JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#DODOMA: Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya #DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa baadhi ya Bandari za Bahari na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za #Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Soma https://jamii.app/DPWorldSaga

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Accountability
πŸ‘7❀2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA

Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema β€œTuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza β€œKama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”

Soma https://jamii.app/BungeJuni10

#JFHuduma #Governance #TZDPWorld
πŸ‘4❀3
RASMI: BUNGE LAPITISHA AZIMIO LA KUUNGA MKONO MKATABA WA TANZANIA NA DP WORLD
-
Bunge limepitisha Makubaliano kuhusu Ushirikiano wa #Tanzania na Kampuni ya #Dubai ya #DPWorld katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa baadhi ya Bandari za Maziwa na Bahari zilizopo Tanzania Bara, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam
-
Makubaliano ya Mkataba huo yaliibua maswali kutoka kwa Wananchi ikiwemo thamani na muda wa utekelezaji, pia sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi, migogoro katika utekelezaji mikataba iliyosababisha baadhi ya nchi kuvunja mikataba
-
#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Accountability
πŸ‘Ž24😱9πŸ‘5❀1
PADRI KITIMA: MWEKEZAJI ANAPOKUJA, SERIKALI ISITUMIKE KUUMIZA RAIA WAKE

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (#TEC), Padri Charles Kitima amesema baada ya kukaa kikao na Serikali wamejulishwa kuwa licha ya Bunge kuridhia azimio la Mkataba wa Bandari na Kampuni ya #DPWorld bado kuna nafasi ya mkataba huo kurekebishwa

Baada ya kikao cha Viongozi wa dini mbalimbali na Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa, Padri Kitima amesema β€œPamoja na hivyo tunahakikisha sauti ya Wananchi hazipuuzwi.”

Ameongeza β€œKuna umuhimu wa kuzingatia #HakiZaBinadamu pale Mwekezaji anapopewa eneo, Serikali isitumike kuumiza raia wake, tumekumbusha kuhusu hilo.”

Soma https://jamii.app/UfafanuziWaMbarawa

#Governance #FreedomOfSpeech #JFUwajibikaji23 #JamiiForums
πŸ‘10❀1
PADRI KITIMA: KWENYE MKATABA WA BANDARI, SERIKALI IUNDE KAMPUNI SIYO YENYEWE ISAINI MIKATABA

Ushauri huo umetolewa baada ya kikao cha Viongozi wa dini mbalimbali na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kujadili mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld

Akizungumza kwa niaba ya Viongozi hao, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (#TEC), Padri Charles Kitima amesema β€œSerikali inatakiwa kuunda Kampuni ambayo hata ikitokea migogoro inayoshtakiwa ni Kampuni na sio Nchi. Mfano inatokea unamnyang’anya Mtu Ekari 10 anaenda kushikilia Ndege ya mabilioni.”

Soma https://jamii.app/UfafanuziWaMbarawa

#TZDPWorld #Governance #FreedomOfSpeech #JamiiForums
πŸ‘11❀1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akichambua kuhusu mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya #DPWorld ya #Dubai, Balozi Mstaafu, Dkt. #WillibrodSlaa anasema β€œNimegundua tatizo la ajabu, tunajua suala la Bandari ni la Muungano lakini #Zanzibar wana Sheria yao ya Bandari, inakuwaje Nchi moja ina bandari mbili, hilo ni tatizo la Katiba.”

Ameongeza β€œKuna mambo mengi hata Bunge limefichwa, kilichofanyika juzi ni uhuni, kama Bunge halijui kuwa Bara kuna Sheria ya Bandari na Zanzibar pia ipo na halijakemea wakati #Katiba haijarekebishwa basi Bunge hilo ni la ajabu sana.”

Soma https://jamii.app/SlaaJuni13

#Siasa #Governance #FreedomOfSpeech #JamiiForums
πŸ‘7
RC CHALAMILA: WANAOTAKA KUANDAMANA WAACHE MARA MOJA

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Mkoa wa #Dar, #AlbertChalamila amewataka Raia waliokusudia kuandamana kupinga Mkataba wa #Tanzania na #DPWorld waache mara moja akisema huu sio muda wa Maandamano

Mapema wiki hii Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Deusdedith Soka aliitisha maandamano ya Amani kuelekea Ikulu ya #Magogoni kwa lengo la kupinga mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na DP World

Soma https://jamii.app/StopMaandamano

#PeacefulProtests #Democracy #DPWorldSaga
πŸ‘3πŸ”₯1πŸ€”1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Maandamano hayo ya Amani kuelekea Ikulu ya #Magogoni, yaliitishwa na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Deusdedith Soka, kwa lengo la kupinga mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na #Dubai kupitia kampuni ya #DPWorld

Soma https://jamii.app/PeacefulProtests

#JamiiForums #DPWorldSaga #PeacefulProtests #Democracy
πŸ‘3
#JEWAJUA: Baada ya kupata Ugumu katika Utekelezaji wa Mkataba wake na DP World, Bunge la #Somalia lilikubaliana kuipiga Marufuku kampuni hiyo huku ikieleza Mkataba huo unapingana na Katiba, Kanuni za Uwekezaji wa Kigeni na Sheria nyingine za Nchi

Taarifa ya Azimio la Bunge inasomeka "DP World ilikiuka waziwazi Uhuru na Umoja wa Somalia na hivyo DP World imepigwa marufuku Nchini Somalia,"

#DPWorld ilisaini Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari ya Berbera mwaka 2016. Hata hivyo, Mkataba haukuvunjika kutokana na Masharti yake kuwa magumu pamoja na upande mwingine wa Somalia kuutetea.

Soma Zaidi https://jamii.app/DPWSomalia

#JamiiForums #Governance #Accountability #DPWorldSaga
πŸ‘7😁6😱2πŸ‘Ž1πŸ”₯1πŸ₯°1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa #CHADEMA, John Mnyika, amesema Wabunge wanaojiita 'Chawa wa Mama' hawawezi kusimama kwa niaba ya Wananchi kwakuwa wanalipa fadhila badala ya kuiwajibisha Serikali

Akigusia suala la #DPWorld na Bandari, amesema kama Bunge lingewajibika Kikatiba, lingekataa Makubaliano hayo kama Bunge la #Marekani lilivyoikatalia Kampuni hiyo kuendesha Bandari zake Mwaka 2006 licha ya Rais #GeorgeWBush kushinikiza ipewe Mkataba

Soma https://jamii.app/MnyikaBunge

#JamiiForums #Democracy #Accountability #JFUwajibikaji23
πŸ‘10❀3
MBEYA: Mahakama Kuu ya Kanda, imeombwa kuharakisha maombi ya usikilizwaji wa Kesi ya kupinga Mkataba wa Uwezekezaji kati ya #Tanzania na #Dubai pamoja na kusitisha shughuli zozote za #DPWorld kwenye Bandari

Wakili wa Waleta Maombi, #BonifaceMwabukusi, amesema Mahakama ichukue uamuzi huo ili kutopoteza Rasilimali za Nchi kwa kuwa utekelezaji wa suala hilo unalalamikiwa, pia tayari kuna Kesi Mahakamani kati ya Serikali na Wanachi

Soma https://jamii.app/DPWolrdMBY

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji23 #Accountability #DPWorldSaga
πŸ‘7πŸ‘4
Serikali imewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa Kijamii na Kiuchumi kati ya #Tanzania na #Dubai, yanayohusisha Uwekezaji wa Bandari kupitia Kampuni ya #DPWorld, ikiiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya isisikilize na kuitupilia mbali

Kesi hiyo iliyopaswa kusikilizwa leo, Julai 20, 2023 ilifunguliwa na Wanasheria Alphonce Lusako, Emmanuel Kalikenya Changula, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi kwa niaba ya Watanzania, wakipinga makubaliano hayo, na kudai baadhi ya ibara zina masharti mabovu ambayo hayana maslahi kwa Taifa

Soma https://jamii.app/KesiKutupiliwaMbali

#Demokrasia #Democracy #SakataLaDPWorld
πŸ‘7
MBEYA: Mahakama Kuu ya Kanda imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Wakili Boniface Mwabukusi na wenzake waliopinga Serikali ya #Tanzania kuingia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na #Dubai katika Uwekezaji wa Bandari kupitia #DPWorld

Kwa upande wake Wakili Boniphace Mwabukusi amesema β€œKwa kuwa Mahakama imesema haina Mamlaka ya kuingilia shughuli za Bunge, sisi tunakwenda kutumia Civil Parliament (Bunge la Wananchi) tutatoa siku 14 wabadili Mkataba huu.”

Soma https://jamii.app/KesiYaBandari

#Governance #Diplomacy #JamiiForums
😁5πŸ₯°4😒4
#HAKIZABINADAMU: Shirika la Kimataifa la #AmnestyInternational limetoa wito kwa Mamlaka kuwaachia mara moja na bila masharti #WillibrodSlaa, #BonifaceMwabukusi, na #MdudeNyagali, ambao walikamatwa kati ya Agosti 12 na 13, 2023 kwa kudaiwa kutoa kauli za Uchochezi

Dkt. Slaa, Mwabukusi na Nyagali kwa nyakati tofauti wamekosoa hadharani Makubaliano ya Uwekezaji katika Bandari za Tanzania Bara kati ya #Tanzania na #UAE kupitia Kampuni ya #DPWorld. Mwabukusi aliongoza ombi la Mahakama akidai Makubaliano hayo yana vifungu vinavyokiuka #Katiba ya Tanzania na kuhatarisha Uhuru na Usalama wa Taifa

Soma https://jamii.app/AmnestyTamko

#JamiiForums #DPWorldSaga #SakataLaDPWorld #Accountability #Democracy #FreeSpeech #FreedomOfExpression
πŸ‘5
Akifafanua kuhusu uwekezaji wa Kampuni ya #DPWorld katika Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Plasduce Mikeli Mbossa amesema Watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia #DPWorld hivyo hakuna atakaye poteza ajira

Vilevile, Jukumu la Ulinzi na Usalama katika eneo la Bandari na yale yalikodishwa kwa DP World yataendelea kubaki chini ya Serikali

Soma https://jamii.app/MkatabaDPWorld

#JamiiForums #DPWorldSaga #Governance
πŸ‘2❀1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari, Plasduce Mikeli Mbossa amesema Serikali ya Tanzania ina haki ya kujiondoa kwenye Mkataba na DP World pale itakapoona kuna haja ya kufanya hivyo

Pia, amesema Mwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam atalipa kodi zote za Serikali kwa Kuzingatia Sheria za Tanzania

Aidha, ameeleza kuwa Sheria za Tanzania ndizo zitakazotumika katika Utekelezaji wa Mkataba na #DPWorld, lakini pia Mkataba utatoa fursa kwa Watanzania kushiriki katika Uwekezaji huu kupitia Vifungu vya Sheria vinavyolinda maudhui ya Ndani

Soma https://jamii.app/MkatabaDPWorld

#JamiiForums #DPWorldSaga #Governance
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akiongelea Mkataba wa Tanzania na #DPWorld, Rais Samia Suluhu Hassan amesema linapokuja jambo jipya lazima kunakuwa na maoni tofauti na ni Haki yetu kutoa maoni kwa kuwa hiyo ndiyo Demokrasia yetu hivyo Wananchi watoe maoni yao

Amesema pia ni jukumu la Serikali kubeba maoni na kuyafanyia kazi na hilo ndilo Serikali yake imefanya

Soma https://jamii.app/MkatabaDPWorld

#JamiiForums #FreedomOfExpression #FreedomOfSpeech #Accountability #Governance #DPWorldSaga
πŸ‘1
Akiongelea Mkataba wa Tanzania na #DPWorld, Rais Samia Suluhu Hassan amesema, "Mikataba hii iliyosainiwa imezaliwa kutoka katika Makubaliano ya Awali. Lile dude lile lililoleta maneno mengi, ndio limezaa mikataba hii kama ilivyoridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Ameendelea " Nashukuru Baraza la Mawaziri kwa Kubariki mikataba hii Mitatu kwa Mazingatio ya Kifungu cha 2 cha Sheria ya Ubia namba 6 ya 2023, 'Private Partnership Act' (CAP103) na kifungu cha 2 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 2003"

Soma https://jamii.app/MkatabaDPWorld

#JamiiForums #FreedomOfExpression #FreedomOfSpeech #Accountability #Governance #DPWorldSaga
πŸ‘1
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema kutokana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (Gati Namba 0-7), Watumishi wa Bandari hiyo wametakiwa kuchagua kubaki #TPA au kusitisha mkataba wa ajira na kuajiriwa na Kampuni ya #DPWorld papo hapo

Taarifa ya TPA imeeleza mabadiliko hayo yanatokana na Mkataba kati ya TPA na DP World ya #Dubai kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa Gati husika kwa kipindi cha Miaka 30 kuanzia Oktoba 22, 2023

TPA imeeleza Watumishi watakaoridhia kujiunga na DPW kwa hiyari wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao (Notice) Makao Makuu ya TPA kabla ya Machi 29, 2024 na wale ambao hawatapenda kujiunga na DP World watabaki TPA

Soma https://jamii.app/WatumishiBandari

#JFUwajibikaji #JFHuduma #Diplomacy #JamiiForums
πŸ‘7❀2πŸ‘Ž2πŸ”₯1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, ameitaka Serikali kueleza kwanini Mikataba ya Uwekezaji katika Bandari ya Dar kupitia Kampuni ya #DPWorld haijawasilishwa Bungeni ili ijadiliwe na kuhakiki vipingele vilivyokubaliwa kwenye Mikataba hiyo

Akiwasilisha hoja yake wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026, Mpina ameeleza kwa mujibu wa Sheria ya β€˜Natural Resources' Kifungu cha 12, Mikataba yote ya rasilimali lazima ipelekwe Bungeni

Soma https://jamii.app/MpingaDPWorld

#JamiiForums #Governance #Accountability #Transparency #OpenGovernment
πŸ‘1