JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAHAMU YANAYOJIRI KUHUSU CHANJO YA #COVID19 (SEHEMU YA 2)

- Chanjo inayotengenezwa na Kampuni ya #Pfizer na #BioNTech imeripotiwa kuwa na uthabiti wa zaidi ya 90% huku ile ya #Moderna ikielezwa kuwa na uthabiti wa 94.5%

- Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwa sasa haliwezi kuthibitisha upatikanaji wala usalama wa chanjo yoyote kwa kuwa bado zipo katika majaribio

Soma - https://jamii.app/VaccineCOVID19
#Vaccines
'SYSTEM' ZA CHANJO YA #COVID19 YA PFIZER ZADUKULIWA

> Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya nyaraka kuhusu chanjo ya #Pfizer na #BioNTech zimeingiliwa

> Chanjo hiyo ilionesha uwezo wa kinga kwa asilimia 95 kwa watu 30,000 waliojaribiwa

Soma - https://jamii.app/PfizerCyberAttack
#DigitalSecurity
KOREA KASKAZINI YASHUTUMIWA KUDUKUA TEKNOLOJIA YA KUTENGENEZA CHANJO YA #COVID19

> Shirika la Kijasusi la Korea Kusini limeituhumu Nchi hiyo kuiba teknolojia toka Marekani ya utengenezaji wa #Pfizer

> Haijabainishwa kiasi cha taarifa zilizoibwa

Soma https://jamii.app/NorthKoreaUdukuzi
EMA YAIDHINISHA CHANJO YA #PFIZER KWA WENYE MIAKA 12-15

Shirika la Dawa Ulaya (EMA) limeidhinisha Chanjo dhidi ya #COVID19 ya Pfizer-BioNTech kwa Watoto wa miaka hiyo

Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya(EU) zitaamua ikiwa zitaitoa kwa kundi hilo

Soma > https://jamii.app/PfizerWatotoEU
MAREKANI: CDC KUJADILI KUVIMBA KWA MOYO KWA WALIOPATA CHANJO YA #PFIZER NA MODERNA

Watu 226 wameripotiwa kuwa na tatizo la #Myocarditis na #Pericarditis baada ya kupata chanjo

Wengi wamepona lakini 41 bado wana dalili, 15 wamelazwa na 3 wapo ICU

Soma - https://jamii.app/ChanjoMoyo
#UVIKO3
WHO: NCHI TAJIRI ZIGAWE CHANJO KWA NCHI MASIKINI

Kampuni zinazotengeneza Chanjo za #Moderna na #Pfizer zimetakiwa kutoa kipaumbele kwa nchi masikini

> Mataifa tajiri yamelaumiwa kufanya ulimbikizaji kwa hofu kuwa Chanjo ya tatu itahitajika

Soma https://jamii.app/ChanjoTajiri
#UVIKO3
KENYA YAAZIMIA KUCHANJA WATU WOTE IFIKAPO DESEMBA 2022

Wakenya milioni 1.04 hadi sasa wamepata Dozi ya Kwanza ya #AstraZeneca, huku wanaotakiwa kuchomwa ni milioni 26

> Watu 416,000 wanaweza kuchomwa Chanjo ya #Pfizer kama Dozi ya Pili

Soma https://jamii.app/2022Chanjo
PFIZER YATENGENEZA DOZI YA KWANZA KWA KIRUSI KIPYA CHA DELTA

Kampuni ya Chanjo ya #Pfizer imetangaza kutengeneza Chanjo ya kukabiliana na Kirusi kipya cha #COVID19 aina ya #Delta ambapo majaribio yanapangwa kuanza Agosti hii

Soma - https://jamii.app/PfizerDeltaDose
#UVIKO3
MAREKANI: CHANJO YA ZIADA YAIDHINISHWA KWA KUNDI MAALUM

Mamlaka ya Chakula na Dawa(FDA) imeidhinisha Chanjo za ziada za #Pfizer na #Moderna kwa watu ambao kinga yao ya mwili imeathiriwa

Imefanya hivyo kutokana na kuwepo Kirusi Delta

Soma > https://jamii.app/USBoosterVaccines

#UVIKO3
TANZANIA KUPOKEA DOZI 500,000 ZA PFIZER

Akiwa Mwanza Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema, "Hizi #Pfizer ni sehemu ya Dozi 3,700,000 za Chanjo zitakazoletwa na COVAX Facility. Mwisho wa mwezi Oktoba zitakuja hizo Laki Tano"

Soma - https://jamii.app/PfizerTZ

#UVIKO3
#COVID19: IFAHAMU CHANJO AINA YA #PFIZER

Imeidhinishwa na WHO kuwa salama kwa Watu wenye miaka 12 na zaidi. Pia, imethibitika kuwa salama kwa Wajawazito

Inatolewa kwa Dozi mbili ambapo Dozi ya pili hutolewa siku 21 - 28 baada ya Dozi 1

Soma - https://jamii.app/FahamuChanjo

#UVIKO3
MAREKANI YAIDHINISHA PFIZER KWA WATOTO WA MIAKA 5 HADI 11

Chanjo hiyo dhidi ya #COVID19 imeidhinishwa kwa Watoto walio na umri huo, ikielezwa Wataalamu wamebaini ina ufanisi wa 91%

Tayari wenye miaka 12 na zaidi wameruhusiwa kupata #Pfizer

Soma https://jamii.app/PfizerChanjo

#UVIKO3
TANZANIA YAPOKEA DOZI 499,590 ZA #PFIZER

Waziri kwa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Tanzania imepokea Dozi 499,590 za Chanjo hiyo dhidi ya #COVID19

Asema kufikia Novemba 19 takwimu zinaonesha Wananchi 1,359,624 wamefikiwa na Chanjo

Soma - https://jamii.app/PfizerTanzania

#UVIKO3
AFRIKA KUSINI: Serikali imeomba Kampuni za Johnson & Johnson na #Pfizer kuchelewesha utoaji wa Chanjo kutokana na kuwa na Chanjo nyingi kwenye maghala

35% ya Wananchi wameshapata Chanjo kamili huku Nchi ikiwa na dozi Milioni 16.8 ghalani

Soma - https://jamii.app/StockVaccineSA

#UVIKO3
TANZANIA YAPOKEA DOZI 376,320 ZA CHANJO YA MODERNA

Hii ni Awamu ya Kwanza kwa aina hii ya Chanjo kuingia Nchini. Dozi hizo zitatumika kuchanja Watu 188,160

Hadi sasa Tanzania imepokea Dozi 6,408,950 zikijumuisha #Sinopharm, J&J na #Pfizer

Soma - https://jamii.app/ModernaTZ
#UVIKO3
#COVID19: Kampuni ya #BioNTech pamoja na mshirika wake #Pfizer, wameomba kibali cha dharura Marekani, cha matumizi ya Chanjo ya Corona kwa Watoto chini ya miaka 5

Wakipata Kibali itakuwa Chanjo ya 1 kutumika kwa Watoto kuanzia Miezi sita

Soma - https://jamii.app/BioNtechInfants

#UVIKO3 #JFAfya
NCHI TATU ZA AFRIKA KUPEWA VIFAA VYA KUZALISHA CHANJO

Kampuni ya BioNTech na #Pfizer zitaleta Vifaa vya kutengeneza Chanjo #Rwanda, Senegal na Afrika Kusini Julai 2022

Vitawezesha utengenezaji wa Chanjo ya #CoronaVirus, #Malaria na Kifua Kikuu

Soma - https://jamii.app/VifaaChanjo

#JFAfya
#MODERNA YADAI KUIBIWA TEKNOLOJIA YA KUTENGENEZA KINGA YA UVIKO-19

Imefungua mashtaka dhidi ya Kampuni ya #Pfizer na #BioNTech ikidai wameiba Teknolojia yao ya kutengeneza Dawa kinga iliyotengenezwa Marekani Miaka ya nyuma 2010 na 2016

Soma - https://jamii.app/Covid19Technology

#COVID19
👍8😁1