JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DEMOKRASIA: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai nyumba ya Mwenyekiti wa Chama hicho - Taifa, Tundu Antipas Lissu imezingirwa na Polisi huku Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia akidai Polisi hao wanataka kufanya upekuzi

Akielezea hali ilivyo, Msaidizi wa Lissu, David Djumbe amesema awali Polisi walifika alfajiri wakiwa na Magari manne na kuanza kugonga geti lakini hawakufunguliwa. Baadaye walikwenda kwa Mjumbe wa shina, ambaye aliwapigia simu Wanafamilia akisema Polisi hao wamekuja hapo kufanya upekuzi, ndipo akaambiwa mwenye nyumba (Lissu) hayupo hawawezi kuwafungulia”

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alipoulizwa sababu ya askari hao kufika mahali hapo, amesema ni ulinzi wa kawaida

Zaidi https://jamii.app/NyumbaKuzingirwa

#JamiiForums #Accountability #Governance
👍1
Mtaalamu wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari wa EAC, Lilian Kiarie akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025 amesema Teknolojia imeimarisha Uandishi wa kiraia huku Watu wa kawaida wakipewa uwezo wa kuripoti matukio kwa wakati halisi, jambo ambalo limepanua Demokrasia ya upatikanaji wa habari

Ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kushikilia misingi ya ukweli, uadilifu na uwazi, pamoja na Serikali na wadau kulinda Uhuru wa Kujieleza na kukuza ubunifu, ili kuhakikisha Uandishi wa habari unabaki kuwa nguzo ya Demokrasia hata katika enzi za Akili Mnemba

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Media Foundation, Dastan Kamanzi akizungumza katika Siku ya Kwanza ya Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ameyataja mambo matatu muhimu wanayohitaji Waandishi wa Habari ili kuboresha kazi zao

Amesema “Waandishi wanahitaji mambo matatu muhimu ili kuboresha kazi zao, kwanza ni Shauku inayohusisha kubadilika na kukua. Pili, ni Utayari unaohusisha Uwekezaji wa maarifa na Uwekezaji wa muda, tatu wanahitaji kudhamiria na kujikita kwenye Majukumu yao”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #AIandMedia #HakikiTaarifa #FactsChecking
1
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, Jumanne Muliro akizungumza na JamiiForums amesema Makada wa CHADEMA waliokamatwa Aprili 24, 2025 ni Makamu Mwenyekiti, John Heche na Katibu Mkuu, John Mnyika na walirudi wakiwa salama

Akielezea sababu ya kuwafukuza Wanachama wa CHADEMA eneo la Mahakama siku hiyo alisema “Sisi tuliweka mazingira mazuri kwa Mahakama kufanya kazi. Kwani hao CHADEMA peke yao ndio wenye kesi? Pale Kisutu kuna Mahakimu wangapi? Kama Mahakimu wapo 20, kesi moja ya Lissu ndio isimamishe kesi nyingine 19? Hao wanyonge wengine wasisikilize kesi zao? Iweje Watu kama 3,000 waje pale Mahakamani wapige kelele Dunia yote ijue?”

Ameongeza “Walisema tunataka Mahakama imwachilie Lissu la sivyo tutachukua hatua, kwa hiyo ulitaka tusubiri hiyo hatua? Ulitaka tusubiri ushahidi? Sisi kazi yetu ni kuzuia uhalifu usifanyike”

Zaidi https://jamii.app/WaliokamatwaAprili24

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance
ARUSHA: Akishiriki Majadiliano katika Siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mercy Ndegwa, Mwakilishi wa Kampuni ya Meta amesema Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na wadau pamoja na Serikali kuboresha Mazingira ya Kidigitali ikiwemo watumiaji wa majukwaa hayo kuingiza kipato

Amesema "Tumeona platforms zetu za WhatsApp na Instagram zimekuwa zikifanya vizuri na kupiganiwa na Watu wengi, tunaona namna gani ya kuweka njia ya kuingiza Fedha (Monetization), tunafanya hivyo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kwa ukaribu wakiwemo JamiiAfrica"

Ndegwa ameongeza "Tumepitisha mambo kadhaa ikiwemo masuala ya Kodi, ambayo kabla ya kuchukua Maamuzi tunashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutimiza hilo, ili lifanyike kwa njia sahihi, pamoja na hivyo tunazidi kufikiria vitu kwa ajili ya kuboresha ‘tools’ zetu"

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
1
Akizungumzia suala la Waandaa Maudhui kunufaika kupitia Majukwaa ya Kidigitali, Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica amesema "Tumezungumza na wenzetu #Meta, tunashirikiana nao na baadhi ya vikao kati yetu na wao tutafanya kwa njia ya Digitali ili Wadau wengine washiriki na waweze kutoa maoni yafanyiwe kazi. Mikutano hiyo itashirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo wa Serikalini na Sekta Binafsi"

Awali Mwakilishi wa Meta, Mercy Ndegwa alisema wameona Majukwaa yao ya Whatsapp na Instagram yamekuwa yakifanya vizuri, hivyo kwa kushirikiana na Wadau wanatafuta namna ya kuweka njia ya kuwawezesha Watumiaji wa majukwaa hayo kujipatia Fedha (Monetization)

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍2
ARUSHA: Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) yanaendelea, leo Aprili 29, 2025 ikiwa Siku ya pili ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Awali, Aprili 27, 2025 Washiriki na Wadau mbalimbali walishiriki katika mbio (Fun Run) za Kilometa Tano kisha Aprili 28, 2025 kulifanyika mijadala tofauti ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua

Fuatilia https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Akizungumza katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema Wanahabari wana uwezo mkubwa wa kutengeneza ajenda ya kuwafanya Wananchi wote waelekeze Mawazo yao katika jambo fulani

Amesema “Ningekuwa na uwezo ningewashawishi watusaidie kwa nguvu zao zote kubadilisha aina ya Habari zinazosikika kwa Wananchi, Habari ina nguvu kubwa sana, inaamua aina ya chakula, mavazi na kila kitu.”

Makonda ameongeza “Wanahabari wakiamua watatusaidia kututengenezea mwelekeo wa Habari za kiuchumi na nyingine za maendeleo, hilo ni jambo zuri.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
NIGERIA: Mahakama Kuu ya Wilaya ya Shirikisho (FCT) huko Abuja, imemhukumu Peter Nwachukwu, Mume wa Marehemu mwimbaji wa nyimbo za Injili, Osinachi, adhabu ya kifo kwa kunyongwa baada ya kumkuta na hatia kwa kumuua Osinachi kwa makusudi, Aprili 8, 2022

Ingawa taarifa za awali zilidai kuwa Osinachi alifariki kutokana na Ugonjwa wa Saratani, ushuhuda kutoka kwa Familia, waumini wenzake Kanisani na Majirani, ulifichua kuwa alikuwa mwathirika wa Ukatili wa majumbani

Mashahidi walieleza kuwa Nwachukwu alimkanyaga Osinachi kifuani kabla ya kifo chake. Baadaye Nwachukwu alishtakiwa kwa makosa 23, yakiwemo kuua kwa makusudi, vitisho vya jinai, ukatili dhidi ya Watoto na vipigo kwa Mwenzi wa Ndoa

Soma https://jamii.app/HukumuMumeOsinachi

#JamiiForums #HakiZaBinadamu #Accountability
1
ARUSHA: Balozi wa Saudi Arabia-Tanzania, Yahya bin Ahmed Okeish amesema kuna uwekezaji mkubwa ambao unafanywa na Taifa lake katika masuala ya Kidigitali kwa kuwa huko ndipo Dunia inapoelekea

Amesema wamewekeza kwenye Akili Mnemba (AI) kutokana na ukuaji wa Teknolojia na kwamba zaidi ya Dola Bilioni 20 (Tsh. Trilioni 53) zimewekezwa kwa ajili ya ushirikiano na Wadau wa Digitali lengo likiwa ni kuendana na Mabadiliko ya Teknolojia

Ameongeza “Mwaka 2024, Saudi Arabia ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika masuala ya ulinzi wa Kidigitali na Mawasiliano, hali hiyo iliongeza Uaminifu kwa Wawekezaji na wageni walifika katika Taifa letu.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia