Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Wakili #TunduLissu ametangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa kwa kupata Kura 513 (51.5%) akifuatiwa na #FreemanMbowe aliyepata Kura 482 (48.3%) pamoja na Odero Odero aliyepata kura moja tu (0.01%)
John Heche ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kwa kupata Kura 577 dhidi ya Ezekia Wenje aliyepata Kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata Kura 49
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar ameshinda Said Mzee Said kwa Kura 625 sawa na 89% ya Kura 706 huku halali zikiwa 700 na sita zimeharibika
Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Demokrasia

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amempa maelekezo Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Elias Magembe aliyechukua nafasi ya Prof. Tumaini Joseph Nagu ambaye alitenguliwa, kusimamia masuala ya mlipuko wa Magonjwa ili Nchi iwe salama
Amesema hayo wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Chamwino, leo Januari 22, 2025
Ikumbukwe, Januari 20, 2025, Rais Samia alitangaza uwepo wa Maambukizi ya Virusi vya #Marburg ambapo Mtu mmoja alikutwa na Maambukizi hayo Wilayani Biharamulo, Kagera
Soma https://jamii.app/SamiaJan22
#JamiiForums #Afya #Governance #PublicHealth

MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anasema Wananchi wa Kijiji cha Nyangβomango, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi tunatumia Maji yaliyotuama kwenye madimbwi hivyo kuhatarisha Afya zao
Anadai changamoto hiyo inawaathiri Wanafunzi wa TIA Campus ya Mwanza, wanaosoma katika tawi lililofunguliwa hivi karibuni katika eneo hilo, ambao wanalazimika kupanga mbali kama Buhongwa ili kuepuka adha hiyo jambo linalosababisha changamoto kubwa katika Masomo yao
Soma https://jamii.app/KeroMajiMwz
#JamiiForums #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Accountability #Governance

π1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu wa Kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara baada ya matokeo kutangazwa, Mwenyekiti Mpya, Wakili #TunduLissu, amemshukuru Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake, Freeman Mbowe akisema wameweka "a golden standard" ya Uchaguzi wa Chama
Lissu amesema "Tumefanya kitu ambacho hatujawahi kufanya katika Chama hiki tangu kianzishwe, tumefanya Uchaguzi ambao hatujawahi kufanya katika Historia yetu kama Chama"
Soma https://jamii.app/LissuMktCDM
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA
Lissu amesema "Tumefanya kitu ambacho hatujawahi kufanya katika Chama hiki tangu kianzishwe, tumefanya Uchaguzi ambao hatujawahi kufanya katika Historia yetu kama Chama"
Soma https://jamii.app/LissuMktCDM
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akiongea baada ya kutangazwa Mshindi wa Nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Wakili #TunduLissu, amesema katika Uchaguzi huo kulikuwa na misuguano, mivutano na matatizo ya hapa na pale lakini hakukuwa na mizengwe
Soma https://jamii.app/LissuMktCDM
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA #Accountability

π2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, #FreemanMbowe, amesema Uchaguzi wa kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama hicho umeacha majeraha mengi ndani mwao, hivyo Viongozi wapya wakakiponye Chama
Soma https://jamii.app/MboweKaongea
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA #Accountability
Soma https://jamii.app/MboweKaongea
#JamiiForums #Demokrasia #Governance #UchaguziCHADEMA #Accountability
Je, Mfumo wetu wa Uchaguzi unahimiza Uwajibikaji na Uadilifu wa Viongozi?
Tunapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, ni muhimu kuchambua changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho kwa pamoja. Usikose kujiunga nasi kwenye mjadala huu kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku
Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza na kuchangia maoni kuhusu mustakabali wa Demokrasia yetu
Kushiriki Bofya https://jamii.app/MjadalaUchaguziJAN30
#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability

KATAVI: Mdau aliyejitambulisha kuwa Mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika ndani ya JamiiForums.com ametoa wito kwa Serikali kuwalipa Vijana wanaojitolea kwenye Hospitali hiyo kutokana na baadhi kuondoka na kusababisha uwepo wa kazi nyingi kwa uchache wa Watumishi
Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma Juma amesema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo ila analifuatilia
Soma https://jamii.app/WanaojitoleaWapewePosho
#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji
Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma Juma amesema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo ila analifuatilia
Soma https://jamii.app/WanaojitoleaWapewePosho
#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza jukumu lake la Kikatiba kwa kusimamia usalama kwenye mikutano na shughuli za Vyama vya Siasa bila kujali itikadi ya Chama chochote
Bashungwa amesema anapongeza #Uwajibikaji wa Jeshi hilo wakati wa Uchaguzi wa #CHADEMA na Mkutano Mkuu wa #CCM, kisha kusisitiza hilo liendane na Vyama vya Siasa kuwajibika katika kutii Sheria
Amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, leo Januari 22, 2025
Soma https://jamii.app/PolisiKusimamiwVyama
#JamiiForums #Governance #Accountability #ServiceDelivery

DAR: Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amemteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho akiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama uliofanyika leo Januari 22, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City
Pia, ameteua Manaibu Katibu Wakuu wa Chama kama ifuatavyo; Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara pamoja na Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Aidha, amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Kamati kuu ambao ni Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama, Rose Mayemba, Salma Musa Kasanzu na Hafidh Ally Salehe
Soma https://jamii.app/MnyikaAteuliwaCHADEMA
#JamiiForums #Democracy #Siasa

π3β€2
Wivu ni mwizi wa furaha. Badala ya kujilinganisha na wengine, sherehekea safari yako na utumie mafanikio ya wengine kama msukumo wa kuendelea mbele.
#JamiiForums #AmkaNaJF #Goodmorning #MorningQuote #Maisha #LifeTips #LifeLessons

MAREKANI: Mwanamuziki Chris Brown amewasilisha kesi dhidi ya Kampuni ya filamu, Warner Bros. Discovery, akiidai Kampuni hiyo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.2, akidai kwamba Kampuni hiyo imechapisha taarifa za uongo na zinazomdhalilisha kupitia 'Documentary' ya "Chris Brown: A History of Violence"
Mwanasheria wa Chris, Levi McCathern amesema "Kesi hii ni kuhusu kulinda ukweli, licha ya kupewa ushahidi kuwa taarifa hizo si za kweli bado Kampuni hiyo iliandaa 'documentary' hiyo na kuichapisha kwa makusudi wakifahamu wako kinyume na majukumu yao kama Waandishi wa Habari."
Soma https://jamii.app/ChrisVsWarner
#JamiiForums #WarnerBros #HumanRights

Kuasili Mtoto ni mchakato wa kisheria ambapo Mtu au Wanandoa huchukua jukumu la kumlea na kumtunza Mtoto ambaye si wa kwao kwa kumzaa
Baada ya kuasili, Mzazi aliyemuasili Mtoto anakuwa na Haki na anawajibika kutimiza majukumu yote kama Mzazi, na Mtoto anapata Haki zote za Kisheria na Kijamii kama vile Urithi, Malezi na Ulinzi
Mchakato wa kuasili humpa Mtoto asiye na Familia au anayehitaji msaada nafasi ya kupata Malezi bora, Upendo na Msaada wa Kijamii. Pia, ni njia ya Watu au Wanandoa wasio na uwezo wa kupata Watoto kuwa na Familia
Soma https://jamii.app/KuasiliMtotoTZ
#JamiiForums #Malezi #Familia #ChildRights