JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Timu ya #Yanga imeshinda Magoli 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC na hivyo kuendelea kubaki kileleni katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha Pointi 79, nafasi ya pili inashikwa na #Simba ambayo imefikisha alama 78 baada ya kuifunga Kagera Sugar Goli 1-0

Kutokana na matokeo hayo bingwa wa ligi hiyo msimu huu anatarajiwa kujulikana wiki ijayo Jumatano Juni 25, 2025 ambapo Yanga itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa mwisho kabisa wa Ligi Kuu Msimu wa 2024/25

Soma https://jamii.app/LigiKuuMatokeo

#JFSports #JFLigiKuu25 #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Lugata Wilayani Sengerema, wameandamana kupinga hatua za viongozi wa Chama hicho ngazi ya Kata kuzuia ujenzi wa Ofisi ya chama hicho, baada ya Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo, kuahidi kuijenga ofisi hiyo kwa gharama zake

Wanachama hao wamesema kuwa wao kama wanachama wa #CCM wanahaki ya kupata msaada kutoka kwa Mbunge wao ambaye amejitolea kujenga ofisi, lakini kuna vikwazo kutoka kwa viongozi wa Chama hicho ngazi ya Kata na kuomba mamlaka husika kuingilia kati Suala hilo

Soma https://jamii.app/ShigongoAkataliwaKujengaOfisi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #ServiceDelivery
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Addo November kutoka Chama cha Wanasheria wa Serikali amesema “CHADEMA wakija wakitaka kushiriki Uchaguzi nafasi wanayo 'as long as' hatujafikia hatua ya kuanza mchakato wa uchaguzi"

Alisema hayo katika Kongamano la Sheria lililofanyika Juni 21, 2025, alipokuwa akijibu swali la mmoja wa wadau aliyeuliza iwapo CHADEMA bado watakuwa na nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi kama wakiamua

Soma https://jamii.app/CHADEMAKanuniUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025
2
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Akizungumza katika kikao cha ndani na Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ukerewe, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira amesema Utawala Bora ni kutii Katiba na Sheria za nchi, yeyote asiyezingatia hayo ni gaidi

Soma https://jamii.app/WasiraUgaidi

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM, Ally Hapi akishiriki Mjadala wa #CafeTalk amesema ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama kwamba wanaotajwa wote moja kwa moja huwa ni Mafisadi au Wezi, bali ripoti husomwa kisha kuwapa nafasi Watumishi na Taasisi kutoa vielelezo ambavyo havikuwasilishwa wakati wa ukaguzi

Soma https://jamii.app/HapiCAGReport

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Siasa #Governance #Kuelekea2025
Mdau anasema Watu wengi hasa Vijana wanalalamika kuhusu Ajira lakini Moja ya Ajira ambazo huna haja ya kutuma maombi wala kibali cha kuitumia ni Mitandao ya Kijamii

Ukiwa na 'Followers' wengi wanaotembelea kurasa zako, unaweza kutumia fursa hiyo kufanya matangazo ya Bidhaa za Watu wengine kwa malipo nafuu. Kadri unavyofanya matangazo vizuri, ndivyo utakavyowavutia wengine kutangaza nawe

Pia, unaweza kutumia Mitandao ya Kinamii kupata ‘Connections’ za Kibiashara, kutangaza kipaji au uwezo wako, pamoja na kuwaonesha Watu Ubunifu au Taaluma yako

Je, umewahi kupata faida gani kupitia Mitandao ya Kijamii?

Soma https://jamii.app/MitandaoFaida

#JamiiForums #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
3
#MAISHA: Malezi uliyoyapata kutoka kwa Wazazi/Walezi wako yamekuathiri vipi kwenye namna unavyolea/utakavyowalea Watoto wako?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MaleziTulivyolelewa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFStories #JFChitChats #Malezi
DAR: Taarifa ya Chama cha ACT Wazalendo imeeleza, Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa Chama hicho, Janeth Rithe amepewa dhamana baada ya kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini kwa sharti la kuripoti tena Kituoni Juni 29, 2025

Juni 20, 2025, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama cha ACT - Wazalendo, Shangwe Ayo kupitia akaunti yake ya Mtandao wa X, alisema Polisi wamefika katika Ofisi za Chama hicho na kumkamata Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa, Janeth Rithe kwa agizo la Afisa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO)

Soma https://jamii.app/RitheAachiwa

#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica
4
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akichambua Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha #ACTWazalendo, Isihaka Mchinjita, amesema "Athari za ukubwa wa Deni la Serikali linaangukia kwenye mabega ya Wananchi wanyonge, wanaongezewa Kodi, Ushuru na Makato katika Huduma muhimu ili kulipa madeni haya.”

Soma https://jamii.app/ACTKuhusuDeni

#JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Economy
1
Mdau wa JamiiForums.com anadai kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wazazi, Walezi na Ndugu kutumia nafasi zao za Umri, Cheo au Wadhifa kushinikiza baadhi ya Ndugu watoe Ahadi za Michango kwenye Vikao vya Sherehe, jambo linalowaumiza Kisaikolojia na Kiuchumi wanaolazimishwa

Vipi Mdau, umeshawahi kulazimishwa utoe Mchango/Ahadi kwa ajili ya Sherehe?

Soma https://jamii.app/Jobless

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats #JFStories #Maisha
4
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa Askari Polisi wawili kati ya saba waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya Mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamisi aliyekuwa Mkazi wa Kijiji cha Luponda, Wilaya ya Nachingwea, Mkoani Lindi

Azam TV imeripoti kuwa katika kesi hiyo ya mauaji ambayo yalitokea Mwaka 2022 mkoani Mtwara, Watuhumiwa watano wameachiwa huru baada ya Mahakama kuwakuta hawana hatia.

Soma https://jamii.app/PolisiHukumiwa

#JFMatukio #Accountability #Governance #JamiiAfrica #HakiZaBinadamu #JamiiForums
3
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo atakuwa miongoni mwa wazungumzaji katika Mkutano wa 20 wa Utawala wa Mtandao (IGF) utakaofanyika Jijini Lillestrøm, Norway kuanzia Juni 23 hadi 27, 2025

Juni 24, 2025, Maxence Melo atazungumza katika mjadala kuhusu “Miundombinu ya Maslahi ya Umma” (Public Interest Infrastructure), akielezea namna jukwaa la JamiiForums.com linavyotumika kama uwanja wa Wananchi kujadili na kuchochea mabadiliko kwenye jamii yao

Jukwaa la Utawala wa Mtandao (IGF) ni jukwaa la kimataifa linalowaleta pamoja wadau mbalimbali wa Serikali, Sekta Binafsi, Jamii za Kiraia na Wataalamu wa Teknolojia kujadili Sera na mustakabali wa mtandao wa intaneti duniani

Bofya 'link' hii ili uweze kushiriki mtandaoni https://intgovforum.zoom.us/meeting/registerCArMB7gRTWWSC4LXsJ_ybQ

#JamiiAfrica #JamiiForums #AfIGF2025 #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza kuwa Mchezo wa Ligi hiyo wa kukamilisha Msimu wa 2024/25 ambao pia utaamua timu itakayotwaa ubingwa kati ya Yanga dhidi ya Simba (Kariakoo Derby) utachezeshwa na Waamuzi kutoka Nchini Misri

Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar, Msaidizi Namba Moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal, Msaidizi Namba Mbili ni Samir Gamal Saad Mohamed na Mwamuzi wa Akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour

Kamishna wa Mchezo ni Salim Omary Singano kutoka Tanga wakati Mkaguzi wa Waamuzi ni Alli Mohamed kutoka Somalia

Pia, Catherine Chammy kutoka N-Card amesema “Kadi zilezile ambazo zilitumika Juni 15, 2025 kabla ya mechi kuahirishwa na kupangiwa siku nyingine ambayo ni Juni 25, 2025, zitatumika tena.”

Soma https://jamii.app/DabiYaKariakoo

#JFLigiKuu25 #JFSports #JamiiAfrica
2