Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amethibitisha kuwa miili mitatu imetolewa chini ya Lori lililoanguka katika eneo la Kimara Stop Over mpaka kufikia majira ya saa 9 Usiku wa kuamkia leo (Februari 14, 2025)
Pia, Bodaboda sita zimetolewa chini ya Lori hilo ambalo liliacha njia na kuparamia Abiria na Madereva wa Bodaboda waliokuwa pembezoni mwa Barabara
Chalamila amesema walifanikiwa kulinyanyua Lori kwa zaidi ya asilimia 95% na taarifa zaidi za Ajali hiyo zitaendelea kutolewa na Jeshi la Polisi
Soma https://jamii.app/AjaliLoriStopOver
Video Credits: Clouds TV
#JamiiForums #JFMatukio

👍1
MBEYA: Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kueleza kukerwa na vifusi vilivyomwagwa na TARURA tangu mwaka 2024 katika Barabara ya Sangu kwenda Benki Kuu, vifusi hivyo vimeanza kusambazwa Februari 12, 2025
Mdau alidai vifusi hivyo vimesababisha changamoto ya usafiri kwa kufanya barabara hiyo kuwa nyembamba na kusababisha usumbufu kwa wanaopita na magari
Soma https://jamii.app/VifusiKusambazwaMbeya
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii #JFMdau2025

KILIMANJARO: Mdau wa JamiiForums.com kutokea Kitefure Longuo A, Moshi Vijijini anasema eneo hilo lina changamoto ya kutokuwa na Huduma ya Maji hali ambayo inaathiri Watu wengi huku ikiwa imedumu kwa muda mrefu sasa
Ameomba Mamlaka husika kushughulikia changamoto hiyo kwasababu kuna wakati Maji yanapatikana mara moja kwa Wiki au baada ya Siku 9 - 10
Soma https://jamii.app/KitefureMajiHakuna
#JamiiForums #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery

Kabla Mshukiwa hajakamatwa na Polisi ana Haki ya kuelezwa kwanini anakamatwa. Aidha, Polisi mkamataji ni lazima ajitambulishe na kueleza kituo cha Polisi anachotoka
Raia aliyekamatwa ana Haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa Kituo cha Polisi endapo kosa lake linastahili dhamana
Pia, ana Haki ya kufikishwa Mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi
Soma zaidi https://jamii.app/HakiKukamatwaPolisi
#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #KesiYaHaki #HakiZaBinadamu #UtawalaWaSheria

👍4
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Jana, Februari 13, 2025, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba aliwasilisha mapendekezo ya nyongeza ya Tsh. bilioni 945.7 kwenye Bajeti Kuu ya Serikali ya 2024/25 kutoka kwenye ile ya awali ya Tsh. Trilioni 49.3 iliyowasilisha Bungeni Juni 13, 2024
Leo Februari 14, 2025 Wabunge watajadili kuhusu Mapendekezo hayo pamoja na Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha – Mapitio ya Nusu Mwaka 2024/2025.
Soma https://jamii.app/NyongezaBajeti
#JamiiForums #Governance

DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka kushughulikia ujenzi na uboreshaji wa Barabara ya Kichangani kuanzia Shule, Kisimani hadi Msikiti wa Mzee Nandule zilizopo Kisarawe kwani hazipitiki na kupelekea changamoto ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo
Soma https://jamii.app/BarabaraKisaraweIrekebishe
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery

MWANZA: Mwanachama wa JamiiForums.com anasema licha ya uzuri wa Stendi ya Daladala ya Buzuruga ila ukosefu wa Vifaa vya kuwekea uchafu unachafua taswira ya eneo hilo na kuhatarisha #Afya ya Watumiaji
Ameshauri Wasimamizi wa stendi hiyo ambao ni Halmashauri ya Ilemela kuweka vyombo vya kuwekea Uchafu ili kuzuia utupaji holela wa taka na kurundika taka maeneo yasio stahiki.
Soma https://jamii.app/UchafuStendiBuzuruga
#JamiiForums #HudumaZaKijamii #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025 #ServiceDelivery

ARUSHA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma Nchini umebainika zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila Mwezi
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, Wavivu, Wazembe, Wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na Vipaji na Uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi
Aidha, Simbachawene amesema kumeibuka tabia ya baadhi ya Watendaji Wakuu hao pindi Mtumishi mwenye sifa za ziada anapohamia kwenye Taasisi anayoiongoza hupata hofu na kutompangia Majukumu kwa Hisia kuwa ametumwa kumchunguza au kuchukua nafasi yake
Soma zaidi https://jamii.app/WatumishiUmmaLazy
#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #Accountability

👍3
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Ngara ameomba Serikali iingilie kati tathmini ya Fidia iliyofanyika kwa Wakazi waliopata Uharibifu wa Mazao kutokana na kuvamiwa wa Tembo wa Hifadhi ya Burigi
Anasema tathmini iliyofanyika kwa Mujibu wa Sheria ya Wanyamapori inawaumiza Wakulima waliopata hasara pamoja na Familia zilizoathiriwa
Soma https://jamii.app/MazaoFidiaNgara
#JamiiForums #Governance
Anasema tathmini iliyofanyika kwa Mujibu wa Sheria ya Wanyamapori inawaumiza Wakulima waliopata hasara pamoja na Familia zilizoathiriwa
Soma https://jamii.app/MazaoFidiaNgara
#JamiiForums #Governance
👍1
DAR: Baada ya kushushwa na #Simba katika nafasi ya kwanza, #Yanga imerejea kwa kishindo katika nafasi hiyo kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuitandika KMC magoli 6-1 kwenye Uwanja wa KMC
Wafungaji wa Yanga ni Prince Dube (11), Ki Aziz (17, 49, 56), Maxi Nzengeli (90) na Israel Mwenda (90+3) wakati Redemtus Mussa alifunga Goli la #KMC katika dakika ya 51
Yanga imefikisha pointi 49 ikiwa na michezo 19, ikiishusha Simba ambayo ina pointi 48 katika michezo 18 wakati KMC imebaki nafasi ya saba ikiwa na alama 22
Soma https://jamii.app/KMC1Yanga6
#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25

❤2👍2
Bill Nye, Raia kutoka Nchini Marekani anasema Kupiga kura ni nguvu yako kama Raia, Dunia inahitaji Watu wanaotaka kuifanya kuwa mahali pa Haki kwa wote.
#HakiYaKupigaKura #Demokrasia #JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #Democracy

👎1
Mdau umepokea mualiko au zawadi gani katika kuadhimisha sikukuu ya Wapendanao?
Mjadala zaidi https://jamii.app/ValentineDayCelebrations
#JamiiForums #LifeStyle #ValentinesDay2025

Kila unapopokea au kutoa rushwa, unahujumu maendeleo yako binafsi, jamii yako, na taifa kwa ujumla
Rushwa inaharibu mifumo ya haki, inavunja ndoto za vijana, na kuzorotesha huduma za msingi kama elimu, afya, na miundombinu
Kila kura, kila uamuzi, na kila hatua tunayochukua inaathiri mustakabali wa nchi yetu. Tusikubali kuuza haki na utu wetu kwa faida ya muda mfupi. Kataa rushwa kwenye Uchaguzi
#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji

❤1👍1