JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UHISPANIA: Kipa wa #FCBarcelona, Wojciech Szczesny amesema anasubiri mwongozo wa Mkewe na Familia yake kabla ya kusaini Mkataba mpya wa kuendelea kubaki Klabuni hapo au kuondoka

Kipa huyo wa zamani wa Arsenal, alisajiliwa Oktoba 2024 ikiwa ni Mwezi mmoja tangu atangaze kustaafu akitokea Juventus, alipewa nafasi hiyo baada ya kipa chaguo la kwanza Marc-Andre ter Stegen kuumia goti

Szczesny na Luczenko walifunga Ndoa Mwaka 2016 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa Miaka mitatu, walikutana wakati akiwa anaichezea #Arsenal

Soma https://jamii.app/SzczesnyTransfer

#JamiiForums #JFSports #Michezo
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson aliyasema hayo jana, Mei 13, 2025 wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Kwanza, Cleopa David Msuya huko Usangi - Mwanga

Zaidi https://jamii.app/KwendaMbinguni

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa kichama wa Kinondoni, Henry Kilewo ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho na kueleza “Hatuendi kuanza upya, tunabadili Jukwaa.”

Akizungumza na Wanahabari, leo Mei 14, 2025, Kilewo ambaye pia ni Mwanachama wa Kundi la G-55 ndani ya chama hicho amesema “Chama kama kimepoteza mwelekeo wa Kiuongozi, kimepoteza mwelekeo wa kutovumiliana Kidemokrasia. Nimekubaliana na nafsi yangu kuwa dhana iliyonivutia kujiunga CHADEMA haipo tena.”

Soma https://jamii.app/G55Mei14

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍1
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema yeye pamoja na Viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi wametembelea Kivuko cha Mto Rajabu ambapo Awamu ya Kwanza imekamilika na wapo kwenye utaratibu wa kuanza Awamu ya Pili

#Gambo, kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii ameandika “Jana pamoja na Viongozi wa Chama tulitembelea Kivuko cha Mto Rajabu kwenye Kata ya Sakina. Kivuko hiki Awamu ya Kwanza imekamilika na sasa tupo kwenye utaratibu wa kuanza awamu ya pili! Kazi na Utu: Tunasonga Mbele”

Soma https://jamii.app/GamboKivuko

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Accountability #Uwajibikaji
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akiongelea mwenendo wa biashara na uwekezaji Nchini amesema taarifa ya 2022/23 kupitia Dirisha la Uwekezaji la Pamoja (One stop facilitation Centre) inaonesha kuwa miradi 240 ilisajiliwa, yenye thamani ya Trilioni 11.4, ambapo miradi 94 ni ya wageni, 89 Watanzania na 57 wabia

Ameeleza kwa mwaka 2023/24 maombi kwenye Tume ya Kugawa Ardhi kwaajili ya Uwekezaji yalikuwa 191 ambapo 130 yalikuwa ya Kampuni za wageni na 61 ya Watanzania hali inayoonesha wageni wanaongoza katika kupewa ardhi ya uwekezaji na uwekezaji kuliko Wazawa

Ameyasema hayo akichangia Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara Bungeni, leo Mei 14, 2025

Zaidi https://jamii.app/MpinaBungeniMei14

#JamiiForums #JamiiAfrica #Biashara #Uwekezaji #Uchumi
Raia wa Norway huwa na utaratibu wa kuwaacha Watoto wao nje iwe ni msimu wa joto au wa baridi kali kwa madai kuwa ni njia moja wapo ya Watoto hao wachanga kupata hewa safi na kujenga kinga dhidi ya Magonjwa kama Mafua na kikohozi

Utaratibu huu ukifanyika wakati wa baridi Watoto huvishwa nguo za joto na kuachwa kwenye Magari ya Kutembelea Watoto (Stroller) na mara nyingine hutumia Kipima Joto kufuatilia hali ya hewa

Mdau unaweza kumuacha mwanao nje kwenye baridi ili kuimarisha kinga yake dhidi ya Magonjwa ya Msimu wa Baridi?

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #ParentHood #Lifestyle
👍1
MANYARA: Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Joseph Nyamoko na Issa Masoud wamefariki Dunia baada ya kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama

Taarifa ya Jambo TV imeeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amesema tukio hilo limetokea katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro na kuwa mipango ya kusafirisha miili ya askari hao inaendelea kwa uratibu wa Jeshi la Polisi na Familia za wahusika

Aidha, Nyamoko na Issa kila mmoja ameacha Mke na watoto wawili

Soma https://jamii.app/RadiSimanjiro

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
😢6👍3
Tuchague kuwa watu wa kutafakari kabla ya kuzungumza. Tuchague kuchukua hatua zinazotokana na ukweli, si hisia, kwa sababu maneno yana nguvu na maamuzi yana athari

Pale kunapokuwa na sintofahamu, epuka kutoa hukumu bila kujiridhisha, kwani hukumu na maamuzi yasiyoangaliwa kwa makini yanaweza kuvunja zaidi kuliko kujenga

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha
👍1
ENGLAND: Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min (32) amefungua kesi Polisi dhidi ya Mwanamke ambaye alidai ana ujauzito wa staa wake akidai kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kupata fedha

Wanasheria wa Son wanadai Mdada huyo alitoa madai hayo Juni 2024 na akataka fedha ili anyamaze, wiki iliyopita Son akaamua kufungua mshtaka kwa kuamini mtu huyo alikuwa na lengo la kumlaghai ili ajipatie fedha

Son hana mke wala Mtoto anayetambulika na aliwahi kunukuliwa akisema “Baba alisema unapooa kipaumbele cha kwanza ni familia, mke na Watoto kisha soka. Nataka kuhakikisha nitaendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu, nikistaafu ndio nitaanza kutafuta Watoto.”

Soma https://jamii.app/SonBlackmail

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa wito kwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kurejea kumbukumbu za Bunge kuona taarifa za utekaji zilishawahi kuwasilishwa Bungeni Mwaka 2018 na hazikufanyiwa kazi

Amesema hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alivyowasilisha hoja kuhusu uwepo wa matukio ya utekaji na mauaji nchini na kuomba Bunge kusimama kwenye nafasi yake katika kuisimamia Serikali ili kuhakikisha matukio hayo yanakoma

Soma https://jamii.app/PondaUtekajiMei14

Video Credits: Jambo TV

#JamiiForums #HumanRights #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau anadai baada ya malalamiko ya Mwananchi yaliyotolewa Machi 16, 2025 kupitia JamiiForums.com kuhusu Wakazi wa Chanika Zingiziwa kutokuwa na huduma ya umeme, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilifika na kuweka miundombinu kadhaa ikiwemo Nyaya na Nguzo

Anaeleza Wananchi waliamini kadhia ya kukosa umeme inaondoka lakini anadai TANESCO hawakufunga transfoma, hivyo huduma haikuunganishwa na hata mchakato wa kujiandikisha kuunganishiwa umeme haujafanyika na kwamba wanapouliza mamlaka hiyo hawapati majibu sahihi

Mdau anahoji “Transfoma zitakuja lini na mbona hakuna maelezo yaliyonyooka? Inakuwa kama umeme ukifika tutapewa bure, tunapata hasara nyingi kwa kutokuwa na huduma hiyo"

Soma https://jamii.app/UmemeZingiziwa

#JamiiAfrica #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Susan Kiwanga aliyekuwa Mbunge Jimbo la Mlimba 2015- 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa Miaka 20, akitangaza kujiondoa katika Chama hicho Mei 13, 2025, ametaja miongoni mwa sababu zilizomfanya aingie kwenye Kundi la G-55 ni Kaulimbiu ya 'No reforms, No election' kufanywa azimio la Chama

Soma https://jamii.app/KaulimbiuChama

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #Governance
KENYA: Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema Chama chake kiitwacho 'Democracy for the Citizens Party (DCP)' kinalenga ujumuishaji na kina Wanachama wa makundi yote wakiwemo #GenZ

Gachagua pia alitaja Viongozi wa Chama hicho wakiwemo David Mingati (Mwenyekiti), Cleophas Malala (Naibu Kiongozi wa Muda wa Chama) na Cate Waruguru (Kiongozi wa Wanawake)

Aidha, Gachagua ametangaza kuwa Chama hicho kitazinduliwa rasmi Juni 4, na baadaye ataanza ziara ya Miaka Miwili kote nchini kueneza Sera za chama na kuomba uungwaji mkono. Pia, amewataka wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa 2026 kupitia Chama hicho kuanza kujisajili

Soma https://jamii.app/ChamaKipyaGachagua

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Demokrasia
👍1🔥1
GEITA: Wanafunzi wa Shule ya Msingi Rubambangwe na Sekondari ya Rubambangwe, Kitongoji cha Iyozu, Kata ya Muungano Wilayani Chato wanatumia mitumbwi kutoka katika makazi yao kisha wanatembea umbali wa zaidi ya Kilometa 4 ili kufika katika Shule

Akielezea changamoto hiyo, Diwani wa Kata ya Muungano, Charles Kapembe amesema amewasilisha maoni ya Wananchi hao kwenye vikao halali vya Baraza la Madiwani na tayari amezungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa ajili ya utatuzi

Mkurugenzi wa Halmashauri, Mandia Kihiyo alipoulizwa amesema Halmashauri inakusudia kuchonga mtumbwi wenye thamani ya Tsh. Milioni 2 kupunguza adha ya Wananchi kuvuka na watakapopata pesa watajenga Daraja la kudumu

Soma https://jamii.app/IyozuChato

#JamiiForums #Accountability #Elimu
👍1