MDAU-DAR: TCU FUATILIENI MIFUMO YA KUJIUNGA VYUO INACHEZEWA NA BAADHI YA VYUO
Anadai baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutoa majina ya walioteuliwa kujiunga na vyuo, wale walioteuliwa kwenye zaidi ya chuo kimoja wana changamoto ya kulazimishwa kujiunga kwenye vyuo ambavyo sio machaguo yao
Anadai baadhi ya vyuo vinaingia kwenye mfumo huo na ‘kuthibitisha’ kwa niaba ya Mwanafunzi bila ridhaa ya mhusika, hivyo Mwanafunzi akiingia anaona tayari amechaguliwa jina katika chuo fulani na kutakiwa kuendelea na udahili ikiwemo kulipa ada na gharama nyingine
Mdau mwingine anatoa mfano akidai Chuo cha Afya cha SJCHAS ambacho ni Tawi la Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT) kimeweka utaratibu wa kutaka kila Mwanafunzi aliyetuma maombi kulipa ada na gharama nyingine ndipo apewe kiunganishi ‘link’ cha kuingia kwenye mfumo wao, utaratibu ambao upo nje ya maelekezo ya #TCU
Soma https://jamii.app/ChuoTCU
#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance #Accountability

👍5❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
PROF. MKENDA: ASILIMIA 20 HADI 30 YA WAHITIMU WA SHULE ZA MSINGI HAWAENDELEI NA MASOMO YA SEKONDARI
Waziri Akizungumzia kuhusu mchakato wa Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na mabadiliko ya Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu, Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema Rasimu hiyo itasaidia kuondoa changamoto hizo ili kufikia hatua ya Wahitimu wote kuendelea na masomo ya Sekondari
Kuhusu Mtaala wa masomo ya Amali, amesema “Amali ni ufundi stadi, humo ndani kuna mafunzo ya ufundi pamoja na vipaji kama vile muziki, michezo n.k. Lengo anayehitimu Darasa la 6 awe na ustadi bila kusubiri afike Shule maalum, pia masomo hayo hayatamzuia Mwanafunzi yeyote kuendelea na masomo yake ya Chuo Kikuu.”
Soma https://jamii.app/ElimuMfumo
#JFHakiElimu #Governance #JamiiForums

❤6👍4
JamiiForums iliendesha mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Klabu ya Waandishi wa Mkoa wa Kigoma. Mafunzo yalijumuisha Waandishi wanaofanya kazi kwenye Vyombo vya Habari vya Kidigitali (Online Media) na vya Kawaida (Mainstream Media)
Mafunzo yaliyotolewa ni mwendelezo wa Makubaliano kati ya JamiiForums na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) yanayolenga kuwajengea uwezo Waandishi hasa katika kuandika Habari zenye Maslahi kwa Umma
Malengo mengine ni kuhamasisha Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Haki ili kuchochea Uwajibikaji, Demokrasia na Utalawala Bora. Mafunzo haya ni endelevu na yanalenga kufikia Waandishi wengi zaidi katika Klabu zote nchini.
#JamiiForums #DigitalRights #CitizenJournalism #JFDigitali

👍7
#TETESI: Mshambuliaji #RomeluLukaku Raia wa Ubelgiji anatarajiwa kutua AS Roma kwa mkopo wa Tsh. Bilioni 16 kuungana na #JoseMourinho aliyewahi kuwa Kocha wake miaka kadhaa iliyopita
#Chelsea imekubali ofa ya Tsh. Bilioni 15 badala ya Tsh. Bilioni 25 iliyotaka awali ili kumruhusu Lukaku (30) kwenda kwa mkopo ambapo pia atalazimika kupunguza mshahara wake anaolipwa kwa sasa Tsh. Bilioni 1 kwa wiki
Awali, #InterMilan ilitaka kumsajili baadaye ikajitoa katika mchakato, #Juventus nayo ilionesha nia lakini mashabiki wa timu hiyo waliandamana wakidai hawamtaki. Aidha, Lukaku alikataa ofa ya kuhamia #AlHilal ya #SaudiArabia
Soma https://jamii.app/LukakuRoma
#JFSports #JamiiForums

👏5👍2
Tangu kupatikana kwa Uhuru, Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) imeongozwa na Wakurugenzi 11 walioshika nafasi hizo kwa idadi ya miaka inayotofautiana kulingana na mahitaji ya Utawala husika
Emilio Mzena ndio Mkurugenzi wa kwanza wa TISS na aliongoza Idara hiyo kwa miaka 14 ambayo ni mingi kuzidi wengine waliomfuatia. Mzena alipewa heshima kwa jina lake kutumika katika Hospitali ya Viongozi ya Mzena
Hadi sasa, aliyeongoza kwa muda mfupi ni Said Hussein Masoro aliyeteuliwa Januari 2023 na kuondolewa Agosti 28, 2023 ambapo ameteuliwa kuwa Balozi. Idara hiyo imepata Mkurugenzi mpya, Balozi Ali Idi Siwa ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Oparesheni za Ndani za TISS.
Soma https://jamii.app/TISSDGS
#JamiiForums #Governance #Accountability #NationalSecurity

👍8
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, amesitisha uzinduzi wa Soko la Zakhiem baada ya kubaini kuna Madalali wamechukua Fedha za Wafanyabiasha kwaajiili ya kuwauzia Vizimba kinyume na utaratibu
Chalamila ametoa muda wa Wiki Moja kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchunguza waliofanya njama hiyo na kuwachukulia hatua za Kisheria
Soma https://jamii.app/SokoZakhiem
#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji23 #SerikaliBilaRushwa #JFHuduma #KemeaRushwa #SocialJustice

👍11
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga, amesema upangwaji wa Mikopo ya Elimu ya juu unaongozwa na Sheria za Bodi ya Mikopo na inawahusu wenye sifa za kujiunga na Elimu ya Juu lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za Elimu
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Sophia Mwakagenda aliyehoji sababu za kuwepo ugumu wa upatikanaji wa Mikopo kwa Wanafunzi waliosoma Shule binafsi
Soma https://jamii.app/BungeAgosti29
#Governance #JFHakiElimu #JamiiForums #ServiceDelivery

👍4
MDAU-ARUSHA: KATA YA MURIET HATUNA HUDUMA YA MAJI KWA MIEZI MIWILI
Mdau wa JamiiForums.com anadai Wananchi wa Mtaa wa #Agape, Kata ya #Muriet hawana huduma ya maji kwa mwezi Julai na Agosti 2023 na hakuna maelezo ya kueleweka kutoka kwenye Mamlaka
Mdau anadai licha ya Wananchi kufanya jitihada za kuwasiliana na kufikisha kero hiyo kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) wamekuwa wakijibiwa kuwa kuna changamoto ya ‘Valvu’ zaidi ya hapo hakuna ufafanuzi mwingine, hali inayowapa wakati mgumu kutafuta maji kutoka maeneo tofauti
Soma https://jamii.app/MajiMuriet
#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #JamiiForums #ServiceDelivery

#BUNGENI: Mbunge Kasalali Emmanuel Mageni akizungumza kuhusu mafao ya Mifuko ya Hifadhi ya Kijamii, amehoji Serikali itawasilisha lini hoja ya kufuta Kikokotoo cha Mafao kilichopo kwasababu hakikubaliwi na Watumishi na Wastaafu
Akitolea Ufafanuzi, Naibu Waziri, Patrobas Katambi, amesema mpango wa Serikali ni kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu Kanuni Mpya ya Mafao ya Kikokotoo iliyotangazwa Julai 1, 2022, akitoa mfano sehemu ya maboresho ya mafao ya mkupuo yalikuwa 25% na baada ya mabadiliko yamekuwa 33%
Soma https://jamii.app/BungeAgosti29
#Governance #JamiiForums

👏5👍4❤2
Kwa mujibu wa Kifungu cha 60 (3) (b) na 60 (6) (b) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 ni makosa kwa Kampuni kufichua/kuruhusu Taarifa Binafsi kuonwa (Access) na asiye Mhusika wa Taarifa hizo
Mfano: Kuruhusu Mtu yeyote kuweza kupata taarifa za mmiliki wa Gari kwa kuingiza namba ya usajili wa Gari ya Mhusika kwenye Mifumo ya Kiteknolojia
Ukiukwaji wa Kifungu hiki kwa Kampuni au Shirika utapelekea Adhabu ya kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi shilingi bilioni tano.
#JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #DigitalRights #JFDigitali