JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: Serikali imehimiza bado dau la Tsh. Bilioni 11.5 linamsubiri mwenye taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa muhalifu wa kivita, Joseph Kony anayesakwa kwa zaidi ya miaka 15

> Anatuhumiwa kutumikisha Watoto Vitani na Kingono

Soma https://jamii.app/KonyBounty

#HumanRights
👍3
KABUDI: TRILIONI 360 ZA MAKINIKIA ZILIKUWA HAZILIPIKI

Profesa Palamagamba Kabudi amesema Dola Bilioni 190 zilizotakiwa kulipwa na Kampuni ya Acacia Julai 2017 kama kodi, Malimbikizo na faini ya ukwepaji kodi hazikuwa kodi halali bali kodi inayobishaniwa

Soma https://jamii.app/Makinikia

#Governance #Uwajibikaji
👍9👎8🤯6😁5💩3🥰2😢2
MAREKANI: #AngelinaJolie anamtuhumu Mumewe wa zamani, Mwigizaji #BradPitt kwa kumshambulia yeye na Watoto wao huku akiwamwagia Pombe wakati wa safari binafsi ya Ndege iliyopelekea Talaka yao Mwaka 2016

Pitt amepinga tuhuma hizo

Soma https://jamii.app/PittAndJolieSaga

#DomesticViolence
👍4
RAIS NIGERIA: UDHALILISHAJI WA KINGONO UMEKITHIRI VYUONI

Rais Muhammadu Buhari amesema Tume Huru ya Mienendo ya Ufisadi na Makosa Mengine yanayohusiana inachunguza Unyanyasaji wa Kijinsia kama matumizi mabaya ya Mamlaka ktk Taasisi za Elimu

Soma https://jamii.app/RushwaNigeria

#HumanRights
👍2
#AFYA: Wanaougua Ugonjwa wa #Kisukari au Shinikizo kubwa la Damu, wanashauriwa kutumia Dawa vizuri bila kuacha

Magonjwa hayo ndiyo chanzo kikubwa cha kufeli kwa figo

Soma https://jamii.app/HealthyKidneyTips

#JFAfyaJamii
👍9
OKTOBA 5: SIKU YA WALIMU DUNIANI

Siku hii inaadhimishwa kama ishara ya Heshima na Shukrani kwa Walimu na Mchango walionao katika Ustawi wa Wanafunzi, Jamii na Taifa

Ili kuleta Mabadiliko katika Sekta ya Elimu, ni muhimu Walimu wasikilizwe, na mazingira yao ya kazi yaboreshwe

Bila Walimu Bora, ni vigumu kupata Elimu Bora

Soma https://jamii.app/WTD2022

#WorldTeachersDay
👍93
MAREKANI: Tajiri #ElonMusk amekubali kuinunua #Twitter baada ya Timu ya Mawakili wanaomwakilisha kubaini Mahakama haitokuwa na uamuzi mzuri upande wao hivyo wanaridhia kuinunua ili kumaliza kesi

Hisa za Twitter zimepanda hadi 23% baada taarifa hiyo

Soma https://jamii.app/ElonTwitter

#DigitalRights
👍13
Baada ya zoezi la kupokea Makala za Shindano la #StoriesOfChange kukamilika Septemba 15, 2022 kinachoendelea sasa ni Majaji kupitia maandiko yaliyowasilishwa

Washindi wa shindano hili watatangazwa Novemba 18, 2022 na zawadi zitatolewa kwa Washindi 20

#SOC2022
👍17👎1
IFAHAMU TEKNOLOJIA SAIDIZI (ASSISTIVE TECHNOLOGY)

Ni Vifaa au Programu yoyote inayolenga kuongeza, kudumisha, au kuboresha uwezo wa utendaji wa Watu wenye Ulemavu, Wazee na wenye Magonjwa mbalimbali

Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza utoaji wa Teknolojia Saidizi kuunganishwa katika sekta zote muhimu za maendeleo zikiwemo #Afya, Elimu na Ajira

Zaidi https://jamii.app/ATech1
👍6
MDAU: NI JUKUMU LA SERIKALI KUWEKEZA KATIKA ELIMU NA VIPAJI VYA WATU WAKE

Anasema Serikali inapaswa kuweka kipaumbele cha uwekezaji katika #Afya, #Elimu na #Lishe ya Wananchi kwani ni muhimu katika kukuza Uchumi wenye nguvu, Ushindani na unaostawi

Ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha fursa za Elimu iliyo bora zinapatikana kwa Wananchi ili kukuza Ubunifu

Soma https://jamii.app/UwekezajiElimuVipaji

#ServiceDelivery
👍4
RUVUMA: ASKARI WA JWTZ AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA MAUAJI

Sajenti Batsin Sanga amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua kwa risasi Veronica Kayombo (Mtalaka wake) na Mwanajeshi mwenzake

Mauaji hayo yalitokea Desemba 27, 2018

Soma https://jamii.app/HukumuSongea

#SocialJustice
👍4🤔3
UGANDA: WATUHUMIWA KUPIMWA UKIMWI, TB NA MALARIA KWA LAZIMA

Taarifa iliyosomwa na Naibu DPP imesema lengo ni kuwalinda Askari, Wafanyakazi wa Idara za Haki na kujua mapema hali za Afya za Watuhumiwa na kuzuia maambukizi mengine

Soma https://jamii.app/SuspectsTest

#PublicHealth #Accountability
😁2
UTAFITI: 95% YA WANAOFANYA KAZI NJE YA OFISI HUTAZAMA FILAMU MUDA WA KAZI

Walipoulizwa kwanini hutazama Filamu na Tamthilia muda wa kazi, 68% walisema inafanya Siku yao kuwa ya furaha zaidi, 65% ni sehemu ya starehe na 44% inawafanya wawe makini zaidi

Soma https://jamii.app/RemoteStreams

#DigitalRights
👍11
NINI KIFANYIKE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU?

1) Mazingira bora ya kufundishia: Ili kuwafanya Walimu kuzingatia majukumu yao, mazingira ya kazi yanahitaji kuwa rafiki

2) Upatikanaji wa Huduma za Msingi: Walimu wa Shule za Umma zilizopo Vijijini wanakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo Maji na Umeme

Zaidi https://jamii.app/WalimuTZ

#WorldTeachersDay #TeachersDay2022
👍4
MATUKIO YA WATU KUFARIKI KWENYE VIWANJA VYA SOKA

Indonesia Watu 174 (2022), Misri 73 (2012), Ghana 126 (2001), Guatemala 82 (1996), Afrika Kusini 43 (2001) na 42 (1991)

England 96 (1989), Nepal 90 (1988), Ubelgiji 99 (1985), England 56 (1985)

Soma https://jamii.app/VifoUwanjani

#JFSports
👍4
#JFDATA: Zaidi ya Watu Bilioni 1 Duniani wanahitaji angalau kifaa kimoja cha Usaidizi kwa ajili ya Mawasiliano na Utambuzi. Wengi wao hawawezi kupata kutokana na gharama kuwa kubwa

Wakati ufikiaji wa Teknolojia Saidizi (#AssistiveTechnology) ukiwa 3% katika Nchi masikini na za Kipato cha Kati, kwenye Mataifa tajiri uwezekano wa Wananchi kupata vifaa hivyo vya usaidizi ni 90%
👍5
DALILI ZA EBOLA: Homa ya ghafla, Uchovu wa kina, Maumivu ya Misuli, Maumivu ya Kichwa, Koo kukauka. Hii hufuatiwa na kutapika, kuhara, vipele, Figo na Ini kushindwa kufanya kazi. Wakati mwingine Damu huanza kuvuja ndani na nje ya Mwili

Baada ya dalili hizo kuonekana, Ugonjwa unaweza kubainika kati ya siku Mbili hadi 21 na hapo ndipo Mgonjwa anaweza kuambukiza wengine. Thibitisho la Ugonjwa huu hupatikana Maabara pekee.

#JamiiForums #EbolaOutbreak
👍2
DRC: Ripoti ya UN imebaini matukio 6,782 ya Ukatili na Mateso maeneo yaliyoathiriwa zaidi na Migogoro ambapo 44% ya Mateso yalifanywa na Maafisa wa Serikali ikiwemo Majeshi ya Ulinzi na Polisi

Juni 2021 - Mei 2022 kulikuwa na matukio mengi

Soma https://jamii.app/CongoReport

#HumanRights
👍1
AFYA: #FoodPoisoning husababishwa na ulaji wa Chakula Kichafu kilichobeba Vimelea wa Magonjwa hasa Bakteria na Virusi, au Sumu zake

Husababisha Maumivu makali ya Tumbo, Kuharisha, Kutapika, Kiungulia, Uchovu na Homa kali zaidi ya Nyuzijoto 38.9

Soma https://jamii.app/FoodPoisoningTips

#JFAfyaJamii
👍3
MDAU: Viongozi wa Serikali ya Mtaa ndio msingi wa mambo makubwa katika Uongozi wa Nchi, wao wanapolega ndivyo ambavyo wale wa juu wanaonekana hawafanyi kazi

Mfano matukio kama ya 'Panya Road' taarifa sahihi zilitakiwa zianzie kwao kwa kuwa wao ndio wanaowajua Wananchi

Je, utendaji wa Viongozi wa Mtaani kwako upoje?

Soma: https://jamii.app/UongoziWaMtaa

#JFUwajibikaji
👍3👏3