JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2023, uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji, Dkt. Eliezer Feleshi

Sheria zilizowasilishwa kufanyiwa marekebisho ni Sheria ya Nguvu ya Atomu Sura ya 188, Sheria ya Mamlaka ya Nchi juu ya Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449

Nyingine ni Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba Mali na Rasilimali Asilia na Sheria ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, Sura ya 159

Kuhusu marekebisho ya Sheria ya Nguvu ya Atomu Sura ya 188, amesema Kifungu cha 4 kinarekebishwa ili kuongeza mawanda ya udhibiti kwa kushusha viwango vya vyanzo mbalimbali vya mionzi inayosimamiwa na sheria hiyo

Soma https://jamii.app/BungeAgosti29

#Governance #JamiiForums
πŸ‘3❀1
#MICHEZO: Klabu ya Singida Fountain Gate imetangaza kuachana na Kocha Hans van der Pluijm ambapo nafasi ya Kocha Mkuu imekabidhiwa kwa Msaidizi wake, Mathias Lule hadi hapo Uongozi wa Klabu utakapofanya maamuzi tofauti

Taarifa ya Singida imeeleza maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya Pluijm kuamua kujiuzulu mwenyewe kutokana na sababu binafsi

Soma https://jamii.app/SingidaKocha

#Sports #JamiiForums
πŸ‘8❀1
LIGI KUU: YANGA YAPIGA MPIRA MWINGI, YAICHAPA JKT 5-0 NA KUTINGA KILELENI

Yanga imefanikiwa kushika usukani wa Ligi Kuu Bara baada ya kuichakaza #JKTTanzania kwenye Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam na kufikisha Pointi 6 na Magoli 10 ya kufunga katika Mechi 2 za msimu wa 2023/24

Klabu hiyo inaweka rekodi ya kufunga mabao mengi kuliko timu nyingine huku ikiwa haijaruhusu lango lake kuguswa hata mara moja msimu huu.

Soma https://jamii.app/YangaAgosti29

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘10πŸ”₯4❀1
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa tamko hilo baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai baadhi ya Vyuo vinaingilia Mfumo wa Udahili kwenye akaunti za Wanafunzi na kufanya uthibitisho bila ridhaa ya mhusika hasa kwa waliopata nafasi ya kuchaguliwa zaidi ya chuo kimoja

Katibu Mtendaji wa #TCU, Prof. Charles Kihampa asema wamepokea taarifa hizo na wanazifanyia uchunguzi, ikibainika kuna Vyuo vinafanya mchezo huo hatua kali za Kisheria zitachukuliwa

Anasema β€œMwanafunzi ambaye amekwama au kulazimishwa na chuo awasiliane na TCU. Pia, kutakuwa na madirisha matatu ya Udahili ikiwezekana tutaongeza moja.”

Soma https://jamii.app/TCUUdahili

#JamiiForums #JFHakiElimu #JFHuduma #Governance #Accountability
πŸ‘13
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kwa mujibu wa Ripoti ya #SpeedtestGlobalIndex ya Julai 2023, #AfrikaKusini ndio Nchi yenye Intaneti ya Simu yenye Kasi zaidi Barani Afrika ikiwa na uwezo wa kupakua 'Megabits' 45.06 kwa Sekunde

#Tanzania iko nafasi ya 14 Afrika ikiwa na Kasi ya 'Megabits' 21.07. Kwa upande wa Afrika Mashariki, #Uganda imetajwa kuongoza ikiwa na Kasi ya 'Megabits' 38.53, #Rwanda 27.34 na #Kenya 24.20

Vipi Mdau, unaridhishwa na Kasi ya Intaneti ukilinganisha na gharama unazolipa?

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #InternetSpeed
πŸ₯΄5❀3πŸ‘1
WANAHARAKATI: KUTOA ELIMU YA KATIBA KWA MIAKA MITATU, ITAFIKA 2030 HATUTAKUWA NA KATIBA MPYA

Wanaharakati wa #Katiba na #HakiZaBinadamu wamekosoa kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, juu ya kutoa elimu ya Katiba kwa kipindi cha Miaka mitatu, wakidai mpango huo unalenga kuchelewesha mchakato na upotezaji wa Fedha za Umma

Tamko limetolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (#THRDC) na Jukwaa la Katiba (#JUKATA), wakipendekeza muda wa kuandaa Katiba hadi ipatikane na kutumika usizidi Miaka mitano

Soma https://jamii.app/TamkoKatiba

#Democracy #KatibaMpya #Governance #Demokrasia #JamiiForums
😁2πŸ‘1
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu amemteua Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Katika nafasi ya Waziri wa Nishati, Biteko atachukua nafasi ya January Makamba aliyehamishwa Wizara

Katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko atakuwa akishughulikia masuala ya uratibu wa shughuli za Serikali

Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Biteko alikuwa ni Waziri wa Madini.

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#Governance #JamiiForums
πŸ‘12❀5
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi ya Dkt. Damas D. Ndumbaro

Kabla ya Uteuzi huo, Pindi Chana alikuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘5πŸ‘Ž2
#UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Januari Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Dkt. Stergomena Tax

Kabla ya Uteuzi huo, Makamba alikuwa Waziri wa Nishati

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘Ž10πŸ‘6πŸ‘5
ο»ΏUTEUZI: JERRY SILAA AWA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Anachukua nafasi ya Dkt. Angeline Mabula

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘6πŸ‘1
STERGOMENA TAX AREJESHWA WIZARA YA ULINZI

Dkt. Stergomena Lawrence Tax amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenda kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Amewahi kuwa Waziri wa Ulinzi kuanzia Mwaka 2021 hadi 2022

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘6
RAIS SAMIA AVUNJA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI. AUNDA WIZARA MBILI MPYA

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kuunda Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi

Amemteua Prof. Makame Mbarawa aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuwa Waziri wa Uchukuzi

Amemteua Innocent Bashungwa, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuwa Waziri wa Ujenzi

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governace
πŸ‘4
UTEUZI: ANTHONY MAVUNDE ATEULIWA KUWA WAZIRI WA MADINI

Rais Samia Suluhu amemteua Anthony Peter Mavunde kuwa Waziri wa Madini

Kabla ya Uteuzi, alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘2
UTEUZI: KAIRUKI AONDOLEWA TAMISEMI, APELEKWA MALIASILI NA UTALII

Rais Samia Suluhu amemhamisha Mohamed Omary Mchengerwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI

ο»Ώο»Ώο»ΏAidha, Angellah Jasmine Kairuki amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwenda kuwa Waziri wa Maliasili na Utali

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
πŸ‘8πŸ€”1
#UTEUZI: ALEXANDER MNYETI NAIBU WAZIRI KILIMO

Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Mbunge wa Misungwi, Alexander Mnyeti kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

Soma https://jamii.app/CabinetReshufle

#JamiiForums #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: DAKTARI 'FEKI' AKAMATWA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa, Mkazi wa Dar es Salaam amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akidaiwa kujihusisha na vitendo vya kutapeli Wananchi katika Jengo la Mwaisela

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Aminiel Aligaesha amesema hilo limefanikiwa kutokana na ulinzi kuimarishwa Hospitalini hapo na mtuhumiwa amefikishwa Kituo cha Polisi Selander

Soma https://jamii.app/MuhimbiliAgosti30

#JFMatukio #JamiiForums
πŸ‘4
GABON: Rais Ali Bongo aliyekaa madarakani kwa miaka 14, amewekwa kizuizini na Jeshi la Nchi hiyo muda mfupi baada ya Jeshi hilo kutangaza kuwa halikubaliani na matokeo ya Urais na hivyo linayafuta pamoja na kuwaondoa kazini Viongozi wa Taasisi zote za Umma

Wengine waliokamatwa ni Mtoto wa Rais, ambaye ni Mshauri wake wa karibu, Noureddin Bongo Valentin, Katibu Mkuu Kiongozi, Makamu wa Rais, Washauri wengine wa Rais na Maafisa Wakuu wa Chama Tawala cha PDG

Kwa mujibu wa Jeshi, Viongozi hao wanatuhumiwa kwa Uhaini, Ubadhirifu, Rushwa na Kughushi Saini ya Rais na tuhuma nyingine

Soma https://jamii.app/GabonCoup

#JamiiForums #Governance #Democracy #Accountability
πŸ‘13😁9
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Saa chache baada ya Kikundi cha Jeshi la #Gabon kutangaza kumuondoa Madarakani Rais #AliBongo na kumuweka Kizuizini, Kiongozi huyo ameonekana katika Video akiomba msaada kwa Nchi alizoziita Marafiki

#JamiiForums #Governance #Accountability #Democracy #GabonCoup
😁7πŸ‘2❀1πŸ‘1
UTEUZI: MNYETI AHAMISHIWA WIZARA YA MIFUGO, SILINDE APELEKWA KILIMO

Rais Samia amefanya uhamisho wa Manaibu Waziri kama ifuatavyo;

David Silinde aliyekuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anakuwa Naibu Waziri Wizara ya Kilimo

Alexander Mnyeti aliyeteuliwa leo Agosti 30, 2023 kuwa Naibu Waziri Wizara ya Kilimo anaenda kuwa Naibu Waziri - Mifugo na Uvuvi

Aidha Rais, amemteua Mhandisi Aisha Amour kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi

#JamiiForums #Governance
πŸ‘4❀1
UTEUZI: Rais Samia amemteua Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Y. Sefue kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango

Wengine walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume hiyo ni Omar Issa ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela

Pia, Ami R. Mpungwe ambaye ni Balozi Mstaafu na Mjasiriamali pamoja na Maryam Salim ambaye ni Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia Nchini Cambodia wameteuliwa katika nafasi hiyo

#JamiiForums #Governance
πŸ‘2