JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Siku moja kabla ya mchezo dhidi ya #Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Uongozi wa #Simba haujatuma wawakilishi katika Mkutano uliohusisha Wanahabari ambao ni maalum kwa ajili ya kuzungumzia mtanange huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Juni 25, 2025

Taratibu za Ligi hiyo ni kuwa siku moja kabla ya mchezo, timu husika zinatakiwa kutuma Kocha na Mchezaji kuzungumza na Wanahabari kuhusu mchezo unaofuata ambapo ni ratiba pia inayofuatwa na Azam TV ambao wanahusika kurusha matangazo ya Ligi

Soma https://jamii.app/SimbaMkutanoni

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
🤣4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwassa ameipa siku mbili Kampuni ya IFS Consulting Limited ambayo ilipewa tenda na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ya kupakia na kushusha Mizigo, kuwalipa Wabeba Mizigo malipo yao wanayodai ya Wiki Tisa katika Bandari ya Bukoba

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mgomo uliofanywa na Wabeba Mizigo Juni 23, 2025, wakidai stahiki zao kiasi cha Tsh. Milioni 18 ambapo Meneja IFS Consulting Limited Kagera, Godfrey Ismail, amesema wameshakusanya Tsh. Milioni 6 ya Fedha wanayodaiwa na wanaendelea na mchakato

Baada ya maelekezo hayo ya Mkuu wa Mkoa, Wabeba mizigo wameendelea na Kazi wakiisubiri, Jumatano ya Juni 25, 2025 kujua hatima ya malipo yao

Soma https://jamii.app/BukobaBandarini

Video Credits: Azam TV

#Accountability #JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JamiiForums #JamiiAfrica
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza Bungeni, Juni 24, 2025, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema “Utafiti uliofanyika hivi karibuni ukionesha Watanzania wengi wanaunga mkono Serikali ya chama hicho unatakiwa kupingwa kwa Utafiti mwingine na sio wapingaji kujibu kwa hasira kwani hali iliyopo ni nzuri sana.”

Soma https://jamii.app/UtafitiCCM

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Kutambua haki zako bila kuelewa na kutimiza wajibu wako ni sawa na kuwa na gari bila mafuta, linaweza kuwa la kisasa na lenye uwezo lakini haliwezi kukupeleka popote.

Jamii bora hujengwa na raia wanaotambua kuwa haki huambatana na wajibu

Vijana tushiriki katika shughuli za kimaendelo, mikutano ya kijamii na majukwaa mbali mbali ili kuhakikisha Haki zetu zimezingatiwa na kushauri maboresho tunayoyataka kwenye jamii yetu

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza #Bungeni leo, Juni 24, 2025 ametoa ufafanuzi wa utofauti kati ya Deni la Taifa na Deni la Serikali

Amesema Deni la Taifa linahusisha Deni la Serikali na Sekta Binafsi, mfano inapotokea Mfanyabiashara amekopa katika Taasisi za Kifedha, wakati Deni la Serikali linahusiana na Mapato ya Serikali

Soma https://jamii.app/DeniUfafanuzi

#Uchumi #Economy #JamiiForums #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza kuhusu hoja ya Deni la Taifa amesema ni vema Wananchi wakajadiliana kuhusu matumizi ya Mkopo na sio ukubwa wa deni lililopo

Mwigulu ameyasema hayo Bungeni leo Juni 24, 2025

Soma https://jamii.app/DeniTakwimu

#JFUchumi #JFEconomy #JamiiForums #JamiiAfrica
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akisema tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, ni muhimu kutafakari kwa makini iwapo Viongozi tuliowachagua waliwakilisha maslahi yetu kikamilifu

Mdau, Mbunge wako ni nani, na juhudi zake Jimboni kwako zimetimiza matarajio yako? Unampa alama ngapi kati ya 10 kulingana na utendaji wake?

Mjadala https://jamii.app/RateYourMP

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amekutana na Walimu Shule za Msingi na Sekondari Wilayani hapo kuwashukuru kwa ushirikiano na ametoa Tsh. Milioni 2 yakununua matofali ya kujenga Ofisi za Chama cha Waalimu Hai

Kikao hicho kilifanyika Juni 21, 2025, Mjini Bomang'ombe

Soma https://jamii.app/MbungeWaHai

Video: Bananafm Tz

#Siasa #Accountability #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika amesema kitendo cha Jaji Hamidu Mwanga, aliyepangwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake Wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama hicho, kutotokea Mahakamani ni mwendelezo wa kutotenda Haki

Mnyika ameeleza kuwa tayari wameshaandika barua ya kuonesha kutokuwa na Imani na Jaji huyo na kutaka ajiondoe na shauri hilo apangiwe Jaji mwingine

Katika kesi hiyo Said na wenzake wanadai CHADEMA imekuwa ikiitenga #Zanzibar katika masuala mbalimbali, ikiwemo mgawanyo wa Rasilimali Fedha

Soma https://jamii.app/JajiKesiYaCHADEMA

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #Siasa
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanachama wa #ACTWazalendo, Wakili Peter Madeleka, amesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025 kwa ya kudai “reforms” kipindi hiki ni kosa la Jinai

Amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi TV ambapo ameongeza kuwa ana uhakika wa kushinda Ubunge katika Uchaguzi wa 2025 kwa kuwa licha ya changamoto zilizopo bado nafasi ipo kwa Vyama vya Siasa

Madeleka ambaye aliwahi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi kabla ya kujipambanua kuwa Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, alijiunga na ACT, Mei 2025

Soma https://jamii.app/MadelekaKauli

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025
Kujiheshimu si tu kuhusu namna unavyowatendea wengine, bali zaidi ni namna unavyojitendea mwenyewe. Kujitunza ni tendo la upendo wa ndani, ishara ya kwamba unatambua thamani yako na unathamini maisha yako katika ukamilifu wake

Unapojitunza, unatangaza kuwa nafsi yako ina thamani. Unapojithamini, unawaonesha wengine jinsi ya kukuheshimu. Unapokuwa na amani ndani yako, una uwezo wa kuwapa wengine toleo bora la ‘wewe’ na si kilichobaki.

Jitunze, Jiheshimu, Jipende!

#GoodMorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #Selflove
2🙏2
Juni 16 - 17, 2025, JamiiAfrica iliendesha mafunzo maalum kuhusu Akili Unde katika Uandishi wa Habari (AI in Journalism) yaliyolenga kukuza Uelewa na Ujuzi wa Teknolojia katika Taaluma ya Habari

Mafunzo hayo yalilenga kuendana na Mabadiliko ya Dunia na Teknolojia ya Habari ambapo Wanafunzi walijifunza na kujadiliana masuala anuai kuhusu AI ikiwemo matumizi, faida na changamoto zinazotokana na Teknolojia hiyo hususan suala la Upotoshaji wa Taarifa

Mafunzo haya yaliyohusisha Wakufunzi na Wanafunzi wa Shahada ya Uandishi wa Habari pamoja na Uhusiano wa Umma yalitoa fursa ya kujua namna teknolojia inavyobadilika mara kwa mara na namna ya kukabiliana na taarifa zisizo sahihi zinazozalishwa na AI.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AIJournalism #FactChecking
1
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024 amependekeza mambo kadhaa kwa Shirika la Posta ili kuboresha Huduma hasa kwa njia ya Mtandao

Anasema ingawa Shirika la Posta limejitahidi kukabiliana na Maendeleo ya Kiteknolojia kwa kiwango fulani, bado kuna changamoto kama vile kutokuwa na Miundombinu ya Kidijitali ya kutosha, ufinyu wa Upatikanaji wa Huduma za Posta katika maeneo ya Vijijini na Ushindani kutoka kwa watoa Huduma wa Kampuni binafsi.

Soma https://jamii.app/PostaHudumaMtandao

#JamiiForums #ServiceDelivery #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Familia ya Flavian Methew Nyandikuu (85) Mkazi wa Mwenge Mlalakuwa, Mtaa wa Nyendikuu imedai Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa ‘imewapora’ Viwanja viwili ambavyo wamevimiliki kihalali kwa Miaka 40 na kudai Viwanja hivyo vimekabidhiwa kwa Watu wengine kinyume cha utaratibu

Msemaji wa Familia, Fortunatus Buyobe amesema “Ni Viwanja Namba 2107 na 2120 vipo Kilongawima, Mbezi Beach, ilikuwa sehemu ya shamba baadaye vikapimwa, miaka kadhaa nyuma kuna Wavamizi walijitokeza, kesi ikaenda Mahakamani, Mzee Nyandikuu akashinda na nyaraka halali zipo.”

Akifafanua kuhusu mgogoro huo, Wakili Barnaba Luguwa amesema “Nimepitia nyaraka za hukumu zimeonesha viwanja vinamilikiwa kihalali na Mzee Nyandikuu.”

Akihojiwa na ITV kuhusu madai hayo, Kamishna wa Ardhi Mkoa, Shukran Kyando amesema “Sisi hatujawahi kummilikisha mlalamikaji hiyo ardhi wala hatujawahi kumpa ofa, ardhi ile ilipimwa Mwaka 2000.”

Soma https://jamii.app/FamiliaYaNyandikuu

#JFMatukio #JamiiForums #Accountability #CivilRights
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wameanzisha mijadala tofauti kuhusu tabia ya Wabunge kutelekeza Majimbo yao na kusubiri hadi Miezi michache kabla ya uchaguzi ndio wanarudi kumalizia miradi na ‘vi zawadi vya hapa na pale’ ili kuwahadaa wapiga kura

Mdau mmoja amesema kama maendeleo anayoyaona sasa yangekuwa yanafanyika kwa utaratibu tangu mwaka wa kwanza wa uongozi, jamii ingekuwa mbali sana

Mdau mwingine amesema Wananchi wanapaswa kujifunza na kutambua tofauti kati ya maendeleo ya kweli na propaganda za kisiasa. Kwa wale wanaotaka kuendelea kuongoza, wajue kuwa Wananchi wa sasa si kama wale wa zamani, macho na masikio yao yako wazi

Mdau, vipi ‘hekaheka’ za jimboni kwako?

Soma https://jamii.app/WabungeMlikuwaWapi

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery