JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SOMALIA: Maeneo ya karibu na Ikulu ya Rais wa #Somalia Mjini #Mogadishu yameshambuliwa kwa mabomu muda mfupi baada ya Bunge kuidhinisha Baraza la Mawaziri lenye Wajumbe 75

Somalia, taifa lililopo katika pembe ya Afrika linakabiliwa na Umasikini na janga la njaa

Soma - https://jamii.app/BomuIkuluSom
👍7
#SOMALIA: UNHCR imesema ukame wa kihistoria Nchini humo umepelekea Watu 1,000,000 kuyakimbia makazi yao

Idadi ya wanaokabiliwa na Njaa inatarajiwa kuongezeka kutoka Watu milioni 5 hadi zaidi ya milioni 7 Miezi kadhaa ijayo

Soma - https://jamii.app/SomaliaNjaa
#HumanRights
👍4😢2
#SOMALIA: Baada ya shambulizi la risasi na mabomu lililoua Watu 21 na kujeruhi 117 katika Hoteli, Rais Hassan Sheikh Mohamud ameahidi vita kali ya kutokomeza Kundi la Al-Shabaab

Aidha, Serikali ya #Norway imedai katika tukio hilo la #Mogadishu kuna raia kadhaa wa Norway wameuawa

Soma - https://jamii.app/AttackInSomalia

#Governance
👍9
UNICEF imesema Nchini #Ethiopia, #Kenya na #Somalia idadi ya Watu wanaokabiliwa na uhaba wa Maji imeongezeka kutoka Milioni 9.5 hadi Milioni 16.2 ndani ya Miezi 5

Nchi za Afrika Magharibi na Kati za Burkina Faso, Chad, #Mali, Niger na #Nigeria, Watoto Milioni 40 wapo katika hatari kubwa ya kukosa Maji

Soma - https://jamii.app/MajiAfrika

#HumanRights
👍10
#SOMALIA: Kwa mujibu wa Takwimu za UNICEF, Watoto 730 wamefariki dunia katika Vituo vya Lishe kati ya Januari - Julai 2022. Inahofiwa idadi hiyo inaweza kuongezeka

Magonjwa yanayosumbua Watoto wengi ni Utapiamlo, Surua, Kipindupindu na #Malaria

Soma https://jamii.app/NjaaSomalia2022

#JFAfya
😢5👍2
#SOMALIA: BOMU LA KUJITOA MHANGA LAUA MWANAJESHI

Wanajeshi wengine 6 wamejeruhiwa katika tukio hilo ndani ya Kambi ya Jeshi ya #Mogadishu

Kundi Al Shabaab limejitaja kuhusika na limedai bomu hilo limeua Wanajeshi 32 na kujeruhi 40

Soma - https://jamii.app/BomuSomalia

#Terrorists
🤯4👍3👎3
SOMALIA: Watu 100 wamefariki na 300 kujeruhiwa katika Milipuko ilitokea katika Magari mawili Jijini #Mogadishu

Rais wa #Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amelaumu Al-Shabaab kuhusika

Pia Mwandishi wa kujitegemea, Mohamed Isse Kona, ni kati ya waliouawa

Soma https://jamii.app/100PeopleKilled

#HumanRights
👍3😢3🤔1
#SOMALIA: Mahakama ya Kijeshi imemhukumu kifo Mohamed Abdulkadir Sheikh Ibrahim, Afisa wa Polisi aliyekutwa na hatia ya kumchoma Visu Mfanyabiashara Abdifatah Ali hadi kusababisha kifo chake

> Walikuwa wakigombea Kiberiti cha Sigara

Soma https://jamii.app/SomaliaKiller

#PoliceBrutality
👍2
MWANAJESHI WA UGANDA AWAUA WENZAKE WATATU KWA RISASI

Tukio limehusisha Wanajeshi wa Uganda waliopo #Mogadishu Nchini #Somalia chini ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa #Afrika

Mtuhumiwa amedhibitiwa na uchunguzi unaendelea kubaini chanzo

Soma https://jamii.app/MauajiSomalia

#Diplomacy
👍11🤔2
NCHI 10 ZENYE KIWANGO KIKUBWA CHA RUSHWA DUNIANI

Wakati #Ushelisheli (Seychelles) ikiongoza kwa Nchi za Afrika katika kupambana na #Rushwa na #Ufisadi kupitia ripoti ya #TransparencyInternational (CPI), Somalia imeshika nafasi ya mwisho (180) Afrika na Duniani kote

Ripoti ya #CPI inafanya makadirio ya Viwango vya Rushwa kwenye Sekta za #Umma kwa kutumia kipimo cha 0% hadi 100%, ambapo #Somalia imeonesha kukabiliana na Ufisadi na Rushwa kwa 12% tu

Soma https://jamii.app/CPI2022

#Transparency #Accountability #JFGovernance #CPI2022
👍4
ITALIA: BOTI YAZAMA, WAHAMIAJI 59 WAFARIKI

Inadaiwa ilibeba zaidi ya abiria 150 - 200, kati yao 80 wamesalimika

Boti iligonga mwamba wakati ikitokea #Turkey ikiwa na raia wa #Afghanistan, #Pakistan, #Somalia na #Iran wanaokimbia Nchi zao

Soma https://jamii.app/ItaliaBotiKuzama

#Diplomacy
👍4💔4😁1🤯1
AL-SHABAAB WAUA WANAJESHI 54 RAIA WA UGANDA

Rais wa #Uganda, #YoweriMuseveni amesema mauaji yametokea katika kambi ya walinda Amani Nchini #Somalia

Wiki iliyopita Museveni alisema kumetokea vifo vya Waganda lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu Wanajeshi hao wanaohudumu katika Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika Nchini Somalia (ATMIS).

Soma https://jamii.app/UGSoldiersKilled

#Governance #JamiiForums
👍4😱4😢4
#JEWAJUA: Baada ya kupata Ugumu katika Utekelezaji wa Mkataba wake na DP World, Bunge la #Somalia lilikubaliana kuipiga Marufuku kampuni hiyo huku ikieleza Mkataba huo unapingana na Katiba, Kanuni za Uwekezaji wa Kigeni na Sheria nyingine za Nchi

Taarifa ya Azimio la Bunge inasomeka "DP World ilikiuka waziwazi Uhuru na Umoja wa Somalia na hivyo DP World imepigwa marufuku Nchini Somalia,"

#DPWorld ilisaini Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari ya Berbera mwaka 2016. Hata hivyo, Mkataba haukuvunjika kutokana na Masharti yake kuwa magumu pamoja na upande mwingine wa Somalia kuutetea.

Soma Zaidi https://jamii.app/DPWSomalia

#JamiiForums #Governance #Accountability #DPWorldSaga
👍7😁6😱2👎1🔥1🥰1
KENYA: Polisi wanawashikilia Abdirahman Shaffi Mkwatili(25) na Sadam Jafari Kitia(30) waliokiri walikuwa wakielekea kujiunga na #AlShabaab, baada ya kuwakamata Julai 12, 2023 wakiwa na daftari lililoandikwa kwa Kiswahili ambalo linadaiwa walikuwa wakitumia kuwaongoza kutoka #Tanzania hadi Jilib, #Somalia

Kukamatwa kwao kumekuja Wiki 2 baada ya Watanzania wengine watatu, Abdul Saif Salimu, Zuberi Ngare Mtondoo na Seif Abdalla Juma, waliodaiwa kuwa katika harakati za kujiunga na kundi hilo kukamatwa Nchini Kenya kufuatia taarifa za Wananchi

Soma https://jamii.app/AlShabaabWaTZ

#JamiiForums
👍111👎1
Uturuki imetoa Hati ya Kimataifa ya Kukamatwa kwa Mohamed Hassan Sheikh Mohamud ambaye ni Mtoto wa Rais wa #Somalia, Hassan Sheikh Mohamud baada ya kudaiwa kumgonga mwendesha Pikipiki Jijini Istanbul ambaye alifariki Siku 6 baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata

Mohamed alishikiliwa kwa muda kisha kuachiwa baada ya kudaiwa kosa lilikuwa upande wa mwendesha Pikipiki

Meya wa #Istanbul, Ekrem İmamoglu ameonesha picha za CCTV za tukio hilo la Novemba 30, 2023 zinazodaiwa kuonesha Pikipiki iligongwa kwa nyuma. Askari walipofika nyumbani kwa Mohamed wakajulishwa ana wiki hayupo eneo hilo, ndipo Hati ya Kukamatwa ikatolewa ikiaminika amekimbia Nchi

Soma https://jamii.app/MohamudSomalia

#Diplomacy #Governance #Accountability #JamiiForums
👍21
UTAFITI: Mwaka 2023 umetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi ya Raia ndani ya kipindi cha Miaka 10 iliyopita kulingana na Utafiti wa Shirika la Kutoa Misaada Kuhusu Vurugu za Kivita (AOAV) la England

Ongezeko la vifo kwa Asilimia 112 ni kutoka Mwaka 2022 hadi 2023 ambapo vita ya #Israel na #Hamas imechangia kwa kiasi kikubwa ikifuatiwa na migogoro inayoendelea Urusi na #Ukraine, Sudan, #Myanmar na #Somalia

Milipuko ya 2023 ilikuwa 7,307 kutoka 4,322 ya Mwaka 2022, vifo vya Raia vilikuwa 15,305 na matumizi ya silaha zinazorushwa hewani yaliongezeka kwa 226% (kutoka matukio 519 hadi 1,694)

Soma https://jamii.app/Milipuko2023

#HumanRights #CivilRights #Governance #JamiiForums
👍41
SOMALIA: Mahakama ya Kijeshi Kaskazini mwa #Somalia imewahukumu adhabu ya kifo raia 6 wa Morocco kwa kile kilichoelezwa wana uhusiano na Kundi la Kigaidi, pamoja na hivyo wahusika wana nafasi ya kukata rufaa, ikitokea wakashindwa adhabu itatekelezwa kwa kupigwa risasi hadi kifo

Majina ya wahusika ni Mohamed Hassan, Ahmed Najwi, Khalid Latha, Mohamed Binu Mohamed Ahmed, Ridwan Abdulkadir Osmany na Ahmed Hussein Ibrahim

Wakati huohuo, Mahakama imewahukumu raia wa #Ethiopia na Somalia, vifungo vya Miaka 10 gerezani kila mmoja kutokana na kuhusika katika kesi hiyo. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama amewaambia Waandishi wa Habari kwamba raia wa Morocco walikamatwa Puntland kufuatia uchunguzi uliofanyika kwa Mwezi mmoja

Soma https://jamii.app/SomaliaHukumu

#Diplomacy #Governance #JamiiForums
👍81
DIPLOMASIA: Nchi ya #Somalia imekuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya kukamilisha hatua zote zilizohitajika ili kujiunga na Jumuiya hiyo

Sekretarieti ya #EAC imechapisha taarifa inayoonesha Ujumbe wa Somalia ukikabidhiwa Hati yake ya Kuidhinishwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ikiwa ni utekelezaji wa Makubaliano yaliyoafikiwa Novemba 2023 na Wakuu wa Nchi nyingine za EAC

Somalia inakuwa Mwanachama wa nane wa EAC ikiungana na #Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, #Kenya, Sudan Kusini, #Tanzania, Rwanda na #Uganda.

Soma https://jamii.app/SomaliaEACOkays

#JamiiForums #Diplomacy #Governance #EACDecides
👎31
Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeitaka #Somalia kutoruhusu marekebisho ya #Katiba ambayo yanalenga kupunguza umri wa Utu uzima kwa madai hali hiyo itadhoofisha Haki za Watoto

Mabadiliko yaliyopendekezwa ambayo yatajadiliwa #Bungeni leo, Machi 30, 2024 yanapendekeza Umri wa Utu Uzima wa Miaka 15 na Miaka 18 kama Umri wa kuwajibika Kisheria

Human Rights Watch imesema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawaweka Wasichana katika hatari kubwa ya Ndoa za Utotoni, ambazo huathiri Afya zao, haswa Afya ya Uzazi, upatikanaji wa Elimu, na Ulinzi wao dhidi ya Unyanyasaji

Soma https://jamii.app/SomanChildAge

#JamiiForums #HumanRights #InvestInWomen #ChildProtection #HakiWatoto
👍81
Ripoti ya Utafiti ya Taasisi ya Reporters Without Borders (RSF) iliyotolewa Mei 3, 2024 imeonesha #Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kati ya Nchi zinazolinda Uhuru wa Vyombo vya Habari upande wa Afrika Mashariki

Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa Mwaka 2023 hadi 97 huku #Kenya ikishika nafasi ya 102 kutoka 116 na #Somalia ikiwa nafasi ya 141

Baadhi ya vigezo vilivyotumika ni misingi ya Kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa Wanahabari

Nchi 10 Bora katika ripoti hiyo ni Norway, Denmark, Sweden, Uholanzi, Finland, Estonia, Ureno, Ireland, Switzerland na Ujerumani

Soma https://jamii.app/RSFReport24

#JamiiForums #PressFreedom #UhuruWaHabari2024 #PressFreedom2024 #FreePress2024
👍3👏1