JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LINDI: TAKUKURU KUCHUNGUZA JENGO LA ZAHANATI LILILOGHARIMU TSH. MILIONI 75

Naibu Waziri, Deogratius Ndejembi ametoa agizo hilo baada ya kukagua jengo la Zahanati ya Mtakuja na kusema haliendani na thamani ya fedha iliyotumika

Soma https://jamii.app/PCCBRuangwa

#KemeaRushwa
👍7🤔2
UTAFITI TAKUKURU: Asilimia 78 ya waliohojiwa walisema kwa wastani kiwango cha Rushwa kinaonekana kuwa cha chini huku Asilimia 22 wakisema bado kipo juu

Kundi kubwa la Wahojiwa walisema Viwango vya Rushwa vimepungua kati ya Mwaka wa Fedha 2014/2015 na 2019/2020

Mnamo 2009, Rushwa ilionekana kuwa tatizo kubwa kwa asilimia 91.1 ya waliohojiwa (kwa wastani).

#JamiiForums #KemeaRushwa
👎4
TANZIA: MBUNGE WA JIMBO LA AMANI AFARIKI DUNIA

Spika Wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ametoa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani (CCM) Zanzibar, Mussa Hassan Mussa, kilichotokea leo Oktoba 13, 2022 Nyumbani kwake

Soma https://jamii.app/MbungeAfariki

#Democracy
👍3🤔1
KENYA: SERIKALI YAPIGWA FAINI YA TSH. BILIONI 23.3 KWA KUTOLIPA MIKOPO YA SGR

Ni baada ya kuchelewesha rejesho la Tsh. Bilioni 356.3 kutoka kwenye mkopo wa Tsh. Trilioni 7.4 zilizojenga reli ya SGR kutoka Mombasa hadi Naivasha

Soma https://jamii.app/SGRDeniKE

#ServiceDelivery
🥴10😁3👍1
UMUHIMU WA SIKU YA KUPUNGUZA HATARI ZA MAAFA DUNIANI

Kufahamisha Umma kuhusu hatua za kupunguza Uharibifu unaosababishwa na Majanga kama Ukame, Mvua kubwa, au Magonjwa ikiwemo Utunzaji wa Mazingira na Uboreshaji wa Sekta Ya Afya

Soma https://jamii.app/DRRDay

#DRRDay
👍6😁1
UTAFITI TAKUKURU: Kwa ujumla Taasisi zilizoongoza katika Uadilifu na Utoaji mzuri wa Huduma za Umma ni pamoja na;

Jeshi la Wananchi (JWTZ) lililoonekana kuwa na ufanisi zaidi kwa Asilimia 61.6 likifuatiwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kwa Asilimia 55.4 pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa Asilimia 47.7

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (asilimia 46.4), na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (asilimia 43.5).

#JamiiForums #KemeaRushwa
👍11😁6
DAR: MAKONDA APEWA SIKU 14 KUWASILISHA UTETEZI MAHAKAMANI KUHUSU UPORAJI GARI

Amri hiyo imetolewa leo Oktoba 13, 2022 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

> Anadaiwa kupora Range Rover, mali ya Mfanyabiashara Patrick Kamwelwe

Soma https://jamii.app/PaulRange

#JFGovernance #Accountability
👍14👎2
MALAWI: Serikali imeomba msaada wa Chanjo zaidi za Kipindupindu kutoka Umoja wa Mataifa (UN), ikihofia mlipuko mwingine kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha

Nchi hiyo imerekodi visa 4,420 tangu Machi 2022

Soma https://jamii.app/CholeraMalawi

#JFAfya
👍5🌚3
MDAU: IPO HAJA YA WAZAZI KUPEWA ELIMU JUU YA ADHABU WANAZOWAPA WATOTO

Anasema Wazazi watambue adhabu kali pekee hazimfunzi Mtoto zaidi ya kumuumiza. Pia, Mtoto hujifunza zaidi baada ya kukosea na kuelekezwa vizuri, Akili yake hupokea na kutii mapema kuliko kupigwa na kuumizwa.

Anashauri Serikali itoe Elimu kwa Wazazi kuhusu Malezi yanayohusisha Adhabu za vipigo ambavyo baadhi yao wanafanya bila kujua madhara kwa Mtoto baadaye.

Soma https://jamii.app/KidsAbuse

#HakiMtoto #Malezi #JFMaisha
👍6🔥2
UTAFITI TAKUKURU: Taasisi ambazo zilionekana kutofanya kazi kwa ufanisi katika utoaji wa Huduma za Umma ziliongozwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Asilimia 33.9

Jeshi la Polisi (Asilimia 31.8), Mahakama za Wilaya na Mwanzo (Asilimia 25.8), Vyama vya Wafanyakazi (Asilimia 22.7) na Mifuko ya Pensheni (Asilimia 22.6)

Mtazamo wa kutokuwa na Ufanisi kwa
NIDA unachangiwa na Shinikizo la Taasisi hiyo kutoa vitambulisho kwa wingi katika Muda mfupi.

#KemeaRushwa #JamiiForums
👍8👎3
Mwalimu Nyerere tunamuenzi kwa mengi ikiwemo Falsafa zake za Elimu ya Kujitegemea, Rushwa ni adui wa Haki na Muungano wa Kitaifa

Pia, Umahiri, Ujasiri na Busara zake katika Kuongoza harakati za Uhuru wa #Tanganyika kutoka kwa Waingereza

Soma https://jamii.app/NyerereDay2022

#JamiiForums
👍7
KENYA: MLINZI WA MKE WA RAILA ODINGA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Nyanza, Karanja Muiruri amesema Mlinzi huyo Barrack Jaraha ameuawa akiwa nyumbani kwake saa 11 alfajiri, na uchunguzi kubaini sababu umeanza

Soma https://jamii.app/MlinziRaila

#HumanRights
👍6👎1🤔1
KABILA, TABORA: Watoto wa familia moja umri wa miaka 10 na 17 wamejeruhiwa kwa bomu aina ya Stick Hand Grenade walilookota wakati wakichunga ng’ombe ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Misitu ya Pori la Igombe wakijua ni chuma chakavu

Soma https://jamii.app/BomuTbr

#JFMatukio
👍7🤔4
DKT. MPANGO: MWALIMU NYERERE ALICHUKIA RUSHWA

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amesema tokea enzi za Uhuru Mwl. Nyerere alisisitiza Uhuru, Amani na Umoja na hakupendezwa na masuala ya #Rushwa

Amesema, “Baba wa Taifa alichukia sana rushwa. Sasa sisi Viongozi tunatenda Haki? Hatuwadai Rushwa wanyonge? Wanyonge wanapata Haki yao?"

#JamiiForums #KemeaRushwa #NyerereDay
👍3
#JFAFYA: Binadamu huhitaji Vitamini D ili kuimarisha Kinga ya Mwili na Afya ya Mifupa, na Kupambana na aina mbalimbali za #Saratani

Upungufu wake husababisha kupungua ujazo wa mifupa, Maumivu ya Misuli, na Kinga ya Mwili kudhoofu

Soma https://jamii.app/VitaminDTips

#JFAfyaJamii
👍2🔥1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baraza la Mitihani (NECTA) limesema linafanyia Kazi malalamiko ya Mwanafunzi aliyedai kubadilishiwa namba akiwa chumba cha Mtihani na litahakikisha anapata Haki yake

Iptisum S. Slim aliyefanyia Mtihani Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic amedai kufanya Mitihani 5 kwa namba 40 na Mtihani mmoja akarudishwa kwenye namba yake 39

Soma https://jamii.app/NECTANamba

#JFGovernance #Uwajibikaji
👍10🔥3🤔2
DAR: SHULE YA SEKONDARI YAKOSA MAJI KATIKA VYOO VYA WANAFUNZI

Shule ya Sekondari Ulongoni A inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo Uzio, Miundombinu chakavu kwa baadhi ya Madarasa na Maabara

Pia, kuna Upungufu wa Walimu wa Sayansi

Soma https://jamii.app/MajiShuleDar

#HakiMtoto
👍7
KENYA: WATOTO WA MATAJIRI KULIPA ADA KUBWA ZAIDI VYUO VIKUU

Bodi ya Ufadhili imesema uamuzi huo unalenga kupunguza uhaba wa Fedha kwenye Vyuo vya Umma, kuongeza mikopo kwa Wasiojiweza na kupunguza utegemezi kutoka Hazina

Soma https://jamii.app/AdaVyuoKE

#Governance #Education
👍8🎉1
TETESI: UHUSIANO WA MBAPPE NA PSG WAZIDI KUHARIBIKA

#KylianMbappe anaweza kuvunja Mkataba na Paris-Saint Germain kutokana na kukerwa na baadhi ya mambo ikiwemo Wachezaji wenzake kumtenga

Mbappe analipwa Paundi 650,000 (Tsh. Bilioni 1.5) kwa Wiki

Soma https://jamii.app/MbappePSG

#JFSports
👍9😁4
DODOMA: Kamati ya Bunge (PIC) imeagiza Serikali kulipa Tsh. Bil 21.8 za hasara iliyotokana na kushuka kwa bei ya Pamba Mwaka 2019

> Serikali iliagiza Bei ibaki Tsh. 1200 na sio Tsh. 900 kwa maelezo itafidia hasara hiyo

Soma https://jamii.app/BeiPamba

#JFGovernance #Uwajibikaji
👍7