JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com anasema amekutana na changamoto ya kurudishiwa nauli yake baada ya kudai Tiketi ya Kieletroniki kwenye Basi, licha ya kwamba alifanya 'booking' ya Safari muda mrefu

Mdau ametoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kutatua changamoto hiyo, kwa sababu inasababisha baadhi ya Watu kupoteza pesa kwani wengine hutakiwa kukabidhi tiketi hizo Ofisini kwaajili ya uthibitisho

Soma https://jamii.app/LATRATiketiEFD

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #HudumaZaKijamii
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Ezekia Wenje, ambaye ni Mtia nia wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) - Bara amezungumza na Wanahabari, leo Januari 16, 2025, amesema kulikuwa na mpango wa kumpindua Mwenyekiti wa chama hicho #FreemanMbowe wakati akiwa gerezani

Soma https://jamii.app/WenjePress

#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
👍21
Vikwazo, changamoto, na maneno ya watu hayawezi kukuzuia kufikia ndoto zako.

Ni maamuzi yako na jinsi unavyochukua hatua ndivyo vitakavyoamua safari yako ya mafanikio.

Jiamini, songa mbele, na usikubali kujizuia

#JamiiForums #MorningQuote #Goodmorning #LifeLessons #LifeTips
KILIMANJARO: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia na kushughulikia madai ya utozwaji wa Tshs. 40,000/= ili kusajili Wanafunzi wa Darasa la Kwanza katika Shule za Serikali katika Kijiji cha Mengwe, Wilayani Rombo

Soma https://jamii.app/HelaKutozwaUsajiliWanafunzi

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
UWAJIBIKAJI: Desemba 9, 2024 Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito na kuomba Serikali kufuatilia madai ya 'upigaji' wa fedha za Wananchi uliotokea katika Kata ya Kabondo, Wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu

Mkuu wa Wilaya ya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura amesema "Ujenzi umeanza na sasa umefikia ngazi ya lenta lakini TAKUKURU nao wanaendelea na kazi yao"

Soma https://jamii.app/MichangoShuleMeatu

#JamiiForums #Governance #Accountability
1👍1
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Adam Namamba amezungumza na JamiiForums kuhusu madai ya changamoto ya malipo kwa Watumishi Chuoni hapo, amesema yanachelewa kutokana na Mtumishi kukosea au kuchelewa kurejesha fomu, hivyo mfumo unapata changamoto

Amesema kuhusu fedha za kujikimu kutotolewa zinaweza kuchelewa kutokana na changamoto ya Kimfumo, pia wakati mwingine inatokana na makosa ya Mtumishi akichelewa kufanya marejesho

Ameongeza tangu Awamu iliyopita ya Serikali, fedha zote za Taasisi zinaingia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivyo kunakuwa na mchakato wa kutoka taasisi moja kwenda nyingine.

Zaidi, soma https://jamii.app/OUTStahikiStaff

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
👍3🔥1
Baadhi ya Wadau ndani ya JamiiForums.com wamedai walipotoa taarifa Polisi kuhusu kuibiwa Simu au vifaa vingine vya kielektroniki kulikuwa na hali za kuwataka walipie gharama mbalimbali kwenye Ufuatiliaji na uchunguzi wa taarifa hiyo ikiwemo 'Nauli za kufuatilia Wahalifu'

Vipi Mdau, ulipoibiwa Simu na kutoa Taarifa Polisi ulitakiwa kulipia gharama yoyote au utaratibu wa kukuhudumia ulikuwaje?

Mjadala https://jamii.app/SimuZaWizi

#JamiiForums #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii #Accountability
👍1
RUVUMA: Mdau aliyejitambulisha kama mkazi wa Songea Kijijini, ametoa wito kwa Waziri wa Ardhi kutatua mgogoro wa ardhi kwa kupima upya ardhi katika Kata ya Liganga

Mdau amedai kuwa katika mgogoro huo aliyekuwa kiongozi pamoja na Mwenyekiti aliyeshiriki kuwauzia ardhi wamewageuka, kwa kuwa wamehadaiwa na upande wa pili

Soma https://jamii.app/MgogoroArdhiSongea

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #JFMatukio
👍1