JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mhitimu wa Igabiro Training Institute of Agriculture ilichopo Muleba amedai Wahitimu wa awamu mbili chuoni hapo hawajapata vyeti licha ya kukamilisha taratibu zote

Akizungumza na JamiiForums, Mkuu wa Chuo, Sadoki Stephano amesema "Wahitimu waliosoma Mifugo Vyeti vyao vinatoka #NACTVET, upande wa Kilimo matokeo yao na Vyeti vinatolewa na Wizara."

Aidha, ameongoza kwa kusema kuwa kuna vyuo zaidi ya 9 ambavyo havijapata vyeti kwani vipo kwenye mchakato na vitapatikana ndani ya mwezi kutoka sasa

Soma https://jamii.app/VyetiChuoIgabiro

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji
1
MBEYA: Mdau anadai kukosekana kwa Huduma ya Maji maeneo ya Isyesye kumeathiri biashara na huduma za kijamii na kudai kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kutokea kwa changamoto ya aina hiyo na wanapofuatilia hawapati majibu sahihi

Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA UWSA), CPA.Gilbert Kayange anasema “Uzalishaji haukidhi mahitaji, kuna maboresho ya mitambo sehemu na mafundi wapo kazini tangu juzi kurekebisha ili huduma irejee.”

Ameongeza “Kumaliza tatizo hilo jumla, tuna Mradi wa Mto Kiwira ukikamilika ndani ya mwaka mmoja na nusu, utazalisha Maji Lita Milioni 117 kwa siku. Kuhusu Isyesye, miaka mitatu nyuma walikuwa na changamoto kubwa ya kukosa maji zaidi ya mwezi lakini sasa ikitokea ni kwa siku kadhaa tu.”

Soma https://jamii.app/IsyesyeMaji

#JFHuduma #JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
MAREKANI: Moja ya masharti waliyowekewa Watu Januari 20, 2025, kabla ya kuingia katika ukumbi wa Capital One Arena, Jijini Washington DC ilikuwa ni kuacha mabegi na mikoba nje ili waweze kushuhudia uapisho wa Rais #DonaldTrump

Soma https://jamii.app/CapitalOneAreaInstructions

#JamiiForums #Democracy
2
Maisha ni safari yenye changamoto lakini mafanikio huja kwa wale wanaosimama imara na kupambana bila kukata tamaa.

Usikate tamaa, kila hatua unayopiga unakaribia kwenye ushindi wako.

#JamiiForums #LifeLessons #LifeTips #Maisha #MorningQuote #Goodmorning #AmkaNaJF
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wagombea wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti Zanzibar katika Uchaguzi wa CHADEMA, Said Mzee Said na Said Issa Mohamed wanapigiwa kura upya baada ya nafasi hiyo kukosa mgombea aliyefikisha zaidi ya Asilimia 50 ya kura zilizopigwa

Hayo yametangazwa na Katibu Mkuu wa #CHADEMA, John Mnyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City

Kutokana na matokeo hayo, Mnyika amesema matokeo ya nafasi nyingine ya Makamu Mwenyekiti Bara na Mwenyekiti Taifa yatachelewa kutangazwa licha ya kukamilika na Wawakilishi wa Wagombea kutangazwa

Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #JFDemocracy #Demokrasia
DAR: Kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), Mwanasiasa, #FreemanMbowe amempongeza na kumtakia heri #TunduLissu licha ya kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa #CHADEMA hayajatangazwa

Mbowe ameandika “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.”

Baada ya andiko hilo, John Heche akajibu “Asante sana Mwenyekiti, umetujenga na kutulea, umeonesha Demokrasia kwa kuongoza timu kusimamia uchaguzi wa wazi, huru na haki. Historia ya Tanzania itakukumbuka, kama mtu uliejenga Demokrasia na kuleta mageuzi makubwa kwenye Nchi na chama chetu.”

Soma https://jamii.app/MboweAkubali

#JamiiForums #Siasa #JFDemocracy #Demokrasia
👍21
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakati matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa #CHADEMA yakisubiriwa kutangazwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City, baadhi ya Wanachama wameonekana wakifurahia muziki wakiongozwa na #TunduLissu ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti akishindana na #FreemanMbowe na Odero Odero

Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Demokrasia
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar katika Uchaguzi wa #CHADEMA, Said Issa Mohamed, ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho na hivyo nafasi kubaki ikiwaniwa na Said Mzee Said

Said Mohamed amesema amefanya maamuzi hayo baada ya kushauriana na mshindani mwenzake na kuwa hana kinyongo kwa kitakachoendelea

Akizungumzia baada ya maamuzi hayo, Katibu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kinachofuata ni upigwaji wa kura wa siri ambapo Wajumbe watatakiwa kuchagua kwa NDIYO au HAPANA

Soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #JFDemocracy #Demokrasia
1
ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Maktaba ya Vitabu iliyopo Mjini Unguja kushughulikia ukosefu wa huduma ya maji ambayo imekuwa kero kwa Wanachama na Watumishi

Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim kuhusu suala hilo amesema anafahamu kuhusu suala hilo na tayari wanalishughulikia

Soma https://jamii.app/MaktabaHakunaChoo

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery