JamiiForums
โœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBEYA: Watu 5 wamefariki na 31 kujeruhiwa ktk ajalli iliyotokea leo Okt. 11, 2022 katika Kijiji cha Ibula ikihusisha basi la Kyela Express na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likisafirisha msiba kutoka Dodoma kwenda Wilayani Kyela

Soma https://jamii.app/AjaliMabasi

#JFMatukio
๐Ÿ˜ข8๐Ÿ‘3
KAMPALA: KIFO CHA KWANZA CHA EBOLA CHARIPOTIWA

Aliyefariki alianza kuhudumiwa kienyeji, kisha akapelekwa hospitali. Alikutana na watu 42 kabla ya kifo chake

Kifo hicho kinafanya idadi ya waliofariki kwa #Ebola Uganda kufikia 19

Soma https://jamii.app/EbolaKampala

#PublicHealth
๐Ÿ‘9๐Ÿค”5
Kumuelimisha Binti ni suala kubwa zaidi ya kumpeleka Shuleni tu, Kunahusisha kuhakikisha anahisi kuwa salama akiwa Shuleni; Kuwa na Fursa ya kukamilisha Ngazi zote za #Elimu na Kupata Ujuzi wa kushindana katika Soko la #Ajira

Wasichana wanaopata #Elimu kwa Usawa wana Uwezekano mkubwa wa kuwa na Maisha Bora na kuepuka Ndoa katika Umri mdogo

Soma https://jamii.app/ElimuMtotoWaKike

#DayOfTheGirl
๐Ÿ‘8
MAREKANI YAIWEKEA VIKWAZO TALIBAN KWA KUKANDAMIZA WANAWAKE

Imechukua hatua hiyo kama adhabu kwa ukandamizaji unaofanywa tangu waingie madarakani Agosti 2021

> Vikwazo vinawahusu Wanachama wa sasa na wa zamani wa Taliban

Soma https://jamii.app/Taliban

#WomenRights
๐Ÿ‘5
KENYA: WABUNGE WATAKA SERIKALI KUZUIA WANAWAKE KWENDA KUFANYA KAZI ZA NDANI UARABUNI

Ni Kutokana na ripoti za Unyanyasaji wa Wafanyakazi wahamiaji katika Nchi hizo

Pia, Wameitaka Wizara ya Kazi kutoa ldadi ya Wakenya wanaofanya Kazi huko na hali ya Usalama wao

Soma https://jamii.app/KenyanDomesticWorkers

#HumanRights
๐Ÿ‘16๐Ÿ‘2
MDAU: DHANA YA KIONGOZI WA UMMA ATOKEE KATIKA UMASIKINI HAIFAI

Anasema dhana hiyo imesababisha Viongozi wengi wa juu kutoweka wazi ukweli kuhusu Mali wanazomiliki kama wanavyotakiwa kufanya, wakihofia kuonekana hawafai kuongoza

Soma https://jamii.app/SifaZaKiongozi

#Accountability
๐Ÿ‘8
MDAU: WANAFUNZI WENGI WANAOFELI 'LAW SCHOOL' TATIZO LINAANZIA VYUO VYA SHERIA

Anasema chanzo ni sifa za Udahili wa Wanafunzi wanaostahili kusomea Sheria kwani kuna Vyuo ambavyo hadi wanaopata alama ya D katika Masomo wanapata Nafasi

Anasema Asilimia kubwa ya wahitimu wa Sheria hawawezi hata kuandaa kiapo (Affidavit) na kuandaa Mashtaka (Plaint au Charge) au Utetezi

Soma https://jamii.app/MaoniLawSchool

#JFSheria
โค6๐Ÿ‘6๐Ÿค”3๐Ÿ‘1
#JFAFYA: Vidonda vya Tumbo ni Michubuko inayotokea kwenye Kuta za Mfumo wa Chakula, hasa kwenye sehemu ya Tumbo au pia sehemu ya kwanza ya Utumbo Mdogo

Ukubwa wa vidonda hivi hutofautiana na pia Dalili zake mara nyingi hutegemea Umri pamoja na eneo husika vilipo

Soma https://jamii.app/UlcersTips

#JFAfyaJamii
๐Ÿ‘10
SERIKALI IWAJIBIKE KUWALINDA WANANCHI DHIDI YA ULAGHAI NA UTAPELI MITANDAONI

Anasema ukimya wa Serikali kwenye matukio hayo na kuacha Kampuni zikiendelea kujitangaza kuwa zinasaidia Watu kuwekeza Fedha Mitandaoni na kuvuna zaidi kunafanya Watu wengi waendelee kupoteza Fedha zao

Anashauri Serikali ihakikishe inadhibiti utapeli wa Kampuni hizo ambazo baadhi yake zinatajwa kuwa na leseni na vibali vya kufanyia kazi. Kinyume na hapo Watu watapoteza Imani na Fursa zinazopatikana Mitandaoni kwa hofu ya utapeli.

Soma https://jamii.app/Scammers

#JFMaisha
๐Ÿ‘9
INDIA: SERIKALI YASITISHA UZALISHAJI WA DAWA ZILIZOUA WATOTO GAMBIA

Mkaguzi wa Dawa alibaini Kiwanda hakikufanya majaribio ya Dawa 3 kati 4 zilizosababisha vifo huku Dawa moja haikuwa na tarehe ya kutengenezwa wala mwisho wa matumizi

Soma https://jamii.app/DawaIndia

#PublicHealth
๐Ÿ‘3โค1
#JFAFYA: Maambukizi ya Bakteria wa H.pylori hutokea baada ya Kula Chakula au Kunywa Maji yenye vimelea hivi

Dawa za Kupunguza Maumivu zinapotumika pasipo kufuata Ushauri wa Wataalamu huharibu na kuvunja Mfumo wa Kinga unaolinda Kuta za Tumbo

Aidha, Uvutaji wa Sigara hupelekea kutokea kwa tatizo hili na huongeza ukubwa wa athari zake

Soma https://jamii.app/UlcersTips

#JFAfyaJamii
๐Ÿ‘13
Ulikuwa unajua hili?

#JamiiForums
๐Ÿ‘12๐Ÿ˜ฑ8๐Ÿ‘Ž1
DODOMA: DKT MWAKYEMBE KUONGOZA UCHUNGUZI MTIHANI WA SHULE YA SHERIA NCHINI

Kamati hiyo ina Wajumbe 7 akiwemo Mhitimu, John Kaombwe na itafanya Kazi siku 30 kuanzia Oktoba 13

Baada ya hapo, Mwenyekiti atatoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu walichobaini

Soma https://jamii.app/LawSchoolSaga

#Governance
๐Ÿ‘21
MDAU: TUNAHITAJI UONGOZI UNAOWEZA KUBADILI MAAMUZI YASIYO SAHIHI YANAPOGUNDULIKA

Anasema Watu wanapolalamika kwamba #Tozo ni kikwazo, Uongozi haupaswi kusema Wananchi watazizoea

Wanapaswa kukubali kuwa walifanya Maamuzi ambayo hayakuwa Sahihi na kuweka utaratibu mzuri ambao hautakuwa mwiba kwa Watu kama ilivyo sasa

Soma https://jamii.app/MaonoUongozi

#Accountability
MDAU: USIFUATE MKUMBO KWENYE BIASHARA ZA MTANDAONI

Anasema Changamoto za Maisha zimesababisha Watu wengi hasa Vijana kukimbilia Biashara za Mtandaoni pasipo ufahamu wa kutosha

Anashauri kabla hujaanza zingatia Rasilimali Pesa (Mtaji wako), Muda, Vifaa na uelewa wako

Soma https://jamii.app/Mtandaoni

#DigitalRights
๐Ÿ‘11๐Ÿฅฐ2
MAGU: MCHUNGAJI ATUHUMIWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 6

Nurdin Abdallah anadaiwa kutenda Ukatili huo mara kadhaa kwa Mtoto wake

Alimchukua Mtoto kwa Mama yake baada ya kutengana Julai 2022, ambapo Mama wa mtoto alihamia Wilaya ya Bunda

Soma https://jamii.app/TuhumaMchungaji

#HakiMtoto
๐Ÿ˜ข13๐Ÿ‘4๐Ÿค”4๐Ÿคจ3๐Ÿ˜1
UNGUJA: WATU 14 WAKAMATWA WAKIDAIWA KUWA PANYA ROAD

Vijana hao (6 kutoka Dar) wanadaiwa kujihusisha na uhalifu kwa kutumia silaha za jadi kupora na kujeruhi Watu Mkoa wa Mjini Magharibi

Wengine nane wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi

Soma https://jamii.app/PanyaRoadUnguja

#JFMatukio
๐Ÿ‘7
NIGERIA: ZAIDI YA WATU 500 WAFARIKI KWA MAFURIKO

Idadi hiyo imefikiwa kutokana na mafuriko yalitokea wiki za hivi karibuni

Watu 1,500 wamejeruhiwa na wengine milioni 1.4 wamekimbia Makazi yao ikiwemo katika Mji wa #Abuja

Soma https://jamii.app/NigeriaFloods

#Floods
๐Ÿ‘5๐Ÿค”4
ANNA MAKINDA: VIJANA MSITEGEMEE KUAJIRIWA TU

Amewataka vijana kutumia fursa za maeneo wanayoishi na kutotegemea ajira za Serikalini/Sekta Binafsi

> Amesema kupitia Zoezi la Sensa amebaini vijana wengi hawana shughuli za kuingiza kipato

Soma https://jamii.app/UshauriKwaVijana

#Uwajibikaji
๐Ÿ‘Ž19๐Ÿ‘13๐Ÿค”5โค3๐Ÿคฉ1
Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari ya Maafa Duniani hutumika kuongeza Ufahamu kuhusu Athari za Majanga ya Asili na ya Kibinadamu

Pia, kutambua juhudi za Jumuiya na Watu Binafsi Duniani kote za kupunguza uwezekano na athari za Majanga

Soma https://jamii.app/DRRDay

#DRRDay
๐Ÿ‘6