JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Je, ni sahihi kwa Mgombea kutoa fedha, mahitaji ya kijamii au misaada mingine kwa wapiga kura? Ni sehemu ya Kampeni au mbinu za kushawishi Wapigakura kinyume cha maadili ya Uchaguzi? Sheria inasemaje? Jamii ina uelewa?

Kuelewa masuala haya kutamwezesha kila Mwananchi kufanya maamuzi sahihi na kushiriki katika uchaguzi kwa uelewa mpana

Usikose kushiriki katika mjadala huu muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kujifunza au kutoa maoni yako, leo, Februari 13, 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kujiunga, bofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mdau kuwa makini unapoweka taarifa zako binafsi hadharani kwani unahatarisha usalama wako ikiwa zitafika mikononi mwa watu wenye nia mbaya na wakazitumia vibaya taarifa hizo

Soma https://jamii.app/MlinziTaarifaZako

#JamiiForums #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Mbunge wa Viti maalum, Ester Bulaya amekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Freeman Mbowe na Mwenyekiti mpya Tundu Lissu kwa Uchaguzi Huru na wa Haki

Bulaya amesema "Tundu Lissu anao uwezo wa kukiongoza Chama cha CHADEMA na kukifikisha kwenye Demokrasia ya kweli"

Ameyasema hayo akiwa Bungeni leo, Februari 13, 2025 wakati akichangia Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Jijini Dodoma

Soma https://jamii.app/UwezoLissuCHADEMA

#JamiiForums #Governance #Democracy
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#SIASA: Kauli ya Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba inakuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya kusema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anao uwezo wa kukiongoza chama hicho na kukifikisha kwenye Demokrasia ya kweli

Mwigulu ameyasema hayo tarehe 13 Februari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)

Soma https://jamii.app/LissuHatoshiCHADEMA

#JamiiForums #Governance #Democracy
Mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?" upo hewani muda huu kupitia X Spaces ya JamiiForums na utafanyika hadi Saa 2:00 Usiku

Wazungumzaji Wakuu katika mjadala ni Joseph Kasongwa Mwaiswelo (Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU), Dkt. Ananilea Nkya (Mwenyekiti wa Bodi – JUKATA), Zitto Kabwe (Mwanasiasa ACT Wazalendo) na Wakili Maduhu William (LHRC)

Shiriki kuimarisha #Demokrasia yetu kwa kusikiliza, kutoa maoni, mapendekezo au kuuliza maswali

Kushiriki, bofya hapa: https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akizungumza katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?" Wakili kutoka LHRC, William Maduhu, amesema suala la kutoa zawadi wakati wa Uchaguzi ni suala mtambuka, Miaka ya nyuma ilikuwa desturi kwa Mgombea yeyote kutoa zawadi kwa Wapigakura au Wananchi

Ameongeza “Mwaka 2005, LHRC ilitoa changamoto kuhusu suala hilo Kisheria Mahakamani, ndipo Mahakama Kuu ikaeleza kuwa kutoa takrima ni sehemu ya kushawishi Wapigakura. Baada ya hapo yakafuata mabadiliko ya Sheria yaliyoondoa vitu vinavyoweza kuchangia ushawishi kwa Wananchi wakati wa Uchaguzi”

Wakili Maduhu amesema pamoja na uwepo wa Sheria kadhaa kupinga viashiria vya Rushwa Nchini lakini matukio ya Wagombea au watia nia kuendelea kutoa zawadi kwa Wapigakura bado yapo

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Wakili (LHRC), William Maduhu amesema Mwaka 2020, TAKUKURU iliwakamata baadhi ya Wagombea kwa kuwa na dalili za kutoa #Rushwa, baadaye Hayati Rais Magufuli akasema mhusika aliyekamatwa alikuwa na sherehe ya kuzaliwa, hiyo ikachangia TAKUKURU kumuachia mtuhumiwa aliyekamatwa. Imekuwa ikionekana Wanasiasa wana nguvu ya kupindisha vitu vinavyoashiria suala la Rushwa ”

Ameongeza kwa kusema eneo la rushwa ni suala gumu kwa kuwa kuna malalamiko mengi na matukio ya zawadi kutolewa kwa wapigakura lakini bado TAKUKURU imekuwa haichukui hatua na ikitokea wametoa tamko la kuwakamata watuhumiwa wa rushwa huwezi kuona nini kinaendelea baada ya hapo

Wakili Maduhu amesema “Nadhani ni vizuri TAKUKURU wakasema kwanini wanaonekana kutokuwa na Meno makali dhidi ya Wanasiasa au wana hofu kuwa wanapoingia Madarakani wanaweza kuwa mabosi wao”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akichangia katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?", Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma (TAKUKURU), Joseph Kasongwa amesema “Tunapopokea tuhuma zozote za Rushwa iwe wakati au kabla ya Uchaguzi, inapobainika hivyo suala hilo lazima tulifikishe Mahakamani”

Amesema kuhusu suala la kutangaza Watuhumiwa wa #Rushwa kwanza huwezi kutangaza kila hatua za Kimahakama na kuna kulinda Heshima ya Mtu kwa kuwa hizo bado ni tuhuma na huwa kuna mchakato wa uchunguzi

Ameongeza kuwa Sheria ya #Rushwa haijatoa nafasi kwa TAKUKURU kumchukulia Mtu hatua za Kinidhamu hivyo inapotokea chochote huwa sheria inafuatwa kwa kufika Mahakamani na sio kumchukulia Mtu hatua za kinidhamu

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma (TAKUKURU), Joseph Kasongwa, amesisitiza Elimu kutolewa kwa Wananchi ili wanapotoa taarifa kuhusu Rushwa basi wawajibike pia kwa kutoa ushirikiano zaidi

Amesema “Sheria ya Rushwa kwa sasa imetuongezea wigo mpana sana, tutafika hadi kwenye Michezo, Bonanza na hata kwenye masuala ya urembo mfano mashindano ya Miss Tanzania”

Amesema “Tunapopokea tuhuma kwetu hiyo ni sehemu ya Jinai, jambo la msingi ni kuona kama kuna nia ovu inayoambatana na zawadi hiyo. Lakini kama inatoka kama Zawadi bila kuwa na nia yoyote nyuma yake hiyo inakuwa haina madhara”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akizungumza katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?", Mwenyekiti wa Bodi (JUKATA), Dkt. Ananilea Nkya, amesema “Suala la Rushwa kabla ya Mwaka 2005, Rushwa ilikuwa inafanyika waziwazi kwa kutumia jina la Takrima ikiwa ni kama Zawadi ya waziwazi. Baadaye Sheria ikasema hiyo siyo Zawadi bali ni Rushwa, lakini mtazamo wangu ni kuwa Rushwa imeongezeka kuliko ilivyokuwa awali ”

Ameongeza kuwa “Watu wengi wanailaumu TAKUKURU, Mimi nasema tusiwalaumu wao kwa kuwa zamani Rushwa ilitolewa waziwazi kwa jina la Takrima tofauti na sasa ambapo inafanyika kwa usiri mkubwa”

Amesema zamani Rushwa ilikuwa inaweza kutolewa kwa njia ya Chakula, Nguo au kitu kingine chochote cha kuwahadaa Wananchi lakini sasa hivi Rushwa inatolewa kwa ukubwa zaidi na kwa kificho kiasi kwamba TAKUKURU ni ngumu kuweza kumkamata Mtu sababu mambo mengi yanafanyika gizani

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akizungumza katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?", Mwanasiasa (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema “Hakuna anayeweza kubisha kuwa kuna matumizi makubwa ya Fedha katika Chaguzi zetu kiasi kwamba ni jambo gumu kutofautisha Rushwa na Zawadi nyakati za Uchaguzi na hasa katika Mwaka wa Uchaguzi”

Ameongeza kuwa “Hali ya Rushwa sio tu kwa Wanasiasa bali pia hata kwa Dola, ndio maana nyakati za Uchaguzi unaweza kukuta Viongozi wakubwa wakitoa ahadi ambazo zinaweza kutafsiriwa au kutumika kama sehemu ya ushawishi wa nguvu zao kuelekea kwa Dola”

Amesema unaweza kukuta Mgombea ni Rais au Waziri anaweza kutumia nafasi yake wakati wa Kampeni za Uchaguzi kutoa maelekezo ya kimamlaka na hivyo kutumika kama sehemu ya ushawishi wakati ni jambo ambalo halitakiwi kufanyika hivyo

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akichangia katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?", Assenga Kimaro (Mdau) amesema “Suala sio zawadi, bali kitu kinachotolewa kwa Wananchi wakati au kuelekea katika Uchaguzi kwa asilimia zote hiyo ni Rushwa, sababu Wananchi wao hawatoi ila wanapokea kutoka kwa Wagombea au Watiania”

Amesisitiza “Tunasema ni zawadi kwa Wananchi, Mgombea anawapongeza nini Wananchi? Hiyo ni Rushwa ila tu inatumika katika jina tofauti”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Wakili William Maduhu (LHRC) amesema “Kuna wakati Viongozi wanatumia Madaraka yao kutoa ahadi na kutoa vitisho kwa Wananchi kuwa hawatakiwi kuwachagua wapinzani wakati wa Uchaguzi lakini huwezi kuwasikia TAKUKURU wakiingilia kati hapo”

Amesisitiza kwa kutolea mfano Wabunge wa sasa waliopo Madarakani wanaenda kwenye Majimbo kutoa vitu mbalimbali ikiwemo Pikipiki, Baiskeli n.k. lakini watia nia wengine wakienda kufanya hivyo TAKUKURU wanawakamata

Ameongeza kuwa “Inavyofanyika ni kuwa Mbunge ambaye ana nia ya kugombea tena akifanya hivyo ni sawa lakini yule mwenye nia ya kugombea yeye akifanya hivyo anaambiwa anatoa Rushwa

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Wakili (LHRC) William Maduhu amesema “Pamoja na yote kuna kawaida ambayo inachangia Rushwa, Wananchi tumewageuza Wabunge kuwa ATM”

Amechangia mjadala huu kwa kusema kuwa Mtu akiwa na shida anamfuata Mbunge kumuomba msaada, hivyo Mwananchi wa aina hiyo akipewa zawadi baadaye lazima ashawishike

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mwanasiasa (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema “Wakati wa Kura za maoni za CCM huwa ni kawaida kuwasikia sana TAKUKURU lakini baada ya hapo huwezi kuwasikia tena”

Ameongeza kwa kusema “TAKUKURU ni kama wanakuwa na jukumu la kudhibiti Rushwa ndani ya CCM lakini huwaoni wakati wa Uchaguzi Mkuu, hata unapotoa taarifa kwa Mamlaka nyingine za Usalama, inachukuliwa kawaida kwa maana hakuna anayechukua hatua”

Amesema kuwa kwa sasa sio mjadala tena kuwa kuna Rushwa au hakuna wakati wa Uchaguzi, inajulikana kinachoendelea

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
👍1
Mwenyekiti wa Bodi (JUKATA), Dkt Ananilea Nkya amesema “Rushwa imetokana na Wananchi kutoamini mifumo ya Uchaguzi, wanaona bora wachukue hela kwa kuwa wanaowachagua wakifika kwenye Uongozi wanaenda kuchukua hela nyingi, hivyo nao wanachukua chao mapema”

Ameongeza kuwa “Kupunguza Rushwa katika Uchaguzi tunatakiwa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, hapo namaanisha ni Tume ambayo haichaguliwi na Rais aliyepo Madarakani, inatakiwa iwe inajitegemea na hata upatikanaji wa wafanyakazi uwe wa tofauti na ulivyo sasa”

Amesema kuwa “Sasa hivi Mgombea anaweza kuwa hata na Tsh. Milioni 500 katika Uchaguzi na akakwama kushinda. Sasa hivi wale waliopo Madarakani na wana nia ya kugombea ndio wanakuwa na hela nyingi na nguvu pia”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Akichangia mjadala Mwenyekiti wa Bodi (JUKATA), Dkt Ananilea Nkya amesema “Tuliona katika Uchaguzi uliopita kuna Kiongozi aliyekuwa Madarakani yeye ndio alikuwa anaamua nani ashinde”

Amesema Wagombea wanapitishwa na wenye Mamlaka kwa kuangalia “Huyu yupo karibu na mimi”, Huyu atanihoji maswali mengi” n.k. Yote hayo yanatokana na kuwepo kwa Mifumo mibovu ya kuchagua Watu

Amesema kuwa “Tukiendelea hivi tutakuja kujutia kwa kuwa kunaweza kuwa na hatari kubwa zaidi, ninakubaliana na wale wanaosema 'No reform No election'”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mwanasiasa (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema jamii ikiamua kudhibiti Rushwa inawezekana, wakati wa Uchaguzi wa Chama kimoja Rushwa ilidhibitiwa sana, baadaye uchaguzi wa Vyama vingi matumizi ya Fedha hayakuwa makubwa lakini kadiri Miaka inavyoenda matumizi ya Fedha yanazidi kuongezeka

Ameongeza kwa kusema “Ni lazima tuwe na Katiba imara ambayo inaweza kukataa mifumo na njia za Rushwa. Tunapokuwa na Chaguzi ambazo mtu mmoja anakuwa na nguvu ya kumpitisha Mgombea fulani kutokana na nafasi yake itakuwa ngumu kudhibiti Rushwa”

Amesema kuwa #Rushwa ya Uchaguzi ndio inazaa Rushwa nyingine na kukosekana kwa Uwajibikaji, kwani Kiongozi akishafanya hivyo akashinda lazima atatafuta namna ya kurejesha Fedha alizozipoteza awali

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma (TAKUKURU), Joseph Kasongwa amesema kuwa #Rushwa ni tabia, kwenye Uchaguzi Rushwa inapotolewa pande zote zinakuwa na furaha, hiyo imechangia kuwa changamoto kumpata Mtuhumiwa

Ameongeza kwa kusema “ Imefika hatua hatuoni kama Rushwa ni adui, hiyo inachangia ugumu wa kupambana nayo, mfano wakati Tanzania ikipambana na Idd Amini, Watanzania wote tulikuwa kitu kimoja, lakini kama wote tukiwa hatuna mtazamo sawa ni vigumu kuizuia Rushwa”

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
2👍1
Rushwa ya uchaguzi inawafanya viongozi waliochaguliwa kwa njia isiyo halali kutowajibika kwa Wananchi, kupuuza mahitaji ya msingi kama elimu, afya, miundombinu na ajira na badala yake kujikita katika kulinda maslahi yao binafsi

Matokeo yake ni ufisadi, ukosefu wa maendeleo na maisha magumu kwa Wananchi wa kawaida. Kataa kununuliwa. Chagua kiongozi kwa misingi ya uwezo, maadili na dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa wote.

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji