Taarifa ya Naibu Waziri Kivuli Habari, Mawasiliano na TEHAMA, wa Chama cha ACT Wazalendo, Emmanuel Ntobi imetoa wito kwa Serikali kufungulia mitandao ya kijamii ya X (Twitter), Clubhouse na Telegram huku ikisema hatua ya kuifungia ni mwelekeo wa Serikali kutaka kuficha matukio, taarifa na habari mbalimbali zinazohusu uchaguzi mkuu 2025 na michakato yake yote
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Kufungiwa mitandao ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 (1) na (2) inayotoa uhuru wa kutoa mawazo, kutafuta na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi na uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati, pamoja na haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani, ambayo ni muhimu kwa shughuli za wananchi na muhimu kwa jamii
Soma https://jamii.app/SerikaliMitandaoACT
#JamiiForums #JamiiAfrica #DigitalRights #Accountability #Democracy #Governance

❤2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel akiwa anajibu swali la Mbunge Hawa Bananga amesema bima ya afya haina lengo la kusaidia wasiojiweza
Amesema "Usisahau kwamba Bima ya afya sio mfuko wa kusaidia wasiojiweza, ni watu wanachangia fedha zao, halafu ziwatibu pale watakapokutana na matatizo”
Zaidi https://jamii.app/BimaYaAfyaWasiojiweza
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFAfya #Accountability #ServiceDelivery #Governance #BimaYaAfyaKwaWote

Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) imeamuru vituo vyote vya televisheni na redio kusitisha mara moja matangazo ya moja kwa moja ya maandamano, ikidai kuwa ni ukiukaji wa Katiba ya Kenya na Sheria ya Mawasiliano na kutoa onyo kuwa vyombo vitakavyokaidi agizo hilo vitakumbana na hatua za kinidhamu.
Katazo hili imekuja wakati maandamano ya kitaifa yakiendelea kuadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano ya Juni 25, 2024 ya Vijana ya kupinga muswada wa fedha, yaliyogharimu maisha ya takriban watu 60
Maandamano ya mwaka huu, yaliyopewa jina la “Siku ya Uwajibikaji wa Vijana,” yamelenga masuala ya uwazi wa kifedha, haki za binadamu, na mageuzi ya usalama. Serikali imeweka ulinzi mkali katika maeneo nyeti kama Ikulu na Bunge, huku barabara kuu zikifungwa mapema asubuhi
Soma https://jamii.app/June25Maandamano
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #PoliceBrutality #HumanRights

Vituo vya Televisheni vya KTN na NTV vimeondolewa hewani baada ya kuendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Maandamano, ikielezwa kuwa ni baada ya kukiuka amri ya kutoonesha matangazo hayo
Hata hivyo, matangazo yanaendelea kupitia kurasa za #KTNNews na #NTVLive kwenye YouTube na pia kwenye kurasa za KTN Facebook na X (Twitter)
Mapema leo, Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) iliamuru vituo vyote vya televisheni na redio kusitisha mara moja matangazo ya moja kwa moja ya maandamano ikidai kuwa ni ukiukaji wa Katiba ya Kenya na Sheria ya Mawasiliano
Soma https://jamii.app/KTNKe
#JamiiAfrica #JamiiForums #Democracy #FreePress

DAR: Timu ya #Yanga imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 kwa kuifunga #Simba Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa ikiwa ni ushindi wa Tano mfululizo dhidi ya Wapinzani hao wa Jadi
Ushindi huo uliotokana na Magoli ya Pacome Zouzoua na Clement Mzize unaifanya Yanga kumaliza Ligi kwa kuwa na Pointi 82 huku Simba ikibaki na alama 78
Michezo mingine iliyopita ya timu hizo Simba 0-1 Yanga (Oktoba 19, 2024), Yanga 1-0 Simba (Agosti 8, 2024), Yanga 2-1 Simba (Aprili 20, 2025) na Simba 1-5 (Novemba 5, 2023)
Soma https://jamii.app/YangaBingwa25
#JFSports #KariakooDerby #JamiiForums #JFLigiKuu25

Kuwa Mwananchi bora ni kuishi kwa Misingi ya Haki, Usawa na kuheshimu majukumu yetu katika Jamii. Tunapojifunza kuwa na maoni ya kujenga, kuuliza maswali ya msingi na kushiriki kikamilifu katika mambo yanayoathiri Maisha yetu, tunajifunza pia kuwa Viongozi wa kesho
Kiongozi mzuri huanza kwa kusikiliza, kuelewa matatizo ya Wananchi wake na kuyatatua kwa pamoja, hivyo Kijana usiache kushiriki, kuhoji na kusimamia Uwajibikaji kwa kila mmoja wetu
#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment

KENYA: Mahakama Kuu imetangaza kusitisha agizo la Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) la kupiga marufuku vituo vyote vya runinga na redio kurusha matangazo ya moja kwa moja ya maandamano, na kwamba kituo chochote kilichozimwa kutokana na agizo hilo kirejeshwe hewani mara moja
Jaji Chacha Mwita, ameagiza vituo vya NTV, KTN na K24 kurejeshwa hewani kutokana na ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na Chama cha Wahariri wa Kenya (KEG) kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali
Matangazo ya vituo hivyo yalizimwa wakati kukiwa na maandamano makubwa ya kitaifa dhidi ya Serikali, kuadhimisha Mwaka mmoja tangu maandamano ya Juni 25, 2024 ya Vijana ya kupinga muswada wa fedha, yaliyogharimu maisha ya takriban Watu 60
Soma https://jamii.app/KenyaJune25Updates
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #PoliceBrutality #HumanRights #FreePress

😁3❤2
Mara nyingi tunakimbizana na maisha, tukisahau kuwa msingi wa ndoto zetu zote ni mwili wenye afya bora. Hakuna mafanikio yatakayokuwa na maana bila afya njema
Kila chaguo unalofanya leo, kama kula Mlo sahihi, kufanya Mazoezi au kupumzika vya kutosha ni Uwekezaji katika Maisha yako ya baadaye
Usingoje hadi uanze kuugua ndipo utambue thamani ya fya. Anza leo na hatua ndogo, kunywa Maji ya kutosha, tembea zaidi, punguza Msongo wa Mawazo na kula Mlo kamili
#JamiiForums #JamiiAfrica #GoodMorning #AmkaNaJF

👍1
#KENYA: Watu takriban 16 wameripotiwa kufariki kufuatia maandamano ya “Siku ya Uwajibikaji wa Vijana” yaliyofanyika jana, Juni 25, 2025, katika kuadhimisha Mwaka mmoja tangu Maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu(KNCHR), Dkt. Raymond Nyeris, zaidi ya Watu 400 walijeruhiwa, wakiwemo Waandamanaji, Maafisa wa Polisi na Waandishi wa Habari. Kati ya hao wengi walitibiwa na kuruhusiwa kurudi Nyumbani, huku 83 wakihitaji Matibabu zaidi
#KNCHR pia imesema Watu 61 walikamatwa na kuzuiliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi, wengi wao wakiwa kutoka Kaunti ya #Nairobi
Soma https://jamii.app/MaandamanoCasualties
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Governance

❤1
DAR: Barabara ya Kivule kwenda Banana ambayo imekuwa ikilalamikiwa na Wadau wa JamiiForums.com imeanza kukarabatiwa ambapo kwa takribani wiki nzima kumekuwa na mchakato wa maboresho unaoendelea
Desemba 17, 2023 mmoja wa Wadau aliandika wakati wa Mvua hali huwa mbaya kiasi kwamba shughuli muhimu zilikuwa hazifanyiki kutokana na Barabara kuharibika kwa kiwango kikubwa huku kukiwa hakuna ushirikiano kutoka kwa Viongozi wao kuhusu maboresho
Soma https://jamii.app/BarabaraKivule
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #JamiiAfrica

Mdau wa JamiiForums.com anaeleza Serikali ilianzisha Mfumo wa Public Employee Performance Management Information System (PEPMIS) ili kurahisisha Utendaji wa Watumishi lakini bado baadhi ya Watumiaji wanapitia changamoto
Anadai kipengele cha kupima Utendaji wa Mtumishi, Wakuu wa Idara ya Halmashauri ya Kigoma Ujiji hawana uelewa mzuri wa kukitumia hali ambayo imesababisha Watumishi wa ngazi za chini kuwa na alama 0% wakati mhusika akiingia katika akaunti yake anaona alama nzuri na ametekeleza majukumu yake inavyotakiwa
Anahoji Afisa Utumishi, Afisa Elimu, Wakurugenzi n.k wanapokuwa hawatekelezi majukumu yao katika Mfumo wa PEPMIS mbona hawachukuliwi hatua? Uzembe wao unachangia wale wa chini wakose Haki zao za msingi.
Soma https://jamii.app/MfumoWaPEPMIS
#Accountability #JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JamiiAfrica

Katika Mazingira yenye ushindani wa Kisiasa, Kijamii na Kibiashara, Waandishi wa Habari wanakumbana na changamoto kama Shinikizo kutoka kwa wenye Mamlaka, Upendeleo wa Vyombo au Wahariri na ushawishi kutoka kwa Wafadhili au Wamiliki wa Vyombo vya Habari
Katika yote haya, ukweli na Haki ya Wananchi kupata Taarifa sahihi vinapimwa kila Siku. Je, ni taarifa zote zinahitaji Mizania? Tunawezaje kuhakikisha kuwa Habari haipindishwi kwa maslahi binafsi au ya Taasisi fulani?
Kufahamu haya na mengine, usikose kujiunga nasi kwenye Mjadala wa Mizania kwenye Uandishi wa Habari, tutachambua maeneo muhimu yanayohitaji Mizania, namna ya kukabiliana na shinikizo na Ulinzi wa Uhuru wa Habari
Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025

Mdau wa JamiiForums.com anaandika “Ningependa kufichua uovu wa #Rushwa unaoendelea katika Vituo vya Ukaguzi wa Mazao ya Kilimo na Maliasili vilivyopo njia ya Segera - Dar kupitia Bagamoyo, hata ukiwa na risiti zote za Ushuru wanakulazimisha utoe pesa kwa kitisho cha kukufanyia ukaguzi zaidi.”
Anaongeza “Wanajua umebeba Mali za kuoza ama unawahi kufikisha Mzigo Sokoni basi wanakuambia ukaguzi huo wa ziada utafanyika kukipambazuka."
Anaongeza "Kwakweli ni uonevu uliokithiri. Mamlaka za Serikali ikiwemo #TAKUKURU ifanye uchunguzi kwani tunaoumia ni wengi katika suala hili.”
Soma https://jamii.app/UkaguziWaMazao
#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica #Uwajibikaji