JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kuna mambo mengi huwa tunapitia na kupambana kuweka sawa. Muda mwingine hakuna anayejua wala kutambua kuwa unapambana

Usikate tamaa endelea kupambana na kuweka mambo sawa kwani baada ya muda utaona matokeo

#JamiiForums #LifeTips #MorningQuote #AmkaNaJF
🔥3
Andiko hili la Stories of Change linatoa mapendekezo ya kushughulikia Changamoto kadhaa ambazo Watu hukutana nazo kwenye Tovuti mbalimbali za Taasisi za Umma na wakati mwingine walipopiga Simu kwa Wahusika Mpokeaji wa Simu hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na Utendaji Kazi wa tovuti hizo

Soma https://jamii.app/TovutiUmmaSOC23

#JamiiForums #SOC2023 #ICT #TEHAMA #DigitalWorld #SerikaliMtandao
1👍1
Mdau ndani ya JamiiForums.com anadai kila akijaribu kufanya maendeleo kwa Wazazi anashindwa kutokana na pesa alizochanga kuishia kwenye mambo ya ovyo bila yeye kujua

Unamshauri nini Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/RohoYaUmaskini

#JamiiForums #LifeStyle #LifeTips
MICHEZO: Hizi ni kauli zilizotolewa na Mshambuliaji wa Al-Ittihad, #KarimBenzema (37) pamoja na mstaafu Ronaldo Luís Nazário de Lima (48) kwa wakati tofauti, wakijibu hoja ya #CristianoRonaldo (40) anayeichezea Al-Nassr aliyoitoa Februari 2025, akijielezea kuwa yeye ndiye Mchezaji Bora wa Muda Wote kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye mchezo wa soka

Soma https://jamii.app/NukuuSoka

#JFSports #JFNukuu #JFQuote #JamiiForums
👍21
#Demokrasia haiwezi kuwepo bila Uhuru wa Watu kutoa maoni yao, hata kama yanapingana na Mawazo ya wengi au ya Watawala

Haki ya kutokubaliana ni msingi wa mijadala yenye Afya, ambapo mawazo tofauti yanakutana, na mwelekeo bora kwa Jamii unatengenezwa.

#SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyMatters #FreedomOfSpeech #HumanRights
Mashirika, Taasisi na Watu Binafsi wametakiwa kuwa makini wanapotumia Taarifa Binafsi za Watu, kwani kufanya hivyo bila idhini ya mhusika au Wahusika ni kinyume cha Sheria na adhabu yake kwa Mchakataji wa Taarifa (Mtu au Taasisi) inaweza kufika hadi Faini ya Tsh. Milioni 100

Mkurugenzi wa Tafiti za Ulinzi wa Taarifa na Teknolojia wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Noe Nnko amesema faini hiyo ipo Kipengele cha 47 cha Faini za Kiutawala kinachoeleza Tume inaweza kuchukua hatua ya kutoza faini na kiwango cha juu hicho.”

Ameongeza "Taasisi zinapaswa kuwa na Afisa wa Taarifa Binafsi aliyefundishwa kutunza taarifa za Watu kwa usahihi. Mbali na faini pia kuna fidia kwa mwathirika itakayopimwa kulingana na madhara atakayopata ya kifaragha.”

Soma https://jamii.app/FineDataPrivacy

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
👍21
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Taifa, Tundu Lissu amesema “Mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo wa Rais, ambao unadhibitiwa kutoka juu mpaka chini ya Rais na mnafahamu Rais wa nchi hii ni Mwenyekiti wa CCM, na Marais wa CCM wametumia udhibiti wao wa mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kwamba CCM inabaki madarakani kwa njia zozote, nyingi haramu"

Ameongeza “Bila mabadiliko hakuna uchaguzi na siyo bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi, hiyo siyo lugha yetu, lugha yetu ni bila mabadiliko uchaguzi hautafanyika, ndiyo lengo letu”

Ameyasema hayo leo Machi 2, 2025 wakati wa mkutano wa CHADEMA na Jukwaa la Wahariri (TEF) katika Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/CHADEMAHatususiUchaguzi

#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu25 #Democracy
👍2
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kuwa kimepokea kwa masikitiko taarifa za kutekwa kwa Wananchi wawili (Dar es Salaam na Kigoma) katika mazingira yanayotia shaka na kudai matukio hayo yanatoa picha ya wazi kuwa Jeshi la Polisi linahusika moja kwa moja au linashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda raia na mali zao

Taarifa ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Dahlia Majid Hassan imesema “Tumepokea taarifa kuwa Februari 28, 2025, Method Damian Kumdyamka (45) alitekwa nyumbani kwake Sinza, Dar na watu wanane waliokuwa na silaha na gari aina ya Prado. Licha ya familia yake kutoa taarifa na kutembelea vituo vyote vya Polisi Dar, hajapatikana kwa siku 3 sasa.”

Soma https://jamii.app/ACTUtekajiMachi2

#JFMatukio #HumanRights #Accountability #JamiiForums
👍1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons