JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAN UNITED YABAMIZWA GOLI 6-3

#ManUnited imekubali kipigo hicho kutoka kwa #ManCity katika Premier League

Wafungaji wa City wamefunga magoli matatu (hat trick) kila mmoja (Phil Foden na Erling Haaland) wafungaji wa United ni Antony na Martial

Soma https://jamii.app/ManDerby
😁18🀑6πŸ‘5πŸ‘Ž3
#SRILANKA: SERIKALI YAFUTA KODI ZOTE KWENYE TAULO ZA KIKE

Ofisi ya Rais imeagiza kufutwa mara moja kwa Ushuru wa Forodha, Ushuru unaolipwa Viwanja vya Ndege na Kodi nyingine za ndani zinazogusa Malighafi za kutengeneza Bidhaa zote za Usafi wa Wanawake

Soma https://jamii.app/SriPads

#WomensRights
πŸ‘16πŸ‘4
#JFAFYA: β€˜Heat Stroke’ au Kiharusi cha Joto ni hali ambayo huweza kutokea baada ya Mifumo ya Mwili kushindwa kudhibiti ongezeko la ghafla la Joto kubwa linaloweza kufikia zaidi ya Nyuzi Joto 41

Huweza kumpelekea Mtoto kupoteza fahamu, kuweweseka, kuzunguzungu, Kiu kali, Degedege pamoja na kufeli kwa Viungo vya ndani ya Mwili na kusababisha kifo au changamoto za kudumu

Soma https://jamii.app/HeatStrokeTips

#JFAfyaJamii
WAZEE WASIACHWE NYUMA KIDIJITALI

Kutokana na changamoto za Uzee ni muhimu Wazee kuwezeshwa kutumia Teknolojia ya Digitali kwani itawasaidia kwa Afya na uystawi wao. Mfano; Kupata dondoo za Afya na Maisha zilizopo Mtandaoni

Ni muhimu kwa Jamii kutafuta njia za kuwawezesha Wazee katika ushiriki huru wa Kijamii kupitia Mtandao

Soma https://jamii.app/WazeeNaDijitali

#DigitalWorld
πŸ‘9❀2πŸ‘Ž2
SIMBA YAONGOZA LIGI KWA USHINDI WA 3-0

Simba SC imeifunga Dodoma Jiji katika Mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkapa

Magoli yamefungwa na Shaibu β€˜Ninja’ (amejifunga), Moses Phiri na Kyombo. #Simba imefikisha pointi 13 katika Mechi 5

Soma: https://jamii.app/SimbaDodomaJiji

#JFSports
πŸ‘2
UTEUZI: BASHUNGWA AHAMISHIWA ULINZI, KAIRUKI APELEKWA TAMISEMI

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo kwa kumteua Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Pia, amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

#JamiiForums #JFGovernance
πŸ‘4πŸ”₯2
UTEUZI: DKT. STERGOMENA ACHUKUA NAFASI YA BALOZI MULAMULA

Rais Samia amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anachukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula

#JamiiForums #JFGovernance
πŸ‘9πŸ₯°2
MOROGORO: Watoto 100 wa Kitongoji cha Maloweke Wilayani Gairo wamekosa fursa ya kupata Elimu kutokana na kukosa Shule, huku Shule za karibu zikiwa Umbali wa Kilometa 11

DC wa Gairo, Jabir Makame ameagiza Halmashauri kupeleka Mwalimu ujenzi wa Madarasa ukikamilika

Soma > https://jamii.app/ShuleMoro

#ServiceDelivery
πŸ‘7πŸ€”2
Mathalani matapishi, Choo, Mate, Mbegu za Kiume (Semen) na Damu. Maambukizi yanaweza kutokea pia iwapo Ngozi yenye uwazi ya Mtu asiye na Ugonjwa itakumbwa na Majimaji yenye kirusi yaliyomo kwenye Nguo chafu za Mgonjwa, Mashuka au Sindano zilizotumika

WHO haishauri Familia au Jamii kuhudumia Wagonjwa wanaoweza kuwa na dalili za Ebola Majumbani mwao. Badala yake wanatakiwa wapate Huduma Hospitali au Kituo cha Afya kilicho karibu.

#JamiiForums #EbolaOutbreak
πŸ‘4πŸ‘2
Rais Samia Suluhu Hassan akiapisha Viongozi wateule Ikulu - Dar Es Salaam amesema "Katika viapo vyetu tunaapa kuilinda #Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania. Muungano wenye pande mbili na mtatumika sehemu zote sawa kwa jinsi Katiba ilivyogawa majukumu"

Zaidi: https://jamii.app/IkuluLeo

#Uapisho #JamiiForums
πŸ‘Ž6πŸ‘5
RAIS SAMIA: WAZIRI HUWEZI KUJIONDOA KWENYE MAAMUZI YA SERIKALI
-
Rais Samia amewataka Mawaziri Wateule kujua kuwa wao ni sehemu ya Serikali hivyo Maamuzi ya Serikali ni yao kulingana na viapo vyao

Amesema, β€œLinaloamuliwa na Serikali wewe Waziri ni lako na unatakiwa ulibebe ukalifanyie kazi kwa misingi uliyoelekezwa. Huwezi kusema nimeelekezwa hivi ila mimi sikutaka hivi lakini imebidi nifanye hivi kwa sababu nimeelekezwa, huwezi kujitoa”

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance
πŸ‘9
MOROGORO: MWANAMKE AFUNGWA JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 12

Shani Suleiman (35) alikamatwa baada ya Mama mzazi wa mtoto, kumwekea mtego nyumbani kwake ambapo alirekodi tukio hilo kwa kutumia simu janja

Soma https://jamii.app/MwanamkeAbakaMtoto

#HakiMtoto
😁15πŸ‘5πŸ€”3
BURKINA FASO: ALIYEONDOLEWA MADARAKANI AJIUZULU NA KUKIMBIA NCHI

Paul-Henri Damiba amekwenda uhamishoni Nchini #Togo baada ya kuhakishiwa Usalama wake na kurejeshwa kwa Utawala wa Kiraia ndani ya Miaka miwili

> Ametawala kwa Siku 252

Soma https://jamii.app/DamibaBF

#Democracy
πŸ‘4😁4
UHURU WA KUJIELEZA UNA NAFASI GANI KATIKA DEMOKRASIA?

#UhuruWaKujieleza na Kupata Taarifa ni Haki muhimu katika Demokrasia na Ushirikishwaji Wananchi. Kuruhusu mtiririko huru wa mawazo pia huimarisha Uwazi na Uwajibikaji

Kushindwa kujieleza kwa uhuru kuna athari ya moja kwa moja kwenye ushiriki wa Kidemokrasia kwani kunapunguza ushiriki wa watu katika Mijadala inayogusa Maisha yao ya kila siku

#FreedomOfExpression #RightToInformation
πŸ‘6
UGANDA: Dkt. Mohamed Ali aliyefariki kwa #Ebola amezikwa Nchini humo ili kuepusha Maambukizi kuingia #Tanzania

> Miongozo ya Wizara ya Afya inaagiza wanaofariki kwa Ebola kuzikwa palepale wanapofia

Soma https://jamii.app/AliAzikwa

#PublicHealth #EbolaOutbreakUG
πŸ‘11😒6🀨5
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SPIKA TULIA: ATAKAYEMSEMA VIBAYA RAIS, SHUGHULIKENI NAYE

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, amewataka Vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki ktk kumsema vibaya Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Zaidi https://jamii.app/TuliaRaisKusemwa

#Democracy #FreeSpeech
πŸ‘Ž18πŸ‘5
RUSHWA YA NGONO: Wahanga wengi wamekuwa waoga kutoa Taarifa wanapobaini au wanapoombwa #RushwaYaNgono kutokana na uvujaji wa Taarifa hizo

Aidha, uoga wa kuzungumza pia unasababishwa na Urasimu wa Mfumo wa uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na mrejesho hafifu wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya walalamikiwa

#VunjaUkimya
πŸ‘2
MIFUMO YA BIOMETRIKI INAZINGATIA NA KUHESHIMU HAKI YA FARAGHA?

Mataifa mbalimbali ikiwemo #Tanzania yamekuwa yakitumia Mifumo hiyo inayohusisha Alama za Vidole katika Utoaji wa Huduma kama usajili wa Namba za Simu, Vitambulisho na Hati za Kusafiria

Kila Mtu ana Haki ya Faragha ikiwemo katika Mawasiliano na Taarifa zake Binafsi

Ni muhimu kuwa na Misingi imara itakayohakikisha Taarifa hizo zinalindwa na zipo salama

Soma https://jamii.app/PrivacyBiometric

#RightToPrivacy
πŸ‘3
MDAU: WAZAZI ONGEENI NA WATOTO KUHUSU UBAKAJI NA ULAWITI

Anasema matukio hayo yanachangiwa na Watoto kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu madhara ya vitendo hivyo na wengine wanafahamu kuhusu matukio hayo lakini hawajui namna sahihi ya kuyakabili

Ameshauri Wazazi/Walezi kuacha dhana kuwa watawambia wakiwa wakubwa, kwani kufanya hivyo ni kuwaacha watoto hatarini bila ya msaada wowote

Mjadala https://jamii.app/UkatiliElimu

#HakiMtoto
πŸ‘6
TANZANIA YACHAGULIWA BARAZA KUU LA ITU

Imekuwa miongoni mwa Nchi 13 za Afrika zitakazowakilisha katika Baraza la Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kwa 2023 - 2026

Baraza hilo linasimamia masuala ya Kisera ya Mawasiliano ya Simu

Soma: https://jamii.app/BarazaLaITU

#DigitalRights
πŸ‘6πŸ‘1