JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: Januari 20, 2025 Serikali ilitangaza mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya #Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera baada ya Mtu mmoja kukutwa na Maambukizi

Kufuatia taarifa ya mlipuko wa Ugonjwa huo, Serikali imetoa mwongozo wa Wasafiri wanaoingia na kutoka Mkoani Kagera kwa kuandaa Ushauri wa Usafiri Na. 15 Januari 21, 2025 ili kudhibiti usambazaji na ueneaji wa Ugonjwa huo Nchini

Soma https://jamii.app/TravelAdvisoryMarburg

#JamiiForums #Afya #Governance #PublicHealth
👍1
Je, Mfumo wetu wa Uchaguzi unahimiza Uwajibikaji na Uadilifu wa Viongozi?

Tunapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, ni muhimu kuchambua changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho kwa pamoja. Usikose kujiunga nasi kwenye mjadala huu kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza na kuchangia maoni kuhusu mustakabali wa Demokrasia yetu

Kushiriki Bofya https://jamii.app/MjadalaUchaguziJAN30

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
👍1
DAR: Mdau ametoa wito yafanyike maboresho katika Shule ya Msingi ya Sinza, akidai baadhi ya majengo ni chakavu na yanahatarisha Usalama wa Walimu na Wanafunzi, kwa kuwa yanatumiwa kama sehemu ya kuhifadhia baadhi ya vitu, kupikia na mara nyingi Wanafunzi wanaingia kucheza

Soma https://jamii.app/ShuleSinzaKuchakaa

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
Katika kuipata "Tanzania Tuitakayo", Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024 alipendekeza Mageuzi ndani ya Jeshi la Polisi ili kuondoa dhana mbaya na Hofu iliyojengeka ndani ya Wananchi

Unakubaliana na mapendekezo ya Mdau huyu? unadhani yanatekelezeka?

Soma zaidi https://jamii.app/SOC24JeshiPolisi

#JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Idara ya Uhamiaji imetoa taarifa kuhusu Wachezaji Watatu wa Timu ya Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Bara, kuwa wamepewa uraia wa Tanzania baada ya kuomba

Wachezaji hao ni Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana), Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire) na Muhamed Damaro Camara (Guinea)

Taarifa ya Uhamiaji imeeleza wahusika waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357 na kuwa maombi yao yamekubaliwa na ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

Soma https://jamii.app/UhamiajiWachezaji

#Sports #JamiiForums #JFDiplomacy
👍3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Jopo la Mawakili wanaomwakilisha Mwanasiasa Dkt. Wilbrod Slaa kwenye Kesi ya Jinai Namba 993 ya Mwaka 2025, wamewasilisha maombi mawili Mahakama Kuu Kanda ya Dar, kupinga kunyimwa dhamana kwa mteja wao, licha ya kuwa ni haki ya mshtakiwa kupewa dhamana

Pia, wanapinga uhalali wa kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ombi ambalo litasikilizwa Januari 24, 2025 kwenye Mahakama hiyo

Hata hivyo, mshtakiwa Dkt. Slaa amerejeshwa rumande huku maombi hayo yakiendelea kusikilizwa

Soma https://jamii.app/DhamanaSlaaJan

#JamiiForums #CivilRights #JFMatukio
Mafanikio hayapaswi kuwa mwisho wa safari ya furaha, badala yake, furaha ndiyo inayofungua milango ya mafanikio.

Unapofanya kile unachokipenda kwa moyo wa dhati, unaweka msingi imara wa kufanikisha ndoto zako.

Chagua kuwa na furaha katika safari yako kwa sababu furaha ni nguvu inayosukuma mafanikio mbele

#JamiiForums #Maisha #LifeTips #MorningQuote #AmkaNaJF
Rushwa inatajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazokwamisha Chaguzi Huru na za Haki, ikiwazuia Vijana kushiriki kikamilifu hususan kugombea nafasi za Uongozi hivyo Wananchi kukosa Uwakilishi sawa wa Makundi ya Kijamii

Ili kujadili changamoto ya Rushwa katika Uchaguzi na nafasi ya Vijana kuleta mabadiliko chanya, usikose kujiunga nasi katika Mjadala kupitia Xspace ya JamiiForums, Januari 28, 2025 kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 2 Usiku

Kushiriki, bofya https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kukamilisha uchunguzi ili kubaini chanzo na kudhibiti usambazaji wa Mafuta yaliyoathiri wakazi wa Yombo Dovya (Temeke) ili yasizidi kuathiri Watu wengine huku akisisitiza walioathirika na Mafuta hayo wapatiwe msaada wa Matibabu

Soma https://jamii.app/AthariMafutaYombo

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery