JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Yanga SC imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kutoa dozi ya 2-1 kwa Ruvu Shooting

#Yanga imefikisha pointi 13 ikiwa sawa na Simba SC ambayo inaongoza Ligi kwa tofauti ya Magoli ya kufunga na kufungwa.

Soma https://jamii.app/RuvuYanga
#Sports
πŸ‘8πŸ‘6πŸ”₯5πŸ‘Ž2
TUNDURU: POLISI WAZUIA ZIARA WAKIDAI KUNA VITISHO VYA UGAIDI

Hiyo imetajwa kuwa sababu ya Jeshi la Polisi kuzuia ziara ya kichama ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, katika Wilaya ya Tunduru

Soma https://jamii.app/TunduruVitisho

#JFSiasa
πŸ‘Ž14πŸ‘6
ALIYETOKA GEREZANI KWA MSAMAHA WA RAIS ADAIWA KUFANYA MAUAJI

Nestory Elias (62) aliyeachiwa huru kutoka gerezani Mei Mosi, 2022 anatuhumiwa kumuua Mwajuma Sadru (75), Mkazi wa Mtaa wa Bong'ola, chanzo kikiwa ni Mgogoro wa eneo la Biashara

Soma https://jamii.app/MfungwaMoro

#JFMatukio
😒6πŸ‘1
#JFAFYA: Hali ya β€˜Pica’ husababishwa na uwepo wa Upungufu mkubwa wa Madini Chuma ambayo hupelekea kutokea kwa tatizo la upungufu wa Damu. Pia Upungufu wa Madini ya Zinc, au aina mbalimbali za Vitamini B

Wajawazito hushauriwa kula mlo kamili pamoja na Virutubisho vyenye utajiri wa Madini Chuma na Asidi za Foliki (FEFO), Zinc pamoja na aina mbalimbali za Vitamini B ili kujikinga na hali hii

Soma https://jamii.app/PicaTips

#JFAfyaJamii
πŸ‘3
#TANZANIA: Imeelezwa kuwa Mtu mmoja katika kila Watu 8 ana tatizo la Afya ya Akili, wakati awali ilikuwa Mtu mmoja katika kila Watu 10

Pia, Wanawake 4 kati ya 10 wenye Miaka 15 hadi 45 wamefanyiwa Ukatili wa Kimwili huku Wanawake wawili kati ya 10 ikiwa ni Ukatili wa Kingono na wote wanaelekea kupata tatizo la Afya ya Akili

Soma https://jamii.app/AfyaAkiliTZ

#MentalHealth
🀯7πŸ€”4πŸ‘3🀑2
KAGERA: Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Dkt. Ama Kasangala, amesema Serikali haitafunga Mipaka yake na #Uganda bali itajikita ktk kutoa Elimu ya namna ya kujikinga na Maambukizi ya #Ebola

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Issessanda Kaniki, amesema Serikali imeweka Maabara Tembezi ya kupima Virusi vya Ugonjwa wa #Ebola iliyofungwa katika Kituo cha Afya Kabyaire, Wilaya ya Misenyi

Soma https://jamii.app/MpakaEbola

#JFAfya #PublicHealth
πŸ‘Ž8πŸ‘4πŸ€”1
MARA: WAOMBA MAMLAKA YA KUWASHUGHULIKIA MAJAMBAZI KIMILA

Wakazi wa Kijiji cha Nyamakobiti, Kata ya Majimoto wameomba ruhusa watumie Mila na Desturi zao kumaliza uhalifu huo wakieleza wanawafahamu Majambazi kwasababu wanaishi nao

Soma > https://jamii.app/UjambaziMara

#JFMatukio
πŸ‘10🀑6
SARATANI YA MATITI: Ni Saratani inayowaathiri zaidi Wanawake Duniani

Mara nyingi, dalili ya kwanza huwa uvimbe kwenye Titi au Kwapa, japokuwa haimaanisha moja kwa moja kuwa kila uvimbe ni Saratani

Unapohisi uvimbe wowote usio wa kawaida, ni muhimu kuonana na Mtaalamu haraka iwezekanavyo kwani Saratani hii ikigundulika mapema, uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi

#BreastCancerAwarenessMonth #PublicHealth #BreastCancer
πŸ‘6
#JFUWAJIBIKAJI: Rushwa ni janga ambalo lina athari hasi katika Jamii. Linasababisha kucheleweshwa Maendeleo na kudhoofisha utoaji wa Huduma za Msingi

Vitendo vya #Rushwa huumiza Wananchi kwani vinachepusha Rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo kwa Manufaa ya wachache

Umewahi kuombwa "Chochote kitu" ili kupatiwa Huduma ya Msingi?
πŸ‘6
#JFDATA: Inakadiriwa kuwa 81% ya takriban Watu Bilioni 1 wenye changamoto ya Utambulisho kutokana na kukosa Vielelezo muhimu wanatokea Afrika (Kusini mwa Jangwa la Sahara - Milioni 494) na Asia Kusini - Milioni 312

#JamiiForums
πŸ‘6
MUHIMBILI: Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali (MNH), Prof. Mohamed Janabi, ameagiza Wagonjwa kupelekwa Wodini kwa Magari ya Wagonjwa na sio kusukumwa Vitandani

> Pia, Miili ya marehemu ibebwe kwa Ambulance sio Vitanda kama awali

Soma https://jamii.app/JanabiMNH

#SeriviceDelivery
πŸ‘16
DAR: AIRTEL YADAIWA TSH. MIL 490 KWA KUTUMIA SAUTI YA MTU BILA RIDHAA YAKE

Nixon Bandago amefungua kesi Mahakama Kuu kwa kutoridhia sauti ya "Airtel the Smartphone Network" kutumika kwenye matangazo ya Biashara

Zaidi https://jamii.app/AirtelTZ

#DigitalRights #DataProtection
😁22πŸ‘13❀3
NECTA: WENYE MAHITAJI MAALUM WAONGEZEWE DAKIKA KWENYE MITIHANI YA DARASA LA 7

Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA amesema wenye mahitaji maalum waongezewe Dakika 20 kwa kila Saa ktk Somo la Hisabati na Dakika 10 kwa kila Saa kwa Masomo mengine

Soma https://jamii.app/MahitajiMaalum

#HakiMtoto
πŸ‘11πŸ‘2
POLISI: UCHUNGUZI UNAONESHA MKE WA MASANJA ALIMKATAA KIMAPENZI ALIYEJIUA

Uchunguzi wa awali unaonesha Joas Steven, aliyekuwa Katibu wa Kanisa la 'Feel Free Church' linaloongozwa na Emmanuel Mgaya alipata mfadhaiko na kujiua kwa kujinyonga

Soma https://jamii.app/KatibuKujinyonga

#JFMatukio
πŸ‘9😁4πŸ€”4
MWANZA: ZUMARIDI NA WENZAKE WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mashtaka yao ni kufanya shambulio la kudhuru Mwili, kuzuia Askari kutekeleza majukumu yake na kuzuia Ofisa wa Umma kutekeleza majukumu yake

Ushahidi wa utetezi utaanza Oktoba 17, 2022

Soma https://jamii.app/ZumaridiKesi3

#SocialJustice
πŸ‘8
MAPINDUZI YA KIDIGITALI YASIWAACHE NYUMA WATU WENYE ULEMAVU

Ujumuishaji wa Kidigitali unapaswa kutomwacha yeyote. Hii itasaidia kukuza Maendeleo jumuishi

Kusaidia Watu wenye Ulemavu kukuza Ujuzi wa Kidigitali kunaweza kuwatengenezea fursa mpya

Zaidi https://jamii.app/DigInclusion

#DigitalRights
πŸ‘8
KENYA: RAIS RUTO ARUHUSU KILIMO CHA MAHINDI YALIYOZUIWA KWASABABU ZA KIAFYA

Ameidhinisha uingizwaji wa Mazao na Vyakula vilivyobadilishwa Vinasaba (GMO) kwa lengo la kukabiliana na Njaa kali

Pia, amepunguza Bei ya Mbolea kwa nusu bei

Soma https://jamii.app/GMOKE

#Accountability
πŸ‘12😁2
Takriban 15% ya idadi ya Watu duniani wanaishi na aina fulani ya Ulemavu

Idadi kubwa ya Watu wenye Ulemavu katika Nchi za Kipato cha Chini hawana Ujuzi/Ufahamu mpana wa Mitandao, au wanapata changamoto ya kuifikia na kuitumia kupata Elimu, Kazi na Huduma mbalimbali

#DigitalRights
πŸ‘6πŸ€”2πŸ”₯1
INDIA: RAIA WA KENYA WAKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

Faridah alikutwa na Gramu 980 zinazodhaniwa kuwa #Cocaine na Nyanzangu akiwa na Kilo 5.16 zinazoshukiwa kuwa #Heroine

Watuhumiwa hao wanaweza kufungwa hadi miaka 20 jela wakikutwa na hatia

Soma https://jamii.app/DrugsInIndiak
#DrugTrafficking
😱5πŸ‘2
BEI MPYA ZA MAFUTA: Kuanzia Oktoba 5, 2022 kwa Dar Petroli itauzwa Tsh. 2,886, Dizeli Tsh. 3083 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,275 kwa lita

EWURA imesema hiyo ni kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hizo kwenye Soko la Dunia

Soma https://jamii.app/EWURAOct

#JFGovernance #ServiceDelivery
πŸ‘8πŸ”₯1πŸ‘1