JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewahimiza Vijana (Gen Z) nchini humo kutokata tamaa katika mapambano yao ya kutafuta Demokrasia na Utawala bora

Amesema hayo Januari 17, 2024 katika Kanisa la Nairobi Chapel ambapo amesema kuwa ni makosa kwa raia kubaki kimya huku rasilimali zao zikitumiwa vibaya na Viongozi

Aidha, baada ya kauli hiyo ya Kenyatta, Rais William Ruto amemtuhumu kwa kuchochea Vijana kufanya fujo

Soma https://jamii.app/GenZMsikateTamaa

#JamiiForums #Accountability #Governance
👍2👎2
Unapojiwekea malengo yako kumbuka kuangalia Maendeleo yako mara kwa mara

Kujua nini umefanikiwa kukifanya na kipi hujakifanikisha kutakusaidia kujua unakosea wapi, unatakiwa kuboresha wapi na unatakiwa kubadilika wapi ili uweze kuyafikia malengo uliyojiwekea

#JamiiForums #LifeLessons #LifeTips #Maisha #MorningQuote #Goodmorning #AmkaNaJF
TABORA: Baada ya Mdau kutoa wito kwa mamlaka kushughulikia vitendo vya kihalifu vinavyofanyika mitaa ya Chuo cha Polytechnic College, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa, Richard Abwao amezungumza na JamiiForums na kusema "Ofisi ya RCO (Mpelelezi wa Makosa ya Jinai) inalifuatilia suala hilo."

Upande wa Mkuu wa Chuo cha Polytechnic amesema "Tumefikisha taarifa hiyo kwa Jeshi la Polisi katika Ofisi ya RPC wanafahamu changamoto hiyo, tukio kubwa la hivi karibuni lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu ambapo kuna Mwanafunzi alijeruhiwa vibaya na wahalifu hao."

Soma https://jamii.app/PolisiKufatiliaUhalifuTabora

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFMatukio #CivilRights
👍1
MAREKANI: Rais #DonaldTrump amesaini takriban amri 200 za Kiutendaji, baada ya kuapishwa kama Rais wa 47 wa Nchi hiyo, zikihusisha mabadiliko makubwa kwenye Uhamiaji, Uchumi, Afya, Mazingira, na Masuala ya Jinsia

Miongoni mwa amri inayozungumziwa zaidi ni kukomesha Uraia wa Kuzaliwa. Trump amesema hatua hiyo inalenga kukomesha Utalii wa Uzazi, (Birth Tourism) ambapo Watu huenda Marekani kwa makusudi ya kujifungua ili Watoto wao wapate uraia

Aidha, Trump amefuta amri 78 za mtangulizi wake, #JoeBiden, ambazo zilihusisha kupunguza utoaji wa Gesi chafu, kulinda Ardhi ya Serikali, na kupunguza gharama za Dawa

Soma https://jamii.app/TrumpsExcutiveOrders

#JamiiForums #TrumpExcutiveOrders #Governance #Democracy #Demokrasia #Diplomacy
2
Mdau wa Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu vigezo vinavyozingatiwa na Muuzaji simu iwapo simu imepata matatizo na mteja anataka kuirudisha

Mdau, huwa unazingatia vilivyoandikwa kwenye 'Warranty Card'?

Mjadala zaidi https://jamii.app/BiasharaSimuKariakoo

#JamiiForums #LifeStyle
Unakubaliana na hoja ya Mdau? Je, wewe umeshajiwekea Malengo na Vipaumbele kwa mwaka 2025?

Mjadala zaidi https://jamii.app/2025Vipaumbele

#JamiiForums #LifeTips #Maisha
SIMIYU: Barabara ya Bariadi - Itilima imeanza kufanyiwa marekebisho baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuelezea kero hiyo ya kuharibika kwa Barabara na kujaa mashimo kuanzia Bariadi hadi Itilima ambapo Wananchi walilazimika kusafiri kwa Saa Mbili badala ya Dakika 30 kwa Gari

Soma https://jamii.app/MatengenezoBarabaraItilima

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Vipi wewe, ni jambo au kitu gani hukufanya upatwe na Hofu kubwa unapokiona au kukifikiria kwenye Maisha?

Mjadala https://jamii.app/HofuKuuMaisha

#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFStories #JFChitChat
👍1