JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Siku ya Saratani Duniani huadhimishwa Februari 4 kila mwaka ikiangazia kutoa elimu na uelewa kuhusu Saratani.

Ugonjwa wa Saratani umekuwa miongoni mwa chanzo kikubwa cha vifo vingi Duniani kwa rekodi za mwaka 2020

Miongoni mwa njia za kuzuia ugonjwa ni kuepuka uvutaji wa sigara, kufanya mazoezi, kuzingatia mlo bora wenye matunda na mbogamboga na kupunguza matumizi ya pombe

Zaidi https://jamii.app/WorldCancerDay2025

#JamiiForums #WorldCancerDay2025 #UnitedByUnique
Haki ya kupata Elimu siyo tu Haki ya Kisheria, bali pia ni chombo cha kuwawezesha Watu, kuondoa Umasikini, na kuleta Maendeleo katika Jamii

Bila Elimu, Mtu anaweza kunyimwa fursa ya Maisha bora, kushindwa kujitetea dhidi ya Ukandamizaji au kushindwa kushiriki katika Maendeleo ya Jamii

Aidha, Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa kubadilika ili kukidhi mahitaji ya Jamii na Maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kiteknolojia

Soma https://jamii.app/ElimuHakiMsingi

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #HakiYaElimu #ElimuKwaWote
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DR- CONGO: Wahudumu wa Afya wameendelea na shughuli ya mazishi ya watu waliouawa kwenye mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yaliyohusisha jeshi la nchi hiyo na Wapiganaji wa Kundi la M23

Aidha, Mkuu wa Ujumbe Mdogo Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu Mashariki mwa DRC, Miriam Favier amesema kuna hitaji la dharura la kuizika miili hiyo, kwani vyumba vingi vya kuhifadhia maiti vimejaa, hali inayoonesha kuna hatari ya kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko

Soma https://jamii.app/MapiganoDRCM23

#JamiiForums #CongoWar #M23Rebels
ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kuweka Askari wa Usalama Barabarani au Kamera katika barabara ya Kwerekwe Makaburini kwenda Fuoni kutokana na ajali zinasababishwa na madereva kudharau Alama na Sheria za Barabara

Soma https://jamii.app/ZanzibarKeroKuvukaBarabara

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery #JFMdau2025
1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com amelalamikia kero ya Nyumba moja kutiririsha Majitaka mtaani kwa Makusudi, ambapo wakazi wa maeneo hayo ya Msasani-Mikoroshini wamekuwa wakiathirika kwa Harufu huku wakihofia kupata magonjwa

Mdau ametoa wito kwa Serikali kuchunguza suala hili kwa kina na kuwawajibisha wale wote wanaohusika na tatizo hilo, kwasababu Serikali za Mitaa na NEMC hawajashughulikia licha ya kuripotiwa mara kadhaa

Soma https://jamii.app/MajiTakaMsasani

#JamiiForums #JFHuduma #JFMdau2025 #ServiceDelivery #Governance #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#HALIYAHEWA: Akizungumza leo, Februari 4, 2025 jijini Dodoma, Msemaji wa Jeshi la Zimamoro na Uokoaji, Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi ametoa tahadhari kwa wakazi wa mabondeni kuwa makini katika kipindi cha mvua zinazotarajiwa kuanza

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imetoa tahadhari ya uwepo wa majanga baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuripoti uwepo wa mvua za wastani na juu ya wastani katika baadhi ya mikoa nchini huku ikiwataka Wananchi kuwa makini katika kipindi hicho pamoja na kuviasa Vyombo vya usafiri kutopita katika maeneno yanayopita maji kwa kasi

Soma https://jamii.app/MvuaTahadhariBondeni

#JamiiForums #HaliYaHewa
👍1
DAR: Barua iliyoandikwa na Geofrey Paulo aliyejitambulisha kuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha TLP ameeleza kuwa wote walioshiriki Uchaguzi wa TLP Februari 2, 2025 ambapo Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama, walikuwa Wanachama Feki na kwamba walivalishwa fulana za chama tu

Barua imeeleza kuwa wamemuandikia barua Msajili wa Vyama kupinga mchakato wote na kuwa suala lao likifika Mahakamani watakaoshtakiwa ni Mwenyekiti na Katibu wake walioitisha mkutano huo ambao walikiuka Katiba ya TLP kisha kesi hiyo itasimamiwa na jopo la Mawakili wasiopungua Sita

Ikumbukwe katika Uchaguzi huo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alisema Mkutano umefuata taratibu zote na kuwa kuna mambo ya ndani ya chama yanayoendelea ambayo wao hayawahusu

Soma https://jamii.app/SiasaTLP

#JFDemocracy #JamiiForums #Siasa
👍2
Leo unaweza kupewa pesa lakini kesho utabaki na uongozi mbovu na Jamii isiyoendelea

Chagua mabadiliko ya kweli, si pesa za muda mfupi, kataa na puuza Viongozi wanaotoa Rushwa

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Ndani ya JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko Mwanachama anaongea na Wanawake akisema Usiogope kumuacha Mwanaume kwa hofu ya kutopata mwingine, kama unaona dalili na tabia zisizofaa kabla ya Ndoa, jua zitaongezeka mara 10 baada ya kuoana

Shiriki Mjadala huu na mingine mingi kwa kubofya https://jamii.app/KeKuzaaNdoa

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #LifeLessons #JFChitChats #JFStories
2