JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kila unapokubali pesa ili kumpa mtu uongozi, unajidhuru wewe mwenyewe na jamii yako

Viongozi wanaonunua kura hawawezi kuwa na nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi, bali wataangazia kurudisha pesa walizotumia badala ya kuleta maendeleo. Usiuze 'kesho' yako

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Haki ya kupiga kura siyo tu tendo la kupiga kura, bali inapaswa kujengwa juu ya:

Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi. Wananchi wanapaswa kuwa na Taarifa sahihi kuhusu Wagombea, Sera zao, na Athari za maamuzi watakayoyafanya

Pia, inahusisha Uhuru wa kuchagua bila shinikizo – Wananchi wanapaswa kupiga kura kwa hiari bila vitisho, Rushwa au Upotoshaji

Soma zaidi https://jamii.app/HakiKupigaKura

#HakiYaKupigaKura #Demokrasia #JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights
Mwanachama ndani ya Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali ameomba ushauri kuhusu vita vya Biashara na majirani wanaofanya Biashara zinazofanana na yake baada ya kufanya 'promotion' ya punguzo la bei kwa ajili yakurudisha mtaji wake

Tembelea Mjadala huu zaidi ndani ya JamiiForums.com kwa kubofya https://jamii.app/VitaBiashara

#JamiiForums #LifeStyle #Biashara
DIPLOMASIA: Ikulu ya Marekani imesema hatua ya kujiondoa kwenye Mashirika ya UN inalenga kupinga kile wanachokiita “Upendeleo wa kupinga Marekani” (anti-american bias) katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) lina Wanachama 47 walioteuliwa kwa vipindi vya Miaka mitatu na uhusiano wa Marekani na Baraza hilo ulikuwa unakaribia ukomo ifikapo Desemba 31, 2025

Trump sasa ameondoa kabisa ushiriki wa Marekani kwenye shughuli za Baraza hilo, ikiwa ni pamoja na Ukaguzi wa rekodi za Haki za Binadamu na madai maalum ya Ukiukwaji wa Haki

Soma https://jamii.app/TrumpsExOrders

#JamiiForums #TrumpExcutiveOrders #Diplomacy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Bunge la Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi (NA.13) wa Mwaka 2024 ambao umeongeza likizo ya uzazi kwa wanaojifungua Watoto njiti ambapo itaanza kuhesabiwa wiki 40 baada ya Mama kujifungua huku Baba wa Mtoto akipewa likizo ya Siku saba badala ya Siku tatu.

Akiwasilisha maelezo ya Muswada wa Sheria hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, aliwasilisha Mabadiliko hayo jijini Dodoma Januari 31, 2025

Marekebisho hayo ni Utekelezaji wa alichokisema Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika Sherehe za Mei Mosi 2024, zilizofanyika jijini Arusha ambapo alitangaza kuongezeka kwa Siku za Likizo kwa Wanawake wanaojifungua Watoto Njiti (Kabla ya Wiki 36 za Ujauzito) ambapo kipindi cha uangalizi maalumu hakitahesabika kama likizo ya uzazi.

Soma https://jamii.app/BabaNjitiLikizo

#JamiiForums #MaternityLeave #PrematureBabies #PostnatalCare
1
Februari 6 kila Mwaka, Tanzania huungana na Mataifa mengine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukeketaji kwa Wanawake na Watoto

Mwaka 2003 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilidhinisha tarehe 6 Februari ya kila Mwaka kuwa Siku rasmi ya maadhimisho ambapo kwa upande wa Tanzania Maadhimisho haya yalianza kufanyika mwaka 2010

Kichocheo kikuu cha vitendo vya Ukeketaji hapa Nchini ni Mila na Desturi za baadhi ya Makabila katika Jamii za kumvusha rika Mtoto wa kike kutoka usichana na kuwa Mwanamke kamili. Jamii inayokeketa huamini Msichana aliyekeketwa anakuwa tayari kuolewa.

Soma https://jamii.app/FGMDay2025

#JamiiForums #FGM #EndFGM #InternationalDayofZeroToleranceforFemaleGenitalMutilation #HerVoiceMatters
1
DAR: Kesi Namba 993/2025 inayomkabili Mwanasiasa mkongwe, Dkt. Willbroad Slaa (76), inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, imeahirishwa mpaka Februari 18, 2025 ambapo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi umekamilika

Dkt. Slaa anakabiliwa na tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye Mtandao wa X ambapo inadaiwa ametenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya Mwaka 2015.

Ikumbukwe, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) amekata rufaa katika Mahakama ya Rufani, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ulioelekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya Dkt. Slaa na kuangalia uhalali wa kesi ya jinai inayomkabili kwa haraka

Soma https://jamii.app/SlaaFeb6

#JFMatukio #JamiiForums
Idadi ya Utumiaji wa Intaneti imeongezeka kwa 16% kutoka Milioni 41.4 kwa robo mwaka iliyoishia Septemba 2024 hadi Milioni 48 kwa robo ya mwaka iliyoishia Desemba 2024.

Idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma hiyo angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu

Aidha, kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Utumiaji wa Intaneti umeongezeka kutoka 26,078,506 kwa mwaka 2020 hadi 48,028,227 kwa mwaka 2024

Soma https://jamii.app/IntanetiData

#JamiiForums #JFData #JamiiAfrica #Internet
👍1
MANYARA: Timu ya Fountain Gate imeilazimisha Simba sare ya Goli 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Matokeo ambayo yanaifanya Simba ibaki nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kwa kuwa na alama 44 nyuma ya Yanga yenye pointi 45

Timu ya #Simba ilianza kufunga kupitia kwa Leonel Ateba dakika ya 57 lakini Fountain Gate ambayo imefikisha alama 21 ilipata goli kupitia kwa Ladack Chasambi aliyejifunga dakika ya 75

Soma https://jamii.app/GatesSimba

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
2
ARUSHA: Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeiamuru Tanzania kufuta adhabu ya kifo katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu, (Sura ya 16) ndani ya mwaka mmoja kutokea Februari 5, 2025 ilipotoa hukumu hiyo

Mahakama imesema Jamhuri ilikiuka Haki ya Kuishi na Haki ya Utu chini ya Kifungu cha 4 na 5 cha Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu katika utekelezaji wa adhabu ya kifo, yaani kunyongwa

Aidha, Mahakama imeiamuru Jamhuri kuchapisha nakala ya Hukumu hiyo kwenye tovuti za Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria, ndani ya miezi mitatu tangu kutolewa kwake na kuhakikisha nakala hiyo inapatikana kwenye tovuti hizo walau ndani ya mwaka mmoja tangu itakapochapishwa.

Soma https://jamii.app/HukumuYaKifo

#CivilRights #HumanRights #JamiiForums