JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YASEMA MSIMAMO KUHUSU 'EPA' UKO PALEPALE

Serikali imekanusha suala la kusaini Economic Partnership Agreement 'EPA'

> EPA ni makubaliano yatakayoruhusu nchi za Ulaya kuingiza bidhaa ktk nchi zinazoendelea bila kutozwa kodi

Soma https://jamii.app/TanzaniaEPA
#JFUchumi
TABORA: Jeshi la Polisi limekamata Watu 9 ambao wametajwa kuhusika na tuhuma za Mauaji na mauziano ya viungo vya Binadamu

Huwachoma Watu na kitu chenye ncha kali Shingoni na kukinga Damu ambayo hununuliwa kwa Tsh. 600,000 kwa chupa.

Soma - https://jamii.app/SehemuZaSiri

#HumanRights #JFMatukio
RIPOTI: UCHAFU HUSABABISHA TAKRIBAN VIFO MILIONI 9 KILA MWAKA

Ripoti ya UN imesema uchafuzi husababisha vifo vingi Duniani kuliko hata vitokanavyo na COVID-19

Uchafuzi umetajwa kusababisha ukiukwaji wa Haki ya kuishi katika Mazingira safi

Soma - https://jamii.app/PollutionDeaths

#JFAfya
UTAFITI: WAENDA KWA MIGUU HUKWEPA MADARAJA KUTOKANA NA UREFU

Wanaovuka Barabara hukwepa kutumia Madaraja kutokana na urefu wa Madaraja, hofu ya Wizi na Uporaji

Hali hiyo ni changamoto kwani 30% ya Ajali zinazotokea zinahusisha watembea kwa Miguu

Soma - https://jamii.app/MadarajaYaJuu
KENYA: MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUMIA MUME PICHA ZA FARAGHA ZA MKEWE

Stephen Kamande anakabiliwa na Mashtaka ya kutuma picha za utupu zinazodaiwa kuchukuliwa akiwa faragha na Mke wa Mtu

Pia anashtakiwa kwa kumsumbua Mwanamke huyo na kumtishia kifo

Soma https://jamii.app/StudPicsKE

#DataPrivacy #DataProtection
Rais wa #Algeria, Abdelmadjid Tebboune amesema Serikali itaanza kuwalipa Vijana wasio na Ajira kila Mwezi dinari 13,000 (Tsh. 230,000) kuanzia Machi 2022

Pia, Vijana hao watanufaika na Bima ya Afya na kuondolewa Kodi kwenye baadhi ya Bidhaa

Soma - https://jamii.app/UnemploymentBenefits

#Governance
👍1
MOROGORO: MTOTO AUAWA KWA MAPANGA NA BINAMU YAKE

Faidhati Ibrahim (13) ameuawa kwa kukatwa na mapanga na Kaka yake ambaye ni Binamu aitwaye Shomari Malima

Ugomvi kati ya Mama wa Marehemu na Mama wa Mtuhumiwa umetajwa kuwa sababu

Soma - https://jamii.app/MtotoMauaji

#JFMatukio
MAGONJWA YA AFYA YA AKILI YANATIBIKA NA KUEPUKIKA, TUVUNJE UKIMYA

Mdau anasema Jamii inapaswa kuwaonyesha Upendo wenye Matatizo ya Afya ya Akili na kutowatenga. Pia, kuwepo utaratibu wa kuwasaidia katika mahitaji yao ya msingi ikiwemo kuwapeleka kupata huduma

Soma - https://jamii.app/AfyaAkiliSOC

#StoriesOfChange #JFAfya
SARATANI: Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya (WHO) Mwaka 2020 zinaeleza ongezeko la Visa vipya vya Saratani linakadiriwa kufikia Milioni 19.3, huku Vifo vikiwa Milioni 10

Ulimwenguni kote, inakadiriwa Visa vipya Milioni 28.4 vya Saratani vinaweza kutokea hadi kufikia Mwaka 2040, huku ongezeko kubwa likiwa katika Ukanda wa Nchi zinazoendelea

#JamiiForums #Cancer #JFData
TANZANIA KUFANYA MAKUBALIANO YA KUTENGENEZA NDEGE NDOGO

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kipo ktk hatua za mwisho za majadiliano na Kampuni ya #Skyleader inayotengeneza Ndege ndogo ili ifanye Uwekezaji wa Ndege hizo Nchini Tanzania

Soma - https://jamii.app/Ultralight
#COVID19: Shirika la Afya (WHO) limesema Maambukizi vya Corona yamepungua kwa 19% Wiki iliyopita. Visa vipya Milioni 16 na Vifo 75,000 viliripotiwa kuanzia Februari 7 - 13, 2022

Virusi aina ya Alpha, Beta na #Delta vinaendelea kupungua

Soma - https://jamii.app/WHOCovid

#UVIKO3
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema baadhi ya Watanzania walijifanya Wagonjwa wa COVID-19 na kwenda kutibiwa #India lakini walikuwa wakibeba #DawaZaKulevya

Watumishi wa Afya wametakiwa kuwa makini wanapotoa vibali

Soma - https://jamii.app/CoronaDawaZaKulevya

#JFMatukio
KIGOMA: WANAFUNZI WADAIWA KUJISAIDIA VICHAKANI BAADA YA VYOO VYA SHULE KUTITIA

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kasaba wako hatarini kupata Magonjwa ya mlipuko kutokana na kutokuwa na Huduma ya Vyoo tangu Mwaka 2020 baada ya vilivyokuwepo kutitia

Soma - https://jamii.app/WnfzVyooTitia

#JFUwajibikaji #HakiMtoto
#SOMALIA: Wanamgambo wa Al-Shabaab wameshambulia Vituo viwili vya Polisi Mjini #Mogadishu na kusababisha vifo vya Watu 5 na majeruhi 16

Shambulio hilo limetokea Februari 16. Serikali imesema shambulio limeshadhibitiwa na Vikosi vya Usalama

Soma - https://jamii.app/AlshababSomalia
#JFLeo
BRUSSELS, UBELGIJI: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya Lissu kukutana na kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali

Lissu amwomba Rais afanye analoweza kwa Mamlaka yake ili Kesi dhidi ya Mbowe iondolewe

Soma zaidi > https://jamii.app/LissuRaisSamia

#Governance
BURKINA FASO: Jeshi Nchini humo limeahidi kushirikiana na ECOWAS katika kurejesha Mchakato wa Uchaguzi wa Kidemokrasia

Hata hivyo, haijawekwa wazi ni muda gani Luteni Kanali Paul-Henri Damiba aliyeapishwa kuwa Rais wa Taifa hilo atakaa Madarakani

Soma - https://jamii.app/UtawalaJeshiBF

#JFDiplomasia
#MICHEZO: TFF imemfungia kwa miaka 5 pamoja na faini Tsh. milioni 6, Shaffih Dauda kujihusisha na masuala ya Soka ndani na nje ya Nchi

Dauda alilalamikiwa kwa kuandika TFF kuwa sio kama Nyumba ya Kupanga inayoongoza kiimla na mwenye Nyumba

Soma - https://jamii.app/ShafiiTFF

#JFSports
UJERUMANI NA AUSTRIA KULEGEZA KANUNI ZA #COVID19

Ujerumani italegeza Kanuni kufuatia Wimbi la Maambukizi kutokana na Kirusi cha #Omicron kuonekana limepita kilele chake

Serikali ya Austria italegeza asilimia kubwa ya Kanuni kuanzia Machi 5

Soma https://jamii.app/KanuniUVIKO

#UVIKO3 #Governance
NCHI TATU ZA AFRIKA KUPEWA VIFAA VYA KUZALISHA CHANJO

Kampuni ya BioNTech na #Pfizer zitaleta Vifaa vya kutengeneza Chanjo #Rwanda, Senegal na Afrika Kusini Julai 2022

Vitawezesha utengenezaji wa Chanjo ya #CoronaVirus, #Malaria na Kifua Kikuu

Soma - https://jamii.app/VifaaChanjo

#JFAfya
RAIS MWINYI: #ZANZIBAR HAINA WAGONJWA WA UVIKO-19

Serikali imesema hivi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja, lakini haiwezi kuweka wazi kama Ugonjwa umeisha moja kwa moja

Imeelezwa, hakuna kisa kipya kwa Wakazi wala Wageni tangu Januari 2022

Soma - https://jamii.app/COVIDZnz

#UVIKO3 #JFAfya