JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Wahalifu mtandaoni hutumia njia mbalimbali za udanganyifu ili kufanya utapeli kwa kukusanya taarifa binafsi au kuingilia faragha za watu

Mojawapo ya mbinu maarufu ni kutuma viungo (links) visivyojulikana au visivyoaminika kupitia barua pepe, ujumbe au kwenye mitandao ya kijamii

Ikiwa utabonyeza kiungo (link) hicho, inaweza kukupeleka kwenye akaunti za udanganyifu zinazokusudia kupata taarifa kama nenosiri

Soma https://jamii.app/MlinziTaarifaZako

#JamiiForums #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka husika kufuatilia mfumo wa Maegesho wa TeRMIS (termis.tamisemi), anadai unaonesha madeni ambayo sio halisi hali inayowaumiza wanaokutwa na kadhia hiyo

Soma https://jamii.app/UpigajiHelaTeRMIS

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka za Usalama kushughulikia changamoto ya vibaka wanaojeruhi na kupora maeneo ya Kibaha kwa Mfipa kwani isipochukuliwa hatua madhara yanaweza kuendelea kuwa makubwa ikiwemo Watu kupoteza maisha

Soma https://jamii.app/VibakaKuporaKibaha

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
DODOMA: Jeshi la Magereza limetakiwa kusimamia mpango wa kuwapa ujuzi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wafungwa wanapokuwa Gerezani na watakaohitimu watunukiwe vyeti vinavyotambuliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea wanaporudi Mtaani

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ambaye amesema “Wale wanaoingia Gerezani bila kuwa na ujuzi kabisa, muangalie namna ya kuwapa ujuzi ili wanapotoka waweze kujikimu kimaisha.”

Bashungwa amesema hayo Februari 14, 2025 alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Magereza na kuzindua Mabasi Saba ya kusafirisha Maabusu

Soma https://jamii.app/WafungwaVeta

#HumanRights #Governance #JamiiForums
👍1
Mdau wa Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu Wanawake wanaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua

Mdau hii ni sahihi? Yapi maoni yako?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WanawakeKujengaSiri

#JamiiForums #LifeStyle #JFMdau2025
👍1
#DIPLOMASIA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahamoud Ali Youssouf ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya #RailaOdinga kutoka Kenya ambaye alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki

Uchaguzi huo uliofanyika nchini Ethiopia, Odinga alishinda duru mbili za kwanza lakini akapoteza duru katika tatu zilizofuata kwa kupata kura 20 huku Mahamoud akishinda kwa kura 23

Aidha, Mahamoud atarithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti Moussa Faki Mohamed ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa Chad anayetarajia kumaliza muhula wake wa pili wa Uenyekiti wa #AU mapema Mwaka 2026

Soma https://jamii.app/MohamoudMwenyekitiAU

#JamiiForums #ChairpersonAU #Diplomasia
👍2
MIUNDOMBINU: ACT Wazalendo kimesema kauli ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kuwa uwekwe utaratibu wa kulipia matumizi ya Barabara ya Mwendokasi kwa wanaokwepa foleni, ni ushahidi jinsi Serikali inavyokosa huruma kwa Wananchi wake na kukosa uwajibikaji kwa maslahi ya Wananchi

ACT imesema mradi huo ulijengwa kwa fedha za Walipa Kodi wa Tanzania, hivyo ni haki ya kila Mwananchi kuutumia bila vikwazo vya gharama na kuwa kufanya hivyo ni ubaguzi wa wazi wa kiuchumi ambapo wasio na uwezo wa kumudu gharama watalazimika kubaki kwenye foleni

Mhandisi Mohammed Mtambo, Waziri Kivuli wa Miundombinu (ACT) amesema “Barabara hiyo ni mali ya umma na haitakiwi kuwa biashara ya kuwanufaisha wachache, Serikali ina wajibu wa kuhakikisha huduma za usafiri wa umma zinabaki kuwa nafuu na kupatikana kwa wote na Serikali ikiona kuna uhitaji huo ‘Express toll road’ au iruhusu sekta binafsi ijenge.”

Soma https://jamii.app/ACTBarabara

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
1👎1
Uongozi bora haujengwi kwa kununua dhamira za watu bali kwa kusimamia maono, uadilifu na kujitoa kwa maendeleo ya taifa.

Wanaonunua uongozi kwa pesa mara nyingi wanakuwa dhaifu mbele ya changamoto, wanatanguliza maslahi binafsi badala ya wananchi na wanahakikisha mfumo wa rushwa unazidi kustawi

Tusikubali siasa za kununua uongozi, tusimame imara kwa uwajibikaji na uadilifu. Jamii bora inaanza na uchaguzi wa Viongozi sahihi

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) - Singida, Sipha Mwanjala ametoa ripoti ya miradi (Oktoba - Desemba 2024) na kubaini ukiukwaji wa Sheria katika miradi inayotekelezwa Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Singida

Amesema baada ya #TAKUKURU kufanya uchunguzi na kubaini kasoro hizo, fedha zote za Kodi ya Zuio na Kodi ya Huduma ambazo zilikatwa lakini hazikupelekwa zilirejeshwa na wahusika na kupelekwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (#TRA) na Halmashauri husika

Soma https://jamii.app/RipotiTAKUKURU

#JamiiForums #Accountability #Governance #KemeaRushwa25
1