JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HISTORIA: Baada ya Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961, Tabora Hotel iliwekwa chini ya usimamizi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na ikajulikana kama 'Tabora Railway Hotel'

Ilitumika kama mahali pa kupokea Wageni na kuwa Jukwaa la Mikutano ya Viongozi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wasomi katika Miaka ya 1970 na 1980

Mwaka 2003, Hoteli hiyo ilifanyiwa ukarabati na kubadilishwa jina tena na kuwa "Orion Tabora Hotel." Maboresho haya yalihusisha kuongeza majengo Mawili mapya yaliyopewa majina ya Mirambo Wing na Nyamwezi Wing

Fahamu Historia hii zaidi https://jamii.app/HistoriaTaboraHotel

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKumbukizi
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Chama cha #Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakijapokea taarifa rasmi kuhusu alipo mjumbe wa Baraza Kuu la Chama hicho, Hilda Newton, ambaye alikamatwa jana Aprili 24, 2025 katika eneo la Mahakama ya Kisutu

Akizungumza leo Aprili 25, 2025, Naibu Katibu Mkuu wa #CHADEMA Bara, Amani Golugwa, amesema walitegemea jina la Hilda litatajwa kwenye taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa jana na Kamanda Muliro, lakini halikuwemo.

Soma https://jamii.app/HildaCDMHajapatikana

#HakiZaBinadamu #JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights
DAR: Jana, Aprili 24 Taasisi ya JamiiAfrica ilizinduliwa rasmi ikichukua nafasi ya iliyokuwa “Jamii Forums”

Uzinduzi huo uliambatana na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taasisi wa miaka 6 unaoelekeza dira mpya ya kujipanua kiutendaji (operational expansion) ndani na nje ya Tanzania; na katika kuchechemua kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi, mamlaka zinazojibu na kuwajibika kwa wananchi na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala anuai ya kimaendeleo

JamiiAfrica ambayo pia inasimamia majukwaa ya JamiiForums, JamiiCheck, Stories of Change, Fichua Uovu na JamiiData imenuia kupanua wigo wa kukuza Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora kidijitali na nje ya mtandao kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali

Soma https://jamii.app/UzinduziJamiiAfrica

#JamiiForums #Rebranding #JamiiAfrica
🔥21🫡1
Mdau, kuna ulazima wa mtu kupokea simu akiwa anakula?

Mtu asipopokea simu yako akakwambia alikuwa anakula utamuelewa?

Mjadala https://jamii.app/TableManners

#JamiiAfrica #Maisha #LifeStyle
Akihutubia Taifa, Rais Samia Suluhu amesema Kamwe falsafa ya 4R haiwezi kuwa kisingizio cha kuvunja Sheria au cha kujenga mazingira yanayohatarisha amani, utulivu na usalama wa Nchi

Amesema "Demokrasia yetu imeendelea kukua na kuimarika hususani kupitia falsafa yetu ya 4R, ambayo itaendelea kuwa nyenzo muhimu ya kukuza Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wananchi kwenye masuala muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu"

Ameongeza "Hata hivyo nataka kusisitiza kwamba, kutekelezwa kwa falsafa ya 4R kunaendana sambamba na kuzingatiwa kwa Katiba na Sheria za Nchi"

Soma https://jamii.app/HotubaYaRais

#JamiiAfrica #Democracy #Governance #JamiiForums
1👍1
DODOMA: Rais Samia Suluhu akilihutubia Taifa, leo Aprili 25, 2025 kuelekea Miaka 61 ya Muungano, amesema Serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwenye Mazingira ya Utulivu na Amani, katika kipindi chote cha matayarisho hadi wakati wa Uchaguzi

Amesisitiza "Kamwe tusiruhusu Uchaguzi huu kuwa chanzo cha Migogoro, Chuki na Mivutano na uvunjifu wa Amani ndani ya Chama, baina ya Vyama au Nchini kwa ujumla."

Ameongeza kuwa "Niseme kuwa hakuna aliye juu ya Sheria na wote tunatakiwa kuendesha shughuli zetu za Kisiasa tukizingatia kuwa Amani na Usalama wa Nchi ndio kipaumbele cha kwanza."

Soma https://jamii.app/HotubaYaRais

#UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia
Mdau wa JamiiForums.com anadai utaratibu wa kuingia katika Stendi ya Mabasi ya Kigoma unaofahamika ni kulipia Tsh. 200 kwa Mtu ambaye hana Tiketi ila wahusika wanadai imepanda hadi kuwa Tsh. 300, na ukitoa hela kubwa Mfano Tsh. 500 au 1,000 hupewi chenji. Wahusika Wanajizungusha kwa kuwa wanajua utaondoka na kuiacha, lakini ukikomaa wanakupa “bablish” za kutafuna ili kufidia.

Aidha, mdau amedai kuwa Mgambo wamekuwa na tabia ya kuchelewesha Abiria kuingia ndani ya Stendi hiyo kupanda mabasi, ili kupata Kamisheni ya Bodaboda anapomkimbiza Mtu mzani kuifuata gari

Ametoa wito kwa Serikali kufuatilia na kushughulikia changamoto katika Stendi hiyo

Soma https://jamii.app/ChenjiKigomaBablish

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii #JamiiAfrica #ServiceDelivery