JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MANYARA: Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Joseph Nyamoko na Issa Masoud wamefariki Dunia baada ya kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama

Taarifa ya Jambo TV imeeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amesema tukio hilo limetokea katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro na kuwa mipango ya kusafirisha miili ya askari hao inaendelea kwa uratibu wa Jeshi la Polisi na Familia za wahusika

Aidha, Nyamoko na Issa kila mmoja ameacha Mke na watoto wawili

Soma https://jamii.app/RadiSimanjiro

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
😒6πŸ‘3
Tuchague kuwa watu wa kutafakari kabla ya kuzungumza. Tuchague kuchukua hatua zinazotokana na ukweli, si hisia, kwa sababu maneno yana nguvu na maamuzi yana athari

Pale kunapokuwa na sintofahamu, epuka kutoa hukumu bila kujiridhisha, kwani hukumu na maamuzi yasiyoangaliwa kwa makini yanaweza kuvunja zaidi kuliko kujenga

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha
πŸ‘1
ENGLAND: Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min (32) amefungua kesi Polisi dhidi ya Mwanamke ambaye alidai ana ujauzito wa staa wake akidai kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kupata fedha

Wanasheria wa Son wanadai Mdada huyo alitoa madai hayo Juni 2024 na akataka fedha ili anyamaze, wiki iliyopita Son akaamua kufungua mshtaka kwa kuamini mtu huyo alikuwa na lengo la kumlaghai ili ajipatie fedha

Son hana mke wala Mtoto anayetambulika na aliwahi kunukuliwa akisema β€œBaba alisema unapooa kipaumbele cha kwanza ni familia, mke na Watoto kisha soka. Nataka kuhakikisha nitaendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu, nikistaafu ndio nitaanza kutafuta Watoto.”

Soma https://jamii.app/SonBlackmail

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa wito kwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kurejea kumbukumbu za Bunge kuona taarifa za utekaji zilishawahi kuwasilishwa Bungeni Mwaka 2018 na hazikufanyiwa kazi

Amesema hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alivyowasilisha hoja kuhusu uwepo wa matukio ya utekaji na mauaji nchini na kuomba Bunge kusimama kwenye nafasi yake katika kuisimamia Serikali ili kuhakikisha matukio hayo yanakoma

Soma https://jamii.app/PondaUtekajiMei14

Video Credits: Jambo TV

#JamiiForums #HumanRights #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau anadai baada ya malalamiko ya Mwananchi yaliyotolewa Machi 16, 2025 kupitia JamiiForums.com kuhusu Wakazi wa Chanika Zingiziwa kutokuwa na huduma ya umeme, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilifika na kuweka miundombinu kadhaa ikiwemo Nyaya na Nguzo

Anaeleza Wananchi waliamini kadhia ya kukosa umeme inaondoka lakini anadai TANESCO hawakufunga transfoma, hivyo huduma haikuunganishwa na hata mchakato wa kujiandikisha kuunganishiwa umeme haujafanyika na kwamba wanapouliza mamlaka hiyo hawapati majibu sahihi

Mdau anahoji β€œTransfoma zitakuja lini na mbona hakuna maelezo yaliyonyooka? Inakuwa kama umeme ukifika tutapewa bure, tunapata hasara nyingi kwa kutokuwa na huduma hiyo"

Soma https://jamii.app/UmemeZingiziwa

#JamiiAfrica #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Susan Kiwanga aliyekuwa Mbunge Jimbo la Mlimba 2015- 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa Miaka 20, akitangaza kujiondoa katika Chama hicho Mei 13, 2025, ametaja miongoni mwa sababu zilizomfanya aingie kwenye Kundi la G-55 ni Kaulimbiu ya 'No reforms, No election' kufanywa azimio la Chama

Soma https://jamii.app/KaulimbiuChama

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #Governance
KENYA: Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema Chama chake kiitwacho 'Democracy for the Citizens Party (DCP)' kinalenga ujumuishaji na kina Wanachama wa makundi yote wakiwemo #GenZ

Gachagua pia alitaja Viongozi wa Chama hicho wakiwemo David Mingati (Mwenyekiti), Cleophas Malala (Naibu Kiongozi wa Muda wa Chama) na Cate Waruguru (Kiongozi wa Wanawake)

Aidha, Gachagua ametangaza kuwa Chama hicho kitazinduliwa rasmi Juni 4, na baadaye ataanza ziara ya Miaka Miwili kote nchini kueneza Sera za chama na kuomba uungwaji mkono. Pia, amewataka wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa 2026 kupitia Chama hicho kuanza kujisajili

Soma https://jamii.app/ChamaKipyaGachagua

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Demokrasia
πŸ‘1πŸ”₯1
GEITA: Wanafunzi wa Shule ya Msingi Rubambangwe na Sekondari ya Rubambangwe, Kitongoji cha Iyozu, Kata ya Muungano Wilayani Chato wanatumia mitumbwi kutoka katika makazi yao kisha wanatembea umbali wa zaidi ya Kilometa 4 ili kufika katika Shule

Akielezea changamoto hiyo, Diwani wa Kata ya Muungano, Charles Kapembe amesema amewasilisha maoni ya Wananchi hao kwenye vikao halali vya Baraza la Madiwani na tayari amezungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa ajili ya utatuzi

Mkurugenzi wa Halmashauri, Mandia Kihiyo alipoulizwa amesema Halmashauri inakusudia kuchonga mtumbwi wenye thamani ya Tsh. Milioni 2 kupunguza adha ya Wananchi kuvuka na watakapopata pesa watajenga Daraja la kudumu

Soma https://jamii.app/IyozuChato

#JamiiForums #Accountability #Elimu
πŸ‘1
Ukimuuliza Mtanzania kuhusu Nchi za #Nordic, yaani Sweden, Norway, Denmark, Finland au Iceland, wengi watasema: β€œAaah zile nchi za maisha bora! Kule hakuna rushwa! Elimu ni bure na watu wao wana furaha kweli kweli”

Lakini, ni hayo tu unayoyajua?

Je, unajua uhusiano wao na Afrika ukoje? Wanavyotumia teknolojia kusaidia jamii? Tamaduni zao za kipekee? Au ushirikiano wao wa kimataifa unaoleta maendeleo ya kijamii?

Ni muda wa kuonesha maarifa yako. Bofya link na uone ni kwa kiasi gani unaelewa kuhusu Nchi za Nordic: https://jamii.app/NordicDodoso

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
MOROGORO: Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Tume haitamvumilia yeyote atakayehusika kuvuruga zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kujiandikisha katika vituo zaidi ya kimoja

Amesema hayo katika mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki (BVR), Kilosa na Mvomero na kuongeza Sheria inayosimamia hilo ni Kifungu cha 114(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili litaingia katika mzunguko wa pili Mei 16 hadi Mei 22, 2025, likihusisha mikoa ya Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Manyara, Lindi, Mtwara, Morogoro na Dar es Salaam kwa Tanzania Bara pamoja na Mikoa yote ya Tanzania Zanzibar

Soma https://jamii.app/INECYaonya

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
πŸ‘1
Taasisi ya CIPESA (Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa) kwa kushirikiana na wadau wengine, wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, Safaricom na Airtel Kenya, kupinga vitendo vya kiholela na visivyo halali vya kuzuia huduma ya intaneti nchini humo

Kesi hiyo inajikita kwenye ushahidi wa kiteknolojia kutoka Mashirika ya Kimataifa kama Cloudflare, Open Observatory of Network Interference (OONI) na Internet Outage Detection and Analysis (IODA), ambayo yamedhihirisha kuwepo kwa vitendo vya makusudi vya kupunguza kasi ya intaneti na kufunga baadhi ya majukwaa kama vile Telegram

Zaidi https://jamii.app/KeepItOnKE

#DigitalRights #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression #Governance #Accountability
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com anasema Stendi ya Makumbusho imechakaa na imekuwa kero kwa watumiaji na madereva wa daladala. Anadai hata maeneo ya abiria kuketi wakiwa wanangojea magari nayo yamechakaa, mvua ikinyesha ndio majanga, abiria wanakimbilia kujisitiri kwenye maduka ya watu au kwenye magari

Anadai kuna wakati magari yanalazimika kushusha abiria maeneo ya nje ili kuepuka kuingia stendi, lakini hata ikifanyika hivyo wahusika wanayanyapia na kutoza faini. Anatoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuwajibika kurekebisha stendi hiyo

Soma https://jamii.app/StendiMakumbusho

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Governance #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Uwajibikaji
πŸ‘3❀1