JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, #TunduLissu amefikishwa Mahakama ya Kisutu baada ya kuhojiwa na Ofisi ya Upelelezi Kanda Maalumu, ambapo Mkurugenzi wa Sheria #CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi alinukuliwa akisema anatuhumiwa kwa tuhuma za Uhaini na kutoa taarifa za uongo

Taarifa zaidi ya kinachoendelea Mahakama zitafuata

Soma https://jamii.app/LissuKisutuApr10

#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #TunduLissu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la Uhaini

Lissu amefikishwa Mahakama hiyo leo Aprili 10, 2025 na kusomewa shitaka hilo huku kesi ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025

Ikumbukwe Lissu alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/KesiLissuKuhairishwa

#JamiiForums #HumanRights #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Usafiri wakiwemo wamiliki wa malori, Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania na Mawakala wa Forodha Wilayani Tunduma wamedai changamoto ya foleni iliyopo mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma inatengenezwa na Watu kwa maslahi yao binafsi

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo amesema ameunda Kamati Maalumu kuchunguza na kubaini sababu kwa kuwa suala hilo limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara

Ikumbukwe, Oktoba 1, 2023, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Serikali ina mkakati gani wa kuondoa foleni ya malori Tunduma”, pia Mei 31, 2025, Mdau mwingine aliandika “Mifumo ya Kikodi katika Mpaka wa Tunduma ni tatizo, inasababisha foleni kubwa. Kwanini Tanzania haitumii mfumo sawa na Zambia?”

Soma https://jamii.app/TundumaFoleni

#Accountability #Uwajibikaji #JamiiForums #ServiceDelivery
Kwa kutoa taarifa za ukweli na kuandika Habari bila Upendeleo, Vyombo vya Habari hufungua Macho ya Wananchi na husababisha shinikizo kwa Viongozi na Taasisi kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya kifisadi

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
UCHUMI: Mwaka 2024, bidhaa kubwa zilizouzwa kutoka Marekani kwenda China zilikuwa Maharage ya Soya – ambayo hutumika hasa kulisha Nguruwe Milioni 440 Nchini China. Marekani pia ilisafirisha Dawa na Mafuta ya Petroli kwenda China

Kutoka China kwenda Marekani, kulikuwa na wingi wa Vifaa vya Kielektroniki, Kompyuta na Vitu vya Kuchezea (Toys). Idadi kubwa ya Betri, ambazo ni muhimu kwa Magari ya Umeme, pia zilisafirishwa kutoka China.

Aidha, wakati Maumivu ya Ushuru yakitarajiwa, China imetoa msamaha wa Ushuru kwa Asilimia 100 kwa Nchi 33 za Afrika kwa Bidhaa zao zote zinazoingia kwenye Soko la Nchi hiyo.

Fahamu zaidi https://jamii.app/TrumpvsChinaTZ

#JamiiForums #Tariffwar #TrumpRecession #TrumpTariffs
1
DAR: Mshereheshaji, Anthony D. Luvanda akihojiwa na Clouds FM Machi 18, 2025, alisema Tasnia hiyo imekuwa ikivamiwa na Watu wengi ambapo wapo wanaofanya vitu kinyume cha Sheria na kukiuka faragha za Watu kwa kuchapisha picha na video ambazo zinadhalilisha Utu

Soma https://jamii.app/NukuuLuvanda

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka hususani TAMISEMI kufuatilia changamoto iliyopo katika Shule ya Misingi Kitonga, Ilala ya Wanafunzi kuwa wengi kuliko Miundombinu ili kuona namna bora ya kuitatua na kupunguza msongamano wa Wanafunzi

Aidha, Mdau anadai Wanafunzi wengi wamekuwa wakipata changamoto kufika Shuleni hasa kipindi cha Mvua kutokana na Miundombinu mibovu ya Barabara inayotumika kuelekea kwenye Shule hiyo

Soma https://jamii.app/KitongaShule

#JamiiForums #Accountability #Elimu #Governance
RUVUMA: Mdau anadai uchakavu wa madarasa katika Shule ya Msingi Lipepo, Kata ya Nalasi, Tunduru Kusini umesababisha Wanakijiji kujichanga na kuanza ujenzi wa Darasa 1 lakini nguvu zao ziliishia njiani, wakaahidiwa kuongezewa nguvu na Kiongozi wao lakini hilo halijatimia

Mdau ametoa wito kwa Wadau mbalimbali na Serikali kuwasaidia kuboresha Vyoo na kuwajengea miundombinu mipya ya Madarasa

Soma https://jamii.app/ShuleYaLipepo

#JamiiForums #ServiceDelivery #PublicHealth #Elimu
ENGLAND: Hatimaye Mshambuliaji, #MohamedSalah amesaini mkataba mpya kuendelea kubaki Liverpool kwa mshahara wa Pauni 350,000 (Tsh. Bilioni 1.2) kwa wiki baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu suala la Mkataba wake ambao ulitarajiwa kumalizika Juni 2025

Baada ya kusaini amesema “Nimefurahi, tuna timu nzuri, tuna nafasi ya kushinda mataji mengine, nimecheza hapa kwa Miaka Nane, naamini nitatimiza Miaka 10.”

Salah (31) amefunga Magoli 243 katika mechi 394 alizoichezea Liverpool, msimu huu katika #PremierLeague amefunga Magoli 27 na Asisti 17

Soma https://jamii.app/SalahContract

#JFSports #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Naibu Katibu Mkuu Bara – (CHADEMA), Amani Golugwa akizungumza na Wanahabari leo, Aprili 11, 2025 akiwa Makao Makuu ya Chama Mikocheni amesema Chama chake hakijawahi kutoa tishio la kutaka kuipindua Serikali wala kutishia maisha ya Rais

Soma https://jamii.app/CHADEMAAprili11

Video Credits: Ipanda Online TV

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
JF KUMBUKIZI: Mdau ukiona picha hii unakumbuka wapi?

#JamiiForums #JFKumbukizi #JFChitChats
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehoji ukimya wa Mamlaka za Serikali kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya #CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla aliyedai CHADEMA inachangisha fedha kwenda kununua Virusi vya Ebola na Mpox

Hoja hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Bara – CHADEMA, Amani Golugwa leo, Aprili 11, 2025 alipozungumza na Wanahabari, akizitaka Mamlaka kuchukua hatua kwa kuwa kauli hiyo inaichafua Nchi katika Sekta mbalimbali

Soma https://jamii.app/CHADEMAAprili11

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Naibu Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuelewa lugha za Kisiasa zinazotumika kwa kuwa nyingine hazimaanishi vile zinavyotamkwa, amesema hayo leo Aprili 11, 2025 alipozungumza na Wanahabari

Soma https://jamii.app/CHADEMAAprili11

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Hii ni moja ya 'comments' kwenye Mjadala uliopo JamiiForums.com ambao unasema Watanzania wengi wanaishi kwa mazoea kwa kuendelea kuwachekea Viongozi wanaolitia Taifa hasara bila kutambua kuna kundi la Wachache wanaotumia Nguvu ya wengi kujifaidisha

Nawe unaweza kushiriki Mjadala huu hapa https://jamii.app/WatzTuacheMazoea

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Democracy #KuraYakoSautiYako
👍2