JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA YA AKILI

Kutoa Elimu kuhusu #AfyaYaAkili ikiwepo jinsi ya kuitunza, namna ya kuzungumzia na wapi pa kupata msaada ikiwa unapitia/unafahamu anayepitia changamoto hii

Kupunguza vihatarishi vya Afya ya Akili ikiwemo Migogoro ya Kimapenzi, Unyanyapaa wa Watu wenye Mahitaji Maalum na kuepuka dhana au Mila potofu katika Jamii

Soma https://jamii.app/AfyaYaAkili2022

#MentalHealthDay
πŸ‘6
UTAFITI TAKUKURU: Ilibainika Taasisi zinazoongoza kwa Rushwa Nchini #Tanzania ni:

Jeshi la Polisi limeshika nafasi ya kwanza (asilimia 45.6), likifuatiwa na Sekta ya Afya (asilimia 17.9) na Mahakama ya Sheria ilishika nafasi ya tatu kwa asilimia 11.9

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilishika nafasi ya nne (asilimia 6.1).
Miongoni mwa Kampuni, TRA ilishika nafasi ya pili ikionesha mwingiliano wa karibu kati yake na Sekta ya #Biashara

Taasisi hizi zilizoorodheshwa juu ni Sekta zilezile kama zilivyotambuliwa/zilizoripotiwa na NGACS ya 2009. (Jeshi la Polisi, Vituo vya Afya na Mahakama za Sheria)

#JamiiForums #UtafitiTAKUKURU #KemeaRushwa
πŸ‘11🀯2
RIPOTI: WATOTO WA KIUME 1,114 WAMELAWITIWA KWA MWAKA 2021

Idadi hiyo ni sawa na wastani wa Watoto 93 kila mwezi, huku imeelezwa kuwa 60% ya vitendo hivyo vimetokea kwenye ngazi ya familia

Soma https://jamii.app/UkatiliWatoto2021

#DomesticViolence #ChildRights #JamiiForums
πŸ‘6πŸ€”2🀯1
MOSHI: Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya imeahirishwa kwa mara ya 10 leo Oktoba 10, 2022 hadi Oktoba 24, 2022

> Mwendesha Mashtaka wa Serikali amesema ndani ya siku 90 upelelezi utakamilika kama Mwongozo mpya unavyotaka

Soma https://jamii.app/SabayaOktoba10

#JFMatukio
πŸ‘8
UTEUZI: Rais Samia amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Gabriel Paschal Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu

Pia, amemteua Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu

Soma https://jamii.app/WakiliMkuu

#Governance
πŸ‘14❀5
#JFAFYA: Wataalamu wa Afya wanasema Maziwa Fresh huleta ahueni ya muda mfupi kwa kutengeneza Utando juu ya Kuta za Vidonda

Pia, huongeza uzalishwaji wa Tindikali Tumboni pamoja na Vimeng’enya vingine ambavyo husababisha Maumivu makali zaidi baadaye

Soma https://jamii.app/UlcersTips

#JFAfyaJamii
πŸ‘9
MDAU: USTAHIMILIVU WA KIDIJITALI KATIKA TAASISI HULINDA HESHIMA

Anasema Taasisi hujenga Uaminifu wa kweli kwa Wateja wake kwa kuhakikisha Usalama wa Taarifa zao na Huduma Bora, hasa pale zinapojitokeza Changamoto za Kidigitali kama Kudukuliwa

Ameshauri Wafanyakazi kupatiwa Mafunzo yatakayowawezesha kupata ujuzi mpya wa Kidigitali ili kuendana na kasi ya Mabadiliko ya #Teknolojia

Soma https://jamii.app/DigitalResilience2

#DigitalWorld
πŸ‘6
WANAFUNZI 26 TU KATI YA 633 WAMEFAULU LAW SCHOOL YA TANZANIA

Idadi hiyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya Mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia Mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kushindwa

Wanasheria na wadau wengine wametaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu wakieleza Nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama Shuleni hapo

Soma https://jamii.app/LSTFails

#SocialJustice
πŸ‘9πŸ€”6
Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike huadhimishwa ili kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa Watoto wa Kike katika jamii

Pia, Kuangazia Changamoto zinazowakabili na kuangalia namna za kuwainua na kuwawezesha kufikia Malengo Yao

Soma https://jamii.app/GirlChildDay2022

#DayOfTheGirl
πŸ‘2
MTUHUMIWA ANA HAKI YA KUJUA UKOMO WA UPELELEZI WA MASHTAKA DHIDI YAKE

Mwongozo mpya wa Mashtaka unawaagiza Wakuu wa Mashitaka na Vyombo vya Uchunguzi kukamilisha Upelelezi ndani ya Siku 90

> Endapo Siku zitazidi, DPP atoe kibali maalumu

Soma https://jamii.app/DDPMashtaka

#JFHakiRaia
πŸ‘7πŸ”₯1
DAKTARI: MIREMBE KUNA WAGONJWA WANAUME WENGI KULIKO WANAWAKE

Veronica Lyimo ambaye ni Daktari wa Mirembe amesema upande wa umri wanapokea zaidi vijana wa umri wa miaka 20 hadi 45

> Ameongeza kuna Watu wenye umri wa miaka 50-70 lakini ni wachache

Soma https://jamii.app/Mirembe

#PublicHealth #JFAfya
πŸ‘5
NI HAKI YA MTUHUMIWA KUPEWA DHAMANA ENDAPO UPELELEZI HAUJAKAMILIKA

Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022, inawaagiza Wakuu wa Mashtaka na Vyombo vyote vya Uchunguzi kumpa Mtuhumiwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea

Kifungu cha 131A kimeweka ulazima wa kukamilisha Upelelezi kabla ya kufungua Mashtaka isipokuwa kwa makosa makubwa na yanayosikilizwa na Mahakama Kuu

Soma https://jamii.app/DDPMashtaka

#JFHakiRaia
πŸ‘6
KATIBU MKUU TEC: SERIKALI HAIWEZI KUDHIBITI RUSHWA BILA UWAZI

Padre Dkt. Charles Kitima amesema Wananchi wanapaswa kujua matumizi kwenye Miradi yote kwa ngazi mbalimbali ili kudhibiti wizi na Ubadhirifu wa Fedha za Umma

Soma https://jamii.app/KitimaRushwa

#KemeaRushwa #JFHakiRaia
πŸ‘6
Siku ya Mtoto wa Kike hutumika kama fursa ya kusaidia na kuimarisha Wasichana ili waweze kuishi Maisha Bora kwa kuangazia #Haki zao na namna ya kupunguza na kuondoa kabisa Vikwazo vya Kitamaduni, Mfano: Ndoa za Utotoni

Hata baada ya Dunia kuendelea katika nyanja Muhimu kama #Teknolojia, bado Wasichana wananyimwa Haki zao za Kimsingi kama Kupata Elimu bora, Huduma za Kiafya

Soma https://jamii.app/GirlChildDay2022

#DayOfTheGirl
πŸ‘6
MDAU: TUNAHITAJI VIONGOZI WANAOWAJIBIKA KWA WAKATI

Anasema, Kiongozi anayewajibika ni yule ambaye hasubiri kushtuliwa nini kifanyike pindi Changamoto za Kijamii au Kiuchumi zikijitokeza

Ametoa Wito kwa Viongozi Kuwajibika mapema katika kutatua Changamoto za Watu kabla hali haijawa mbaya na kuishia kutoa sababu zisizoeleweka

Soma https://jamii.app/MaonoUongozi

#accountability
πŸ‘4
INDIA: WANAKIJIJI HUZIMA INTANETI NA RUNINGA KWA MUDA ILI WAZUNGUMZE

Wakazi wa Kijiji cha #Maharashtra wamedai kujitangazia β€˜Uhuru’ kutoka ktk Dunia ya Kidigitali

Wanazima kila Siku Saa 1:00 - 2:30 Usiku wakiamini Watu wengi wamekuwa walevi wa Mitandao

Soma https://jamii.app/OfflineDaily

#DigitalRights
πŸ‘14❀9πŸ‘5
VYANZO VYA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI

1. Kibaiolojia - Inaweza kusababishwa na kurithi au kuumwa Magonjwa

2. Kisaikolojia - Baadhi ya visababishi ni Malezi, kutengana kwa Wazazi, Ugumu wa Maisha, kufiwa

3. Kijamii - Inaweza kusababishwa na changamoto za Kiuchumi, Ndoa na Upweke

Soma https://jamii.app/Mirembe

#JFAfya
πŸ‘9❀2
LINDA AFYA YAKO YA AKILI NA YA WENGINE

Ukarimu pamoja na Tabia Njema za Kushukuru, Kusamehe na Kuomba Msamaha wengine pamoja na Kuridhika husaidia kuilinda Afya ya Akili

Pia, ni Muhimu kuwa na Matumizi mazuri ya Mitandao ya Kijamii

Soma https://jamii.app/AfyaYaAkili2022

#MentalHealthDay
πŸ‘17πŸ‘1
AINA KUU MBILI ZA UMILIKI WA ARDHI TANZANIA

Umiliki wa kimila kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 (1999) na Umiliki kwa Hati, Mmiliki anaweza kumiliki kwa hati ya miaka 33, 66 au 99 na anakuwa na hadhi ya upangaji

Soma https://jamii.app/ElimuYaArdhi

#HakiRaia
πŸ‘9
RIPOTI IMF: UKUAJI UCHUMI WA DUNIA UTASHUKA HADI 2.7% MWAKA 2023

Mfumuko wa Bei utafika 9.5% huku nafuu ikitarajiwa Mwaka 2024

Nchi tajiri zaidi Duniani (G8) utakua kwa 1.1% kutoka 2.4% ya 2022

Kusini mwa Jangwa la Sahara utakua 3.7% kutoka 3.6%.

Zaidi https://jamii.app/IMF2023

#EconomyCrisis
πŸ‘11