JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akihojiwa na Kituo cha #Clouds, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Shabani Hamis Taletale (Babu Tale) amesema hana la kusema kuhusiana na Matukio ya Utekwaji wa Raia kwasababu hakuna mtu aliyetekwa jimboni kwake

Aidha, ameongeza kuwa hajawahi kushiriki kwenye mambo mengine sababu alipoingia #Bungeni 'focus' yake ilikuwa ni kwenye jambo moja tu (Jimbo lake) kuhakikisha wanapata Barabara na mwaka huu Rais ameridhia ombi lake hivyo amefanya kazi yake kikamilifu

Zaidi https://jamii.app/UtekajiMoro

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice #Uwajibikaji #Accountability #Governance #Kuelekea2025
👎3👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga amewataka Wasimamizi wa Uchaguzi kutenda haki ili watoe matokeo sahihi na wasihusike katika kuongeza wala kupunguza idadi ya Kura Halali

Alitoa kauli hiyo, Aprili 15, 2025 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Soma https://jamii.app/MagangaKuhusuHaki

#Governance #Accountability #JamiiForums #Democracy
👍31
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, Bungeni Aprili 15, 2025, alitoa wito kwa Wananchi kutowapigia kura Wagombea wanaotoa #Rushwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025

Zaidi https://jamii.app/MagangaKuhusuHaki

#Governance #Accountability #JamiiForums #Democracy #KemeaRushwa #Uwajibikaji
1
ARUSHA: Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Murieti, Steven Jacob (35) ambaye iliripotiwa ametekwa na ‘Watu Wasiojulikana’ Asubuhi ya Mei 16, 2025 amepatikana akiwa na majeraha kadhaa ya kupigwa

Awali, Kusaga TV ilinukuu familia ya Steven ikisema watekaji wakikuwa na gari aina ya Land Cruser nyeupe isiyokuwa na Namba za Usajili

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa amesema “Sina hiyo taarifa”. Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Arusha, SACP Justine Masejo zinaendelea kutokana na simu yake kutopokelewa

Soma https://jamii.app/StevenJacobMchungaji

#JamiiForums #HumanRights #Accountability
👍2
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Barabara ya Musoma - Mwanza imekuwa ikitengenezwa mara kwa mara lakini hata miezi miwili haiishi inafumuka, ina matuta kuliko Barabara za Changarawe wakati ni barabara kubwa (cross country road)

Anadai kipande cha Nyanguge - Lugeye kilifumuka hata kabla ya mwezi mmoja kumalizika, kilichofuata wakaanza kuweka viraka

Anatoa wito Mamlaka husika kusimamia ubora kwa kuwa hali inavyoendelea wanaoumia ni wengi na madhara kwa Watu na Vyombo vya Usafiri yanaongezeka

Soma https://jamii.app/MusomaMwanza

#Accountability #JamiiForums
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Murieti, Steven Jacob Gumbo (35) ambaye iliripotiwa ametekwa na ‘Watu Wasiojulikana’ Mei 16, 2025 amezungumza na Wanahabri na kueleza kuwa Watu waliomchukua walijitambulisha kuwa ni Askari Polisi na wanamhitaji kwa ajili ya mahojiano

Amesema Watu hao walimchukua kwa nguvu huku wakimpiga, akapelekwa sehemu ambayo hakuifahamu na kuingizwa kwenye chumba kisha kuanza kumshambulia

Ameongeza “Naomba nisiongee mengi, sababu ya kutekwa ni ishu za Mtandao. Walichukua maelezo, wakanipeleka porini West Kilimanjaro, wakachukua simu yangu na kunitaka nifute video zangu zote, wakazungumza vitu ambavyo siwezi kuvisema kwa sasa kisha wakanitelekeza hapo.”

Soma https://jamii.app/MchungajiJacob

#JamiiForums #JFMatukio #HumanRights
Mtumiaji wa JamiiForums.com ame'share' picha zikionesha hali halisi ya Barabara ya Mbezi Makabe (Kwa Pesapesa) na changamoto ya usafiri wanayokutana nayo Watumiaji wa Barabara hiyo hasa msimu huu wa Mvua, akitoa wito kwa Mamlaka husika na Viongozi wa eneo hilo kushughulikia uboreshaji wa barabara hiyo

Zaidi https://jamii.app/MakabeKwaPesapesa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance
Nchi ya Denmark inatajwa mara nyingi kuwa kinara kwenye Nchi zenye kiwango kidogo cha Ufisadi kutokana na Uhuru mkubwa wa Vyombo vya Habari, Uwazi na Upatikanaji wa Taarifa kuhusu Matumizi ya Fedha za Umma, Viwango vikubwa vya Uadilifu kwa Maafisa wa Umma na Mfumo huru wa Mahakama

Raia wa Denmark huweka sehemu kubwa ya Mapato yao binafsi kwenye Kodi, wakiwa na Imani kuwa Rasilimali hizo zitatumika kwa manufaa ya wote.

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #TheNordics
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Lucas Matata amesema Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya Kisheria ya kumuwezesha kubatilisha uteuzi wa Viongozi wa Chama cha Siasa

Amesema kwamba suala hilo siyo sehemu ya majukumu yake na kuwa kauli ya kuingilia na kuchukua maamuzi haizingatii misingi ya Sheria na haina dhamira njema kwa Chama

Pia, amehoji Mbatia alipoondolewa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alichukua uamuzi upi ili kulinda nafasi halali ambayo alikuwa nayo

Soma https://jamii.app/WakiliMatata

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
CAF: Mchezo wa Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) umekamilika kwa #Simba ya Tanzania kupoteza magoli 2-0 ikiwa ugenini dhidi ya #RSBerkane ya Morocco

Wachezaji waliosababisha kilio kwa Simba ni Mamasou Camara dakika ya 8 na Oussama Lamlaoui dakika ya 14

Kutokana na matokeo hayo sasa kila kitu kinaelekezwa katika mchezo wa pili ambao bado kuna utata kama utacheza kwenye Uwanja wa Mkapa (Dar es Salaam) au New Amaan Complex (Zanzibar)

Je, unadhani Simba inaweza kupindua matokeo au ndio imeisha hiyo?

Soma https://jamii.app/BerkaneSimba

#JamiiForums #CAFCC #JFCAF25
🔥1
Kujisamehe na kusamehe wengine ni hatua muhimu ya kujikomboa kutoka katika maumivu ya zamani

Kujisamehe ni kujipa nafasi ya kukua na kujifunza, bila kujihukumu milele, huku kusamehe wengine kukituondolea mzigo wa chuki na machungu

Msamaha hauhalalishi makosa, bali huleta uhuru wa ndani na kutupa amani ya kweli. Kuanzia leo tujifunze kusema "Nimesamehe na najisamehe pia"

Jumapili Njema!

#GoodMorning #AmkaNaJF #Maisha #LifeLessons #Lifelessons
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima ametoa wito kwa Wananchi kutochana karatasi ambazo zina orodha ya Wapigakura katika vituo kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuathiri zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Soma https://jamii.app/INECYaonya

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
MICHEZO: Timu ambazo zimeshinda Kombe la Shirikisho Africa (CAF Confederation Cup) mara moja ni: FAR Rabat, Hearts of Oak, Stade Malien, FUS Rabat, MAS Fez, AC Léopards, Al Ahly na USM Alger.

Zilizobeba Kombe hilo zaidi ya mara moja ni: CS Sfaxien (3), RS Berkane (2), Étoile du Sahel (2), TP Mazembe (2), Zamalek (2) na Raja CA (2)

Soma https://jamii.app/CAFWinners

#JFSports #JamiiForums #JFCAF25 #CAFCC
🤣1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanasiasa na Waziri wa zamani wa Sheria wa Kenya, Martha Karua amedai kuzuiwa kuingia nchini Tanzania akiwa na Watetezi wengine wa Haki za Binadamu na Mawakili wenzake, Lynn Ngugi na Gloria Kimani

Karua ameposti na kueleza akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Pasipoti yake ilichukuliwa, akazuiwa kwa Saa moja bila maelezo yoyote na kwamba walikuwa wanasubiri kurejeshwa walipotoka

Amesema yeye na wenzake walialikwa na Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Kenya pamoja na Chama cha Wanasheria wa Uganda

Soma https://jamii.app/KaruaDeported

#JamiiForums #Diplomacy #JFMatukio
👍1