JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAGERA: Magari yanayosafiri kutoka Bukoba kuelekea mikoa mingine yamekwama Kyetema kutokana na barabara ya dharura inayotumiwa na magari kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea Mkoani hapo

Barabara imejaa tope na maji, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri, mvua kubwa imenyesha usiku wa kuamkia Mei 15, 2025

Ikumbukwe Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya alinukuliwa akisema hakuna mpango wa kujenga daraja mbadala eneo la Kanoni kwa kuwa halipo katika mkataba, hivyo Wananchi waendelea kutumia njia ya kuzunguka kupitia Nyakanyasi, Kashura na Kashozi Road ili kuingia katikati ya Mji

Soma https://jamii.app/KageraBarabara

#JFMatukio #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Haji amesema baadhi ya abiria wa Treni ya SGR wamekuwa chanzo cha kero ya kelele baada ya kutumia vilevi, hivyo ameshauri Mamlaka husika kuangalia suala hilo

Ameyasema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, leo Mei 15, 2025

Soma https://jamii.app/PombeSGR

#JFHuduma #JamiiForums #ServiceDelivery
👍1
MWANZA: Jeshi la Polisi limemkamata na linamhoji Diana Edward Bundala "Mfalme Zumaridi" (42), Mkazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa kwa tuhuma tofauti ikiwemo kuwaeleza Watoto yeye ni Mungu wao mwenye uwezo wa kuwatenganisha na kifo

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali

Pia, Jeshi hilo limewaomba Wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi

Soma https://jamii.app/ZumaridiAkamatwa

#JFMatukio #JamiiForums
👍1
Ikiwa unashiriki Mazungumzo na Watu wanaopiga Majungu dhidi ya wengine, ni ishara kwamba hata wewe hutahifadhiwa pindi utakapoondoka.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifelessons #Maisha #AmkaNaJF #GoodMorning
Mdau wa JamiiForums.com anadai Mazingira ya Chuo cha Marian hayaridhishi hasa kipindi cha mvua na Mara kadhaa wamefikisha malalamiko yao kwa Utawala lakini huwa wanaishia kutoa ahadi tu za kufanya maboresho

Ametoa wito kwa Uongozi wa Chuo hicho kuchukua hatua za haraka kushughulikia changamoto hiyo, kwasababu hali iliyopo inahatarisha Afya za Wanafunzi

Zaidi https://jamii.app/BagamoyoMarian

#JamiiForums #HudumaZaKijamii
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Mwananchi wa Mtaa wa Somelo, Kata ya Zingiziwa, Ilala amembana Diwani wake kwa maswali, akitaka kufahamu yapi ameyafanya Diwani huyo tangu alipoingia Madarakani, akidai toka wamchague hajawahi kufika hata kuwashukuru Wananchi wake kwa kumchagua

Zaidi https://jamii.app/DiwaniWaSomelo

#JamiiForums #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #Accountability #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti Wizara ya Uchukuzi 2025/2026, Mei 15, 2025, Mbunge Livingstone Lusinde amesema “Watu waheshimu miundombinu na utaratibu ili Taifa lisonge mbele lakini mambo madogo yasiwaumize kichwa mfano Mtu akisema No Reforms No Election, geuza kidogo na mwambie No Election No Reforms.”

Aidha, amesisitiza elimu itolewe kuhusu huduma ya usafiri wa Treni ya SGR na Treni ya Reli ya Kati kwa Wananchi ili watambue umuhimu wake na ili walinde miundombinu inayotumika

Soma https://jamii.app/LusindeMei15

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025
MWANZA: Kampuni ya Meli Tanzania (#TASHICO) imesema inatarajia kutoa taarifa na tarehe rasmi ya kurejea kwa safari za kawaida kwa Meli ya New MV Victoria ambayo imekuwa katika matengenezo tangu Machi 4, 2025

Soma https://jamii.app/MvVictoriaMei15

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akijibu hoja za Wabunge walioeleza kuwa kuna Wajawazito wengi na Watoto chini ya umri wa miaka mitano wamekuwa wakilipishwa fedha katika Hospitali za Serikali kinyume na maelekezo ya Serikali, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuna wakati busara inatumika licha ya uwepo wa Sheria na Kanuni

Soma https://jamii.app/MatibabuBure

#JamiiForums #PublicHealth #Accountability #JFHuduma
Mei 14, 2025, Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia Ukurasa wake rasmi katika Mtandao wa X alisema utani wa Kisiasa ni mzuri lakini ni muhimu sana kufanyika kwa namna ambayo unalinda Heshima na Utu wa Wanawake

Soma https://jamii.app/UtuWanawakeSiasa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #JFWomen #WomenInPolitics
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Bahi, Kenneth Ernest Nollo ameshauri Serikali kupunguza kodi ya kuingiza simu kutoka nje ya Tanzania ili kuwezesha Watanzania wengi kutumia Simu Janja kwa kuwa hali hiyo itasaidia ongezeko la Watumiaji wa Intaneti

Awali, Nollo alisema, takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TCRA) za Machi 2025 zinaonesha kuna laini za simu Milioni 90, Watumiaji wa Intaneti ni Milioni 49, simu zinazomilikiwa zisizo simu janja ni milioni 56 wakati simu janja ni milioni 24, hali inayoonesha bado matumizi ya intaneti ipo chini

Soma https://jamii.app/KennethNollo

#JamiiForums #DigitalWorld #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Bahi, Kenneth Ernest Nollo amesema kuna mazingira kadhaa yanayosababisha Watu wengi kutotumia intaneti ikiwemo baadhi ya Mitandao ya Simu kuwa na huduma mbovu ya intaneti

Amesema hayo wakati anachangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Mwaka wa Fedha wa 2025/26, Mei 16, 2025

Soma https://jamii.app/NolloKuhusuIntaneti

#JamiiForums #DigitalWorld #DigitalRights
👍1
DAR: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ameeleza Matumizi ya Tiketi za Karatasi katika usafiri wa ‘Mabasi ya Mwendokasi’ yatafutwa rasmi ifikapo Juni 30, 2025 na baada ya hapo watakaotumia kadi ndio watakaoruhusiwa kusafiri kwa kutumia mabasi ya mfumo wa DART

Taarifa ya DART imeeleza kuwa utaratibu huo wa matumizi ya kadi hautahusisha Wanafunzi na katika kurahisisha zoezi hilo bei ya kadi moja itakuwa inauzwa kwa Tsh. 1,000 (ilikuwa inauzwa Tsh. 5000) kuanzia kesho Mei 17, 2025

Aidha, ikumbukwe Septemba 2024, Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa alizindua matumizi ya Kadi hizo na kutoa maelekezo kuhakikisha zinatumika lakini kwa asilimia kubwa DART imeendelea kutumia Tiketi za Karatasi

Soma https://jamii.app/TiketiZaMwendokasi

#JFMatukio #ServiceDelivery #JamiiForums
1
Katika dunia yenye maneno mengi na vitendo vichache, uaminifu umekuwa rasilimali adimu. Si kila anayesema ukweli anaishi kwa ukweli na si kila anayeahidi ana nia ya kutimiza.

Uaminifu wa kweli huonekana pale mtu anapochagua kuwa mwaminifu hata kama hakuna anayemuangalia, anapotimiza wajibu wake bila kulazimishwa na anaposhikilia ahadi zake hata kama ni vigumu

Tunapokaribisha mapumziko ya Mwisho wa wiki tujiulize; Je, tunaishi yale tunayoyasema?

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #Lifelessons
👍1