JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MOROCCO: Takriban Watu 2,862 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2562 wamejeruhiwa kufuatia Tetemeko la Ardhi lililoipiga Nchi hiyo mwishoni mwa Wiki iliyopita. Ni Tetemeko la pili kusababisha maafa makubwa tangu mwaka 1960 Nchi hiyo ilipopigwa na Tetemeko lililoua zaidi ya Watu 12,000

Takwimu za Emergency Event Database zinaonesha tangu mwaka 1946, Nchi za Morroco, Algeria, Misri na Libya kutoka eneo la Kaskazini mwa Afrika zimekumbwa na Matetemeko 10 yaliyosababisha Vifo takriban 22,938 na Majeruhi zaidi ya 85,000

Soma https://jamii.app/QuakeUpdate

#JamiiForums #EarthQuake #ClimateChange #MoroccoEarthQuake #JFMatukio #JFUpdates
😒3πŸ€”2πŸ‘1
Wakati Bara la Afrika likiendelea kukabiliana na masuala kama vile Umaskini, Ongezeko la Magonjwa Yanayoambukiza na Yasiyoambukiza na Mtikisiko wa Masuala ya Kiutawala katika baadhi ya Nchi, Matukio ya Watu kujiua nayo yanaendelea kuwa janga linalokua kwa kasi

Mbali na changamoto za masuala ya Kijamii, Kiuchumi, Kitamaduni, Migogoro ya Kifamilia na Matumizi ya Dawa za Kulevya, Changamoto za Afya ya Akili zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Vifo vya Kujitoa Uhai Barani Afrika

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO) limezitaja Nchi 10 zenye idadi ndogo ya Vifo vya Kujiua ambazo ni Sierra Leone, Sao Tome, Algeria, Misri, Mauritania, Tunisia, Nigeria, Sudan, Sudan Kusini na Mali

Soma https://jamii.app/SuicideRateAF

#JamiiForums #MentalHealthAwareness #JFAfyaAkili #SuicideMortalityRate
❀2😁2πŸ‘1πŸ€”1
Haki ya Kupata Taarifa (#AccessToInformation) inahakikisha Wananchi wanawajibika kwa kufanya Maamuzi wakiwa na Taarifa Sahihi badala ya kutenda kwa Ujinga au Taarifa Potofu

Pia, Haki ya kupata Taarifa hutumikia kama 'Kiangalizi' cha kuhakikisha Viongozi waliochaguliwa wanashikilia Viapo vyao vya Ofisi na kutekeleza matakwa ya waliowachagua

Soma https://jamii.app/AccessToInformation

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘3
Akizungumza katika Siku ya Pili ya Mkutano Maalum wa Vyama vya Siasa wa Kujadili Hali ya Demokrasia na Siasa Nchini, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Abdul Nondo amesema ili kuwa na Uchaguzi wa Huru na wa Haki, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe na TAMISEMI, uingizwe kwenye Sheria Ya Uchaguzi

Amesema "Wamesema kuna Muswada wa Sheria ya Uchaguzi ambao unapaswa kupelekwa Oktoba na Novemba, tunataka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uwepo kwenye hiyo Sheria ya uchaguzi na sio Sheria ya Serikali za Mitaa. Tukifanya hivyo tutakuwa na Uchaguzi unaopaswa kusimamiwa na Tume ya Uchaguzi na sio TAMISEMI"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘2
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amesema Watu wengi wanaingia kwenye Chaguzi zetu wakiwa na tofauti kubwa kwenye Viwango vya Kiuchumi, hali inayosababisha Watu wenye Uwezo Mzuri wa Kuongoza kukosa nafasi za Uongozi

Amesema "Ni ngumu sana kwa mtu mwenye uchumi mdogo kushinda Uchaguzi Tanzania. Wanaoshinda asilimia kubwa ni Watu wenye uwezo mkubwa kifedha. Tunaomba tuanze kufanya chaguzi za gharama ndogo ili kuwasaidia wenye uwezo mdogo kifedha kupata nafasi"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘2
Mwenyekiti wa Chama cha AAFP Walemavu, Ndonge Said Ndonge amesema CCM ilikosea Vyama vingine vya Siasa kwa kufanya Muafaka na CUF badala ya Vyama vyote. Na hivi sasa wamekuja na neno #Maridhiano ambayo wamefanya na Vyama Viwili pekee (CHADEMA na CUF)

Amesema "CCM waache kufanya Demokrasia ya Ubaguzi ya kukaa na Vyama walivyovikosea peke yake badala yake wakae na Watu wa Vyama vyote vya Siasa kutafuta muafaka na maridhiano"

Kuhusu mwitikio wa Wananchi kupiga kura amesema "Tangu Uhuru nyie tu hamchoki kuongoza CCM? Achieni wengine pia Madaraka. Watu hawajitokezi kupiga kura kwa sababu wanajua tukienda kupiga kura CCM itashinda na tusipoenda kupiga kura bado CCM itashinda"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘7
Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Ivan Maganza amesema Demokrasia ndani ya Vyama vya Viasa haipo, hali inayosababisha Unyanyasaji na Kukatishwa tamaa kwa Vijana na Wanawake wa Vyama husika

Amesema "Ofisi ya Msajili imulike hivi Vyama kwa upande wa Wanawake na Vijana. Demokrasia iimarishwe ndani ya Vyama ili Wananchi waone haja ya kushiriki uchaguzi"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘4❀1😁1
Akizungumzia Mchakato wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya #KikosiKazi, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, Abdul Nondo amesema "Ni muhimu tuwe na ratiba ya utekelezaji, mfano; katika #Maridhiano yaliyokuwa yanafanyika #Zanzibar kulikuwa na ratiba ya utekelezaji"

Ameongeza "Tunapokutana hapa tunajadili bila Serikali kutuambia ratiba ya utekelezaji ni ipi, tutakuwa hatufanyi jambo lolote la msingi"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘6😁2❀1
Uamuzi huo umechukuliwa na Mahakama ya Kitaifa ya Italia yenye dhima ya kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini dhidi ya kiungo huyo wa Juventus, #PaulPogba (30)

Mahakama hiyo imesema Pogba alifanyiwa vipimo baada ya ushindi wa Timu yake dhidi ya #Udinese, Agosti 20, 2023, majibu yalionesha kuwa licha ya kutocheza alikuwa na viwango vya juu vya homoni ya "Testosterone"

Atafanyiwa vipimo kwa mara nyingine na akipatikana na hatia anaweza kufungiwa kucheza Soka kwa muda wa miaka miwili hadi minne

Soma https://jamii.app/PPogba

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘4😁2
Akiongea kwenye Mkutano wa Vyama vya Siasa wa Kujadili Mapendekezo ya #KikosiKazi, Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ACT-Wazalendo, Yassin Mohamed amesema ili Rais apate nishani ya kuaminika, lazima ahakikishe Uchaguzi unakuwa wa Haki. Walioshinda watangazwe na Walioshindwa wasitangazwe kama washindi

Amesema "Kwenye makabrasha tunaona Demokrasia na Amani, lakini haya yote hayawezi kufanyika ikiwa hakuna Haki. Haki ndiyo inayoanza. Vurugu unazozisikia huko nje ni kwa sababu ya kukosekana kwa Haki. Haijalishi tuna Sheria gani au #Katiba gani, ikiwa haki hakuna, vyote havipo"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘1
SIMIYU: MTUHUMIWA WA UBAKAJI AHUKUMIWA VIBOKO 8 NA FIDIA TSH. LAKI TATU

Boniphace Abel (18) Mkazi wa Nyashimba, Magu-Mwanza amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Itilima-Simiyu adhabu ya kuchapwa viboko na kulipa fidia kwa kosa la kumbaka Msichana mwenye umri wa miaka 17 na kumsababishia majeraha

Mwendesha Mashtaka wa Wilaya (Mkaguzi Msaidizi wa Polisi), Jaston Mhule amesema Kifungu cha 131 Kifungu Kidogo cha Pili cha Sheria, Kanuni ya Adhabu kinaeleza Mshtakiwa wa kesi ya ubakaji akiwa na umri wa miaka 18 kushuka chini adhabu yake ni viboko, mwenye umri wa miaka 19 kuendelea adhabu yake ya chini ni miaka 30 jela

Soma https://jamii.app/KesiHukumuSimiyu

#JFMatukio #SocialJustice #HumanRights #JamiiForums
πŸ‘4❀1😁1
Mwenyekiti wa Klabu ya Watanzania waishio Nje ya Nchi (Diaspora Club), Kevin Nyamori amesema Wapiga kura hawapati nafasi ya kuwajua vizuri wagombea kwani muda wa kutangaza nia unaotolewa na Tume ya Uchaguzi ni usiozidi Miezi Miwili. Ni wachache tu huweza kufanya kampeni na kujitangaza kwa Wapiga Kura ndani ya muda huo mfupi

Amesema "Mtu akitangaza leo kuwa ana nia ya kugombea Urais mwaka 2025 itamuathiri vipi Rais aliye madarakani? Kukiwa na uwezo wa kufanya hivi itasaidia Vyombo vya Usalama na Vyombo vya Habari kumchunguza huyu mtu na kumwanika. Kama atakuwa hana mabaya, basi itakuwa ni sifa kwake. Kama atakuwa ana mabaya, basi atajitathmini sababu ya muda mrefu ambao Watu wamemfuatilia na kumwelewa vizuri"

Fuatilia Mubashara https://jamii.app/MkutanoSikuYaPili

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
πŸ‘6
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baadhi Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa (NPC KIUTA) wamelazimika kuishi ndani ya kiwanda hicho kwa siku tatu na wengine wakizuiwa kuingia ndani sababu ikidaiwa ni mgogoro unaoendelea kuhusu uuzwaji wa kiwanda hicho

Kiwanda hicho chenye Watumishi zaidi ya 130 kikiwa chini ya Umiliki wa Wanahisa 152 kimesitisha huduma kwa siku kadhaa ikidaiwa Wanahisa wanakataa mchakato wa kiwanda hicho (Kitalu Namba 13) kuuzwa kwa Mwekezaji anayemiliki Kiwanda cha Superdoll

Soma https://jamii.app/NPCKiuta

#JFUwajibikaji23 #Governance #JamiiForums
πŸ‘2
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya TabiaNchi (GCA)

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Rais wa Senegal, Macky Sall, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Akinumwi Adesina na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Fedha kutoka IMF, Kristalina Georgieva

GCA ni Taasisi inayosimamia masuala ya Uhimilivu wa Mabadiliko ya TabiaNchi ambapo hadi sasa imewezesha upatikanaji wa zaidi ya Tsh. Trilioni 125 ambazo Tanzania itakuwa kati ya Wanufaika kwa miaka 3 ijayo

Soma https://jamii.app/UteuziSamia

#JamiiForums #Governance #ClimateChange #Accountability
❀3😁2πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limepiga marufuku tabia ya baadhi ya Watu wanaojihusisha na matukio yanayotajwa ni kuondoa imani za giza kwenye Makazi ya Watu wanaojulikana kwa jina la β€œKamchape" au β€œLambalamba”
-
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema Watu hao wamejitokeza katika Mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa na Songwe na kuwa wanatumia mbinu hiyo kufanikisha uhalifu alioutaja kuwa ni utapeli, wizi, udhalilishaji, ukiukwaji wa Haki za Binadamu, uporaji na uharibifu wa mali, kuchonganisha na kuchochea mauaji

Hivi karibuni, Mdau wa JamiiForums.com alisema matukio hayo yana mazingira ya Udhalilishaji, Utapeli na nia ya kuharibu amani

Soma https://jamii.app/PolisiKamchape

#Governance #Maisha #Lifestyle #SocialJustice #JamiiForums
πŸ‘5πŸ‘Ž1
Uangalizi wa Uchaguzi una umuhimu mkubwa katika Nchi zilizopitia kipindi fulani cha Mizozo, ambapo makundi ambayo yamekuwa yakishindana yanaweza kuwa na mashaka na Mfumo wa Kisiasa na Mchakato wa Uchaguzi

Kwa namna ya kipekee, Waangalizi au Wasimamizi wa Kimataifa katika Nchi zilizowahi kuwa kwenye vita wanaweza kupewa Mamlaka ya kuthibitisha au kubatilisha Matokeo ya Uchaguzi, japokuwa kwa kawaida Waangalizi hawana uwezo wa kuingilia Mchakato wa Uchaguzi, wanaweza tu kuchunguza, kutathmini na kutoa ripoti

Soma https://jamii.app/ElectionObservation

#JamiiForums #Democracy #Governance #JFDemokrasia #WikiYaDemokrasia2023 #DemocracyWeek2023
❀1
Baada ya kukamilika kwa Uwasilishaji wa Makala za Washiriki na Mchakato wa Majaji kutafuta Washindi kwa kuangalia Vigezo na Masharti vya Shindano la #StoriesOfChange2023 ukiendelea, sasa ni wakati wa wale wanaoelekea kuwa Washindi kutafutwa

Hivyo basi, kama ulishiriki Shindano hili unashauriwa kukaa karibu na Private Message (PM) kupitia akaunti yako ya JamiiForums.com ili usipitwe na ujumbe kutoka JamiiForums

#JamiiForums #SoC2023 #StoriesOfChange #Accountability #Governance
πŸ‘1
Hadi kufikia Januari 2023, Nchi za Kaskazini na Kusini mwa Afrika zilikuwa na idadi kubwa zaidi ya Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii Barani Afrika ambapo Mtandao wa WhatsApp umeongoza kwa kuwa na Watumiaji wengi ukifuatiwa na Facebook

Kwa upande wa Nchi za Afrika Mashariki matumizi ya Mitandao ya Kijamii ni 8.4% nafasi ya pili kutoka mwisho huku Nchi za Afrika ya Kati zikiwa mwishoni kwa 7.4% Barani Afrika. Kati ya sababu zilizotajwa kushusha idadi ya Watumiaji ni pamoja na Gharama Kubwa za Intaneti

Vipi Mdau ni changamoto gani unakutana nayo linapokuja suala la kutumia Mitandao ya Kijamii?

Soma https://jamii.app/SocialMediaAfrica

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #SociaMedia
😁1
#ELIMU: Jumla ya Watahiniwa 1,397,370 wa Darasa la 7 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi Septemba 13 na 14, 2023 Nchini kote, idadi ikiwa na ongezeko la Watahiniwa 13,030 kutoka Watahiniwa 1,384,340 waliofanya Mtihani mwaka 2022

Kati ya Watahiniwa Milioni 1.34 waliofanya Mtihani huo mwaka 2022, Waliofaulu kwa Madaraja A, B na C walikuwa 1,073,402 (79.62%) na waliopata Daraja D walikuwa 310,938, idadi ambayo ilishusha ufaulu kwa 2.35%

Soma https://jamii.app/STD72023

#JamiiForums #Governance #JFHakiElimu #SocialJustice #JFDATA
πŸ‘6❀1πŸ™1
Dalili zinazoonekana sana ni Uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Hufanya Watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana Mishipa ya Mwili

Wakati mwingine Mtoto huweza kupata Homa ambazo hazisikii Matibabu ya kawaida.

Pia, Mtoto anaweza kuanza kukosa choo vizuri, kukojoa Damu, au kuishiwa Damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya Saratani aliyoipata

Soma https://jamii.app/CCAM2023

#JamiiForums #CCAM #ChildhoodCancer #CancerAwareness #PublicHealth
πŸ‘2