JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CAF: YANGA 1-1 AL HILAL

Timu hizo zimetoshana nguvu kwenye Uwanja wa Mkapa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, leo Oktoba 8, 2022

Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 16, 2022, Mshindi wa hapo atasonga mbele hatua ya Makundi ya Michuano hiyo

Soma https://jamii.app/YangaAlHilal

#JFSports #CAF
👍9😁2
#JFAFYA: Changamoto ya Kiungulia kwa Wajawazito hutokana na mabadiliko makubwa ya Mfumo wa Homoni pamoja na kasi ya ukuaji wa Mtoto ambayo huleta mgandamizo kwenye Tumbo la Chakula

Soma https://jamii.app/HeartBurnTips

#JFAfyaJamii
👍8
Ustahimilivu wa Digitali ni uwezo wa kujikwamua kutoka nyakati ngumu anazopitia Mtu Mtandaoni kama vile Kuonewa, Kutukanwa, au kubaguliwa

Hii inajumuisha kuwa na uwezo wa Kuelewa unapokuwa hatarini, kujua la kufanya ikiwa utakutana na Mabadiliko Usiyoyatarajia, kujifunza kutokana na unachopitia Mtandaoni na kuweza kupona kutokana na Misukosuko ya Mtandaoni

Soma https://jamii.app/DigitalResilience

#DigitalRights
👍8
UGANDA: SERIKALI YARIDHIA MAJARIBIO YA CHANJO MPYA ZA EBOLA

Kwa mujibu wa WHO, aina 8 za chanjo zitafanyiwa majaribio baada ya ufanisi hafifu wa chanjo za awali kutokana na kutofautiana kwa aina Kirusi kilichopo nchini humo

Soma https://jamii.app/EVDTrials

#PublicHealth #Governance
👍2😁1
META: HUENDA WATUMIAJI MILIONI 1 WA FACEBOOK WAMEDUKULIWA

Programu zilizobainika kuwa sehemu ya ulaghai huo ni za Afya, Michezo na za Kuhariri Picha, ambapo huwahitaji Watumiaji kuingiza taarifa za akunti zao za Facebook

Soma https://jamii.app/MetaHack

#DataProtection #DataPrivacy
🤔1
IGAD: WATU MILIONI 51 AFRIKA MASHARIKI HAWANA UHAKIKA WA CHAKULA

Pia, ripoti hiyo ya Shirikisho la Maendeleo Afrika (IGAD) imeonesha kuwa Watoto milioni 10 wana Utapiamlo

> Zaidi ya Watu 380,000 wako hatarini kufa kwa njaa

Soma https://jamii.app/IGADFood

#FoodSecurity
👍5
IRAN: KITUO CHA UTANGAZAJI CHA TAIFA CHADUKULIWA WAKATI WA TAARIFA YA HABARI

Kwa sekunde kadhaa wadukuaji waliweka picha ya mtu aliyevaa kinyago ikafuatiwa na sura ya Kiongozi Mkuu, Ali Khamenei akizungukwa na Wanawake wanne waliouawa hivi karibuni

Soma https://jamii.app/IranChaos

#Governance
👍10😱2
NIGERIA: Maafisa wamegundua njia haramu iliyounganishwa kutoka baharini yenye urefu wa kilomita 4 inayodaiwa kupitisha mafuta ya wizi kwa miaka 9

Bomba lipo katika kituo kinachotoa mapipa 250,000 ya mafuta kwa siku

Soma https://jamii.app/OilExport

#Governance #Accountability
👍15
NIGERIA: MASHUA YAZAMA, WATU 76 WAFARIKI

Maafa hayo yametokea katika Jimbo la Anambra, mashua ikiwa imebeba watu 85 kutoka Onukwu kwenda Nkwo Ogbakuba

Pia, watu watatu hawajulikani walipo katika Jimbo la Enugu kutokana na mafuriko

Soma https://jamii.app/76DieAnambra

#Governance
🤔2👍1😢1
HARRY MAGUIRE APEWA MAPUMZIKO MAN. UNITED

Kocha wa #ManUnited, Erik ten Hag ndiye ambaye amempa ruhusa hiyo ili apate muda wa kukaa sawa kiakili na kurejesha kiwango chake kutokana na presha kubwa anayopitia ya kushuka kiwango

Soma https://jamii.app/Maguire

#JFSports
👍10😁5🔥1
#JFAFYA: Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa Watu takriban Bilioni 2.2 wana changamoto za macho zinazohusisha upofu na uoni hafifu

Changamoto hizi zinaweza kuepukika kwa kutibu vizuri Magonjwa yanayoweza kudumaza #Afya ya Macho (Kisukari na Shinikizo kubwa la Damu)

Soma https://jamii.app/HealthyEyesTips

#AfyaJamii
👍5
CAF: AGOSTO 1-3 SIMBA

Magoli ya #Simba SC katika Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa yamefungwa na Clatous Chama, Israel Patrick na Moses Phiri kwenye Uwanja wa 11 de Novembro Jijini Luanda

Mechi ya marudio ni Oktoba 16, 2022, Uwanja wa Mkapa

Soma https://jamii.app/Agosto1Simba3

#JFSports
👍27🔥10👏1🎉1💩1
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya Utafiti kuhusu Hali ya Utawala na Rushwa (National Governance and Corruption Survey – NGACS) Tanzania Bara 2020

Wahojiwa walikuwa na Mitazamo tofauti katika Uelewa wao wa Maana ya Rushwa ambapo Asilimia 63.6 walisema Rushwa ni "Uhitaji wa malipo yasiyo rasmi"

#JamiiForums #KemeaRushwa #UtafitiTAKUKURU
👍7
KENYA: WAATHIRIKA WA VVU WALALAMIKA SIRI ZAO KUVUJA

Sababu ni Kliniki za Wagonjwa wa VVU kuwa maeneo ya wazi katika Hospitali

Waathirika wanadai kuitwa majina yao kwa sauti na watoa Huduma wakati wa kuwapatia Dawa za kupunguza makali ya virusi

Soma https://jamii.app/HIVDataKenya

#DataPrivacy
👍18🥰1
ZANZIBAR: TRA KUPIGA MNADA MALI ZA MBUNGE AKIDAIWA USHURU WA GARI NA KODI

Mbunge Toufky Turky ameshindwa kulipa ushuru wa Gari aina ya Marcedes Benz G Wagon aliloliingiza Nchini Januari 2022

Pia, Kampuni yake ya Mifuko inadaiwa Tsh. Milioni 170.5 huku msamaha wa kodi alioomba ukikataliwa mara mbili

Soma https://jamii.app/TRATurky

#Uwajibikaji
👍12🤔1
UTAFITI TAKUKURU: Wahojiwa waliulizwa ni kwa kiasi gani waliona Rushwa kuwa mbaya katika Jamii ambapo Asilimia 81.5 walisema ni tatizo (44.7% waliona ni tatizo kubwa huku 36.8% waliona kama tatizo la wastani)

Ikilinganishwa na Mwaka 2009, zaidi ya Asilimia 90 ya Maafisa waliohojiwa katika Mikoa 11 walisema Rushwa ilikuwa tatizo kubwa katika Jamii huku Mikoa minne (4) ikiiona Rushwa kuwa si tatizo

#KemeaRushwa #JamiiForums #UtafitiTAKUKURU
👍6
OKTOBA 10: Siku ya Afya ya Akili Duniani ni Siku ya Kimataifa maalumu kwa kutoa #Elimu ya masuala ya #Afya ya Akili

Pia, Uhamasishaji na Utetezi dhidi ya Unyanyapaa wa Kijamii pamoja na athari zake kwa wale walioathiriwa na Walezi wao

Soma https://jamii.app/MentalHealthDay

#MentalHealthDay
👍1
USAMBAAJI WA SARATANI YA MATITI

Kwa kawaida Saratani husambaa kwa njia tatu zifuatazo;

1. Kupitia Tishu - Saratani husambaa kwenye Tishu za kawaida ambazo zimezunguka eneo la Saratani

2. Kupitia mfumo wa Limfu (Lymphatic System) - Saratani huvamia Mfumo wa #Lymph na kufuata Mishipa yake hadi sehemu nyingine za Mwili

3. Kupitia Damu - Saratani inaweza kusambaa kupitia Damu kwa kuvamia Mishipa ya Damu ya Vena (Veins) na Capillaries na kusafiri hadi Sehemu nyingine za Mwili.

#JamiiForums #BreastCancerAwarenessMonth #PublicHealth #JFAfya
👍2
UFARANSA: Mamilioni ya raia wameandamana wakiishinikiza Ufaransa kujitoa NATO na Rais Emmanuel Macron kujiuzulu

Pia, wameitaka Serikali kuacha kutoa silaha kwa #Ukraine kutokana na Uhaba wa Mafuta uliosababishwa na Vikwazo dhidi ya #Russia

Soma https://jamii.app/ParisProtests

#Democracy
👍20😁5👎2
Changamoto za kila siku za Maisha ya Binadamu ndiyo chanzo kikuu cha Matatizo ya Afya ya Akili

Pia, uwepo wa Majanga mapya ya kidunia kama COVID-19 unatajwa kuongeza tatizo la #AfyaYaAkili kwa zaidi ya 25%

Soma https://jamii.app/AfyaYaAkili2022

#MentalHealthDay
👍6