JamiiForums
โœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIASA: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadaiwa kutengua uteuzi wa Wajumbe nane wa Sekretarieti na Kamati Kuu ya CHADEMA, waliothibitishwa na Baraza Kuu la Chama hicho, Januari 22, 2025 kwa maelezo akidi haikutimia wakati wakiteuliwa

Viongozi walioteuliwa na Mwenyekiti wao, #TunduLissu ambao Msajili amewaweka kando hadi Baraza Kuu jingine liitishwe ni; Katibu Mkuu (John Mnyika), Amani Golugwa (Naibu Katibu Mkuu - Bara) na Ally Ibrahim Juma (Naibu Katibu Mkuu - Zanzibar)

Wengine ni Wajumbe wa Kamati Kuu; Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA

JamiiForums inaendelea na jitihada za kuitafuta Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupata ufafanuzi zaidi wa Maamuzi haya

Soma https://jamii.app/MsajiliAtengua

#JamiiForums #Siasa #Kulekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy
๐Ÿ‘2๐Ÿ‘Ž1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Treni inayofanya safari Pugu hadi katikati ya Jiji imepata ajali baada ya behewa kuachia njia maeneo ya Karume, inadaiwa Watu kadhaa wamejeruhiwa

Taarifa zaidi zitafuata

Video Credits: Jamvi Media

Soma https://jamii.app/MabehewaKarume

#JFMatukio #JamiiForums
#MALEZI: Sera ya Uzazi na Malezi nchini Sweden inawapa Wazazi jumla ya Siku 480 za likizo ya Uzazi na Malezi yenye malipo pale Mtoto anapozaliwa au kuasiliwa. Iwapo kuna Wazazi wawili, kila mmoja anapewa Siku 240

Kwa Watoto waliozaliwa mwaka 2016 au baadaye, kila Mzazi ana siku 90 ambazo haziwezi kuhamishiwa kwa Mzazi mwingine kama hazitatumika. Mzazi mmoja (single parent) anapewa Siku zote 480

Wazazi pia wanaweza kuamua kuhamisha hadi Siku 45 za likizo yao kwa Babu, Bibi au Rafiki wa karibu wa Familia, anayewasaidia kulea. Wanaostahili likizo hii ni wanaolea badala ya kufanya Kazi, Kusoma au kutafuta Kazi

#JamiiForums #NordicWeek #ParentHood #LifeStyle
๐Ÿ‘1
Mdau wa JamiiForums.com anasema
kama mamlaka husika haziwezi kuchukua hatua za kuhakikisha Taa za Makutano ya Uhuru-Msimbazi (Kariakoo) zinafanya kazi basi Trafiki awepo muda wote, ili kuepusha ajali, magari kukwaruzana na msongamano wa Vyombo vya Moto ambao ni kero kubwa

Zaidi https://jamii.app/TaaHazifanyikazi

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Kila mafanikio yana safari yake. Usikate tamaa unapokutana na vikwazo; vinafundisha, vinakuimarisha na mwisho vinakuandaa kwa ushindi.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJF #GoodMorning
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kufuatilia malipo ya mitihani ambayo Mwanafunzi hakufanya vizuri (Supplementary Examination), akidai baadhi ya Vyuo vinatoza gharama kubwa kuliko maelekezo ya Serikali

Anadai hiyo inawezekana ikatengenezwa mazingira ya Wanafunzi โ€˜kufelishwaโ€™ ili Chuo kiingize malipo mengi ya Sup

Pia, anadai mifumo ya uendeshaji taasisi hizo za Elimu ikiwemo usajili wa Wanafunzi, matokeo na utoaji vyeti hakuna utaratibu wa kueleweka na kwamba baadhi ya Vyuo vimeweka namba za mawasiliano katika matangazo na mitandao ya kijamii lakini namba zao hazipokelewi na nyingine hazipatikani

Soma https://jamii.app/VyuoVyaKati

#JamiiForums #Accountability
๐Ÿ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdau wa JamiiForums.com anasema tukio la Waamuzi kubughudhiwa na kunusurika kupigwa kama ilivyotokea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake kati ya Simba Queens na Mashujaa Queens, Mei 12, 2025, halitakiwi kuachwa kama lilivyo kwani ikiwa hivyo inaweza kutokea makubwa zaidi ya hapo

Anaeleza kuwa tukio hilo lililohusisha baadhi ya memba wa Benchi la Ufundi wa Simba Queens kuanzisha vurugu baada ya mchezo huo linaweza kuwa ni ishara kuna baadhi ya matukio ambayo sio mazuri yanayoendelea nyuma ya kamera

Mdau anasema kama mtu anaweza kufanya hivyo hadharani kukiwa na kamera, je Waamuzi ambao kawaida sio wazungumzaji katika Vyombo vya Habari, usalama wao upoje?

Soma https://jamii.app/WaamuziViwanjani

Video Credits: Tuzo Online

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema Sheria ya Tanzania inaeleza Mtanzania yeyote aliye nje ya mipaka akiwa na Hati ya Kusafiria (Passport) ni Mtanzania kama wengine lakini Diaspora ni yule ambaye ni Mzaliwa wa Tanzania anayeenda nje na kuukana uraia wake

Soma https://jamii.app/DiasporaUfafanuzi

#JamiiForums #Governance #Diplomacy
#TANZIA: Sifa Bujuni aliyeimba wimbo wa โ€œTanzania Inaelekea Wapi?โ€ yenye kionjo cha โ€œMnatuona Nyani tuโ€ amefariki Dunia hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Baba Mzazi wa Marehemu amethibitisha taarifo za kifo chake

Ikumbukwe, Septemba 13, 2023, Sifa na wenzake Wawili walikamatwa huko Isyesye - Mbeya wakidaiwa kuandaa wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa YouTube

Septemba 19, 2023, Sifa na wenzake Salome Mwampeta (Mwimbaji) na Mtayarishaji wa Wimbo huo, Hezekiel Millyashi George walipandishwa Mahakamani na kusomewa Shtaka la Kusambaza Taarifa za Uongo kwa njia ya Mtandao ambapo wote walikana na baadaye kesi yao kufutwa

Soma https://jamii.app/SifaAfariki

#JamiiAfrica #JamiiForums #FreedomOfExpression #Demokrasia #UhuruWaKujieleza
๐Ÿ‘1
DAR: Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa ajali ya treni ya Mjini kwenda Pugu, iliyotokea Stesheni ya KAMATA kwenye makutano ya reli na Barabara ya Kawawa, jana Mei 13, 2025 imejeruhi Watu 10

TRC imesema ajali hiyo iliyohusisha mabehewa 12 yaliyobeba abiria takribani 1,200 na kuwa Wataalamu wa Shirika na Timu ya Afya ya Shirika, walifika kutoa msaada wa huduma ya kwanza, waliojeruhiwa wawili ni Wanaume na nane Wanawake walikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Amana

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa TRC, Fredy Mwanjala amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo imesababisha mabehewa 6 kuathirika bado hakijafahamika lakini huduma ya usafiri wa treni ya Mjini kwenda Pugu inaendelea kama kawaida leo Mei 14, 2025

Soma https://jamii.app/TreniYaMjini

#JamiiForums #JFMatukio
๐Ÿ‘Ž1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mei 13, 2025 katika Ibada ya kumuaga aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Charles Hillary, Askofu Jackson Sosthenes (wa Kanisa la Anglikani - DSM), alizungumzia Matukio ya watu kuvamiwa, kutekwa na kuuawa, akisema wote wanaofanya vitendo hivyo, wanapora haki na Mamlaka ya Mungu ya kuchukua uhai wa binadamu

Zaidi https://jamii.app/MamlakaYaMungu

#JamiiForums #JamiiAfrica #SocialJustice #HumanRights #Accountability #Governance
๐Ÿ‘1
UHISPANIA: Nyota wa #RealMadrid, Rodrygo inadaiwa hana mpango wa kuendelea kuichezea Timu hiyo kutokana na nafasi anayocheza kutawaliwa na Jude Bellingham na Kylian Mbappe wanaopewa nafasi zaidi

Mtandao wa Marca umeeleza kuwa anataka kuondoka ili kwenda kutafuta sehemu nyingine atakayopata nafasi ya kucheza Mechi nyingi

Inadaiwa kilichomkera zaidi Rodrygo ni kitendo cha kutojumuishwa kwenye kikosi kilichocheza El Clasico (dhidi ya Barcelona), hivyo anajiona hana umuhimu

Soma https://jamii.app/RodrygoTransfer

#JamiiForums #JFSports #Michezo