JamiiForums
βœ”
53.3K subscribers
34.2K photos
2.37K videos
31.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Mwanasiasa Godbless Lema ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Kanda ya Kaskazini amezungumza na Wanahabari, leo Januari 14, 2025 na kutangaza kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho dhidi ya #FreemanMbowe ambaye anatetea nafasi hiyo

Soma https://jamii.app/LemaPress

#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amesema Mwenyekiti wa chama hicho, #FreemanMbowe aliwahi kumwambia kuwa amechoka na anahitaji kupata watu wa kumsaidia kazi hiyo

Soma https://jamii.app/LemaPress

#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
πŸ‘1
#BURUNDI: Washiriki watatu waandamizi wa timu ya ushauri ya Rais Evariste Ndayishimiye wamepelekwa Gereza Kuu la Mpimba, #Bujumbura, wakikabiliwa na tuhuma za Uhaini

Maafisa hao wanatuhumiwa kuwaachia huru baadhi ya Wafungwa wa Makosa ya Ubakaji na Mauaji ambao hawakuwemo kwenye Orodha ya Wafungwa waliopata Msamaha wa Rais

Soma https://jamii.app/SeriorsJailedNdayishimiye

#JamiiForums #Governance
πŸ‘3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema ambaye ametangaza kumuunga mkono #TunduLissu katika kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho, amesema suala la uendeshaji wa chama hautakiwi kutegemea fedha za Mtu mmoja

Pia, amehoji β€œKama Makamu Mwenyekiti wako huwezi kumuamini kumuachia chama, ni nani utamuamini na kumuachia chama?”

Soma https://jamii.app/LemaPress

#JamiiForums #JFMatukio #Siasa #Democracy
πŸ‘3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumzia tabia ya Wazazi/Walezi kutoa adhabu kali kwa Watoto ikiwemo kuwapiga kila mara

Soma https://jamii.app/GwajimaVipigoWatoto

#JamiiForums #Malezi #Maisha #ChildRights #HakiMtoto
❀1
#MICHEZO: Shirikisho la Soka Afrika (#CAF) limetoa adhabu ya faini ya Dola 40,000 (zaidi ya Tsh. Milioni 100) kwa Klabu ya Simba pamoja na kutakiwa kucheza Mechi moja bila Mashabiki, ambapo itakuwa dhidi ya CS Constantine

Adhabu hizo zimetolewa kutokana na vurugu zilizofanywa na Mashabiki katika Mchezo dhidi ya CS Sfaxien wa Desemba 15, 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam

Kutokana na adhabu hiyo, Simba imesitisha mauzo ya tiketi ya mchezo wao ujao na kueleza ambao wameshanunua tiketi, zitatumika katika Mchezo ujao wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho

Soma https://jamii.app/SimbaAdhabuVurugu

#JamiiForums #Sports #JFCAFCC
πŸ‘2😒2πŸ‘1
Kila mafanikio huanza na kujua unachotaka na sababu ya kukitaka

Fanya tafakari ya kina, weka malengo yako wazi, na elewa kwanini ni muhimu kwako. Ukishajua hili, hatua za kufanikisha lengo lako zitakuwa rahisi kufuata

Anza leo kwa kuweka malengo yako wazi na kuyafanyia kazi kwa uthubutu na bidii

#JamiiForums #Maisha #Goodmorning #MorningQuote #LifeTips
πŸ‘1
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kuchunguza Ukarabati wa Kituo cha Mabasi Bukoba, mradi uliotengewa Tsh. Bilioni 1 za Serikali maarufu kwa jina la "Bilioni za Rais Samia” kisha kuonekana kama umetelekezwa tangu Oktoba 2023

Anatoa wito kwa kuwa mara ya kwanza fedha hizo zilitaka β€˜kupigwa’ na baadhi ya Watumishi wa Manispaa ya Bukoba kama alivyosema Mkuu wa Mkoa huo, ifuatiliwe isije kuwa hali hiyo imejirudia na kusababisha Mradi kusimama

Soma https://jamii.app/UkarabatiKituoMabasiKutelekezwa

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
MWANZA: Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto kadhaa ndani ya mfumo wa Chuo Kikuu cha SAUT (Augustine University of Tanzania - SAUT), ufafanuzi umetolewa

Taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha SAUT, Medard Wilfred imesema kuwa mfumo huo umeimarishwa tofauti na uliokuwa unatumika awali na kunapofanyika mabadiliko yoyote ya taarifa za Wanafunzi katika mfumo huo zitaonekana

Soma https://jamii.app/MfumoMatokeoSAUT

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulia Barabara Mtaa wa Chenga ambayo imekuwa kero kwa Wakazi wa eneo hilo

Upande wa Serikali za Mitaa, Mwenyekiti Venance Edward amesema kuwa Changamoto hiyo inajulikana na imewasilishwa TARURA lakini hawajazuia Wananchi kufukia au kushughulikia barabara hizo mbovu

Soma https://jamii.app/BarabaraMtaaChengaMbovu

#JamiiForums #JFUwajibikaji #ServiceDelivery #Accountability
❀2