JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Timu ya #Simba imeingia Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuongoza Kundi A baada ya kuifunga CS Constantine ya Algeria kwa Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa

Magoli yaliyofungwa na Kibu Denis na Leonel Ateba yamepeleka furaha kwa wenyeji licha ya mchezo huo kutokuwa na mashabiki, ambapo Simba imefikisha pointi 13 ikifuatiwa na Constantine yenye alama 12

CS Sfaxien ya Tunisia imeshika mkia Kundini ikiwa na alama 3 licha ya kushinda Magoli 4-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola

Soma https://jamii.app/SimbaCAFJan19

#JFSports #JamiiForums #CAFCC
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza kuelekea katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025

Baada ya hapo, Wajumbe wa Mkutano huo wakaridhia kwa kauli moja kumpitisha Dkt. Nchimbi kuwa Mgombea mwenza

Mapema leo, Januari 19, 2025, Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ulimchagua Rais Samia kuwa Mgombea Urais kwa kupata Kura Asilimia 100 kutoka kwa Wajumbe wote 1,924

Soma https://jamii.app/Nchimbi2025

#JamiiForums #Siasa #Democracy
πŸ‘4
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Kuwa na subira katika safari yako ya mafanikio. Kila hatua unayochukua, hata kama ni ndogo, inakukaribisha karibu zaidi na malengo yako.

Kumbuka, mafanikio hayaji kwa haraka; yanahitaji muda, bidii, na uvumilivu. Usijilinganishe na wengine au kuhisi uko kwenye mashindano. Safari yako ni ya kipekee, na muda wako utafika

Endelea kuamini mchakato

#JamiiForums #LifeLessons #LifeTips #Maisha #MorningQuote #Goodmorning #AmkaNaJF
❀3
MICHEZO: Mkongwe wa Ndondi, #MikeTyson ambaye ana umri wa Miaka 58 anapanga kurejea ulingoni kupigana baada ya kupoteza pambano dhidi ya Jake Paul (28), Novemba 15, 2024 ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kustaafu Miaka 20 iliyopita

Inadaiwa mpango uliopo ni Tyson kupigana na Mkongwe mwenzake, Evander Holyfield (62) ambaye alipigana naye mara ya mwisho Mwaka 1996 kisha pambano likamalizika Raundi ya 11 baada ya Tyson kumng’ata sikio Evander

Holyfield naye alijaribu kurejea ulingoni Mwaka 2021 kwa kupigana na Mwanamichezo wa Mapigano ya MMA, Vitor Belfort (47). Holyfield alikubali kichapo katika Raundi ya Kwanza kwenye pambano hilo

Soma https://jamii.app/TysonComeback

#JFSports #JFBoxing #JamiiForums
ZANZIBAR: Akitoa tathmini ya hali ya Usalama kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera amesema makosa dhidi ya binadamu kwa upande wa mauaji yameongezeka Zanzibar

Amesema ndani ya kipindi hicho yameripotiwa makosa 66 ikilinganishwa na makosa 44 ya Mwaka 2023

Aidha, amewataka Makamanda wa Polisi Mikoa pamoja na Maafisa wa Polisi kuongeza nguvu katika kuzuia Mauaji, Wizi wa Pikipiki na Mifugo, makosa dhidi ya Watalii na makosa ya Usalama Barabarani ambayo yaliongezeka Mwaka 2024 ikilinganishwa na Mwaka 2023

Soma https://jamii.app/MakosaMauajiKuongezeka

#JamiiForums #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Januari huwa ni mwezi wenye changamoto na majukumu mengi kama hukujipanga na ulitumia pesa nyingi kusherekea mwezi Desemba.

Mdau, unatumia mbinu gani kutoboa mwezi huu?

#JamiiForums
❀1
MBEYA: Mdau wa JamiiForums.com anadai elimu ya usafi wa chakula ikitolewa kwa Watoto itawasaidia wajikinge na maambukizi ya Ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuwa kuna mazingira ya uchafu sehemu nyingi zinazouzwa vyakula

Aidha, Desemba 11, 2024, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Yesaya Mwasubila alikiri uwepo wa Kipindupindu na kusema kwa wakati huo kulikuwa na Wagonjwa 22

Soma https://jamii.app/AfyaElimuWatotoMbeya

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #PublicHealth
πŸ‘1
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com amelalamikia kero ya Ulevi wa Pombe za Kienyeji kwa Vijana Mkoani humo akitoa wito wa juhudi za ziada ikiwemo kutoa Elimu kwa Vijana kuhusu madhara ya Ulevi na kushirikisha Viongozi wa Kijamii na Kidini

Aidha, mdau ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia madai yanayohusu Mtandao wa wanaosambaza Ugoro ili kulinda Afya na Maadili ya Vijana

Soma https://jamii.app/UleviVijanaKagera

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFUwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amesema uchunguzi uliofanywa na Wataalam wa Afya waliotumwa Mkoani Kagera kufuatilia taarifa za uwepo wa maambukizi ya Virusi vya #Marburg umeonesha mtu mmoja amekutwa na maambukizi hayo Wilayani Biharamulo

Ameyasema hayo wakati alipotembelewa na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa Ikulu ya Chamwino, leo Januari 20, 2025

Amesema jitihada za Wataalam zinaendelea kufuatilia kuhusu maambukizi hayo na kuwa bado hakuna taarifa ya kifo, hiyo ni mara ya pili kwa maambukizi hayo kutokea Mkoani hapo, awali ilikuwa Machi 2023

Soma https://jamii.app/SamiaWithWHO

#JamiiForums #Afya #Governance #PublicHealth
DAR: Taka zilizokuwa zimerundikwa Barabarani kwa zaidi ya siku tatu eneo la Tegeta - Kwandevu na kusababisha kero kwa waendeshaji wa Vyombo vya moto na kuhatarisha Afya za Wananchi zimezolewa leo asubuhi Januari 21, 2024

Licha ya uchafu huo kuondolewa, baadhi ya Wafanyabiashara wa eneo hilo wameendelea kusisitiza Mamlaka zinazoratibu suala la usafi kuwawekea vifaa maalumu eneo hilo kwaajili ya kumwaga taka au kutafuta eneo mbadala la kukusanya taka hizo, kuliko mtindo wa kuzirundika Barabarani ambapo ni karibu na maeneo wanapofanyia Biashara

Soma https://jamii.app/TakaKwandevu

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #Governance #Afya
πŸ‘1