JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
👍1
ARUSHA: Leo Aprili 28, 2025 ni siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani (#WorldPressFreedomDay2025). Maadhimisho haya yanafanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia na yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu

Kwenye Maadhimisho haya Wadau watajadili mada mabalimbali ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua

Maadhimisho ya WPFD 2025 yanaratibiwa na Taasisi ya JamiiAfrica, Serikali, Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Wadau wengine wa Habari ndani na nje ya Tanzania

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, leo Aprili 28, 2025 JamiiAfrica kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa majadiliano maalum yanayolenga kuchambua Uendelevu wa Vyombo vya Habari Tanzania katika nyakati hizi za Kidijitali

Majadiliano haya yanalenga kuimarisha uhuru wa Vyombo vya Habari, kuchochea ubunifu na uendelevu, pamoja na kuhimiza uandishi wa habari unaotanguliza maslahi ya Umma

#JamiiForums #JamiiAfrica #WPFD2025 #PressFreedom #Democracy
Katika zama hizi za Kidigitali, Mitandao ya Kijamii si tu kwaajili ya kushirikishana taarifa, bali ni Majukwaa ya Biashara, Ushawishi na Maendeleo. Hata hivyo, wabunifu wengi wa Maudhui bado hawajafaidika kikamilifu na fursa hizi

Kwa kutambua hili, Katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayoendelea Arusha, JamiiAfrica na Wadau wengine wameandaa mafunzo kwa wabunifu wa Maudhui yatakayohusisha Utengenezaji bora wa Maudhui na ushirikishwaji wa Watu, Mbinu za kupata kipato kupitia Majukwaa ya Kidigitali, Usalama Mtandaoni na matumizi sahihi ya AI

#JamiiAfrica #JamiiForums #WorldPressFreedomDay #PressFreedom #WPFD2025
ARUSHA: Akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema kwenye Dunia ya sasa, Vyombo vya Habari havihusishi tena Magazeti, Redio na Televisheni pekee

Amesema “Kuna ongezeko la Watengeneza Maudhui wa Kidigitali ikijumuisha Wanablogu, Wapigapicha huru, Vloggers, Podcasters na wengine wengi ambao kwa ubunifu wao, wamepanua mipaka ya Uhuru wa Kujieleza.”

Maxence ameongeza “Tunatambua mchango wao mkubwa katika kuweka Jamii zetu hai kwa taarifa, fikra na mazungumzo muhimu. Tunasisitiza kuwa Uhuru wa Habari lazima uwe shirikishi, ukilinda na kuenzi Haki za makundi yote yanayochangia katika mnyororo wa Mawasiliano ya kisasa.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema “Kuelekea Uchaguzi Mkuu, tunatoa wito kwa Mamlaka, Taasisi, Vyama vya Siasa na Jamii kwa ujumla kuheshimu na kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari, kuhakikisha hakuna vitisho, mashinikizo wala vizingiti vinavyowekwa kwa wanaohakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi, za kina na kwa wakati.”

Ameongeza “Leo tunapenda kukumbushana kuwa Uhuru wa Vyombo vya Habari sio Hisani, bali ni Haki ya Msingi inayodaiwa na kulindwa kila Siku na ni jukumu letu sote – Wanahabari, Watengeneza Maudhui, Wanateknolojia, Watunga Sera na Raia.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema “Ripoti ya UNESCO ya Mwaka 2023 kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari inaeleza kuwa Uwezo wa kupima ubora wa taarifa ni ujuzi muhimu kwa kila Mtu katika karne ya ishirini na moja"

Amesema kuwa katika nyakati hizi, kuimarisha Akili Mnemba si tu hitaji la Mtu binafsi, bali ni jukumu la pamoja kwa tasnia ya Habari na Jamii nzima. Pia, Uhuru wa Vyombo vya Habari unapata maana kamili pale unapochanganyika na Uwajibikaji, Uchambuzi wa kina na uelewa sahihi wa taarifa zinazochakatwa

Maxence ameongeza “Hii inaonesha si Vyombo vya Habari pekee vinavyopaswa kuwa na viwango vya juu vya weledi, bali Jamii inapaswa kujifunza jinsi ya kuwa Wasomaji, Watazamaji na Wasikilizaji makini.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema Kaulimbiu ya Mwaka 2025 katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025 ni “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari.”

Ameeleza kuwa Kaulimbiu hiyo inakumbusha katika nyakati hizi za taarifa nyingi na Teknolojia za Kisasa, kunahitajika uwezo wa ziada kuchuja, kuchambua na kuelewa taarifa kwa umakini wa hali ya juu ili kulinda Uhuru wa Habari na kuhakikisha Uwajibikaji wa wanaohabarisha na wanaohabarishwa

Maxence amesema “Katika Mazingira haya mapya, Akili Mnemba (AI) imekuwa nyenzo isiyokwepeka katika Tasnia ya Habari na Uchakataji Taarifa. Wanahabari na jamii kwa ujumla wanahimizwa kuwa na uwezo wa kuchambua chanzo cha taarifa na kutambua upendeleo au propaganda zinazoweza kuathiri maudhui.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, Balozi wa Sweden-Tanzania, Charlotta Ozaki Macias amesema Dunia inabadilishwa na Akili Mnemba (AI) ambayo ina faida nyingi lakini pia ina changamoto zake ikiwemo upotoshaji wa taarifa na kupungua kwa nafasi ya kiraia

Balozi Charlotta amesema AI zinasisimua na zinatisha pia, zinaweza kuwasaidia Wanahabari kwa kurahisisha kazi na kuchakata kiasi kikubwa cha taarifa n.k hiyo inasaidia kutengeneza habari za ubora wa juu na zenye ushahidi wa kutosha

Anaongeza “AI inaweza pia kutumiwa kufanya upotoshaji wa taarifa, Picha, Video na Maandishi bandia, inazidi kuwa vigumu kujua ukweli ni upi. Hili si tatizo la Kiteknolojia tu, ni tatizo la Uaminifu."

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
ARUSHA: Balozi wa Sweden-Tanzania, Charlotta Ozaki Macias anasema “Nchini Sweden, tumejaribu kuelekeza Maendeleo ya Akili Mnemba (AI) kwa njia ya kimaadili. Mkakati wetu wa kitaifa kuhusu AI unalenga mambo matatu kwa kuwa AI inapaswa kufanya kazi kwa ajili ya Watu, si dhidi yao.”

Ameyataja mambo hayo kuwa ni Kulinda faragha na kuhakikisha usalama wa taarifa za Watu, Kufanya AI iwe wazi, ili Watu waelewe jinsi maamuzi yanavyofanyika na Kupambana na upendeleo ili kuhakikisha AI haisaidii kuendeleza Ubaguzi.

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
ARUSHA: Balozi wa Sweden-Tanzania, Charlotta Ozaki Macias anasema “Nimeona ujasiri wa ajabu miongoni mwa Waandishi wa Habari hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, licha ya Rasilimali chache, udhibiti wa Habari na wakati mwingine hata vitisho kwa Maisha yao lakini wanaendelea mbele.”

Ameeleza hivi karibuni alitembelea Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) akaona changamoto wanazokabiliana nazo, akitoa Mfano Mkoani Manyara, Wanahabari Vijana walivamiwa walipokuwa wakiripoti kuhusu Ukatili wa Kijinsia

Ameongeza “Njombe, Waandishi walieleza Hadithi ya Watoto wenye Ulemavu wanaofichwa na walifanya hivyo kwa kuhatarisha usalama wao binafsi. Hadithi hizi zilinigusa sana na zilinikumbusha kwanini kazi hii ina umuhimu mkubwa.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Mwakilishi wa UNESCO Nchini Tanzania, Michel Toto katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ametoa wito kwa wadau wa Tasnia ya Habari kuwekeza zaidi katika kulinda Ukweli, Uhuru wa Maoni na mustakabali wa Uandishi wa Habari Duniani, akisema Uandishi wa Habari ni nguzo ya Demokrasia, Uwajibikaji na Amani

Amesisitiza kusema ukweli sio kosa, huku akieleza kwa Mwaka 2025 pekee, UNESCO imetoa zaidi ya matamko 90 kulaani mauaji ya Waandishi wa Habari Duniani kote, ambapo Waandishi wengi wamepoteza maisha kwa kuleta ukweli mbele ya Jamii

Aidha, ametoa tahadhari kuhusu changamoto mpya zinazochangiwa na kuibuka kwa Teknolojia ya Akili Mnemba (AI), akieleza kuwa pamoja na fursa, AI inaleta hatari kubwa kwa Haki na Uhuru wa Vyombo vya Habari

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Balozi wa Sweden-Tanzania, Charlotta Ozaki Macias amesema “Kwanini Uhuru wa Kujieleza ni muhimu sana? Na kwanini Nchi kama yangu zinasimama imara kuutetea? Kwasababu tunaamini Watu wanapokuwa huru kusema, kushiriki na kutofautiana, Jamii huwa imara zaidi. Hakuna Mtu au Chama cha Siasa kilicho na majibu yote, ndiyo maana tunahitaji nafasi ya mawazo tofauti kushirikishwa, kupingwa na kuboreshwa.”

Ameongeza “Katika Demokrasia ya Vyama vingi, Uhuru wa Kujieleza unahakikisha Watu wanapata taarifa. Unawasaidia Wapigakura kufanya maamuzi sahihi. Unawafanya Viongozi wawajibike na unaipa nguvu Jamii ya Kiraia kushinikiza Mabadiliko."

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, Balozi wa Sweden-Tanzania, Charlotta Ozaki Macias amesema “Tunapoingia kwenye enzi hii ya Kidijitali, Waandishi wa Habari lazima wakabiliane na mashambulizi Mtandaoni, ufuatiliaji wa Kidijitali na taarifa za uongo. Pia, wanapaswa kutafuta njia za kutumia Teknolojia ili kuelimisha na kuhamasisha.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking