilia kwa ukaribu changamoto zinazojitokeza ili ujenzi ukamilike kwa kuwa imekuwa ni kero kubwa inayosababisha shughuli nyingi za kiuchumi kukwama

Soma https://jamii.app/MwendokasiKarume

#JamiiForums #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi akizungumzia historia ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere amesema aliona mbali juu ya uwezo wa Wanawake katika masuala ya Utawala na aliamini ipo siku Tanzania itakuwa na Rais Mwanamke

Amesema hayo katika uzinduzi wa Kitabu cha β€œMwalimu Julius Kambarage Nyerere: Photographic Journey” Ikulu Chamwino, leo Aprili 26, 2025

Soma https://jamii.app/NyerereKitabuUzinduzi

#JamiiForums #Democracy #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
PEMBA: Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema ipo haja ya kufanyika kwa mabadiliko makubwa ya mfumo wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Nchi zote mbili za washirika zipate haki sawa

Amesema hayo leo Aprili 26, 2025 katika Ukumbi wa Samael Chakechake katika Kongamano Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ameongeza kuwa "Tulianza kulalamikia mambo 11 ya Muungano hapo awali lakini sasa  tunalalamikia mambo 41 bila wenzetu kujali lolote huku mambo yote hayo yakinufaisha upande wa pili wa Tanzania Bara."

Soma https://jamii.app/ACTKuhusuMuungano

#JFMatukio #JamiiForums
Safari yako ya Maisha ni ya kipekee, wengine hawapaswi kuielewa au kuikubali

Cha muhimu ni kuendelea mbele kwa kuzingatia malengo yako

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha
πŸ‘Ž1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kijitonyama, Rev. Eliona Kimaro, anasema "Hapatakuwa na Amani kama hakuna Haki, ukiona Amani ipo mahali ujue ni kazi kubwa ya Haki iliyotangulia, Haki inatengeneza Amani."

Soma https://jamii.app/KimaroShidaYaHaki

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Democracy #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #JFKumbukizi
πŸ‘3πŸ‘1
Eti Mdau, Mtu akikukumbuka na Tsh. 100,000 ya ghafla ghafla Siku yako itakuwa safi eeh?

Mjadala https://jamii.app/WeekendVibes

#JamiiAfrica #LifeStyle #Maisha #JamiiForums
SONGWE: Mdau wa JamiiForums.com anasema Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imefanikiwa kujenga Stendi mpya ya Mabasi eneo la Forest Mlowo, lakini imeanza kutumika huku Miundombinu mingi ikiwa hairidhishi

Anahoji, kulikuwa na ulazima gani wa kuharakisha Magari kuanza kupita kabla ya maboresho kukamilika? Akisisitiza Miundombinu Bora ni muhimu kwa Watumiaji wa Stendi hiyo

https://jamii.app/StendiMlowoMbovu

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #JFMdau2025 #HudumaZaKijamii
❀1
DURBAN: Kama ilivyofanya Mwaka 1993, Simba imefanikiwa kuandika historia ya kufika Fainali ya Michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (#CAF), ni baada ya kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (Confederation Cup) kwa kuitoa Stellenbosch FC ya Afrika Kusini

Hiyo ni baada ya Nusu Fainali ya Pili kumalizika kwa 0-0 kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, hivyo #Simba kusonga mbele kwa faida ya Goli 1-0 ililopata katika mchezo wa kwanza

Simba itacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya CS Constantine (Algeria) dhidi ya RS Berkane (Morocco), ambapo Fainali ya kwanza itachezwa Mei 17, 2025 na marudio ni Mei 25, 2025

Michuano hiyo ilianzishwa Mwaka 2004 baada ya CAF kuunganisha Mashindano ya African Cup Winners' Cup yaliyoanzishwa Mwaka 1975 pamoja na CAF Cup yaliyoanzishwa Mwaka 1992

Soma https://jamii.app/SimbaFainal

#JFSports #CAFCC #JamiiForums
πŸ‘2
Mdau waJamiiForums.com anasema kama Ada ya Mtoto wako ya Mwaka mzima ni kubwa kuliko kipato chako cha mwezi, basi hapo Unajifilisi na kiwango chako cha Maisha kitakuwa duni sana

Anasema ukifuata kanuni hii basi utajikuta Kipato chako cha Miezi 10 iliyobaki kinagharamia mahitaji mengine muhimu na utaishi bila madeni wala Msongo wa Mawazo

Umezielewa hesabu za Mdau au unaona haziwezekani?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KipatoAdaKodi

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons #JamiiAfrica
Picha zikionesha matukio tofauti ya Washiriki mbalimbali wa mbio (Fun Run) za Kilometa Tano zilizofanyika leo Aprili 27, 2025 ikiwa ni Siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo yanafanyika kwa siku tatu Jijini Arusha

Mbio hizo zilizoshirikisha Wadau mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho hayo zilianzia Uwanja wa Gymkhana/Mgambo na kuhitimishwa katika eneo hilo hilo

Soma https://jamii.app/WPFD2025Day1

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
πŸ‘1