#FARAGHA: Sheria ya #Tanzania ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 imeanisha Taarifa Binafsi kuwa ni taarifa zinazomtambulisha Mtu ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote
Taarifa Binafsi ni pamoja na zinazohusu Rangi, Asili ya Kitaifa au Kabila, Dini, Umri au Hali ya Ndoa ya Mtu, Elimu, Historia ya Matibabu, Jinai au Ajira, Namba yoyote ya Utambulisho, Anwani, Alama za Vidole au Kundi la Damu, pamoja na Jina la Mtu
Jina lako huchukuliwa kuwa Taarifa Binafsi kwasababu linakutambulisha na endapo litaunganishwa na Taarifa nyingine huweza kutoa Utambulisho wa kukutofautisha na Mtu mwingine
Soma https://jamii.app/PersonalInformation
#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako

DAR: Mdau ametoa wito kwa UDART kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi ya Mwendokasi kuanza kupakia Abiria Vituo vya Katikati kutokana na changamoto ya Usafiri na Mabasi hayo kujaa kutokea vituo vya mwanzo wa safari
Soma https://jamii.app/VituoKatiUDART
#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery

👍4👎1
DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar, limetangaza kuzifunga kwa muda barabara nne zinazoingia katikati ya Jiji kutokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaotarajiwa kukutana kesho, Jumamosi Februari 8,2025
Taarifa hiyo imeeleza barabara zitakazofungwa ni; Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu, Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Garden kutokea Barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka na Bodaboda na bajaji zimezuiliwa kuingia kwenye maeneo katikati ya jiji hasa barabara zilizotajwa kwa muda kwa sababu za kiusalama wakati wa ugeni.
Soma https://jamii.app/Barabara4KufungwaDar
#JamiiForums #Governance

❤1
Rushwa ni adui wa haki na maendeleo. Kila unapopokea au kutoa rushwa katika uchaguzi, unachangia kuharibu mustakabali wa nchi yetu
Viongozi wanaochaguliwa kwa #Rushwa mara nyingi hutanguliza maslahi yao binafsi badala ya yale ya Wananchi. Kumbuka, kura yako ina thamani kubwa kuliko fedha ya muda mfupi
#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji

❤1👍1
Kufuatia sitisho la msaada huo, ambao Takwimu za hivi karibuni zinaonesha karibu Dola Milioni 440 (Tsh. Trilioni 1.1) zilitengwa na Marekani kama msaada kwa Afrika Kusini Mwaka 2023, pia Ikulu (White House) imetangaza mpango wa kuwahamishia Marekani Wakulima wa Afrika Kusini wenye asili ya 'Kizungu' pamoja na familia zao kama Wakimbizi
Trump amedai Serikali ya Afrika Kusini inataifisha ardhi ya 'Wazungu', huku Mshirika wake, Elon Musk akidai 'Wazungu' hao wameathirika na Sheria za Umiliki wa Ardhi zenye Ubaguzi wa Rangi baada ya Rais Cyril Ramaphosa kutia saini Sheria mpya inayolenga kupunguza pengo kubwa la Umiliki wa Ardhi kati ya Watu 'Weusi' na 'Wazungu'
Zaidi https://jamii.app/MisaadaSA
#JamiiForums #TrumpExcutiveOrders #Diplomacy #Governance #Accountability

👍1
Kupitia chapisho lake katika Mitandao ya Kijamii, Rais #DonaldTrump amesema mtangulizi wake #JoeBiden ndiye alianzisha utaratibu huo Mwaka 2021 alipoagiza Idara za Ujasusi (IC) kumnyima Rais wa 45 wa Marekani (Trump) ufikiaji wa taarifa za Usalama wa Taifa, haki ambayo kawaida hutolewa kwa Marais wa zamani
Aidha, katika chapisho hilo, Trump amesema "Ripoti ya Hur imefichua kuwa Biden ana matatizo ya kumbukumbu na hata alipokuwa kwenye kilele cha uwezo wake, hakuweza kuaminiwa kwa taarifa nyeti. Mimi daima nitalinda usalama wa taifa letu."
Robert Hur ni Mwanasheria Maalum aliyekuwa na jukumu la kuongoza uchunguzi juu ya jinsi Rais Joe Biden alivyoshughulikia nyaraka za siri alipokuwa Makamu wa Rais (2009-2017) zilizopatikana katika maeneo yasiyo rasmi, ikiwa ni pamoja na ofisi yake ya zamani iliyopo Washington, D.C., na nyumbani kwake, Delaware
Soma https://jamii.app/TrumpVsBidenFeb
#JamiiForums #Governance #Accountability #Demokrasia

👍3❤1
Je, ni sahihi kwa mgombea kutoa fedha, mahitaji ya kijamii, au misaada mingine kwa wapiga kura? Ni sehemu ya Kampeni au mbinu za kushawishi wapiga kura kinyume cha maadili ya Uchaguzi? Jamii ina uelewa?
Kuelewa masuala haya kutamwezesha kila Mwananchi kufanya maamuzi sahihi na kushiriki katika uchaguzi kwa uelewa mpana
Usikose kushiriki katika mjadala huu muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kujifunza au kutoa maoni yako, Alhamisi hii, Februari 13, 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia XSpaces ya JamiiForums
Kujiunga, bofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv
#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, #SamiaSuluhuHassan, amewataka viongozi wenzake wa Kikanda kuchukua hatua madhubuti kuhusu hali inayoendelea kuzorota katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (#DRC), akionya kwamba historia itawahukumu vikali endapo watafumbia macho mgogoro kati ya Serikali ya DRC na Vikosi vya #M23 ambao unatajwa kusababisha vifo vya takriban raia 700 huko #Goma
Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, alizungumza hayo akitoa hotuba ya ukaribisho kwa Wakuu wa Nchi waliohudhuria Mkutano wa Pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (#SADC) uliofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam, Tanzania, ukiwa na lengo la kutafuta mwafaka wa mgogoro huo
Zaidi https://jamii.app/MkutanoKuhusuDRC
#JamiiForums

Mwanachama wa JamiiForums.com amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Watu wenye Ulemavu ili kupata Elimu, bado wanakumbana na changamoto za unyanyapaa na Ubaguzi katika Ajira
Anadai hata Vyama vya Walemavu ambavyo vilipaswa kuwa sauti yao, vimepoteza mwelekeo baada ya kunufaika na misaada ya muda
Anatoa wito kwa Mamlaka kuwazingatia Watu wenye Ulemavu katika kutoa Ajira kwani ni ngumu kwao kufanya shughuli za Ujasiriamali
Zaidi https://jamii.app/AjiraVsUlemavu
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #UnemploymentCrisis

DAR: Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Jumuiya za SADC na EAC wa kujadili hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), umemalizika kwa maazimio mbalimbali ikiwemo kusisitiza dhamira thabiti ya kuendelea kuiunga mkono DRC katika jitihada za kujilinda na kujiimarisha
Mkutano huo wa pamoja uliofanyika Ikulu ya Dar, uliwapa viongozi fursa ya kutathmini maendeleo, kuoanisha mikakati na kukuza ushirikiano wa kina zaidi, ukisisitiza kwamba amani na ustawi Barani Afrika vinahitaji juhudi za pamoja na kujitolea katika ngazi zote za utawala
Zaidi https://jamii.app/MaazimioDRCConflict