JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFISA HABARI WA AZAM FC AFUNGIWA MIEZI 3 NA FAINI YA TSH LAKI 5

Thabiti Zakaria amekutwa na kosa la kuwatuhumu Waamuzi kuwanyima penati mbili

Namungo FC imetozwa faini ya Tsh. Milioni 1 na Dodoma Jiji imetozwa faini ya Tsh. Laki 5

Soma https://jamii.app/TPLBAdhabu

#JFSports
πŸ‘6πŸ‘1😁1
#UGANDA: Rais Museven amewaomba radhi Wakenya kwa Tweets za Mtoto wake, Jenerali Muhoozi, kuhusu kuiteka #Nairobi

> Amezungumzia hatua ya kumpandisha Cheo na kusema licha ya kukosea kwake kuna Michango mingi aliyotoa na bado anaweza kutoa

Soma https://jamii.app/YoweriRadhi

#Diplomacy
😁10πŸ‘4πŸ‘Ž2
RWANDA: WANAHABARI WATATU WATOLEWA JELA BAADA YA MIAKA MINNE

Walikamatwa kwa madai ya kueneza habari za uongo dhidi ya Serikali ya Rais Paul Kagame wakitumia Mtandao wa #YouTube

Wamefutiwa Mashtaka yote kutokana na kukosekana kwa ushahidi

Soma https://jamii.app/RwandaMedia

#PressFreedom
πŸ‘10πŸ‘Ž2
MDAU: TOZO BADO NI MWIBA KWA WATANZANIA

Anasema Serikali imeshindwa kuzuia Mfumuko wa bei za Vyakula na Bidhaa muhimu badala yake imeleta #Tozo ambazo hazina #Uwazi na #Uwajibikaji ktk matumizi yake

Ameshauri ikiwa ni lazima kukata Tozo hizo basi zitumike kuchangia #BimaYaAfya kwa kila Mwananchi ili matumizi ya Tozo yamguse Mtanzania mmoja mmoja

Soma https://jamii.app/TozoMwiba

#Governance
πŸ‘28
#IRAN: POLISI WASAMBAZWA VYUONI KUDHIBITI MAANDAMANO YA KIFO CHA MAHSA

Kifo hicho kimeamsha hasira za Raia wanaoshinikiza kuondolewa kwa Sheria na Utawala wa Kiislamu uliopo tangu 1979

> Watu 150 wameripotiwa kufariki kwenye vurugu hizo

Soma https://jamii.app/IranUnrest

#MahsaAmin
πŸ‘10πŸ‘Ž10
NI WAJIBU WA NDUGU KUWAPA MSAADA WA KIJAMII WATU WENYE ULEMAVU

Kwa Mujibu wa vifungu vya 16 na 17 vya Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2010, Kushindwa kutoa Msaada wa Kijamii unaostahili kwa Mtu mwenye Ulemavu, Mahakama kwa Maombi ya Mtu Mwenye Ulemavu au Mwakilishi wake itamwamuru Ndugu kutoa malipo ya kila Mwezi kwa kiwango cha Fedha ambacho itaona kinafaa

Soma https://jamii.app/WatuWenyeUlemavuMsaada

#HumanRights
πŸ‘10
AUSTRALIA: Serikali imelazimika kubadili Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kuzitaka Kampuni za Mawasiliano kushirikiana na Taasisi za Kibenki na Serikali ili kuchunguza na Kudhibiti Mashambulio ya Kimtandao

Kampuni ya Simu ya #Optus ilidukuliwa Sept. 21, 2022 na kupoteza rekodi za wateja milioni 9.8 ikiwemo Pasipoti, Leseni za Udereva na Kitambulisho cha Afya

Soma https://jamii.app/DataLaw

#DataProtection #DataPrivacy
πŸ‘8
#THAILAND: WATU 31 WAMEUAWA BAADA YA ASKARI KUSHAMBULIA SHULE

Polisi wamesema shambulio hilo limefanywa na Afisa wa zamani wa Polisi aliyefyatua risasi na kuchoma Visu Watoto na Watu wazima ktk kituo cha Kulea Watoto wa Shule ya Awali

Soma https://jamii.app/VifoThailand

#HumanRights
😒6πŸ‘4
Ni muhimu kupata Uchunguzi kamili wa Kitabibu kwasababu Saratani ya Matiti inaweza kuonekana kwa namna nyingi

Dalili nyingine za Saratani ya Matiti ni Mabadiliko katika Mwonekano wa Ngozi kama vile kuchubuka, kufifia au wekundu na chuchu kuzama ndani ya Titi

#PublicHealth #BreastCancer #BreastCancerAwarenessMonth
πŸ‘2
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imesema itawachukulia hatua za Kisheria wamiliki wa Magari yenye Namba ambazo hazijatolewa na TRA au Taasisi nyingine za Serikali ambazo zimepewa jukumu hilo Kisheria, ikiwemo kutaifisha Gari husika

Soma https://jamii.app/MarufukuTRA

#Governance
πŸ‘4
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari ya Kimataifa kuhusu Dawa za #Promethazine Oral Solution, Kofexmalin Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold Syrup zilizohusishwa na majeraha ya Figo na Vifo vya Watoto 66 Nchini #Gambia

Soma https://jamii.app/TahadhariYaDawa

#JFAfya
πŸ‘11
MAREKANI KUTOA MAPIPA MILIONI 10 YA MAFUTA BAADA YA OPEC KUPUNGUZA UZALISHAJI

OPEC+ itapunguza uzalishaji wa Mapipa milioni 2 kwa Siku kuanzia Novemba 2022 ili kudhibiti Bei iliyoshuka hadi Tsh. 186,560 kutoka Tsh. 279,840 kwa Pipa

Soma https://jamii.app/OPECPunguzo

#ServiceDelivery
πŸ‘7
TMDA YAKAMATA DAWA ZA NGUVU ZA KIUME NA P2 HATARI KWA UZAZI KANDA YA ZIWA

Dawa hizo ni VEGA 100 ambazo hazina usajili pamoja na Dawa za kuzuia Ujauzito ambazo hazijulikani zilikotengenezwa

> Zimekutwa kwenye 30% ya Maduka ya Dawa

Soma https://jamii.app/TMDABandia

#PublicHealth
πŸ‘5πŸ‘3
#JFAFYA: Goita (#Goiter) ni Uvimbe unaotokea kwenye Tezi ya β€˜Thyroid’ inayopatikana sehemu ya mbele ya Shingo

Huzalisha Homoni za T4 na T3 ambazo huratibu Mifumo mbalimbali ya Mwili ikiwemo Joto, Mihemko ya Mwili, Mapigo ya Moyo na Mmeng’enyo wa Chakula

Soma https://jamii.app/GoiterTips

#JFAfyaJamii
πŸ‘6πŸ₯°1
SERIKALI KUZISAKA DAWA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA WHO

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifelo Sichwale, amesema licha ya TMDA kusema Dawa hizo hazijaingia nchini, Wizara ya Afya itafanya ukaguzi maalumu

Dawa hizo zinaripotiwa kuua Watoto 66 Nchini #Gambia

Soma https://jamii.app/DawaSumu

#PublicHealth
πŸ‘7
#MSUMBIJI: Wizara ya Afya imetangaza kisa cha kwanza cha Ugonjwa wa #MonkeyPox baada ya Mtu mmoja mwenye Historia ya kusafiri kugundulika kuwa na Maambukizi ya Virusi hivyo

Mamlaka zinaendelea kuchukua vipimo vya wanaohusiana na Mgonjwa

Soma https://jamii.app/MozambiqueMonkeyPox

#JFAfya
😒6πŸ‘1πŸ₯°1
UINGEREZA: ELTON JOHN, PRINCE HARRY WAISHTAKI DAILY MAIL

Wanadai wachapishaji hao wameingilia Faragha zao kwa kutumia Vifaa kusikiliza Mazungumzo yao Binafsi kwenye Gari na Nyumbani

#DailyMail yamesema madai hayo yanalenga kuchafua Biashara yao

Soma https://jamii.app/PrinceHarryDailyMail

#DataPrivacy
πŸ‘7
MALORI ZAIDI YA 600 YADAIWA KUKWAMA MPAKA WA KENYA NA #TANZANIA

Yamekwama katika Mpaka wa #Namanga kwa zaidi ya wiki moja ambapo Madereva wamedai mchakato upande wa #Kenya ndio umechangia mkwamo huo licha ya kukamilisha taratibu za vibali

Soma https://jamii.app/NamangaMpakani

#ServiceDelivery
πŸ‘8πŸ€”1
SUDAN KUSINI: Benki ya Dunia imesema haiwezi kutoa Ufadhili wa kujenga Barabara kutokana na Nchi hiyo kukosa Uwazi wa Matumizi ya Fedha

> #Sudan inatajwa kuongoza kwa Barabara mbovu kwa pembe ya Afrika Mashariki

Soma https://jamii.app/RoadFundSK

#Accountability #ServiceDelivery
πŸ‘9
TFF YAZIFUNGIA TANZANIA PRISONS NA SINGIDA BIG STARS KWA KOSA LA USAJILI

Tanzania Prisons ilimsajili Musa Mbise akiwa na mkataba na Coastal Union huku Singida Big Stars ilimsajili kipa Metacha Mnata akiwa na mkataba na Polisi Tanzania

Soma https://jamii.app/TFFBan

#JFSports
πŸ‘7πŸ‘Ž6