JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu ya England, (#PremierLeague) 2023/24 zinashika kasi, #ManchesterCity itakipiga dhidi ya #Arsenal kwenye Uwanja wa Etihad, leo Machi 31, 2024 majira ya saa 12:30 jioni

Msimamo wa Timu Tatu za juu, #Liverpool ina pointi 67, Arsenal (64), na Man City (63), hivyo atakayeshinda kati ya Man. City na Arsenal anaweza kuathiri kiasi fulani mbio za yule atakayepoteza

Takwimu za jumla, Timu hizo zimekutana mara 210, Arsenal imeshinda mechi 99, City 65 na sare zikiwa ni 46 na mara ya mwisho kukutana (Oktoba 8, 2023) Arsenal ilishinda kwa goli 1-0

Unadhani matokeo yatakuwaje leo?

Soma https://jamii.app/CityArsenal

#JFSports #JamiiForums
👍10😁2
Mchezo wa #ManchesterCity dhidi ya #Arsenal umekamilika kwa suluhu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Etihad, matokeo ambayo yanaiwezesha Liverpool kuongoza Msimamo wa #PremierLeague

Arsenal imefikisha pointi 65 na hivyo kushuka hadi nafasi ya Pili ilifuatiwa na Man. City yenye alama 64

#Liverpool ambayo imeshinda 2-1 dhidi ya Brighton inaongoza msimamo kwa kuwa na pointi 67

Soma https://jamii.app/CityArsenal

#JFSports #JamiiForums
👍122
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ya gridi ya taifa kuanzia 8:22 usiku hivyo kusababisha baadhi ya maeneo nchini kukosa huduma ya umeme

TANESCO imeeleza kuwa Wataalamu wao wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma

Shirika limewaomba uvumilivu wateja wake katika kipindi hiki ambacho huduma ya umeme imekosekana

Soma https://jamii.app/UmemeHitilafu

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFUwajibikaji #JFHuduma
👍8🤮5👏1
Mdau wa JamiiForums.com anadai Wafanyabishara Wadogo wa Kariakoo (Machinga) wana wakati mgumu, akitolea mfano wanatakiwa kulipa Tsh. 500 hadi 2,000 kwa Siku kwa Uongozi wa Machinga lakini hakuna utaratibu wa utoaji risiti na wakihoji wanapata wakati mgumu kutoka kwa Mgambo

Pia, anadai wakati wa ukamataji Wanawake wamekuwa wakivamiwa na kunyang'anywa Bidhaa zao na Maafisa wa Kiume kwa nguvu hali ambayo kuna wakati inawadhalilisha Wanawake hadharani, anatoa wito Serikali kufuatilia kinachoendelea na kuchukua hatua

Soma https://jamii.app/MachingaKarikoo

#JFHuduma #JFUwajibikaji #KemeaRushwa #Governance #JamiiForums
👍4
Mdau kutoka JamiiForums.com anauliza kwanini daladala zilizochoka zinaachwa ziendelee kufanya kazi?

Mjadala zaidi bofya https://jamii.app/UsalamaDaladala

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #JFHuduma #KeroZaUsafiri #JFToons
👍42
Katika Maisha kila Mtu anapenda starehe za hapa na pale. Kuna starehe zinazoweza kukupa furaha ya kudumu lakini kuna nyingine huacha Majuto

Kwako Starehe gani ilikupa Hasara kubwa au ya muda mrefu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/HasaraStarehe

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle
👍54
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo anasema Utamaduni wa Mtumishi kuwa na nidhamu ya kuogopa Viongozi unamfanya Mhusika kutokuwa huru kutoa maoni hasa yanapokuwa tofauti na Viongozi wake

#JFQuotes #JamiiForums #Governance #GoodMorning #JFNukuu #LeaderShip #Uongozi
👍92
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Inadaiwa hizi ndio tabia na sifa za Watu waliozaliwa mwezi Aprili. Je, kuna ukweli kiasi gani?

#JamiiForums #AprilBabies
👍131
JIUNGE NA 'CHANNEL' YA TELEGRAM YA JAMIICHECK UWE WA KWANZA KUPATA TAARIFA ZILIZOHAKIKIWA

JamiiForums kupitia Jukwaa lake la #JamiiCheck inaendelea kukupa nafasi ya Kuhabarika, Kuelimika na Kushiriki mchakato wa Kuhakiki Taarifa kila wakati na kwa haraka zaidi, ambapo hivi sasa imekuongezea sehemu nyingine ya kupata taarifa hizo kupitia Mtandao wa #Telegram

Jiunge sasa na 'Channel' yetu ya Telegram kwa kubofya hapa https://t.me/JamiiCheck

#JamiiForums #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #FactsChecking #VisitJamiiCheck
👍1🥰1
Baadhi ya mijadala inayoendelea ndani ya JamiiForums.com kupitia Jukwaa la JF Garage (Magari na Vyombo vya Usafiri)

1. Fanya utafiti kuhusu gari, epuka madalali, epuka gari lililopigwa rangi na kuoshwa engine, huo ni sehemu ya ushauri uliotolewa na Mdau kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa kununua gari lililotumika

Kujua njia nyingine bofya: https://jamii.app/GariTumika

2. Wadau wajadili kuhusu hali walizozipata baada ya kununua gari kwa mara ya kwanza ikiwemo kukosa usingizi na kusahau kama wanamiliki gari

Kushiriki mjadala huu bofya: https://jamii.app/NunuaGariKwanza

3. Mdau anashauri njia mbalimbali zinazoweza kufanya gari lako lidumu muda mrefu ikiwemo kuendesha taratibu, kufanya matengenezo mara kwa mara na kupaki sehemu yenye kivuli

Kushiriki mjadala huu bofya: https://jamii.app/GariKudumuMuda
👍4
Mdau wa JamiForums.com anadai Mfumo wa Mtandao unaowezesha Watumishi wa Serikali kujihudumia katika mambo mbalimbali (Employee Self Service - ESS) una changamoto nyingi ikiwemo kufanya uhamisho kutoka Taasisi moja kwenda nyingine

Anadai hali hiyo imesababisha Watumishi wengi kufuatilia maombi yao katika Ofisi za Utumishi kwa kuwa Mfumo wa Mtandao hauwapi majibu wanayoyategemea na pia wengi hawana uelewa wa kutumia, hivyo anaomba Serikali iangalie suala hilo kwa kuwa wanaoathirika ni wengi

Soma https://jamii.app/UhamishoChangamoto

#Governance #JFHuduma #JFUwajibikaji #JamiiForums
👍5