JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFAFYA: Watu hushauriwa kula Vyakula vyenye utajiri mkubwa wa Madini Joto (Iodine) kama Samaki wa Baharini, Maziwa pamoja na Bidhaa zake, Mayai na Maini ya Wanyama ili kujikinga na Goita

Pia ni vyema kutumia chumvi iliyoongezewa Madini Joto kupikia Chakula

Soma https://jamii.app/GoiterTips

#JFAfyaJamii
👍5
#Uraghbishi ni Falsafa, Mtazamo na namna ya kuwachochea Wananchi kushiriki katika kujiletea Maendeleo

Pia, ni Mtindo wa Maisha wenye lengo la kuwafanya Wananchi washiriki kwenye Uhamasishaji wa Maendeleo katika Maeneo yao

Soma https://jamii.app/Uraghbishi

#JFHakiRaia #Twaweza
👍5
TEKNOLOJIA SAIDIZI: NYENZO MUHIMU KWA USTAWI WA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Teknolojia Saidizi ni pamoja na Kiti cha Magurudumu, Programu ya Kompyuta, 'Keyboard' au 'Mouse' Maalum inayoweza kumsaidia Mtu mwenye Ulemavu kufanya kazi ambayo vinginevyo ingekuwa ngumu au isiyowezekana

Vifaa au Programu Saidizi huwapa watu wote fursa ya kushiriki shughuli za kijamii

Fahamu zaidi https://jamii.app/ATech1

#AssistiveTechnology
👍7
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amesema kuna wakati uliibuka mjadala wa kuongeza muda wa Rais kukaa Madarakani kutoka Miaka 5 hadi 7, wao kama washauri wailikataa hoja hiyo

Asema Heshima kubwa ya #Tanzania ni kuheshimu vipindi viwili vya Miaka 5

Soma https://jamii.app/JKKatiba

#Democracy
👏7👍2
MBEYA: KADA WA CHADEMA ALIYEFUNGWA MAISHA JELA AACHIWA HURU

Gerald Mwakitalu alihukumiwa kutumikia adhabu hiyo Februari 15, 2022 kwa kosa la kudaiwa kuchoma Nyumba ya Mgombea wa CCM wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020

Soma https://jamii.app/KadaCDM

#SocialJustice #Democracy
👍161
Mdau anasema kukosekana kwa Huduma ya Uhakika ya Maji safi kuna athari nyingi kwa Jamii. Mfano: Wanawake na Watoto hubakwa wakifuata Maji Umbali mrefu au Hatari za kiafya kutokana na Kunywa Maji yasiyo salama

Ameshauri Serikali kuwezesha Huduma hii muhimu kwa Wananchi kwa kukomesha ufisadi kwenye fedha za Miradi kwa kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maji

Soma https://jamii.app/HakiYaHudumaYaMaji

#ServiceDelivery
👍5
KIKWETE: WADOKOZI TAASISI NYETI WANAKWAMISHA NCHI

Rais huyo Mstaafu, amesema ufanyaji Kazi kwa Mazoea, Udokozi, Ufinyu wa Utafiti, Ubora hafifu wa Bidhaa uepukwe ili kufikia malengo ya Nchi kwa kuwa kuna baadhi ya Watumishi hawaendi na kasi iliyopo

Soma https://jamii.app/Wadokozi

#Uwajibikaji
👍11
MAWAKILI WATAJWA KUCHELEWESHA MASHAURI YA ARDHI

Mashauri 2000 kati ya 3000 ya Migogoro ya Ardhi yanayosimamiwa na Mawakili ndiyo yaliyochukua muda mrefu kumalizika tofauti na yale ambayo hayawakilishwi na Mawakili

Soma https://jamii.app/MashauriYaArdhi

#Uwajibikaji #ServiceDelivery
👍3
#ZANZIBAR: RAIA WAWILI WA UGANDA WAWEKWA KARANTINI

Kagola Heribery na Mawanda Verai waliingia Visiwani humo kwa kutumia Jahazi

Wapo Karantini ya tahadhari ya maambukizi ya Ugonjwa wa #Ebola ambao umeua Watu kadhaa #Uganda

Soma https://jamii.app/KarantiniPemba

#JFAfya
👍8
DAR: PAUL MAKONDA AFUNGULIWA KESI YA KUPORA GARI

Mfanyabiashara Patrick Kamwelwe amefungua kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akitaka kulipwa fidia ya Tsh. Milioni 240

> Mdaiwa mwingine ni William Malecela (Le Mutuz)

Soma https://jamii.app/UporajiGari

#SocialJustice
👍14
TOYOTA: TAARIFA BINAFSI ZA WATEJA 296,019 ZIMEDUKULIWA

Taarifa zilizovuja ni pamoja na wanaotumia Mfumo wa T-Connect, Barua Pepe na Namba za Simu

> Waathirika ni wateja Duniani kote waliojisajili kuanzia Julai 2017

Soma https://jamii.app/ToyotaData

#DataProtection #DataPrivacy
🤔4😢2👍1
JACOB ZUMA AMALIZA KIFUNGO CHA MIEZI 15

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alianza kutumikia kifungo Julai 7, 2021 kwa kosa la kuidharau Mahakama

Septemba 2021 alitoka Gerezani na kutumikia Kifungo cha nje kwasababu za Kiafya

Soma https://jamii.app/ZumaFree

#Governance
👍10
#AFYA: Mkaa huzalisha gesi yenye Sumu inayoitwa #Carbonmonoxide (CO) ambayo hupelekea mhusika kupatwa na Maumivu makali ya Kichwa, Kizunguzungu, Uchovu Mkubwa, Kuongezeka kwa Mapigo ya Moyo, kukata kwa pumzi na hatimaye kupoteza Fahamu

Pia, huweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwenye Seli muhimu za Ubongo pamoja na kusababisha kifo ikiwa msaada wa haraka hautatolewa

Soma https://jamii.app/SafeCharcoalUsage

#JFAfyaJamii
👍16🙏3
#MICHEZO: YANGA, AZAM FC, KIPANGA KUKIWASHA KIMATAIFA LEO

Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga itaivaa Al Hilal (Sudan) kwenye Uwanja wa Mkapa

Kombe la Shirikisho, Azam FC ipo inacheza na Al Akhdar (Libya). Kipanga ya #Zanzibar ikicheza dhidi ya Club Africain (Tunisia)

#JFSports
HAITI: SERIKALI YAOMBA MSAADA WA KIJESHI KUDHIBITI MACHAFUKO YANAYOONGEZEKA

Waziri Mkuu, Ariel Henry, amesema Nchi yake inakabiliwa na hatari ya Mgogoro mkubwa wa Kibinadamu

> Ubalozi wa Marekani umeshauri raia wake kuondoka haraka

Soma https://jamii.app/HaitiUnrest

#HumanRights
👍2🤯1
BIMA YA AFYA KWA WOTE: FAMILIA YA WATU 6 KULIPA TSH. 340,000

Idadi ya Watu itajumuisha Mchangiaji, Mwenza wake na Wategemezi wasiozidi 4 kwa kipindi cha Mwaka mmoja

Wasio na Familia watachangia Tsh. 84,000 kwa Mtu mmoja kwa Mwaka mmoja

Soma https://jamii.app/BimaPay

#PublicHealth
👍10🤔1
MZAZI MWENZA ANA HAKI YA KUMUONA MTOTO HATA KAMA HATOI MATUNZO

Sheria Namba 21 ya Mwaka 2009 Kifungu cha 38 cha Sheria ya Mtoto kinatoa Haki hiyo na Mzazi/Mlezi anayekaa na Mtoto hapaswi kuipinga

Anayenyimwa Haki hiyo anaweza kufungua Malalamiko Mahakama ya Mwanzo au ya Wilaya iliyopo ndani ya eneo analoishi Mtoto (Awe na chini ya Miaka 18)

Soma https://jamii.app/HakiKwaMtoto

#HakiMtoto
👍15
#ZAMBIA: Mbunge Munir Zulu amesimamishwa Kazi kwa muda wa Mwezi Mmoja baada ya kusema Wabunge ni watu wazima "Wanaonyoa Nywele zao za sehemu za siri"

Ni baada ya kukerwa na Mbunge mwenzie aliyemwita Kijana

Soma https://jamii.app/MPSuspended

#Democracy
😁13👍6
RIPOTI WHO: AFRIKA INAONGOZA KWA IDADI YA WATU WANAOJIUA DUNIANI

Afrika ina Nchi 6 kati ya 10 zenye Viwango vya juu zaidi vya Watu kujiua Duniani ambapo tatizo la Afya ya Akili linachangia Vifo kwa hadi 11%

Takriban Watu 11 kwa kila Watu 100,000 wanajiua Barani Afrika kila Mwaka ikiwa ni juu ya wastani wa Kimataifa wa Watu 9 kwa kila Watu 100,000

Soma https://jamii.app/WHOSuicides

#MentalHealth
👍4
BAADHI YA MAENEO KATIKA MIKOA 17 KUKOSA UMEME OKTOBA 9 NA 10, 2022

Mikoa hiyo ni Dar, Pwani, Tanga, Arusha, Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Simiyu, #Kilimanjaro, Manyara na Songwe

Sababu ni kuzimwa kwa laini 2 kubwa za Umeme

Soma https://jamii.app/UmemeKukatika

#ServiceDelivery
👍4🤯2