JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kimataifa, Elimu inatambulika kuwa Haki ya Msingi kwa Kila Binadamu huku msingi wake ukiwa kwenye kuwepo kwa Vifaa vya kutosha vya kujifunzia, Madarasa, Walimu waliopata mafunzo sahihi, na Rasilimali nyingine ili kuhakikisha kila Mtoto anapata Elimu bora.

Pia, Shule zinapaswa kuwa ndani ya umbali unaofikika, ziwe rafiki kwa Watoto wenye Ulemavu na ziwe na Miundombinu inayofaa. Elimu inapaswa kuwa nafuu kwa Watoto wote bila ubaguzi wa Kijinsia, Rangi, Dini au sababu nyingine yoyote.

Soma https://jamii.app/ElimuHakiMsingi

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights
👍1
SONGWE: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Wizara ya Afya, kuchunguza na kushugulikia kero ya wauzaji kuuza nyama zilizoharibika katika Mitaa ya Mpemba katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma

Amesema afya za walaji zipo hatarini, huku akidai Mamlaka za Afya za Tunduma zinachukulia 'poa' changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/NyamaZilizoharibikaTunduma

#JamiiForums #JFMdau2025 #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Afya #PublicHealth
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SINGIDA: Wanawake katika Kijiji cha Dominiki, Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama wamedai wanalazimika kuchota maji dumu 6 hadi 12 kwa ajili ya kutumia wakati wa kupata Huduma ya Matibabu katika Zahanati ya Dominiki ikiyopo kwenye kata hiyo

Wamesema hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ni changamoto kubwa na wanalazimika kuamka Saa Tisa Usiku ili kuyatafuta

Akizungumzia kuhusu changamoto hiyo, Diwani wa Kata ya Mwangeza, Samwel Charle Bosco amesema uhaba wa maji umewaathiri Wananchi hao na kuwafanya kuwa na rangi mbili mwilini, ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia kero hiyo

Soma https://jamii.app/SingidaMajiWanawake

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
1
Rushwa kwenye uchaguzi ni sumu kwa maendeleo ya Jamii yoyote. Chagua kiongozi mwenye uwezo na maadili na sio yule anayekupa 'kitu kidogo'

Usiyumbishwe, Kesho ya Jamii yako ni muhimu zaidi

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Barua ya Babu Owino kwa Rais Samia imedai alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Maafisa wa Uhamiaji walimzuia na kumjulisha hataruhusiwa kuingia nchini

Anasema hatua hiyo inakiuka haki yake ya kusafiri kama raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mwakilishi wa Bunge la #Kenya, ambalo pia linawakilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

Zaidi https://jamii.app/BabuOwinoTanzania

#JamiiForums #Diplomacy #Accountability #Governance
TABORA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia utengenezwaji wa Barabara ya Igunga hadi Rungwe (Mbeya) kwani imekuwa ikifanyiwa marekebisho mara kwa mara lakini ifikapo wakati wa Masika shida inarudi palepale na imekuwa changamoto kwa wakazi wa eneo hilo

Soma https://jamii.app/BarabaraMbovuIgunga

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFUwajibikaji #JFMdau2025
Viongozi wa Nchi ambao wamekuwa wakirushiana maneno hivi karibuni, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame wanatarajiwa kukutana Dar es Salaam, mnamo Februari 8, 2025 kujadili kuhusu mgogoro unaoendelea Nchini DRC

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa #Kenya, #WilliamRuto ametoa taarifa kuwa mkutano huo utahusisha Viongozi wa Nchi za EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Ruto amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo na kuwa Viongozi hao wa DRC na Rwanda ni miongoni mwa waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo utakaotanguliwa na mkutano wa Mawaziri Ijumaa, Februari 7, 2025

Soma https://jamii.app/MeetingInDar

#JFDiplomacy #JamiiForums
Mwanachama wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la #Biashara, Uchumi na #Ujasiriamali anasema ana Mtaji wa Tsh. 50,000,000 anazotaka kutumia kama mtaji wa biashara lakini muda wa kuisimamia kwa karibu sana ni finyu, anakuwa huru Wiki moja tu kila Mwezi

Unamshauri aanzishe Biashara gani ambayo ataweza kuiendesha hata anapokuwa mbali na eneo la Biashara?

Shiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/BiasharaMbali

#JamiiForums #JiajiriNaJF #Economy
1
Kuharibu karatasi au nyaraka zenye taarifa zako binafsi ambazo huna matumizi nazo tena ni hatua muhimu ya kulinda faragha yako

Njia kama kuzichana karatasi hizo vipande vidogo, kuziteketeza au kuzitumia mashine ya kukata nyaraka (Paper Shredder) husaidia kuzuia taarifa zako kuangukia mikononi mwa watu wasiohusika.

Mdau, unatumia njia gani kuhakikisha usalama wa taarifa zako?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuuharibuNyaraka

#JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
LINDI: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Liwale anatoa wito kwa Serikali na TANESCO kushughulikia changamoto ya Umeme kukatika mara kwa mara inayowakabili wakazi wa Wilaya hiyo kwa takriban Miaka Miwili sasa

Mdau anadai hali hii siyo tu inakwamisha shughuli za Kiuchumi na Kijamii, bali pia inaathiri Maendeleo ya eneo hilo kwa ujumla

Soma https://jamii.app/UmemeKukatikaLiwale

#JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto ya mabomba kutoa maji machafu kwa wiki mbili maeneo ya Kimara kwa Msuguli, Kibanda cha Mkaa, Mbezi Mwisho-Kwa Yusuph na Mbezi Mazulu akidai hali hiyo inaweza kuhatarisha Afya kwa Wakazi wa maeneo hayo

Soma https://jamii.app/MajiMachafuMbeziKimara

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery #JFMdau2025
👍1